Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali Nchi nyingi za ulimwengu unaoendelea, au ule uliokuwa ukiitwa ulimwengu wa ta zimegawika sehemu mbili mbili. Sehemu hizi zinazidi kutoshabihiana kila...

Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Nchi nyingi za ulimwengu unaoendelea, au ule uliokuwa ukiitwa ulimwengu wa ta
zimegawika sehemu mbili mbili. Sehemu hizi zinazidi kutoshabihiana kila uchao
zinatengana kiasi cha kukaribia kupigwa mfano wa masafa ya ardhi na mbingu. Seher
zenyewe ni mijini na mashabani. Sehemu hizi, hasa ukizitia katika mizani ya hali na jia
za watu za maisha, zimetofautiana mno. Kiasi cha tofauti hizi ni kikubwa hadi
kuonekana kama kwamba hazina uhusiano kamwe, mithili ya nchi mbili tofauti.

Hebu sasa tuzingatie yale yana yozifanya sehemu hizi kukosa kufanana. Hapa
tutawajibika kuzizingatia tofauti zilizo bayana baina ya watu wa shamba na wa mijini,
hasa kufungamana na jinsi wanavyoyaendesha maisha yao.

Jambo lililo wazi ni kwamba watu wa mashambani hawajapiga hatua ya maana kuhusu
jinsi wanavyuotakikana kuishi katika karne ya ishirini. Watu hawa bado wanaishi kama
walivyoishi mababu zao. Hawahisi halahala ya jambo lolote. Mategemeo yao ni shamba;
usubiriwe msimu mzuri wa mvua, watu walime, Mungu akineemeshe kilimo, wavune
mavuno mema, Chakula kikiwa tayari, wale, walale, siku nyingine warudie mkondo uo
huo wa kuendesha maisha yao.

Watu hawa maisha yao yamepangika mikondo mitatu tu: kuzaliwa, kuoa au kuolewa, na
kufa. Zaidi ya mikondo hii, maisha ya viumbe hawa hayana mabadiliko makubwa.
Mabadiliko haypendelewi sana huko mashambani. Huko, wanaume ni mabwana,
wanawake ni mfano wa vijakazi na watoto hawana tofauti kubea na watwana. Mwanume
akikohoa, mkewe akimbilie kulikokoholewa, na watoto watetemeke. Wanawake wa
shamba na watoto hawana haki hata ya kunena, wala hawajui haki ni nini.

Kwa upande mwingine, mijini kuna viwanda, kuna majumba, kuna magari na kuna
vyombo vingi sana vya maendeleo ya kisiku izi. Watu wa mijini ni watu wa ulimwengu
kote, wala si watu wa mji mmoja tu. Watu wa mji wowote ulimwenguni huweza
kuwasiliana na wenzao wa miji mingine kokote kule ulimwenguni kwa njia ya runinga.
Pia, kwa watu wa mjini, kuona kiumbe kidogo kabisa kisichoweza kuonekana kwa
macho si ibura hata. Kiumbe cha namna hiyo huonekana kupitia mangala. Na kwa wale
walioondokea kuwa wanajimu wa kisasa, kuziona sayari na thurea zilizoko mbali sana
nasi kupitia ningala ni jabo la kawaida sana.

Watu wa mjini huwa na mabadiliko mengi sana katika maisha yao, wala sio mikondo
aina tatu tu. Kwa mfano, wanawake wa mijini hawakubali tena kuonewa na wanaume.
Wanajua vyema sana maslahi yao na wameiweka menke yao mbele; yaani mahali pao
katika jamii, wakiwa wao ni wanawake. Kupigania haki sawa na wanaume bila kulegeza
kamba. Huku kupambana kimaisha kama wapambanavyo wanaume na kufanikiwa kufanya kazi za kusikika kam vile uwakili, udaktari, uhandisi, urubani na nyinginezo
zilizokuwa zikifanywa na wanaume tu. Wanawake wengine hata ni maprofesa! Kweli
watu wa mijini wameendelea.

a) Toa maelezo kuhusu tofauti zinazosemekana ni bayana baina ya maisha ya watu
wa shamba nay ale ya watu wa mijini.
b) Rejelea “Mungu” katika aya ya tatu na neon “viumbe” katika aya ya nne.
Bainisha uhusiano uliopo baina ya manen haya mawili, hasa ukizingatia jinsi
yavyotumiwa katika habari. Je matumizi haya yankupa hisia gani?
c) Unadhani mwandishi ana maana gani anaposema ya kwamba huko mashambani
“wanawake ni mfano wa vijakazi, na watoto hawana tofauti kubwa na watwana?”
d) Orodhesha vifaa vyovyote vitano vilivyotajwa katika taarifa hii, kisha ueleze
umuhimu wa kila kimoja wapo.
e) “Watu wa mijini ni watu wa ulimwengu kote” Hapa mwandishi anamaanisha
nini?
f) (i) Ni nini maana ya neon menke?
(ii) Mwandishi anamaliza taarifa yake kwa kusema “Kweli watu wa mijini
wameendelea.” Kwa muhtasari, ni tabia gani za wanamiji zilizomfanya
kukiri hivyo.

Answers


Kavungya
fig427620191251.png
(b) Uhusiano
Mungu ndiye mwenye uwezo mkubwa/ ndiye aliyeviumba viumbe
Viumbe ni wategemezi/ hafifu/ hawana uwezo/ wanyonge
Hisia
- Viumbe humtegemea Mungu kiasi kuwa bila yeye wataangamia
- Hisia ya huruma
(c) Wanawake na watoto hawana haki/ ni watumwa
(d) Tarakilishi - Kuwasiliana
Mangala Kuona viumbe vidogo
Nangala kuona sayari ya thurea zilizoko mbali
Runinga kusikiliza na kuona
Simu Kuwasiliana
Ghala Usafirishaji
Viwanda Uandaji wa bidhaa
Majumba makaazi/ Biashara
(e) Waweza kuwasiliana ulimwengu kote kwa kutumia teknologia ya kisasa (vifaa
vilivyo tajwa katika (d)
Kuona nakusikia kote ulimwenguni
(f) (i) Mahali/ nafasi/ hadhi/ wajibu/ jukumu zao katika jamii
(ii) Wameendelea kielimu/ sayansi/ teknolia/ kimawasiliano. Kiufundi
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 09:54

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions

  • Kiambishi- U-hutambulisha majina yote ya ngeli ya U (umoja). Hata hivyo baadhi majina hay huchukua viambishi tofauti tofauti katika wingi. Orodhesha majina ma kama hayo, kisha uonyeshe... (Solved)

    Kiambishi- U-hutambulisha majina yote ya ngeli ya U (umoja). Hata
    hivyo baadhi majina hay huchukua viambishi tofauti tofauti katika wingi.
    Orodhesha majina ma kama hayo, kisha uonyeshe viambilshi hivyo tofauti
    vya ngeli (Katika umoja na Wingi)

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza maana mbili za sentensi: Jua nisemalo ni muhimu kwetu. (Solved)

    Eleza maana mbili za sentensi:
    Jua nisemalo ni muhimu kwetu.

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Akifisha: Sijaona kitabu kizuri kama hiki utaniazima siku ngapi bashiri alimuliza sijaona. (Solved)

    Akifisha:
    Sijaona kitabu kizuri kama hiki utaniazima siku ngapi bashiri alimuliza
    sijaona.

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Nyambua vitenzi vifuatavyo ili kupata majina (nomino) mawili mawili tofauti: (i) Kumbuka ii)Cheka (Solved)

    Nyambua vitenzi vifuatavyo ili kupata majina (nomino) mawili mawili
    tofauti:
    (i) Kumbuka
    ii)Cheka

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Andika kwa umoja Tumewaondoleeni matatizo yenu, yafaa mtushukuru. (Solved)

    Andika kwa umoja
    Tumewaondoleeni matatizo yenu, yafaa mtushukuru.

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Mwanamke wa kisasa anazaliwa na kukulia katika mazingira yaliyobadilika mno. Matazamio yake maishani ni tofauti na yale ya wanawake walioishi mapote... (Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
    Mwanamke wa kisasa anazaliwa na kukulia katika mazingira yaliyobadilika mno.
    Matazamio yake maishani ni tofauti na yale ya wanawake walioishi mapote mawili
    yaliyopita; wanawake makamu ya nyanyake na mamaake-kuu.

    Yeye hatarajii kuzaliwa, kukua, kuolewa, kuwa mke wa bwana, kumzalia watoto, na
    daima dawamu kuwa ‘mwendani wa jikoni’ akawapikia watoto na bwanake chakula; na
    akitoka jikoni aelekee shambani kulima, kichakani kuchanja kuni, mtoni kufua nguo na
    kuteka maji ya kutumia nyumbani. Mwanamke wa kisasa huandamana na mwanamume.
    Akanyangapo mume naye papo huutia wayo wake.

    Mwanamke wa kisasa huenda shule na kujifunza yote yafunzwayo huko. Hushindana na
    wanawake kwa wanaume na kuibuka mshindi si mara haba. Huibuka mshindi katika
    masomo ya lugha, historia, jiografia, hesabu, sayansi na mengineyo, sawa na
    mwanamume.

    Mwanamke wa kisasa hutaka kufanya kazi za kibega, akazifanya. Akataka kuwa
    mwalimu, akawa. Akataka kuwa daktari, akafanikiwa. Almuradi, siku hizi mwanamke
    hufanya kazi yoyote ile afanyayo mwanamume. Kuna wanawake marubani wa ndege,
    masonara, waashi, wahandishi, madereva wa magari, mawakili, mahakimu, mawaziri
    wakuu na hata marais wa nchi. Hakuna kazi isiyofanywa na mwanamke siku hizi.

    Mwanamke wa kisasa hateswi akafyata ulimi. Anapohiniwa yeye hupigania haki yake
    kwa dhati na hamasa. Katu hakubali ‘mahali pake’ katika jamii alipotengewa na
    wanaume wenye mawazo ya kihafidhina yaliyopitwa na wakati.

    Siku hizi mwanamke huolewa tu wakati amepata kazi ya kumwezesha kujikimu maishani
    au pale anapokuwa na hakika kwamba biashara yake, iwapo ni mfanyi biashara, imepiga
    hatua ya kutomrudisha ukutani.

    Mwanamke wa kisasa haamuliwi katika jambo lolote, bali hufanya maamuzi yake
    mwenyewe. Kwa upande mwingine, mwanamume wa ‘kisasa’, ambaye bado amefungwa
    pingu na taasubi za kiume, hapendezwi na mwanamke huyu. Huuma kidole akatamani ya
    kale, lakini wapi! Analazimika kumkubali mwanamke huyu kama mshirika sawa
    maishani, na kuishi naye, apende asipende. Shingo upande analazimika kukubali kwamba
    mabadiliko haya sio mithili ya kiwingu kipitacho, bali ni ya aushi.

    a) Msemo ‘mwendani wa vijungu jiko’ unadhihirisha hali gani ya
    mwanamke katika jamii?
    b) Jamii imemfanya mwanamke kuwa hayawani wa mizigo. Fafanua
    c) Eleza maana ya ‘akanyagapo mume papo huutia wayo wake.’
    d) Zungumzia maswala ya ndoa na elimu huku ukilinganisha mwanamke wa
    kiasili na wa kisasa.
    e) Mwanamume wa kisasa anamwonaje mwanamke wa kisasa?
    f) Taja mifano minne ya ‘mawazo ya kihafidhina.
    g) Eleza maana ya:
    (i) Akafyata ulimu……………………………………………
    (ii) Ukatani…………………………………………………….
    (iii) Taasubi za kiume………………………………………….
    (iv) Aushi…………………….………………………………..

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia kirejeshi ( kihusiano) cha ngeli cha mwisho Mwanafunzi anayefanikiwa maishani ni yule anayesoma kwa bidii na pia anayetii wakuu wake (Solved)

    Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia kirejeshi ( kihusiano) cha ngeli cha mwisho
    Mwanafunzi anayefanikiwa maishani ni yule anayesoma kwa bidii na pia
    anayetii wakuu wake

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Tumia semi hizi katika sentensi kuonyesha maana: (i) Kuchokoachokoa maneno (ii) Kumeza shubiri (Solved)

    Tumia semi hizi katika sentensi kuonyesha maana:
    (i) Kuchokoachokoa maneno
    (ii) Kumeza shubiri

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Tunatumia viashiria vya kuthibitisha kwa mfano kitabu kiki hiki. Sasa kamilisha Ni mbwa …………………….. aliyekula chakula cha mtoto (Solved)

    Tunatumia viashiria vya kuthibitisha kwa mfano kitabu kiki hiki. Sasa kamilisha
    Ni mbwa …………………….. aliyekula chakula cha mtoto

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza tofauti mbili muhimu za kimaumbile kati ya wanyama (i) Kifaru (ii) Nyati (Solved)

    Eleza tofauti mbili muhimu za kimaumbile kati ya wanyama
    (i) Kifaru
    (ii) Nyati

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Watu wafuatao wanafanya kazi gani (i) Mhasibu (ii) Mhazili (Solved)

    Watu wafuatao wanafanya kazi gani
    (i) Mhasibu
    (ii) Mhazili

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Tumia viunganishi vingine badala ya vile vilivyotumiwa katika sentensi hizi: (i) Anayetafuta hachoki hata akichoka keshapata (ii) Ngonjeeni hadi washiriki wote wafike (Solved)

    Tumia viunganishi vingine badala ya vile vilivyotumiwa katika sentensi hizi:
    (i) Anayetafuta hachoki hata akichoka keshapata
    (ii) Ngonjeeni hadi washiriki wote wafike

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Taja madini mawili ambayo yametukuzwa zaidi, moja kwa thamani yake ya kifedha na nyingine kwa kutengeneza vyuma vigumu kuliko madini mengine (Solved)

    Taja madini mawili ambayo yametukuzwa zaidi, moja kwa thamani yake ya
    kifedha na nyingine kwa kutengeneza vyuma vigumu kuliko madini mengine

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Onyesha kielezi, kivumishi, kitenzi na jina katika sentensi: Watu wane walipeperushwa juu kwa juu na upepo mkali (Solved)

    Onyesha kielezi, kivumishi, kitenzi na jina katika sentensi:
    Watu wane walipeperushwa juu kwa juu na upepo mkali

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Akifisha kifungu hiki: Nilopomwendea aliniangalia kisha akaniambia siamini kuwa ni wewe uliyeandika insha hii. (Solved)

    Akifisha kifungu hiki:
    Nilopomwendea aliniangalia kisha akaniambia siamini kuwa ni wewe uliyeandika
    insha hii.

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata Kuna sayansi mpya inayoitwa “cloning” kwa lugha ya Kiingereza. Pengine kwa sasa tuite “kutumbisha.” Sayansi hii tayari imeleta mapinduzi makubkwa... (Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata
    Kuna sayansi mpya inayoitwa “cloning” kwa lugha ya Kiingereza. Pengine kwa sasa tuite
    “kutumbisha.” Sayansi hii tayari imeleta mapinduzi makubkwa katika uzalishaji mimea
    na uvunani. Imesemekana ya kwamba, ghairi ya wivu na kijicho baina ya jamii
    mbalimbali ulimwenguni, aina hii ya sayanzi ina uwezo na kuangamiza kabisa janga la
    njaa katika sayari hii yetu. Kivipi? Rahisi kabisa. Ni kwamba mbegu moja tu ya aina
    yoyote ya mmea, baada ya kuneemeshwa vyumba vyake vidogo ambavyo ndivyo hasa
    msingi wa uhai vinaweza kunyunyiziwa dawa maalum ili vitawanyike mara hata
    mamilioni na kuwa mimea kamili…. Mamilioni!

    Sayansi hii tarari inatumiwa kukuza viazi na vyakula vingine. Hii ina maana ya kwamba
    mashamba makubwa si muhimu siku hizi, yaani vyakula vingi kabisa vinaweza kukuzwa
    mahali padogo sana. Kwa hivyo hivi karibuni tu, kutakuwa hakuna haja ya kupigania
    mashamba.

    Vyema. Hebu sasa tuangalie zilizokwishapigishwa hii sayansi ya “kutumbisha” na mahali
    binadamu alipofika kimaendeleo kwa sababu ya hatua hizo. Jambo la kwanza sayansi hii
    tayari imeshatumiwa kuzalishia wanyama wengi, wengi sana wadogo wadogo kwa lengo
    la kuendeleza mbele utafiti. Kufikia sasa, wanyama hawa waliotengenezwa na binadamu
    katika maabara yake bado wanahifadhiwa mumo humo walimotengenezwa. Hii ni hatua
    kubwa na binadamu anastakili pongezi kwa jinsi anayotumia akili yake kuvumbua ibura
    hizi zote.

    Hata hivyo imesemwa kwamba kuchamba kwingi ni kuondoa mavi. Binadamu kama
    ijulikanavyo, anajaribu sana jujitakasa kwa kujitenga mbali sana na asili yake ya unyama
    ili aufikie ubinadamu mkamilifu. Hapana ubaya hapo. Lakini tukirudi nyuma tunakuta ya
    kwamba binadamu sasa aneingia tama kubwa sana kuliko wakati wowote ule. Tamaa hii
    imeletwa na ujuzi wake katika sayansi hii ya “kutumbisha.” Sasa binadamu ana jua
    vizuri sana kwamba kwa vile ana ujuzi wa kutengeza panya na hata kondoo katika
    maabara basi hata ujuzi wa kutengeneza binadamu pia anao! Na hapo ndipo tatizo lilipo.
    Swali hi hili: Je, ujuzi huu utatufikisha wapi? Na kikomo chake kitakuwaje?

    Binadamu sasa ujuzi wake unamtia wasiwasi. Wataalam wa sayansi hii wamejiuliza mara
    nyingi nini kitakachotokea ujuzi huu utakapomilikiwa na mwenda wazimu mweledi.”
    Watu kadha wa kadha, miongoni mwao wakiwa wanasiasa wamejiuliza mara
    zisizohesabika swali hili: kama Hitler angekuwa na ujuzi huu, angekuwa na lazima gani
    ya kuwaulia mbali wayahudi milioni sita wasiokuwa na hitia isipokuwa na nywele
    nyeusi na hawakuwa weupe sana kama wazungu? Hitler aliamini ya kwamba “mtu
    mzuri” ni mwenye pua ya upanga (kama mzungu), macho ya buluu nywele rangi ya dhahabu na mwenye kimo cha futi sita au zaidi kidogo. Hivyo lengo lake lilikuwa ni
    kubuni taifa la watu wazuri pekee ambao mwisho watautawala ulimwengu na kuenea
    duniani kote. Katika mpango wake, watu weusi wote wangefaa kuangamizwa tu ili watoe
    nafasi kwa watu aliowaona yeye kuwa bora.

    Sasa baada ya sayansi hili ya “kutumbisha” kuvumbuliwa, wataalam wametishika sana.
    Wamewaza jinsi ambavyo Hitler angeweza kufanya kama angekuwa mjuzi wa taaluma
    hiyo.

    Kitisho hiki kimezidi kuwatwanga wataalam na wasiokuwa wataalam hivi majuzi tu
    ilipogunduliwa maiti ya msichana wa miaka kumi na mine huko milima ya Andes,
    Amerika ya kusini. Msichana huyo alikuwa ametolewa kafara miaka karne tano zilizo
    pita lakini hakuoza kwa sababu ya baridi kali ya barafu milimani.

    Kwa sababu ya dukuduku la uvumbuzi ambalo haliishi dhana za kiajabu ubongo wa
    binadamu, wataalamu wa “kuchezea” maumbile walipomwona msichana huyo maiti,
    upesi upesi wakampima. Walipofanya hivyo wakagundua ya kwamba mayai yake ni
    timamu kabisa wala hayajaharibiwa na mpito wa karne. Papo hapo wengine wakajiwa na
    wazo la kuyatoa mayai hayo na kuyahifadhi kwenye mabara. Tamaa ikazidi zaidi ya
    zaidi. Baadhi ya wataalamu wakajiwa na wazo la “kuyaneemesha” mayai hayo na mbegu
    za uzazui za wanaume. Kwa lengo gani? Kuunda watoto amabo mama yao alikufa
    zamani za kale ili waonekane watakuwa watu wa aina gani!

    Sasa fikiria mwenyewe! Watoto hawa wa maabara wakiwa weledi zaidi ya binadamu
    yeyote yeyote wa kisasa lakini watiifu kama mbwa na paka itakuwaje? Hakuna
    atakayefikiria “kutumbisha” ili tuwe na vijitumwa vyetu vipenzi majumbani mwetu
    vinavyofanana nasi badala ya paka na mbwa wasiovishwa nguo?

    (a) Andika kichwa kifaacho kwa nakala hii
    (b) Kutumia sayansi ya “kutumbisha” kunaweza kumsaidia binadamu kuangamiza
    mabaa gani mawili yanayomkabili sasa?
    (c) Unadhani ni kwa nini wanyama waliozalishwa kwa kutumia sayansi hii bado
    wamo maabarani?
    (d) Fafanua methali “kuchamba kwingi nikuondoka na mavi” kulingana na muktadha
    wa habari hii
    (e) Kuna ubaya gani kutumbisha watu?
    (f) Mwandishi anaonekana kutishwa sana na uwezekano wa sayansi ya kutumbisha
    kuishia mikononi mwa “wendawazimu weledi” kwani kuna hatari gani?
    (g) Eleza kwa ukamilifu matatizo yanayoweza kuukumba ulimwengu iwapo mayai ya
    msichana wa Andes yatatumbishwa

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Bila kunyambua, andika maneno mawili ambayo yanatokana na shina moja na neno: imani (Solved)

    Bila kunyambua, andika maneno mawili ambayo yanatokana na shina
    moja na neno: imani

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Tunga sentensi ya neno moja ambayo ina visehemu vifuatavyo vya sarufi - Kiima - Wakati - Kirejeleo - Kiswahili kitendwa - Kitenzi (Solved)

    Tunga sentensi ya neno moja ambayo ina visehemu vifuatavyo vya
    sarufi
    - Kiima
    - Wakati
    - Kirejeleo
    - Kiswahili kitendwa
    - Kitenzi

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Mahali palipohamwa panaitwa? (Solved)

    Mahali palipohamwa panaitwa?

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza maana mbili mbili zinazotokana na sentensi zifuatazo (i) Mtoto alitimua mbio, kuona nyoka (ii) Juma alifagia chakula (iii) Sisikii vizuri (Solved)

    Eleza maana mbili mbili zinazotokana na sentensi zifuatazo
    (i) Mtoto alitimua mbio, kuona nyoka
    (ii) Juma alifagia chakula
    (iii) Sisikii vizuri

    Date posted: June 27, 2019 .    Answers (1)