Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Questions and Answers - Kenyaplex.com

Q&A Categories


Do you have Q&A pairs? Post them here

61049 Questions  View: All | Solved | UnsolvedSearch Results...
 • Tunga sentensi moja moja kudhihirisha matumizi ya i. Posa ii. Poza(Solved)

  Tunga sentensi moja moja kudhihirisha matumizi ya i. Posa ii. Poza

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Kanusha sentensi katika hali ya kuamrisha wingi. Kimbia haraka – Amka -(Solved)

  Kanusha sentensi katika hali ya kuamrisha wingi. Kimbia haraka – Amka -

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Tunga sentensi yenye kivumishi cha jina.(Solved)

  Tunga sentensi yenye kivumishi cha jina.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Tambulisha na ufafanue viambishi vilivyotumika katika Anamfundisha.(Solved)

  Tambulisha na ufafanue viambishi vilivyotumika katika Anamfundisha.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Kanusha sentensi ifuatayo kwa umoja. Nywele zenu hukatika mnapoachana.(Solved)

  Kanusha sentensi ifuatayo kwa umoja. Nywele zenu hukatika mnapoachana.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Huku ukitoa mifano taja miundo ya silabi.(Solved)

  Huku ukitoa mifano taja miundo ya silabi.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Sauti /p/ ni kipasuo, sauti hizi ni gani? i. / f / ii. / l /(Solved)

  Sauti /p/ ni kipasuo, sauti hizi ni gani? i. / f / ii. / l /

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Soma taarifa ifuatayo kasha ujibu maswali Ilikuwa Jumamosi. Nilifika nyumbani kwangu saa moja jioni. Tangu nistaafu miaka miwili awali sikupenda kuchelewa Taarifa ya Habari.(Solved)

  Soma taarifa ifuatayo kasha ujibu maswali Ilikuwa Jumamosi. Nilifika nyumbani kwangu saa moja jioni. Tangu nistaafu miaka miwili awali sikupenda kuchelewa Taarifa ya Habari. Mwezi mmoja ukawa umepita tangu nipewe pesa za kiinua mgongo. Mwezi mmoja mzima nilikuwa katika shughuli za kulipa deni hapa na kulipa karo huku. Kuwekeza kwenye mradi ule na kununua hili. Sasa shilingi laki mbili tu zilikuwa zimesalia katika benki. Watu wengi walinishawishi nijaribu kilimo cha mahindi. Bei ilikuwa imeanza kuimarika. Katika taarifa ya habari jioni hiyo, Waziri wa kilimo alitangazaa bei mpya , shilingi 1,500 kwa kila gunia. Nami nilikuwa naanza kuumakinikia mradi huu. Baada ya taarifa, nilioga nikala na nikaenda kulala. Kwa sababu ya uchovu, usingizi ulinichukuwa mara moja. Usingizini niliota. Katika ndoto niliutekeleza mradi wangu. Msimu huo wa kulima nilitenga hekari kumi za shamba langu. Wataalamu walinishauri kuwa wakati mzuri wa kulima ni wa kiangazi. Mwezi wa Januari ulipoanza tu nilitafuta trekta na kulima. Malipo yalikuwa shilingi 1,200 kila ekari. Katikati ya mwezi wa Mechi, nilitafuta trekta la kutifua shamba tena kwa gharama ya shilingi 15,000 ekari zote kumi. Kufuatia ushauri wa manyakanga wa kilimo, nililipa shilingi elfu kumi na tatu kupiga shamba lote haro. Mwishoni mwa mwezi huo, nilienda mjini kutafuta pembejeo. Kwanza, nililipa shilingi 20,500 kwa magunia 15 ya mbolea. Kisha nilinunua magunia manne ya mbegu ya mahindi yenye uzani wa kilo 25 kwa shilingi 3,300 kila gunia. Mwezi wa Aprili ulipotimia tu, niliamua kupanda ili nipate mazao bora, nilipanda kwa tandazi. Gharama ilikuwa shilingi 1,000 kila ekari. Mvua ilinyesha vizuri na baada ya siku saba, mahindi yalianza kuota. Ilifurahisha kuhesabu mistari ya kijani iliyonyooka. Hali hii iliwezekana tu baada ya kuajiri vijana wa kuwafukuza korongo na vidiri ili wasifukue mbegu mchangani. Baada ya mwezi mmoja, hatua ya kupalilia ilifika. Nilitafuta vibarua wa kupalilia. Malipo yalikuwa shilingi 700 kila ekari. Kumbe kupalilia kulichochea mtifuko wa mahindi. Punde yakawa yananifikia magotini. Hii ikawa ishara kuwa yanahitaji kumwagiwa mbolea ya kunawirisha iitwayo ‘amonia’. Gharama yake ikawa shilingi 1,300 kila gunia. Hivyo , nikalipa shilingi 19,500 kwa magunia kumi na matano. Mahindi yalibadilika kimiujiza. Ghafla tu yalirefuka na kunenepa mashina. Yalibadilika rangi yakapiga weusi. Shamba liligeuka likawa kama msitu wa rangi ya kijani iliyokolea. Wapita njia waliajabia mimea na juhudi zangu. Shamba langu sasa likawa kielelezo. Maafisa wa kilimo wakawa kila siku wanawaleta wakulima wengine kujifunza siri ya ufanisi wangu. Hapo nikaanza kuhesabu mavuno nitakayopata na kukadiri faida. Nilipuuza kabisa ushauri wa wahenga kuwa ‘Usikate majani, mnyama hajauawa.’ Bila taarifa wala tahadhari mvua ilitoweka. Hayakupita majuma mawili mahindi yakaanza kubadilika. Juma moja baadaye mahindi yalinyauka. Badala ya mahindi, shamba likageuka la vitunguu vilivyochomwa na jua. Makisio yangu ya faida yaliyeyuka jinsi ufanyavyo moshi. Lakini ‘Muumba ndiye Muumbua.’Siku moja mawingu yalitanda na mvua ikanyesha , muda si muda mahindi yalianza kunawiri. Kumbe tukio lililowavunja moyo lilikuwa laja. Siku moja mvua kubwa ilinyesha. Asubuhi nilipotoka nje nilipigwa na butwa. Barafu ilitapakaa pote. Shamba lilikuwa limetapakaa barafu nafuu. Nilipotazama upande wa shamba niliona dalili za majani mapya ya mahindi yakianza kuchomoza. Maumbile ni kitu cha ajabu kweli. Muda si mrefu mahindi yalirudia hali yake tena, kasha yakakomaa. Harakati za kutafuta watu wa kuyakata na kuyakusanya zilianza. Gharama ya shughuli hii ikawa shilingi 5,000 kuvuna kusafirisha kutoka shamba na kukoboa kwa mashine magunia 200 yakachukua shilingi 20,500. Kufikia hapo nilikuwa nimetumia takribani shilingi 192,700. Gharama nyingine zilikuwa za usafiri, gharama ya dharura na usimamizi, usumbufu wangu binafsi, gharama ya magunia na kadhalika. Mahindi yalipokuwa tayari kwenye magunia nilifunga safari kwenda mjini kutafuta soko. Niliposhuka tu niliona gazeti. Habari motomoto siku hiyo ilikuwa ‘MAHINDI GUNIA 900/=’ Niligutuka usingizini. MASWALI a) Ni changamoto zipi zinazokumba kilimo. b) Msimulizi alikuwa na kiasi gani cha pesa katika benki baada ya mradi kukamilika? c) Eleza maana ya methali zifuatazo kwa mujibu wa makala. i. Usikate majani, mnyama hajauawa. ii. Muumba ndiye Muumba. d) Eleza mambo mawili yaliyosababisha msimulizi asipate faida alivyotarajia. e) Kwa nini msimulizi alisema maumbile ni kitu cha ajabu? f) Eleza maana ya: i. Kiinua mgongo ii. Manyakanga wa kilimo.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Bainisha nomino katika utungo huu. Watoto wameenda kucheza.(Solved)

  Bainisha nomino katika utungo huu. Watoto wameenda kucheza.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Taja nomino zozote mbili katika ngeli A-WA na uonyeshe miundo yake. (Solved)

  Taja nomino zozote mbili katika ngeli A-WA na uonyeshe miundo yake.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Andika udogo wa: Anacheza ngoma.(Solved)

  Andika udogo wa: Anacheza ngoma.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Tumia kiunganishi kifaacho kuunganisha sentensi hizi. Mwizi alishikwa. Mwizi alipigwa sana.(Solved)

  Tumia kiunganishi kifaacho kuunganisha sentensi hizi. Mwizi alishikwa. Mwizi alipigwa sana.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Bainisha aina za vielezi katika sentensi hii. Mtoto alikimbia mara sita uwanjani kisha akatembea kitausi.(Solved)

  Bainisha aina za vielezi katika sentensi hii. Mtoto alikimbia mara sita uwanjani kisha akatembea kitausi.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Tunga sentensi yenye kitenzi kishirikishi kipungufu. (Solved)

  Tunga sentensi yenye kitenzi kishirikishi kipungufu.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Pigia mstari vivumishi kwenye sentensi hizi na ueleze ni vya aina gani. (i) Mtoto mwenyewe ataleta kalamu. (ii) Kitabu cha Musa hakipo(Solved)

  Pigia mstari vivumishi kwenye sentensi hizi na ueleze ni vya aina gani. (i) Mtoto mwenyewe ataleta kalamu. (ii) Kitabu cha Musa hakipo

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Tunga sentensi katika wakati uliopita hali timilifu. (Solved)

  Tunga sentensi katika wakati uliopita hali timilifu.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Bainisha aina zifuatazo za mofimu. (i) Mtu – (ii) Samaki – (iii) Anasoma –(Solved)

  Bainisha aina zifuatazo za mofimu. (i) Mtu – (ii) Samaki – (iii) Anasoma –

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Andika sauti zenye sifa zifuatazo: (i) Nazali ya kaa laini (ii) Kikwamizo ghuna cha mdomo na meno (iii) Irabu ya nyuma wastani (iv) Kimadende(Solved)

  Andika sauti zenye sifa zifuatazo: (i) Nazali ya kaa laini (ii) Kikwamizo ghuna cha mdomo na meno (iii) Irabu ya nyuma wastani (iv) Kimadende

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Soma shairi ifuatayo kisha ujibu maswali CHEMA HAKIDUMU Chema hakidumu, kingapendekeza, Saa ikitimu, kitakuteleza(Solved)

  Soma shairi ifuatayo kisha ujibu maswali CHEMA HAKIDUMU Chema hakidumu, kingapendekeza, Saa ikitimu, kitakuteleza Ukawa na hamu, kukingojeleza, Huwa ni vigumu, kamwe hutaweza Chema sikiimbi, kwamba nakitweza Japo mara tumbi, kinshaniliza, Na japo siombi, kipate n’ongeza, Mtu haniambi, pa kujikimbiza Chema mara ngapi, kinniondoka, Mwanangu yu wapi? Hakukaa mwaka, Kwa muda mfupi aliwatilika, Ningefanya lipi, ela kumzika? Chema wangu babu, Kibwana Bashee, Alojipa tabu, kwamba anilee Na yakwe sababu, ni nitengenee, Ilahi Wahhabu, mara amtwee. Chema wangu Poni, kipenzi nyanyangu, Hadi siku hini, yu moyoni mwangu, Yu moyoni ndani, hadi kufa kwangu, Ningamtamani, hatarudi kwangu. (Abdalla, Abdilatif, Sauti ya Dhiki) MASWALI: (a) Hili ni shairi la aina gani? (b) Taja na ueleleze aina zozote mbili za bahari katika shairi hili. (c) Eleza umbo la shairi hili.

  Date posted: November 25, 2022.  

 • Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata. Mhudumu: Mnakaribishwa. Menyu hii hapa. Mtakula nini?(Solved)

  Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata. Mhudumu: Mnakaribishwa. Menyu hii hapa. Mtakula nini? Mteja 1: Naomba uniletee mix na ugali. Fanya haraka. Mteja 2: Mhudumu,hebu leta madodo na chemsha mbili. Pia niletee maji ya machungwa. Mhudumu: Sawa. Baada ya dakika moja utapata yote uliyoagiza. Mteja 1: (Akila) Wewe-Please bring me drinking water. Yawe baridi tafadhali. Mhudumu: Ndiyo haya hapa mezani. Glasi ndio hii pia,karibu. Mteja 2: Nina haraka mzee. Wapi tooth pick? Mhudumu: Hizo hapo ,mezani karibu na maji. Mteja 1: (Akiita) Mhudumu,naomba uniletee ugali saucer tafadhali. Mhudumu: Naam. Mteja 2: (Akisimama) Nimeshiba. Hizi hapa pesa Niletee change haraka niondoke. MASWALI a) Ni sajili gani inayohusishwa katika mazungumzo haya? b) Taja sifa zozote tano za sajili hii c) Dondoa msamiati unaotambulisha sajili hii

  Date posted: November 24, 2022.  

 • Tumia herufi mwafaka kuainisha maneno katika sentensi hii. Ingawa anataka kucheza karata,ni mlevi (Solved)

  Tumia herufi mwafaka kuainisha maneno katika sentensi hii. Ingawa anataka kucheza karata,ni mlevi

  Date posted: November 24, 2022.  

 • Sahihisha: Kwenye nilisomea ni bali.(Solved)

  Sahihisha: Kwenye nilisomea ni bali.

  Date posted: November 24, 2022.  

 • Nyambua Filisisha (tenda) (Solved)

  Nyambua Filisisha (tenda)

  Date posted: November 24, 2022.  

 • Tumia kitenzi jina na kivumishi kutunga sentensi.(Solved)

  Tumia kitenzi jina na kivumishi kutunga sentensi.

  Date posted: November 24, 2022.  

 • Andika sentensi hii katika ukubwa. Huyo nyoka alikatwa mkia na mvulana yule.(Solved)

  Andika sentensi hii katika ukubwa. Huyo nyoka alikatwa mkia na mvulana yule.

  Date posted: November 24, 2022.  

 • Taja visawe vya maneno yafuatayo. (i) Damu (ii) Mjinga(Solved)

  Taja visawe vya maneno yafuatayo. (i) Damu (ii) Mjinga

  Date posted: November 24, 2022.  

 • Andika katika udogo na wingi Njusi aliyekuwa na jicho moja alianguka mtoni.(Solved)

  Andika katika udogo na wingi Njusi aliyekuwa na jicho moja alianguka mtoni.

  Date posted: November 24, 2022.  

 • Tumia kiwakifishi kifuatacho kubainisha matumizi yake katika sentensi ili kutoa maana mbili tofauti. Ritifaa(Solved)

  Tumia kiwakifishi kifuatacho kubainisha matumizi yake katika sentensi ili kutoa maana mbili tofauti. Ritifaa

  Date posted: November 24, 2022.  

 • Tunga sentensi ukitumia viwakilishi vifuatavyo. (i) Nafsi viambata (II) Visisitizi(Solved)

  Tunga sentensi ukitumia viwakilishi vifuatavyo. (i) Nafsi viambata (II) Visisitizi

  Date posted: November 24, 2022.  

 • Geuza neno lililopigwa mstari kuwa kiwakilishi Mtoto mbaya aliadhibiwa(Solved)

  Geuza neno lililopigwa mstari kuwa kiwakilishi Mtoto mbaya aliadhibiwa

  Date posted: November 24, 2022.