Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

A : Ohh, dada NaomiB : Dada Ruth (anamsogea kwa bashasha wanakumbatiana). Ahh Mungu asifiwe!A: Asifiwe sanaB: Ehh dadangu, miezi ...mingi...sijakuonaA: dada wee...Nilitumwa huko kusini...

      

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali :

A : Ohh, dada Naomi
B : Dada Ruth (anamsogea kwa bashasha wanakumbatiana). Ahh Mungu asifiwe!
A: Asifiwe sana
B: Ehh dadangu, miezi ...mingi...sijakuona
A: dada wee...Nilitumwa huko kusini ...Kuwahubiria watu injili (mtuo mdogo)singeweza kukata...
B: Ehh, usiwe kama Yona
A: Habari ya siku nyingi?
B; Nzuri Mungu bado ameendelea kunibariki
A: Amen!
B: Nimeendelea kuiona neema yake
A: Amen! Asifiwe Bwana
B: Halleluya
A: Ni Mungu wa miujiza!
B : Amen. Hata nami nimeona neema yake
Bado niko imara katika wokovu katika siku hizi za mwisho
A : Amen !
B : Ni Mungu wa ajabu kweli !
A : Nilikumbana na matatizo lakini nikategemea sala
Kama Paulo na sila… Na nikashinda (anatua). Sikuweza kumpa shetani nafasi…maana
ameshindwa
B : Ameshindwa kabisa


(i) Hii ni sajili ya wapi ? Fafanua
(ii) Taja na ueleze sifa za sajili hii
(iii) Taja na ueleze mambo mawili muhimu yaliyosaidia katika maenezi ya Kiswahili
Afrika mashariki na kati

  

Answers


Maurice
(i) Sehemu za kuabudu/ ibada / mzungumzo ya Kristo

(ii) (a) Matumizi ya lugha iliyojaa upole/ unyenyekevu

(b) Msamiati maalum unaohusiana na dini Fulani. Kwa mfano ‚Yesu“ okoka, ‚
Mungu asifiwe’ ‚ Halleluya, ‚ Amen’ dini ya kikikristo

(c) Huweza kuwapo matumizi ya maneno au makuu kutoka kwa Bibilia mfano. usiwe kama
Yona, Paulo na Sila.

(d) Huwepo matumizi ya msamiati ambao unaeleweka tu katika muktadha huo wa
mazingira yanayohusika tu. Mungu anaendelea kunibariki. ‚Amen“

(e) Lugha haina matumizi ya misimu au hata lugha inayoonekana kama isiyozingatia
adabu; huwa lugha yenye tasfida.

(f) Majina yanayofungamana na ibada inayohusika, injili, sala, Mungu, Bwana asifiwe

(g) Matamshi au lafudhi ya utamkaji wa maneno kutegemea mazingira fulani ya ki-ibada


(iii)-Dini
-Biashara
maurice.mutuku answered the question on October 8, 2019 at 10:48


Next: Niaje wasee! Ma-holiday ndizo hizo tena. Najua ma-mission ni mingi! Lakini jo, mambo imebadilika ! Ni kubaya maze. Usifikirie kila kitu unaona ni reality, ukadhani ni...
Previous: Bw. Mosuka : Mheshimiwa spika, naichukua fursa hii kuipinga hoja iliyowasilishwa na mbunge wa Mahira, mheshimiwa Kochaberi kuhusu suala la kuavya.... (a) Hii ni sajili gani? (b) Eleza...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions