Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Tathmini mchango wa kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki(K.K.A.M) katika kusanifisha lugha ya Kiswahil

Tathmini mchango wa kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki(K.K.A.M) katika kusanifisha lugha ya Kiswahil

Answers


Faith
• Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki ilisaidia kwa kusanifisha maandishi na kuhakikisha mtindo mmoja unazingatiwa katika kuendeleza maneno za kiswahili.
• Kamati ilichapisha vitabu vilivyohitajika na pia vya ziada ambayo iliwasaidia pia katika kazi ya usanifishaji.
• Kamati iliwasaidia na kuwahimiza waandishi wa vitabu vya kiswahili ambao pia walikuja kusaidia katika kazi ya usanifishaji wa kiswahili.
• Kamati ilikuwa ikiwapasha waandishi habari zozote zile kuhusu njia tofauti au mitindo ya kusomesha katika kila nchi .Hii iliwasaidia kwa kuwa usanifishaji ilihusisha nchi zote ili kuepuka kutoeleweka.
• Kamati ilisaidia kwa kuchapisha kamusi mbili.moja ya kiswahili kwa kiswahili na nyingine kiswahili kwa kingereza.Hii ilisaidia wanafunzi na walimu jinsi ya kuendeleza maneno mbalimbali.
• Kamati ilikuwa ikiyajibu maswali yote ya umma na kuchapisha katika jarida la ILC Bulletin.
• Kamati ilisaidia katika usimamizi wa utafiti wa lahaja za kiswahili na mayokeo ya utafiti kuchapishwa kwa studies in Swahili dialects.
• Kamati pia ilikuwa ikiandaa mashindano ya kuandika insha na vitabu ili kuwatia ari waandishi wa kiswahili na Hii ilisaidia sana katika shughuli za usanifishaji wa kiswahili.

Titany answered the question on December 6, 2021 at 09:53

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions