Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

1. Mke wangu wameshanipoka Ndugu zangu, wamedai ububu Wazazi kuzoea kunigombeza

HATIMA YANGU
1. Mke wangu wameshanipoka
Ndugu zangu, wamedai ububu
Wazazi kuzoea kunigombeza

2. Juzi mali lilimbikiza
Furaha lilitanda
Makanwa yalijaziwa
Hoi hoi ikawa desturi

3. Kilabu tulikwenda
Nyama tulichoma
Mahali tulizuru
Tuliteremsha!

4. Leo mambo yamenigeuka
Wao masahibu siwaoni
Matumbo yakaninguruma
Kama radi ya mvua

5. Nyumbani nimebaki pweke
Mke amenitoroka
Watoto wameparara
Skuli kugharamia
Imegeuka balaa belua

6. Ndipo nimeamua
Afadhali kitanzi badala ya balaa
Kumbe kupanga ndiyo maana
Maisha na waasia


(a) Eleza mambo muhimu yanayoelezwa katika shairi hili
(b) Fafanua sifa mbili za anayezungumza katika shairi
(c) Dondoa na ufafanue mbinu zozote mbili za lugha katika shairi hili
(d) Eleza maana ya:-
(i) Ndugu zangu wamedai ububu
(ii) Kumbe kupanga ndiyo maana

Answers


Maurice
(a) (i) Amenyang’anywa mkewe
(ii) Wazazi wake wanamgombeza
(iii) Alipokuwa na mali marafiki walikuwa wengi. Alikuwa akiwapeleka marafiki klabu na
walifurahia pamoja wakichoma nyama.
(iv) Mwandishi hawaoni tena marafiki wote; wameshatoroka. Ana njaa na matatizo
mengi sana.
(v) Amebaki pweke, mke ametoroka na watoto wameparara. Mwandishi hawezi kulipa karo.
Sasa ameamua kujitia kitanzi

(b) (i) Mbadhirifu –a alitumia mali vibaya
(ii) Mpweke – Ndugu hawamsemezi anaishi upweke
(iii) Mpenda anasa =- Alikuwa akinywa pombe na kukaa sana klabuni

(c) (i) Msemo – Balaa belua
(ii) Jazanda – “Juzi” ni wakati uliopita ilhali ‘leo” ni sasa au wakati huu
(iii) Tashbihi – kama radi ya mvua

(d) (i) Ndugu zangu wamedai ububu – Ndugu zangu wamekataa kusema nami yaani hawanisemezi
kwa hali yangu mpya.
(ii) Kumbe kupanga ndiyo maana- Amegundua kuwa angepanga maisha yake tangu awali
atumie vizuri raslimali alizokuwa nazo badala ya kuzifuja
maurice.mutuku answered the question on October 9, 2019 at 06:27

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions