Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Questions and answers: Kiswahili Fasihi

Q&A Categories


Do you have Q&A pairs? Post them here

265 Questions  View: All | Solved | Unsolved



Search Results...
  • Hadhira e pulikeni, kisa changu mpaeni,(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. 1) Hadhira e pulikeni, kisa changu mpaeni, Mpateni mweleweni, mchekeni, mlieni, Funzo lake mpateni, uamuzi mfanyeni, Kisa hiki asilani, sisahau maishani. 2) Cha nne niliingiya, mtoto kafurahiya, Malkia ungedhaniya, duniani meingiya, Mapambo lijipambiya, kung‘ara kikang‘ariya, Kisa change chatokeya, mwanzowe nafunguliya. 3) Darasani lizembea, bidii sikutilia, Starehe nakwambia, nilipenda najutia, Kimadaha litembea, tausi nilitulia, Kisa kilinigonjea, mtume! Ningalijua. 4) Muhula kutamatika, dafu sikufua, kaka, Enda, Ewe, Embe, fika, alama duni, viraka, Nilipokea waraka, mzazi kahitajika, Kisa kijatambulika, nakuomba makinika. 5) Muhula wa pili sasa, nikarudia makosa, Sikupigeni msasa, makali nikayakosa, Kisu sikunoa hasa, sikukata cha darasa, Kisa ndicho hicho sasa, ninakupa pasi pesa. 6) Sasa muhula wa tatu, umetimia wanetu, Mtihani kama chatu, nimeuogopa, mtu, Sijausomea katu, ningalilindaje utu? Kisa mkasa wa chatu, kilinipata wa kwetu. 7) Mbwa katu hafi maji, kiona ufuko, maji, Tajaribu sife maji, hata akiyanywa maji, Ilibidi twende jiji, kuwasaka wajuaji, Kisa change mfumbaji, sasa dawa lihitaji. 8) Mpango ulitolewa, mchango ulipangiwa, Pesa tele litolewa, na simu kununuliwa, Mtandao liwekewa, ‗kunani‘ kupakuliwa, Kisa cha simu kujuwa, linifanya kupagawa. 9) Tulikata dari ona, simu yetu kufichana, Usiku tulikutana, maswali kurushiana, Majibu tulipeana, "panga‘ kabadilishana, Kisa kinajulikana, vile nilivyokazana. 10) Niliyangoja majibu, nikiwa na hamu, babu, Nilikimya kama bubu, nisije toa aibu, Nilivichoma vitabu, bila kuwa na sababu. Kisa kawa masaibu, kashindwa kuyaharibu. 11) Kutangazwa matokeo, nakumbuka hadi leo, Lilishangaza toleo, sikuamini redio, Lipokea matokea, yalinitia kimbio, Kisa change mchocheo, haya yangu mapokeo. 12) Nilifeli mtihani, sababu simu juweni, Najuta nisameheni, nijilaumu moyoni, Ningalijua mbeleni, ningalisoma jamani, Kisa nimemalizeli, wenzangu mzindukeni. 13) Watahiniwa mlipo, msiwe mithili popo, Skuli kwenu kuwepo, nia mpate malipo, Bidii hapo mlipo, toa uzembe pasipo, Kisa change kingalipo, simu daima siwepo! MASWALI a) Taja anwani mwafaka ya shairi hili. b) Fafanua mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi hili. c) Bainisha nafsi lengwa katika shairi hili. d) Changanua arudhi zilizotumiwa na mtunzi wa shairi hili. e) Andika ubeti wa kumi katika lugha nathari. f) Eleza maana ya maneno na vifungu vifuatavyo kwa mujibu wa shairi. g) Eleza maana ya maneno na vifungu vifuatavyo kwa mujibu wa shairi. (i) Sikukata cha darasa (ii) Yalinitia kimbio (iii) Kupagawa

    Date posted: October 2, 2019.  

  • "Leo ni siku, siku ya nyani kufa ambapo miti yote huteleza"(Solved)

    Damu nyeusi na hadithi zingine "Leo ni siku, siku ya nyani kufa ambapo miti yote huteleza" a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Bainisha tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili. c) Huku ukitoa mifano, thibitisha maudhui sita ambayo yamejitokeza katika hadithi ya Damu Nyeusi na wanayoyaendeleza.

    Date posted: October 2, 2019.  

  • Kwa kutoa mifano kumi,eleza vizingiti walivyokumbana navyo wanacheneo wakati wa kupigania mageuzi.(Solved)

    Mstahiki Meya Kwa kutoa mifano kumi,eleza vizingiti walivyokumbana navyo wanacheneo wakati wa kupigania mageuzi.

    Date posted: October 2, 2019.  

  • "Iwapo umefanya, yapo mengi ambayo hayakunyoka."(Solved)

    Mstahiki Meya "Iwapo umefanya, yapo mengi ambayo hayakunyoka." a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Tambua mbinu moja iliyotumika katika muktadha wa dondoo. c) Fafanua kauli kwamba"yapo mengi ambayo hayakunyoka". d) Eleza jinsi baadhi ya wahusika walivyojaribu kuyanyoosha.

    Date posted: October 2, 2019.  

  • "Umenena ndipo ndugu yangu. Hiyo ndiyo tanzia ya Afrika huru."(Solved)

    Kidagaa kimemwozea "Umenena ndipo ndugu yangu. Hiyo ndiyo tanzia ya Afrika huru." a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Ni nini sifa za mvuto zinazowaleta pamoja mzungumzaji na mzungumziwa. c) Tambua na ufafanue mbinu inayotumika katika dondoo. d) Kwa mifano mwafaka fafanua tanzia hiyo inayorejelewa katika dondoo.

    Date posted: October 2, 2019.  

  • "Ikamchagiza kama vile kiu ya mtu aliyekuwa akisafiri jangwani".(Solved)

    DAMU NYEUSI "Ikamchagiza kama vile kiu ya mtu aliyekuwa akisafiri jangwani". (a) Eleza muktadha wa dondoo hili (b) Fafanua sifa zozote nne za mrejelewa (c) Eleza fani uliotumiwa na mwandishi katika dondoo hili (d) Kwa kurejea hadithi zozote tatu,eleza namna wahusika wowote watatu walivyoathiriwa na kiu.

    Date posted: October 2, 2019.  

  • Nonsense! Hivi huyu ana nia gani?(Solved)

    Mstahiki Meya Nonsense! Hivi huyu ana nia gani? (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Taja na ueleze mbinu za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili. (c) Jadili umuhimu wa msemaji katika tamthilia hii. (d) Jadili njia za kuondoa uozo katika jamii ukijikita katika tamthilia ya Mstahiki Meya.

    Date posted: October 2, 2019.  

  • Jadili mbinu zifuatazo kama zilivyotumika katika Mstahiki Meya.(Solved)

    Jadili mbinu zifuatazo kama zilivyotumika katika Mstahiki Meya. (a) Jazanda (b) Uzungumzi nafsia (c) Majazi (d) Methali (e) Taharuki

    Date posted: October 2, 2019.  

  • Eleza dhima ya lakabu kwa kurejelea hoja tano.(Solved)

    Eleza dhima ya lakabu kwa kurejelea hoja tano.

    Date posted: October 2, 2019.  

  • Eleza maudhui ya ukengeushi ukirejea hadithi zifuatazo katika diwani ya Damu nyeusi na hadithi nyingine (Solved)

    Eleza maudhui ya ukengeushi ukirejea hadithi zifuatazo katika diwani ya Damu nyeusi na hadithi nyingine (i) Mke wangu (ii) Damu Nyeusi (iii) Tazamana na Mauti (iv) Mizizi na matawi

    Date posted: October 2, 2019.  

  • "Ulimwengu wake ulivurugika akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo"(Solved)

    Kanda la usufi "Ulimwengu wake ulivurugika akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo" (a) Eleza sifa zozote nne za mrejelewa (b) Kwa nini mrejelewa amelinganisha na tiara iliyopeperushwa na upepo

    Date posted: October 2, 2019.  

  • "Alipofikishwa kwenye zahanati hakushughulikiwa ipasavyo.Ubwete ni ugonjwa mmoja mbaya walioambukizwa madaktari na wauguzi wengi Tomoko"(Solved)

    "Alipofikishwa kwenye zahanati hakushughulikiwa ipasavyo.Ubwete ni ugonjwa mmoja mbaya walioambukizwa madaktari na wauguzi wengi Tomoko" a) Eleza Muktadha wa dondoo hili. b) Dhihirisha jinsi mtunzi alivyoitumia tamathali yoyote moja inayobainika kifunguni . c) Riwaya Ya Kidagaa Kimemwozea ni muhtasari wa maradhi yanayolihujumu Bara Afrika.Tetea rai hii kwa mifano faafu riwayani.

    Date posted: October 2, 2019.  

  • "Wanyonge ndio wanyongwao" ni kauli inayodhihirika vyema kupitia wahusika tofauti katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.(Solved)

    "Wanyonge ndio wanyongwao" ni kauli inayodhihirika vyema kupitia wahusika tofauti katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. Jadili.

    Date posted: October 2, 2019.  

  • Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama,(Solved)

    Soma mashairi yafuatayo kisha ujibu maswali. SIKUJUA! 1. Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama, Zisingenidhuru pembe, ngeu kuniandama, Samli ni lembelembe, na minofu ya minyama. 2. Kama ningefuga mbuzi, na kondoo kundi zima, Ningewajengea zizi, na maziwa nikakama, Ningewachuna na ngozi, kutengenezea ngoma. 3. Kama ningefuga bata, nao kuku kwa ujima, Chakula siyo matata, ni machicha na mtama, Mayai ningeyapata, na kitoweo kizima. 4. Kumbe nimefuga punda, mashuzi ndio heshima, Ni ukaidi na inda, mateke kurusha nyuma, Nyama limekuwa nunda, mfugaji humuuma. Kiitikio Sikujua wa kufuga, mnyama mwenye faida SHAIRI B Afrika na Watu Wake Mimi ninaona mgonjwa Bado amelala kitandani. Kama hatutamtoa miiba iliyobaki Mgonjwa hataweka miguu yake chini Ili kutembea bila ya kujiegemeza. Miiba iliyomo ndani mwetu lazima Pia iondolewe upesi kabla haijaingia Kati ya mfupa na kufa pamoja nasi. Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma Halafu tucheze nao mchezo wa siasa na uchumi. Lakini kuitoa miiba hii Tunahitaji macho makali Mikono isiyotetemeka Moyo usio na huruma Na kuona miiba ilipoingilia. MASWALI (a) Onyesha jinsi ujumbe unaopatikana katika ubeti wa nne wa Shairi A na Shairi la B unavyokatisha tamaa. (b) Eleza maana ya mshororo huu kama unavyojitokeza kwenye ubeti wa pili wa shairi B. Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma. (c) Linganua sifa za kimuundo ukizingatia ubeti wa pili wa Shairi A na Shairi B. (d) Ukizingatia Mshororo wa kwanza kwenye ubeti wa pili wa Shairi A, onyesha jinsi Mshairi alivyotumia kibali chake. (e) Onyesha sifa moja ambayo inadhihirika kwenye shairi la B na ambayo hutawala tungo za aina hii. (f) Nafsi neni amedhihirisha toni gani kwenye shairi A? (g) Taja nafsi mbili nenwa kwenye shairi la B. (h) Andika ubeti wa mwisho wa shairi B kwa lugha ya nadhari.

    Date posted: October 2, 2019.  

  • Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?(Solved)

    SABUNI YA ROHO Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia? Ndiwe suluhu za zama, waja wakukimbilia, Waja wanakutazama, madeni wakalipia, Ndiwa sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima. Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani, Utanunua majoho, majumba na nyumbani, Umezitakasa roho, umekuwa mhisani, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvinja mlima. Matajiri wanakujua, wema wako wameonja, Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja, Sura zao ‗mefufua, wanazuru kila njanja, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima. Ndiwe mvunja mlima, onana na maskini, Watazame mayatima, kwao kumekua duni, Webebe waliokuwa, wainue walio chini, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima. Ndiwe mvunja mlima, wapi kapata uwezo, Umezua uhasama, waja kupata mizozo, Ndiwe chanzo cha zahama, umewatia vikwazo, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima. Umevunja usuhuba, familia zazozana, Waliokuwa mahabuba, kila mara wagombana, Roho zao umekaba, majumbani wachinjana, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima. Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu, Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu, Niondoe jahanamu, ya ufukara wa simu, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima. Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika, Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika, Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika, Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Date posted: October 1, 2019.  

  • Nitafukuzwa mbinguni Kwa ushairi wangu mbaya Lakini hata motoni nitaimba:(Solved)

    Nitafukuzwa mbinguni Kwa ushairi wangu mbaya Lakini hata motoni nitaimba: Wanasema Wanasiasa ni kama jizi Lililosukuma mtoto pembeni Na kunyonya ziwa la mama Wakati amelala usingizi usiku. Wanasema Mwanasiasa afapo Tumejikomboa na domo Moja pana lizibwalo na mchanga Na kilima cha simenti ngumu Lisikike tena hadharani. Wanasema pia Kusema haki Kwa kawaida Wanasiasa hatuwapendi. Kupiga kura ni hasira za mkizi Ni basi tu. Ni Ah! Ah! Wanamalizia Nchi mmefiilisi waacheni walimu Wakajenga taifa jipya. Top grade predictor publishers Page | 63 Kama hamwezi kuona mbali Bure kuweka mkono usoni, Bure hakuna kichwa Kama hamwezi kufikiri. Ng‘ombe amekamuliwa na wazungu Waarabu, wahindi na wao Sasa anatoa damu Vilivyobaki ni chai ya rangi Na madomo mapana zaidi Yaliyo bado hai. Kuimba nimeimba Maswali (a) Mshairi ana dhamira gani? (b) Shairi hili ni la kukatisha tama, tetea rai hii. (c) Onyesha matumizi mawili ya mishata. (d) Eleza mbinu zozote nne za lugha zilizotumika katika shairi hili. (e) Andika ubeti wa mwisho katika lugha tutumbi. (f) Fafanua umbo la shairi hili. (g) Eleza maana ya mafungu ya maneno ya maneno yafuatayo: (i) kupiga kura ni hasira ya mkizi (ii) kuweka mkono usoni (iii) ng‘ombe amekamuliwa.

    Date posted: October 1, 2019.  

  • Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii.(Solved)

    Mstahiki Meya Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii.

    Date posted: October 1, 2019.  

  • Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja.(Solved)

    MSTAHIKI MEYA: Timothy Arege Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja. Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja. (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Fafanua nafasi ya wanaorejelewa kuwa ―"walifanya vizuri kuja" katika tamthilia hii. (c) Migogoro katika tamthilia hii hazikusuluhishwa vyema. Jadili.

    Date posted: October 1, 2019.  

  • Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.(Solved)

    Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.

    Date posted: October 1, 2019.  

  • "Nyamaza boza wewe. Wadhani sisi kazi tunaanza leo? Tumekutana na wauaji wangapi?(Solved)

    Kidagaa Kimemwozea: "Nyamaza boza wewe. Wadhani sisi kazi tunaanza leo? Tumekutana na wauaji wangapi? a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Dondoo hili linadokeza maudhui gani? Kwa kutoa mifano saba kwenye riwaya, bainisha jinsi maudhui hayo yanavyojitokeza.

    Date posted: October 1, 2019.  

  • "Hakujua maisha yake yangechukua mkondo upi. Mzo wa majuto ulimwandama. Ulimwengu wake ulivurugika, akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo"(Solved)

    Kanda la Usufi "Hakujua maisha yake yangechukua mkondo upi. Mzo wa majuto ulimwandama. Ulimwengu wake ulivurugika, akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo" (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Taja na kueleza tamathali ya usemi kwenye dondoo hili. (c) Kwa kutolea mifano, onyesha jinsi anwani Kanda la Usufi inavyoafiki hadithi husika.

    Date posted: October 1, 2019.  

  • "………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee"(Solved)

    Damu Nveusi na Hadithi nyingine "………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee" (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Thibitisha ufaafu wa anwani ya hadithi hii.

    Date posted: October 1, 2019.  

  • Elimu imeshindwa kutimiza lengo la kuwapa vijana uwezo wa kukabiliana na maisha ya kisasa. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea hadithi zifuatazo.(Solved)

    Elimu imeshindwa kutimiza lengo la kuwapa vijana uwezo wa kukabiliana na maisha ya kisasa. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea hadithi zifuatazo. (a) Mke wangu (b) Samaki wanchi zajoto (c) Damu nyeusi.

    Date posted: October 1, 2019.  

  • "Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……."(Solved)

    Kidagaa kimemwozea "Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……." (a) Weka dondoo hili katika muktadha wake . (b) Eleza tamathali mbili zilizotumika katika dondoo hili. (c) Eleza aina za kiu na njaa zilizomkumba mrejelewa wa kwanza. (d) Mrejelewa wa pili alishindwa mtihani wa maisha. Jadili.

    Date posted: October 1, 2019.  

  • Kuvunjwa kwa haki na sheria lilikuwa jambo la kawaida chini ya uongozi wa Mtemi Nasaba bora. Thibitisha ukweli wa Kauli hii ukirejelea riwaya ya Kidagaa...(Solved)

    Kuvunjwa kwa haki na sheria lilikuwa jambo la kawaida chini ya uongozi wa Mtemi Nasaba bora. Thibitisha ukweli wa Kauli hii ukirejelea riwaya ya Kidagaa kimemwozea.

    Date posted: October 1, 2019.  

  • "Duniani kuna watu na viatu"(Solved)

    Tamthilia nzima ya Mstahiki Meya. "Duniani kuna watu na viatu" (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (b) Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.

    Date posted: October 1, 2019.  

  • Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao.(Solved)

    Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao. (i) Diwani wa tatu (ii) Bili (iii) Mhubiri (iv) Diwani I na II

    Date posted: October 1, 2019.  

  • Kila nikaapo hushika tama.(Solved)

    Kila nikaapo hushika tama Na kuwazia hali inayonizunguka. Huyawazia madhila Huziwazia shida Huiwazia dhiki Dhiki ya ulezi Shida ya kudhalilishwa kazini. Madhila ya kufanyiwa dharau Kwa sababu ya jinsia ya kike. Hukaa na kujidadisi Hujidadisi kujua kwa nini Jamii haikisikii kilio changu Wenzangu hawanishiki mikono Bali wananidharau kwa kuukosoa utamaduni Hukaa na kujiuliza I wapi raha yangu uiimwengu huu? I wapi jamaa nzima ya wanawake? MASWALI (a) Shairi hili ni la aina. gani? Eleza (b) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili. (c) Kwa kutolea mifano eleza maana ya mistari mishata. (d) Taja na ueleze tamathali mbili zilizotumika katika shairi hili. (e) Tambulisha nafsi-neni katika shairi hili. (f) Fafanua toni ya shairi hili. (g) Fafanua maudhui mawili ya shairi hili. (h) Onyesha namna nafasi neni anavyosalitiwa. (i) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi. (i) Madhila (ii) Kudhalilishwa.

    Date posted: October 1, 2019.  

  • Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako,(Solved)

    Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali. 1. Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako, Ondoka andama ndiya, nondosheya uso wako, Ondoka wanisikiya, ziwate jeuri zako, Jishughulishe na yako, yangu wayatakiyani? 2. Wasiwasi siitaki, suhuba yako si nzuri, Haistahamilikii, uovu umekithiri, Inganyoshwa hainyoki, ikukutene kikiri, Sikati yako shari, enda zako wasiwasi. 3. Huna kazi ufanyayo, ela kuwafitinisha, Viumbe na zao nyoyo, vitina kuwagotanisha, Hiino ndio kaziyo, yenye kukufurahisha, Ni kazi isiyokuchosha, mno umeizoeya. 4. Mara waja na habari, mambo yalivyo nyumbani, Ati mambo si mazuri, mambo yote tatashani, Wanitaka nifikiri, usemayo ni yakini, Nisononeke moyoni, upate kufurahika. 5. Au mara hunijiya, na kingine kisahani, Kuhusu zao afiya, hao waliyo nyumbani, Huwa husishi nambiya, hali zao taabani, Zingawa wakati gani? Ni zako au ni zao? 6. Na mara kuja mambiya, nitakapotoka humu, Na kwamba yaningojea, nde maisha magumu, Uliloni kusudiya, ni kunitiya wazimu, Kama ndiyo yako hamu, basi unshatahayari. (a) Eleza ujumbe uliojitokeza katika shairi hili. (b) Fafanua muundo wa ubeti wa tatu. (c) Eleza aina ya shairi hili. (d) Fafanua arudhi za utunzi alizozingatia mshairi. (e) Eleza toni ya mshairi. (f) Andika ubeti wa tano katika lugha ya kinathari. (g) Eleza mifano mitatu ya uhuru wa mshairi. (h) Eleza maana ya misamiati ifuatayokama ilivyotumika katika shairi. (i) ndiya (ii) kisahani (iii) nde

    Date posted: October 1, 2019.  

  • Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge, (Solved)

    Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali. 1. Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge, Asinywe yalo na vunju, Yakampa kigegezi, Yakamkibua roho akaona na kinyaa, Awali ndio awali, awali mbovu hamna. 2. Kiwa utalimatia. Utayaramba makombo, Utadata vitu cheche, Kisomo chenye dhamana kikakupa kisogo, Inajuzu ujihimu Mwanafuu darasani, Urauka po mapema, Katu hutayaramba makombo, Hutakosa kisebeho. 3. Dereva hata utingo, Natija ni asubuhi, Wateja utawawahi, Wasaa kuzingatia, Uwafikishe kazini, Kwa wasaa ufaao, Wasije wakateteshwa, Na bosi wao kazini, Nao wakakuapiza. 4. Na ewe mwanazaraa, Mpini uukamate, Kabla jua kuwaka sana, Majasho kutiririsha mwilini, Yang‘oe yote magugu, Kutoka kwa lako konde. 5. Mhadimu mwenye ajizi, Yakujuza ujihimu, Ununue na maziwa, Majogoo uyawahi mapema, Usije ukayadata, Chai mkandaa ukaandaa, Wateja wakuambae mithili ya ibilisi. Maswali (a) Eleza nasaha yoyote inayotolewa kwa wafanyakazi wowote watatu kwenye shairi. (b) Taja sifa zozote za kimuundo zilizotumiwa na mtunzi. (c) Eleza toni ya mshairi. (d) Nafsi nenewa anahimizwa kufanya nini. (e) Andika ubeti wa tatu kwa lugha tutumbi. (f) Toa mifano miwili ya uhuru wa mshairi. (g) Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumiwa kwenye shairi. (i) Maji maenge (ii) Natija (iii) Majogoo

    Date posted: October 1, 2019.