Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. T. Arege: Barabara Barabara bado ni ndefu Nami tayari nimechoka tiki Natamani kuketi Ninyooshe misuli Nituliza akili. Lakini Azma yanisukuma Mbele ikinihimiza kuendelea Baada ya miinuko...

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
T. Arege: Barabara
Barabara bado ni ndefu
Nami tayari nimechoka tiki
Natamani kuketi
Ninyooshe misuli
Nituliza akili.
Lakini
Azma yanisukuma
Mbele ikinihimiza kuendelea
Baada ya miinuko na kuruha
Sasa naona unyoofu wake
Unyoofu ambao unatisha zaidi.
Punde natumbukia katika shimo
Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena
Ghafla nakumbuka ilivyosema
lie sauti zamani kidogo
"Kuwa tayari kupanda na kushuka
Ingawa nimechoka
Jambo moja li dhahiri
Lazima nifuate barabara
Ingawa machweo yaingia
Nizame na kuibuka
Nipande na kushuka.
Jambo moja nakukumbukia:
Mungu Je, nimwombe tena?
Hadi lini? Labda amechoshwa na ombaomba zangu
Nashangaa tena!
Kitu kimoja nakiamini
Lazima niendelee kijitahidi kwa kila hatua mpya
Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
Nikinaswa na kujinasua
Yumkini nitafika mwisho wake
Ingawa wangu mwisho haitauwahi kabla.
(a) Eleza toni ya shairi hili.
B)Mshairi ana maana gani anaposema "Kuwa tayari kupanda na kushuka"
katika ubeti wa tatu?
(c) Fafanua tamathali tano za usemi zilizotumiwa katika shairi hili
ukizitolea mifano mwafaka.
(d) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano wa shairi hili.
(e) Eleza maana ya:
(i) kuruba
(ii) barabara yenye ukungu

Answers


gregory
(a) Eleza toni ya shairi hili.
? Toni ya mahimaini - lazima niendelee kujitahidi kwa kila hatua.
? Toni ya uchovu - Nami tayari nimechoka tiki.
(b) Mshairi ana maana gani anaposema "Kuwa tayari kupanda na kushuka"
katika ubeti wa tatu?
? Kuwa tayari kukabiliana na uzuru na ugumu wa maisha
(c) Fafanua tamathali tano za usemi zilizotumiwa katika shairi hili
ukizitolea mifano mwafaka.
? Taswira - picha inayojitokeza unaposoma kazi ya fasihi n.k. wa miinuko na
kuruba.
? Taswira kinzani - Nizame na kuibuika
? Nipande na kushuka.
? Taashira - Barabara kuimarisha maisha.
? Mswali balagha - hadi lini?
? Uzungumzi nafsi - mizame na kuibuka, -Nipanda na kushuka.
(d) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano wa shairi hili.
? Msemaji ameshangaa kuwa amekuwa akiomba kwa muda na anatilia shaka
iwapo Mungu amechoshwa na maombi yake.
(e) Eleza maana ya:
(i) kuruba
? Hali ya kuwa na vikwazo na magumu ya maisha.
(ii) barabara yenye ukungu
? Mkondo wa maisha ambapo anayokubaliana nayo mja si wazi. Kila hisia
huibua mambo mapya
gregorymasila answered the question on February 7, 2018 at 13:02

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions