Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

“Usiteketeze umati kama kuni zinavyoteketeza moto. Rudi, rudi kwa Mola wako.” (a) Fafanua muktadha wa maneno haya. (b) Eleza hulka tatu za msemewa. (c) Taja maovu anayoyafanya msemewa.

      

“Usiteketeze umati kama kuni zinavyoteketeza moto. Rudi, rudi kwa Mola wako.”
(a) Fafanua muktadha wa maneno haya.
(b) Eleza hulka tatu za msemewa.
(c) Taja maovu anayoyafanya msemewa.

  

Answers


Francis
(a) Fafanua muktadha wa maneno haya.
? Msemaji wa maneno haya ni Mkumbukwa.
? Anamweleza Mkubwa.
? Walikuwa kwake Mkubwa.
? Baada ya Mkumbukwa kuiasi biashara ya mihadarati na kumwosia Mkubwa.

(b) Eleza hulka tatu za msemewa. Msemewa ni Mkubwa. Ana sifa hizi.
? Mwenye bidii - alikuwa akijishughulisha na kazi ya kuuza pweza wa kukaanga na baadaye akauza kipande cha ardhi ili kuingia uongozini.
? Mwenye utani - anamtania utingo kuwa huwa haogi jambo lililomfanya utingo kukimbia kwa kuchekwa na abiria.
? Mwenye tamaa ya mali - alipotanabahi namna viongozi wanavyotajirika kwa kuuza unga, maneno 'unga na utajiri' yalimkaa moyoni kiasi cha yeyé kukosa usingizi usiku huo.
? Ni fisadi - baada ya kutia na kutoa, aliamua kufanya biashara haramu ya kuuza dawa za kulevya. Vile vile alitoa kiasi kikubwa cha pesa ili kuwashawishi wapiga kura kumpendelea na ndipo akaupata ushindi.
? Ni msiri - mwanzoni hakumweleza Mkumbukwa sababu yake kuutafuta uongozi.

(c) Taja maovu anayoyafanya msemewa.
? Kuuza dawa za kulevya ambayo ni biashara haramu.
? Kutoa hongo ili apate uongozi.
? Kumtapeli rafiki yake Mkumbukwa na kumuingiza katika uuzaji wa dawa za kulevya.
? Kutumia pasipoti ya kidiplomasia vibaya.
? Kuwaharibu vijana kwa kuwauzia dawa za kulevya
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 11:29


Next: “Akanyangapo chini ardhi inatetemeka...Amejitia hamnazo. Kabwela kama mimi nina faida gani? (Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine) (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Fafanua mbinu tatu za...
Previous: Kwa kurejelea hadithi za Mapenzi ya Kifaurongo na Shogake Dada ana Ndevu fafanua changamoto zinazowakumba vijana. (a) Mapenzi ya Kifaurongo (b) Shogake Dada ana Ndevu

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions