Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

a) Onyesha vishazi katika sentensi ifuatayo. Uchaguzi uliofanywa nchini Kenya ulikuwa wa amani. b) Bainisha aina za shamirisho katika sentensi: Shule nzuri ilijengewa wanafunzi kwa matofali. c) Eleza...

      

a) Onyesha vishazi katika sentensi ifuatayo.

Uchaguzi uliofanywa nchini Kenya ulikuwa wa amani.

b) Bainisha aina za shamirisho katika sentensi:

Shule nzuri ilijengewa wanafunzi kwa matofali.

c) Eleza sifa mbili za sentensi ambatano na utoe mfano mmoja.

d) Unda nomino kutokana na vitenzi vifuatavyo:
-Tafakari:.
-Sujudu:

e) Eleza maana ya chagizo na utunge sentensi moja kuonyesha maana yake.

  

Answers


johnson
a)
-Uchaguzi uliofanywa nchini Kenya – kishazi tegemezi.
-Ulikuwa wa amani – kishazi huru.

b)
Shule nzuri ilijengewa wanafunzi kwa matofali.

1) Shamirisho kipozi - shule.
2) Shamirisho kitondo - wanafunzi.
3) Shamirisho ala - matofali.

c)
(i) Huwa na mawazo mawili au zaidi (vitenzi viwili).
(ii) Huwa na kiunganishi.
Mama anasoma kitabu lakini baba analala.

d)
(i) Tafakari - kutafakari, tafakuri
(ii) Sujudu - Kusujudu, sijida

e)
Chagizo ni kielezi.
- Walienda ufuani mwa bahari au Wanafunzi walisoma kwa makini.

johnson mwenjera answered the question on March 4, 2018 at 15:10


Next: Define the term specific density?
Previous: a) Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika hali ya kuamuru katika wingi. Njoo hapa. b)Tunga sentensi yenye kitenzi kishirikishi kipungufu. c) Yakinisha sentensi ifuatayo. Asingepigiwa kura, asingekuwa rais wa Kenya. d)...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • (i) Eleza matumizi tofauti ya kiambishi ni katika sentensi ifuatayo. Nitasoma kwa bidii shuleni. (ii) Tunga sentensi ukitumia neno gani kama kiwakilishi na kama kivumishi. (iii)Tunga sentensi ukitumia...(Solved)

    i) Eleza matumizi tofauti ya kiambishi ni katika sentensi ifuatayo.

    Nitasoma kwa bidii shuleni.

    ii) Tunga sentensi ukitumia neno gani kama kiwakilishi na kama kivumishi.

    iii)Tunga sentensi ukitumia kitenzi la’ katika hali ya kutendeshea

    Date posted: March 3, 2018.  Answers (1)

  • Jadili misingi ambayo inaweza kutumika kurekebisha makosa ya kimatamshi katika ujifunzaji wa lugha ya pili(Solved)

    Swali hili linahitaji kubainisha mbinu ambazo mwalimu atazitumia anapofunza ili kumrekebisha mwanafunzi asiyeweza kutamka lugha ya pili ipasavyo.

    Date posted: March 2, 2018.  Answers (1)

  • Misingi inayotumika kurekebisha makosa ya kimatamshi katika ujifunzaji wa lugha ya pili.(Solved)

    Misingi inayotumika kurekebisha makosa ya kimatamshi katika ujifunzaji wa lugha ya pili.

    Date posted: March 2, 2018.  Answers (1)

  • Eleza dhima ya nadharia(Solved)

    Eleza dhima ya nadharia

    Date posted: March 2, 2018.  Answers (1)

  • Jadili dhana ya "Langue" na "parole"(Solved)

    Jadili dhana ya "Langue" na "parole"

    Date posted: March 2, 2018.  Answers (1)

  • Tafsiri kwa kiswahili -base -tenor -soprano -Alto(Solved)

    Tafsiri kwa kiswahili
    -base
    -tenor
    -soprano
    -Alto

    Date posted: March 2, 2018.  Answers (1)

  • Mighani ni nini?(Solved)

    Mighani ni nini?

    Date posted: March 2, 2018.  Answers (1)

  • Unda neno lenye sauti mwambatano KIK(Solved)

    Unda neno lenye sauti mwambatano KIK.

    Date posted: February 27, 2018.  Answers (1)

  • Katika jamii ya kisasa ndoa imo atharini. Kwa kutoa mfano katika tamthlia ya kigogo tetea kauli hii.(Solved)

    Katika jamii ya kisasa ndoa imo atharini. Kwa kutoa mfano katika tamthlia ya kigogo tetea kauli hii.

    Date posted: February 27, 2018.  Answers (1)

  • Fafanua sifa Za Majoka Bin Marara Katika Kigogo(Solved)

    Fafanua sifa Za Majoka Bin Marara Katika Kigogo.

    Date posted: February 26, 2018.  Answers (1)

  • Fafanua Sifa Za Boza Katika Kigogo(Solved)

    Fafanua Sifa Za Boza Katika Kigogo.

    Date posted: February 26, 2018.  Answers (1)

  • DAMU NYEUSI NA HADITHI NYINGINE Msiba unaowapata wanawake katika diwani hii ni wa kujitakia. Thibitisha kwa kurejelea wahusika wafuatao; a) Jamila b) Sela c) Christine d) Lucy e) Kudura (Solved)

    DAMU NYEUSI NA HADITHI NYINGINE
    Msiba unaowapata wanawake katika diwani hii ni wa kujitakia. Thibitisha kwa kurejelea wahusika wafuatao;
    a) Jamila
    b) Sela
    c) Christine
    d) Lucy
    e) Kudura

    Date posted: February 22, 2018.  Answers (1)

  • Jadili jinsi maudhui ya usaliti yanavyofafanuliwa katika tamthilia ya mstahiki Meya. (Solved)

    Jadili jinsi maudhui ya usaliti yanavyofafanuliwa katika tamthilia ya mstahiki Meya.

    Date posted: February 22, 2018.  Answers (1)

  • Riwaya ya kidagaa imeangazia maudhui ya utengano. Thibitisha. (Solved)

    Riwaya ya kidagaa imeangazia maudhui ya utengano. Thibitisha.

    Date posted: February 22, 2018.  Answers (1)

  • Lugha huchangia vipi kuleta; i) Utengano ii) Utangamano katika jamii (Solved)

    Lugha huchangia vipi kuleta;
    i) Utengano
    ii) Utangamano katika jamii

    Date posted: February 22, 2018.  Answers (1)

  • Eleza majukumu manne yanayotekelezwa na lugha katika jamii(Solved)

    Eleza majukumu manne yanayotekelezwa na lugha katika jamii

    Date posted: February 22, 2018.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Ni dhahiri shahiri kwamba uharamia umechipuka kama desturi na mfumo wa maisha katika siku za hivi karibuni. Janga hili limeshamiri...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
    Ni dhahiri shahiri kwamba uharamia umechipuka kama desturi na mfumo wa maisha katika siku za hivi karibuni. Janga hili limeshamiri hususan pembeni mwa bara la Afrika na kanda ya Afrika Mashariki.Taarifa za uharamia zimetawala vyombo vya habari, kiasi cha kwamba haipiti siku bila kuripotiwa visa vipya vya matendo haya mabovu ambayo yanaweza tu kumithilishwa na uhayawani.Matukio haya yamewalimbikizia mabaharia na nchi husika, simanzi na masaibu yasiyoweza kutiwa kwenye mizani.
    Yumkini tatizo hili halitokei pasi na kumotishwa na kitita kikubwa cha fidia kinachodaiwa na maharamia hawa. Aghalabu, suala hili lahusishwa pakubwa na azma na ari ya kuendeleza ujambazi wa kimataifa sawia na ulipuaji wa bomu mijini Nairobi na Dar es Salaam mnamo Agosti 7,1998, na tukio la Septemba 11, mwaka wa 2001 kule Marekani.Maafa na uharibifu wa mali si hoja, la mno kwa maharamia ni kutosheleza matakwa yao. Kwa upande mwingine, ukosefu wa tawala-wajibika katika maeneo kunakotokea unyama huu ni thibitisho tosha la mazingara yanayowezesha na kuruhusu kuchipuka kwa janga hili.
    Mchipuko wa baa la uharamia umelengwa jamii ya kimataifa ambayo ni mhudumu mkuu wa harakati za kusitisha majanga makubwa kama vile njaa, umaskini na magonjwa yaliyosheheni pakubwa barani. Bila shaka, hili ni suala linalosawisishwa na ‘kinyume mbele’. Maharamia wanatishia utangamano wa kimataifa wanapotibua usafiri wa abiria na shehena zinazoelekezwa sehemu tofauti ulimwenguni.
    Matumizi ya kidiplomasia na mashauriano hayaelekei kuzalisha matunda katika juhudi za kudhibiti uharamia. Zaidi ya hayo, matumizi ya nguvu yahusishayo mashambulizi pamoja na maharamia kufunguliwa mashtaka nchini Kenya na Ufaransa kunaelekea kuzipiga jeki juhudi za uharamia ulimwenguni.Aidha, utawala wa nchi kunakochipuka uharamia haujajizatiti kuharamisha doa hili linalotisha ustawi wa kimataifa.
    Mathalan, ni jambo lisilopingika inapobainika kuwa uharamia umedumaza biashara ya kimataifa, hali inayochangia upungufu na ucheleweshaji wa bidhaa muhimu zinazoendeleza ustawi wa uchumi. Dosari hii inaelekea kukwamiza mojawapo wa malengo ya maendeleo ya milenia yanayosisitiza uimarishaji na ushirikiano wa maendeleo na upanuzi wa masoko ulimwenguni. Harakati za kitalii katika kanda ya mashariki ya bara la Afrika zimehujumiwa. Ni muhali kwa utalii kustawi kwenye maeneo yaliyo na tishio la usalama. ltakumbukwa bayana kwamba watalii hawasafiri tu kwa ndege bali hata kwa meli.
    Jitihada za kuweka laini za mawasiliano chini ya bahari ili kurahisisha na kupunguza gharama za mtandao ulimwenguni ni ndoto ambayo haijatimia hadi hivi sasa, kufuatia juhudi za maharamia katika bahari ya Hindi. Kwa mujibu wa hali hii, mawasiliano mepesi na nafuu yasitarajiwe hivi karibuni. Licha ya hayo, shughuli za uvuvi na biashara nyenginezo kwenye kanda ya mwambao zimetiliwa shaka si haba.
    Itabidi mikakati na suluhisho la kudumu liweze kupatikana ili vitendo vya uharamia viweze
    kusitishwa.

    MASWALI

    (a) Kwa nini uharamia umetamalaki ulimwenguni?

    (b) Fafanua dhana ya ‘kinyume-mbele’ kwa mujibu wa taarifa hii.


    (c) Uharamia unaelekea kumtia hofu mwandishi. Fafanua.


    (d) Thibitisha kuwa Kenya imeathirika pakubwa kutokana na vitendo vya uharamia




    (e) Ukirejelea kifungu, eleza maana ya:
    (i) uharamia ………………………………………………………………………………….
    (ii) mtandao …………………………………………………………………………………
    (iii) mwambao ………………………………………………………………………………

    Date posted: February 22, 2018.  Answers (1)

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. T. Arege: Barabara Barabara bado ni ndefu Nami tayari nimechoka tiki Natamani kuketi Ninyooshe misuli Nituliza akili. Lakini Azma yanisukuma Mbele ikinihimiza kuendelea Baada ya miinuko...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
    T. Arege: Barabara
    Barabara bado ni ndefu
    Nami tayari nimechoka tiki
    Natamani kuketi
    Ninyooshe misuli
    Nituliza akili.
    Lakini
    Azma yanisukuma
    Mbele ikinihimiza kuendelea
    Baada ya miinuko na kuruha
    Sasa naona unyoofu wake
    Unyoofu ambao unatisha zaidi.
    Punde natumbukia katika shimo
    Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena
    Ghafla nakumbuka ilivyosema
    lie sauti zamani kidogo
    "Kuwa tayari kupanda na kushuka
    Ingawa nimechoka
    Jambo moja li dhahiri
    Lazima nifuate barabara
    Ingawa machweo yaingia
    Nizame na kuibuka
    Nipande na kushuka.
    Jambo moja nakukumbukia:
    Mungu Je, nimwombe tena?
    Hadi lini? Labda amechoshwa na ombaomba zangu
    Nashangaa tena!
    Kitu kimoja nakiamini
    Lazima niendelee kijitahidi kwa kila hatua mpya
    Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
    Nikinaswa na kujinasua
    Yumkini nitafika mwisho wake
    Ingawa wangu mwisho haitauwahi kabla.
    (a) Eleza toni ya shairi hili.
    B)Mshairi ana maana gani anaposema "Kuwa tayari kupanda na kushuka"
    katika ubeti wa tatu?
    (c) Fafanua tamathali tano za usemi zilizotumiwa katika shairi hili
    ukizitolea mifano mwafaka.
    (d) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano wa shairi hili.
    (e) Eleza maana ya:
    (i) kuruba
    (ii) barabara yenye ukungu

    Date posted: February 7, 2018.  Answers (1)

  • Jadili maudhui ya elimu kwa mujibu wa "Kanda la Usufi", "Shaka ya Mambo" na "Tazama na Mauti(Solved)

    Jadili maudhui ya elimu kwa mujibu wa "Kanda la Usufi", "Shaka ya Mambo" na "Tazama na Mauti

    Date posted: February 7, 2018.  Answers (1)

  • Kwa kutumia mifano mwafaka eleza majukumu matano ya nyimbo katika jamii(Solved)

    Kwa kutumia mifano mwafaka eleza majukumu matano ya nyimbo katika jamii

    Date posted: February 6, 2018.  Answers (1)