Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kiswahili Karatasi Form 4 Term 2 2016 Question Paper

Kiswahili Karatasi Form 4 Term 2 2016 

Course:Kiswahili

Institution: Form 4 question papers

Exam Year:2016




102/2
KISWAHILI
Karatasi 2
Juni 2016
Muda: Saa 2(1 )/2

SEHEMU A: UFAHAMU
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Maisha ya binadamu yamepitia hatua mbalimbali katika karne kadhaa zilizopita, kwa mfano tumeshuhudia mageuko katika uzalishaji wa kawi kuanzia karne za zama za mawe ambapo mawe yalikuwa nyenzo muhimu katika uzalishaji wa kawi nishati. Mojawapo wa nyanja ambazo zimepiga misamba mikubwa ya maendeleo ni ile ya mawasiliano. Maelezo ya jinsi usafiri wa zamani ulivyotegemea uwezo wa binadamu kutembea kutoka sehemu moja hadi nyingine yanasikika kama kadhia za paukwa pakawa.
Tunaishi katika karne ambayo huenda tukashudia maendeleo yasiyokadirika katika uwanja huu. Kwa sasa hivi, tarakilishi imekuwa uwenzo mkuu wa mabadiliko hayo kutokana na nafasi muhimu inayochukua katika maisha yetu. Tangu azali tumesikia msemo kuwa ‘maarifa ni uwezo’ . ukweli wa msemo huu unadhirika bayana tuangaliapo nafasi ya tarakilishi kama jira ya technolojia ya habari na mawasiliano au teknohama. Ubashiri wa mtaalamu wa maswala ya habari Marshal Macluhan, aliyebuni dhana ya ‘kijiji kitandawazi’ katika mwaka wa 1960, unaelekea kutimizika. Mwanahabari huyu alieleza imani yake kuwa mawasiliano yanayohusisha mitambo ya umeme yataunganisha ulimwengu.
Maendeleo makubwa ya wavuti au mdahalisi katika ulimwengu wa sasa yanasababisha mawasiliano ya jamaa, ndungu na watu wanaoishi maeneo mbalimbali. Kasi ya uenezaji wa maarifa imekuwa ya juu sana. Mikahawa ya mdahalishi au vituo vya bwakameme (cyber cafes) vimeenea kila mahali. Inahitaji muda mfupi kusakura kwenye mdahalishi tovuti ya google, yaani ukifungua anwani ya http//www.google. com, unaweza kupata taarifa zozote unazotamani. Kwa njia hii mtumiaji anapata maarifa muhimu kwa bei nafuu na kwa njia nyepesi na rahisi kuliko kulazimika kubukua mabuku ya kila aina kupata taarifa sawa na hizo.
Ili kuweza kuhifadhi enzi hii teknohama, pana haja kubwa ya mataifa yetu kuwekeza katika uwanja huu. Serikali zetu zinapaswa kutambua kuwa jamii kutoijua taaluma ya tarakilishi, angaa ile ya kimsingi, ni kama kutojua kusoma katika enzi zilizopita. Kadiri wakati unavyosonga ndivyo ambavyo tarakilishi inavyochukua nafasi muhimu katika maisha yetu. Katika msingi huu basi lazima ziwepo juhudi za kuyaeneza maarifa muhimu kuhusu matumizi yake. Inahalisi kutambua kuwa mtaka cha mvunguni sharti ainame. Ikiwa tunataka nchi yetu ifaidi matunda ya technolojia ya leo basi hatuna budi kuwa tayari kuwekeza ipasavyo.
Uwekezaji huo unaenda sambamba na juhudi ya kuhakikisha elimu inayohusiana na masuala ya tarakilishi inasambazwa nchini. Elimu hii ndiyo maarifa ambayo yatakuwa nguzo ya msingi ya maendeleo ya nchi siku za usoni. Ni muhimu hata kutoa tahadhari hapa. Katika jamii nyingi huwepo watu ambao kila panapokuwa na mvuvumiko fulani hupenda kuitumia hali hiyo kujinuifaisha. Huweza kufanya hivi kwa kuanzisha vituo vya kufundisha maarifa dufu ya tarakilishi nia yao ikiwa ni kufaidika kutokana na karo ghali wanazotoza. Licha ya kuwa tunasisitiza umuhimu wa kuwepo na kusambazwa kwa elimu ya tarakilishi, pana haja ya kuwepo na viwango. Lazima serikali ihakikishe kuwa pana viwango vinavyodumishwa. Hii itazuia uwezekano wa kuanzishwa kwa shule ambazo lengo lao la msingi sio kuyaendeleza maarifa ya jamii bali kuijaza mifuko ya wachache walioingiwa na shauku ya utajiri.
Ikiwa jamii yetu inataka kutangamana na kwenda sambamba na wakati lazima iwekeze sio kwa mali bali kwa hali kwenye uwanja huu muhimu. Maisha ya kesho yaTAdhibitiswa kwa kiasi kikubwa na tarakilishi. Leo hii hata biashara inaendelea kwa mfumo huu. Huu ndio msingi wa biasharalishi au biashara ya elekroniki (e - commerce) ambayo imeanza kushika kasi ulimwenguni. Biashara ya aina hii inayawezesha makampuni mengi kuwafikia wateja wake popote walipo ulimwenguni. Umbali wa kijiografia sio kikwazo tena kwa kuwa biashara ya aina hii haitegemei makutano ya ana kwa ana kati ya mteja na muuzaji. Lazima ziwepo juhudi nyingi tu za kusambaza na kuienzi taaluma ya tarakilishi mbali pia kuhakikisha kuwa taasisi nyingi zimetarakilishwa ili kwenda sambamba wakati: wakati wa kurundika majalada ofisini kama maghala umepita. Hii ni enzi ya technohama.

Maswali
a) Ili kunufaika na technolojia, sharti nchi yetu ifanye nini?
(alana 2)
b) Ni kwa sababu gani utabiri wa Macluhan umeishia kuwa kweli?
(alama 2)
c) Kwa nini mwandishi anasema kuwa ‘wakati wa kurundika majalada ofisini kama maghala umepita’?
(alama 2)
d) Tambua dhamira kuu ya kifungu hiki.
(alama 2)
e) NI jambo gani linalomfanya mwandishi kusema kuwa mustakali wa binadamu utaendeshwa kwa tarakilishi?
(alama 2)
f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu hiki.
i) Yasiyokadirika
ii) Jira
iii) Kusakura
iv) Mvuvumko
(alama 4)


SEHEMU B: UFUPISHO
Soma kifungu kifuatacho kisha uyajibu maswali yanayofuata.
Nidhamu ni kitu cha maana sana maishani mwa binadamu. Kila mwanafunzi anapaswa kuwa na nidhamu ya hali ya juu sana. Akiwa na nidhamu hiyo, atakuwa mtu mwadilifu, anayeweza kustahiwa na kusadikika katika mambo, shughuli na hali tofauti tofauti.
Kwanza, mtoto mwenye nidhamu huwa kama anga au nuru nyumbani mwao, shuleni na pia katika jamii. Watu wote wanampenda na kumheshimu. Wazee kwa vijulanga wote wanamtegemea kama msimamizi wa mambo nyeti ya maisha yao. Kwa hivyo, dhahiri shairi kwamba mwadilifu hunufaika sana. Kinyume na mkaidi ambaye wahenga walimwambia kwamba atakosa kufaidi hadi siku ya Idi.
Pili, huwadia nyakati ambapo huwa kuna jambo la busara, mathalani jukumu ama dhima fulani ambayo huhitaji tu mwakilishi mmoja darasani, shuleni au katika jamii. Watu hapana shaka watamteua yule mwadilifu kuchukua nafasi kama hiyo. Ndio maana viranja wanaoteuliwa shuleni, huwa ni wanagenzi ambao tayari wamekwisha tiliwa katika mizani na kupigwa msasa madhubuti.
Vile vile, mwadilifu daima atajiepusha na shutuma na majanja yote yanayoweza kuchipuka. Kuna msemo maarufu, kwa busara yake iliyobusarisha mwadilifu, kwamba “aliye kando haangukiwi na mti”. Pia waliambiwa kwamba, “Pili pili usiyoila ya yakuwashiani?”
NI bayana kutokana na misemo hiyo miwili kwamba mwenye nidhamu hawezi kuhusishwa na majanga hatari yanayoweza kuwakumba watu.


Walaini ni vyema kujiuliza, je, nidhamu huanzia wapi, na kwa nini kuna baadhi ya ‘watoto’ ambao ni watovu wa nidhamu? Utovu wa nidhamu huanzia awali sana maishani mwa mja. Mtoto anapozaliwa, anategemea miongozo na mielekeo ya watu wazima ambao wako mazingirani mwake. Ndipo wakale wale waliokaramka walisema kwamba mtoto akibebwa, hutazama kisogo cha nina.
Hivi ni kusema kwamba, nidhamu au utovu wa nidhamu huanzia nyumbani hadi shuleni, kisha hupanuka hadi kufikia kiwango ambapo mja anatangamana na watu wote katika maisha yake. Ikiwa sehemu moja ya ukuaji wa nidhamu maishani mwa mja itasambaratika, basi hawezi akawa mkamilifu maishani mwake.
Kwa vile ni bayana kwamba mabaya yote ayatendayo duniani hulipwa na Mola papa hapa duniani, watovu wa nidhamu wote huishia kuangamia, ama kujuta mno kwa amali zao potovu. Ni kheri mja kujihidi mwenyewe, kwani uhalifu haulipi chochote.

Maswali
a) Eleza umuhimu wa nidhamu (maneno 45 - 50) (alama 1 mtiririko)
(alama 6)

b) Bila kubadilisha maana, fupisha aya nne za mwisho.
(alama 1 mtiririko)
(maneno 55 - 60) (alama 7)


SEHEMU C: MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)
a) Andika vitamkwa vyenye sifa zifuatazo: (alama 2)
i) Irabu ya mbele, wastani.
ii) Kipasuo ghuna cha kakaa laini.

b) Eleza maana ya silabi. (alama 2)

c) Ainisha vitenzi katika sentensi.
Ndege yu taabani, hata hivyo anajaribu kujinasua. (alama 3)

d) Ainisha maneno yaliyopigiwa mstari.
Naam, ameleta machache. (alama 2)

e) Tumia kiwakilishi cha ‘a’ unganifu katika sentensi kuonyesha: (alama 2)
i) Umilikaji
ii) Nafsi katika orodha au nafsi katika kundi.

f) Andika upya ukibadilisha neno lililopigiwa mstari kuwa kielezi. (alama 2)
Komu ameshona nguo nzuri na kuiuza sokoni.

g) Geuza sentensi ifuatayo kwa kufuata maagizo. (alama 2)
Wachezaji hawakucheza mpira kwa sababu ya mvua.
Anza kwa: mpira

h) Andika kwa wingi (alama 2)
Nyundo hii imevunjika mpini wake.

i) Kwa kutolea mfano, fafanua maana ya mofimu huru. (alama 2)



j) Andika sentensi ifuatayo katika hali yakimishi. (alama 2)
Askari wasipopiga doria wala kushirikiana na raia hawatakuwa wametuhakikishia usalama.

k) Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizo kwenye mabano. (alama 3)
i) Nywa (tendesha)
ii) La (tendeana)
iii) Vaa (tendwa)

l) Eleza maana ya sentensi. (alama 2)
Ningalikuwa na pesa ningalinunua nyumba na ningalistarehe.

m) Andika katika usemi wa taarifa. (alama 2)
“ Shughuli yetu itamalizika kesho,” Mama alimwambia Juma
n) i) Eleza maana kirai. (alama 2)
ii) Ainisha virai vilivyopigiwa mstari. (alama 2)

Zana hizi zimeundwa na mafundi wenye ustadi mkubwa.

o) Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha mistari. (alama 4)
Mvua ilinyesha tulipokuwa tukilima.

p) Tumia visawe vya maneno yaliyopigiwa mstari kuandika tena sentensi ifuatayo. (alama 3)
Ukuta umemwumiza mvulana alipokuwa akiuparaga.



SEHEMU D: ISIMU JAMII
a) i) Eleza maana ya Isimu jamii. (alama 2)

ii) Tofautisha dhana zifuatazo: (alama 2)
Pijini na Kirioli

b) Eleza sifa zozote sita za sajili ya shuleni. (alama 6)






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers