Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

a) Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika hali ya kuamuru katika wingi. Njoo hapa. b)Tunga sentensi yenye kitenzi kishirikishi kipungufu. c) Yakinisha sentensi ifuatayo. Asingepigiwa kura, asingekuwa rais wa Kenya. d)...

a) Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika hali ya kuamuru katika wingi.

Njoo hapa.

b)Tunga sentensi yenye kitenzi kishirikishi kipungufu.

c) Yakinisha sentensi ifuatayo.

Asingepigiwa kura, asingekuwa rais wa Kenya.


d) Unganisha sentensi zifuatazo kwa kutumia kiunganishi mwafaka.

Mtoto alikula sana.
Mtoto hakushiba.


e)Tunga sentensi moja ukitumia kihisishi na nomino maalum.


f)Taja aina mbili za mofimu na utolee mfano mmoja mmoja.


g) Tumia amba rejeshi katika sentensi ifuatayo:

Mchezaji ninayempenda ni Messi.



h)Taja sauti mbili za nazali.


i) Andika katika msemo wa taarifa.

Naapa ya kwamba nitatumikia wananchi wa Kenya na nitakuwa mwaminifu, Rais Mteule alisema.

Answers


johnson
a)
Njooni hapa!

b)Mifano ya vitenzi vishirikishi – ni, si, vi, ki, li, ya, i, zi, u.
- Kikulacho ki nguoni mwako au yeye ni mrefu au yeye si mrefu.

c) Angepigiwa kura, angekuwa Rais wa Kenya.

d)Mtoto alikula sana lakini hakushiba. (unaweza tumia viunganishi vya kinyume kama vile ingawa, ingawaje, hata hivyo, ilhali, japo, ijapokuwa, isipokuwa, bali).

e) Lo! Uhuru Kenyatta ameshinda uchaguzi. Au Lo! Uhuru Kenyatta ameshinda uchaguzi!

f)
Mofimu huru – mama, baba, shangazi, kuku.
- Mofimu tegemezi – aliamka, achezaye, kitabu, mtu, miti.

g)
Mchezaji ambaye ninampenda ni Messi.

h)
/m/, /n/, /ny/, /ng/ - zozote mbili


i)
Rais mteule aliapa / alisema ya kwamba / kuwa angetumikia wananchi wa Kenya na angekuwa mwaminifu.
johnson mwenjera answered the question on March 4, 2018 at 15:23

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions