-
Fafanua aina ya hali iliyotumika katika sentensi hii.
Wanasiasa wengi hulalamika kila mara.
Date posted:
October 4, 2019
-
Sahihisha sentensi ifuatayo:
Mwalimu mwenye ako nabidii amepeana mazoezi katika darasa yetu.
Date posted:
October 4, 2019
-
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.
Ilikuwa Jumamosi. Nilifika nyumbani kwangu saa moja jioni. Tangu nistaafu miaka
miwili awali sikupenda kuchelewa Taarifa ya Habari. Mwezi mmoja ukawa umepita tangu nipewe pesa za kiinua mgongo. Mwezi mmoja mzima nilikuwa katika shughuli za kulipa deni hapa na kulipa karo huku. Kuwekeza kwenye mradi ule na kununua hili. Sasa shilingi laki mbili tu zilikuwa zimesalia katika benki. Watu wengi walinishawishi nijaribu kilimo cha mahindi. Bei ilikuwa imeanza kuimarika. Katika taarifa ya habari jioni hiyo, Waziri wa Kilimo alitangaza bei mpya. Shilingi 1,500 kwa kila gunia. Nami nilikuwa naanza kuumakinikia mradi huu. Baaada ya taarifa, nilikoga, nikala na nikaenda kulala. Kwa sababu ya uchovu, usingizi ulinichukua mara moja.. Usingizini niliota. Katika ndoto niliutekeleza mradi wangu. Msimu huo wa kilimo nilitenga ekari kumu za shamba langu. Wataalamu walinishauri kuwa wakati mzuri wa kulima ni wa kiangazi. Mwezi wa Januari ulipoanza tu nilitafuta trekta na kulima. Malipo yalikuwa shilingi 1,200 kila ekari. Katikakati ya mwezi wa Machi, nilitafuta trekta la kutifua shamba tena kwa gharama ya shilingi 15,000 ekari zote kumi. Kufuatia ushauri wa manyakanga wa kilimo, nilipa shilingi elfu kumi na tatu kupiga shamba lote haro. Mwishoni mwa mwezi huo, nilienda mjini kutafuta pembejeo. Kwanza, nililipa shilingi 20,500 kwa magunia 15 ya mbolea. Kisha nilinunua magunia manne ya mbegu ya mahindi yenye uzani wa kilo 25 kwa shilingi 3,300 kila gunia. Mwezi wa Aprili ulipotimia tu, niliamua kupanda. Ili nipate mazao bora, nilipanda kwa tandazi. Gharama ilikuwa shilingi 1,000 kila ekari. Mvua ilinyesha vizuri na baada ya siku saba mahindi yalianza kuota. Ilifurahisha kuhesabu mistari ya kijani iliyonyooka. Hali hii iliwezekana tu baada ya kuajiri vijana wa kuwafukuza korongo na vidiri ili wasifukue mbegu mchangani. Baada ya mwezi mmoja, hatua ya kupalilia ilifika. Nilitafuta vibarua wa kupalilia. Malipo yalikuwa shilingi 700 kila ekari. Kumbe kupalilia kulichochea mtifuko wa mahindi. Punde yakawa yananifikia magotini. Hii ikawa ishara kuwa yanahitaji kumwagiwa mbolea ya kunawirisha iitwayo ‘amonia.’ Gharama yake ikawa shilingi1,300 kila gunia. Hivyo, nikalipa shilingi 19,500 kwa magunia kumi na matano.. Mahindi yalibadilika kimiujiza. Ghafla tu yalirefuka na kunenepa mashina. Yalibadilika rangi yakapiga weusi. Shamba liligeuka likawa kama msitu wa rangi ya kijani iliyokolea. Wapita njia waliajabia mimea na juhudi zangu. Shamba langu sasa likawa kielelezo. Maafisa wa kilimo wakawa kila siwanawaleta wakulima wengine kujifunza siri ya ufanis wangu. Hapo nikaanza kuhesabu mavuno nitakayopata kukadiria faida. Nilipuuza kabisa ushauri wa wahenga kuwa ‘Usikate majani, mnyama hajauawa.’
Bila taarifa wala tahadhari mvua ikatoweka. Hayakupita majuma mawili mahindi yakaanza kubadilika. Juma moja baadaye mahindi yalinyauka. Badala ya mahindi, shamba likageuka la vitunguu vilivyochomwa na jua. Makasio yangu ya faida yaliyeyuka jinsi ufanyavyo moshi. Lakini ‘Muumba ndiye Muumbua.’ Siku moja mawingu yalitanda na mvua ikanyesha. Muda is muda mahindi yalianza kunawiri. Kumbe tukio lililonivunja moyo lilikuwa laja. Siku moja mvua kubwa ilinyesha. Asubuhi nilipotoka nje nilipigwa na butwaa. Barafu ilitapakaa pote. Shamba lilikuwa limetapakaa barafhuku majani ya mahindi yamechanika kama nyuzi. Niliugua. Baada ya wiki moja, nilipata nafuu. Nilipotazama upande wa shamba nikaona dalili za majani mapya ya mahindi yakianza kuchomoza. Maumbile ni kitu cha ajabu kweli. Muda si mrefu mahindi yalirudi hali yake tena, kisha yakakomaa. Harakati za kutafuta watu wa kuyakata na kuyakusanya zilianza. Gharama ya shughuli hii ikawa shilingi 5,000. Kuvuna, kusafirisha kutoka shamba na kukoboa kwa mashine magunia 200 yakachukua shilingi 20,500. Kufikia hapo nilikuwa nimetumia takribani shilingi 192,700. Gharama nyingine zilikuwa za usafiri, gharama ya dharura na usimamizi, usumbufu wangu binafsi, gharama ya magunia na kadhalika. Mahindi yalipokuwa tayari kwenye magunia nilifunga safari kwenda mjini kutafuta soko. Niliposhuka tu niliona gazeti. Habari motomoto siku hiyo ilikuwa: ‘MAHINDI GUNIA 900/=.’ Niligutuka usingizini.
Maswali:
a) Andika kichwa mwafaka kwa kifungu hiki cha habari.
b) Msimulizi alikuwa na kiasi gani cha pesa katika benki baada ya mradi kukamilika?
c) Taja matatizo matatu yaliyotisha mradi wa msimulizi wa kukuza mahindi.
d) Eleza maana ya methali zifuatazo:
(i) Usikate majani, mnyama hajauawa.
e) Eleza mambo mawili yaliyosababisha msimulizi asipate faida alivyotarajia.
f) Kwa nini msimulizi alisema maumbile ni kitu cha ajabu?
g) Eleza maana ya:
(i) kiinua mgongo.
(ii) manyakanga wa kilimo.
Date posted:
October 4, 2019
-
Andika sentensi hii katika usemi wa taarifa
" Nitampokea mjomba iwapo nitampata," Rehema alimwambia shangazi yake.
Date posted:
October 4, 2019
-
Ainisha maneno yaliyopigiwa mstari.
Naam! Amekaa kabla ya mkurungezi mkuu yule.
Date posted:
October 4, 2019
-
Yakinisha sentensi hii:
Hajanivunjia mlango wala kuniibia
Date posted:
October 4, 2019
-
Onyesha mofimu katika:
kilichopewa
Date posted:
October 4, 2019
-
Zingatia picha ifuatayo kisha ujibu maswali.
(a) Tambua kipera cha fasihi simulizi kinachowakilishwa na muktadha wa picha hii.
(b) Toa sababu mbili za jawabu lako katika swali la (a).
(c) Jadili sifa zozote tano zinazotambulisha kipera hiki.
(d) Jadili udhaifu wa kipera hiki katika jamii ya kisasa.
Date posted:
October 3, 2019
-
Kamilisha jedwali
Date posted:
October 3, 2019
-
Bainisha kiima na chagizo katika sentensi ifuatayo.
Walimu hao walifanya kazi yao kwa bidii.
Date posted:
October 3, 2019
-
Eleza matumizi ya “na” katika sentensi ifuatayo.
Wageni na wenyeji walikimbiliana.
Date posted:
October 3, 2019
-
Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia jedwali.
Ouma alianguka mtihani ila Kamau alifuzu vizuri.
Date posted:
October 3, 2019
-
Ainisha vielezi katika sentensi zifuatazo.
(i)Jaribu kujitahidi kisabuni usianguke mtihani.
(ii)Wachezaji wote wameingia uwanjani.
Date posted:
October 3, 2019
-
Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo.
Wanafunzi waliandikiana barua.
Date posted:
October 3, 2019
-
Unda nomino mbili kutokana na neno "kudhulumu".
Date posted:
October 3, 2019
-
Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo
Juma alimchinjia mamake mbuzi mzuri kwa kisu.
Date posted:
October 3, 2019
-
Andika katika usemi wa taarifa
“Nitawatuza watahiniwa wote watakaopita mtihani mwaka huu”. Mwalimu aliwaahidi wazazi.
Date posted:
October 3, 2019
-
Andika sentensi yakinishi kutokana na sentensi ifuatayo.
Utawala mkubwa wa meya haukuzuilika.
Date posted:
October 3, 2019
-
Andika kwa ukubwa na udogo
Sahani zote zimepelekwa nyumbani
Date posted:
October 3, 2019
-
Bainisha aina za vishazi katika sentensi hii
Watoto walioachwa mayatima wamesaidiwa
Date posted:
October 3, 2019
-
Ainisha viambishi na mzizi katika kitenzi
Hawakunichokoza
Date posted:
October 3, 2019
-
Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya jedwali.
Sisi tulipokuwa shuleni tulisoma kwa bidii.
Date posted:
October 3, 2019
-
Eleza tofauti ya kisarufi ya maneno yaliyopigiwa mstari.
i)Hiki ni kitabu cha mwalimu
ii)Hiki ni cha mwalimu
Date posted:
October 3, 2019
-
Andika sifa mbili mbili bainifu za sauti.
i)/e/
ii)/n/
Date posted:
October 3, 2019
-
MUHTASARI
Soma kifungu kifuatacho cha habari kisha ujibu maswali yanayofuatia.
Watu wengi, wanaamini kwamba kufundisha watoto nyimbo shuleni ni kupoteza wakati unaofaa kwa masomo ya maana. Lakini muziki nyumbani na shuleni una manufaa mengi.
Muziki ni kitulizo kikubwa sana cha moyo wa binadamu. Muziki una njia ya kipekee ya kuwasiliana. Baadhi ya ujumbe hauwezi kupitishwa kwa njia nyingine ila kwa muziki.
Muziki umetajwa kumsaidia mtoto kwa mambo yafuatayo:
Kuendeza hisia nzuri, za kuburudisha na kuzuzua. Muziki humsaidia mtoto kuweza kukabiliana na tajriba mbaya nazo. Unampa fursa ya kutoa moyoni simanzi na dhiki yake na hivyo kumrejeshea raha tena. Liwazo la muziki ni dhahiri wakati mtoto anapolala pindi anapoimbiwa bembelezi.
Inaaminika pia kwamba muziki unakomaza akili ya mtoto na ni nyenzo muhimu sana katika hafla yake ya kujifanya mambo, hasa kwenye miaka yake ya mapema. Muziki huhitaji umakinifu ili kutambua miondoko na maneno halisi ya wimbo huo na mambo haya humfanya mtoto kuhamisha umakini huu kwenye masomo mengine darasani. Inaaminika pia kwamba kupitia kwa muziki mtoto anaweza kujifunza mbinu ya kukumbuka mambo anayofunzwa masomoni.
Watoto ambao hujifunza muziki mara kwa mara hujipatia mbinu za werevu shuleni haswa kwenye somo la hesabu na werevu wa mambo mengine kwa jumla. Utafiti umeonyesha kwamba watu wazima ambao walijifunza muziki kabla wafikishe umri wa miaka 12 huwa na utumizi mzuri wa maneno magumu na msamiati kuliko wale ambao hawakujifunza kuimba.
Muziki pia husaidia watoto walio na kasoro za kuzungumza au walio na ulimi mzito wa kuzungumza.
Watoto au watu wazima walio na shida ya kigugumizi huweza kujieleza kwa ufasaha kwa kupitia muziki na jambo hili huboresha kujiamini kwao kwa kibinafsi. Watoto kama hao huweza kujifunza na kuelewa mila na tamaduni zao.
MASWALI
a) Bila kupoteza maana iliyokusudiwa na mwandishi, fupisha aya ya kwanza hadi ya tatu.
(maneno 40 – 45)
MATAYARISHO
NAKALA SAFI
b) Dondoa hoja muhimu zinazojitokeza katika aya ya nne na ya tano. (Maneno 45 – 50)
MATAYARISHO
JIBU
Date posted:
October 3, 2019
-
UFAHAMU
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Mojawapo kati ya misingi na nguzo za maendeleo uliwenguni ni viwanda. Viwanda ni muhimu kwa kuwa ndivyo vinavyoigeuza malighafi inayopatikana na kuwa bidhaa zinazoweza kutumiwa na watu. Katika nchi zinazoendelea, ambazo hazina uwezo mkubwa wa mitaji viwanda vinavyoimarika ni vile vidogo. Hivi ni viwanda ambavyo huhusisha amali za mikono. Kuimarika kwa viwanda hivi vidogo kunatokana na sababu mbalimbali.
Nchi zinazoendelea huwa na masoko finyu sana kwa kuzingatia uwezo wa ununuzi wa wanaolengwa na bidhaa za viwanda . Katika msingi huu viwanda vikubwa vitawiwa ugumu kufanya biashara katika mazingira ambako masoko yake ni finyu au utashi wa bidhaa zake sio mkubwa. Viwanda vidogo pia vinao uwezo wa kuwaajiri wafanyikazi wengi hasa kwa kuwa havina uwezo wa kugharamia mashine. Uajiri huu wa wafanyikazi wengi ni muhimu katika maeneo mengi ambako tatizo la ajira ni mojawapo wa matatizo sugu. Tofauti na mataifa ya kitasmia (yenye viwanda vingi) mataifa mengi yanayoendelea hayana mifumo imara ya kuwakimu watu wasiokuwa na kazi. Utegemezi wa jamaa wanaofanya kazi kwa hivyo unakuwa nyenzo ya pekee ya kuyamudu maisha.
Kuanzisha viwanda vidogo vidogo hakuhitaji mtaji mkubwa tofauti na viwanda vikubwa. Hali hii inasahilisha uwezekano wa watu wengi kujasurisha shughuli yoyote ile. Sambamba na suala hili ni kuwa ni rahisi kujarisha bidhaa mpya kwa kiwango kidogo cha kiwanda kidogo. Ikiwa mzalishaji yeyote atazalisha bidhaa mpya kwa mapanu, kwa mfano kama ilivyo kwa viwanda vikubwa, pana uwezekano wa kupata hasara kubwa. Huenda utashi wa bidhaa hiyo uwe mdogo ukilinganishwa na ugavi wa bidhaa yenyewe. Majaribio mazuri huwa ni kwa kiwango kidogo.
Kuwepo kwa viwanda vidogo huwa chocheo kubwa la usambazaji wa viwanda hadi maeneo ya mashambani. Hali hii inahakikisha kuwa nafasi za ajira zimezambazwa nchini hali ambayo inasaidia kuhakikisha kuwa pana mweneo mzuri wa kimapato nchini. Mweneo huo wa mapato unachangia katika kuboresha uwezo wa kiununuzi wa umma. Huu ni msingi muhimu wa maendeleo. Upanuzi na ueneaji wa viwanda vidogo vidogo ni msingi mkubwa wa kujitegemea kiuchumi. Aghalabu viwanda vikubwa huegemea kwenye mitaji ya mashirika ya kimataifa na huwa msingi wa kuendelezwa kwa utegemezi wa kiuchumi.
Maswali
a)Kwa nini viwanda ni muhimu?
b)Ni nini kiini cha matatizo ya uuzaji wa bidhaa katika nchi zinazoendelea?
c)Eleza faida zinazotokana na kuwepo kwa viwanda vidogo vidogo.
d)Usambazaji wa viwanda katika maeneo ya mashambani una faida gani?
e)Fafanua maana ya msamiati huu kama ulivyotumika katika kifungu.
i)Kujasurisha
ii)Amali
iii)Utashi
Date posted:
October 3, 2019
-
Onyesha shamirisho katika sentensi ifuatayo.
Wanafunzi walikatiwa keki na mwalimu kwa kisu.
Date posted:
October 3, 2019
-
Onyesha kiima na kiarifa katika sentensi ifuatayo.
Wanafunzi watakaolala darasani wataadhibiwa vikali.
Date posted:
October 3, 2019
-
Onyesha aina za virai katika sentensi hii.
Wazazi wetu watawasili kesho saa tatu.
Date posted:
October 3, 2019
-
Eleza matumizi mawili ya "ka".
Date posted:
October 3, 2019