Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Tathmini kiwango cha matumizi ya lugha ya Kiswahili katika vituo vya redio na magazeti ya Tanzania

Tathmini kiwango cha matumizi ya lugha ya Kiswahili katika vituo vya redio na magazeti ya Tanzania

Answers


Faith
Baada ya mataifa ya Afrika Mashariki kupata uhuru.Kiswahili kilikuzwa na kuendeleza katika nyanja mbalimbali za kitaifa na kimataifa.Kila taifa lilibuni sera zake kuhusu matumizi ya Kiswahili katika miktadha tofauti tofauti. Kenya, Tanzania zilijaribu kukikuza na kuendeleza kwa kutumia katika biashara, elimu, siasa na vyombo vya habari. Kutokana na juhudi hizi Kiswahili kimeenea sana kiwango cha kuwa lugha ya taifa na lugha rasmi.

Katika vyombo vya habari, sio vyote katika nchi hizi hutumia lugha ya Kiswahili. Kwa zenye zinatumia lugha hii hukuza na kuendeleza kwa kiwango kikubwa. Dhima kuu ya vyombo vya habari ni kutoa huduma kwa jamii. Huduma hizo ni kama vile kuifahamisha na kuihamasisha jamii kuhusiana na matukio mbalimbali yanayojiri kila siku. Katika mkabala huo hujaribu kutumia lugha husika ili kukidhi mahitaji ya mawasiliano kwa wanajamii wanaolengwa. Hata hivyo ,hujaribu kutumia lugha sanifu ili kuhakikisha kuwa matumizi yake yanakuzwa kwa kuzingatia kanuni zake za kisarufi na fasihi vilevile.
Howard(2002) na Kandagor (2011) wanadai kuwa katika hali ya kawaida vyombo vya habari hufikia hadhira kubwa na huwasilisha ujumbe wa aina tofauti tofauti kuhusu nyanja tofauti za maisha.Vilevile huwafikia watu wengi kwa wakati mmoja.Vyombo vya habari vina uwezo mkubwa wa kuendeleza au kuharibu lugha. Kiswahili kinanufaika sana kutokana na jukumu muhimu linalotekelezwa na vyombo vya habari katika harakati za kukikuza, kukiendeleza na kukisambaza. Nchini hizi redio na gazeti viko katika mstari wa mbele katika kukiendeleza Kiswahili.

Vyombo vya habari ni zao la maendelezo ya sayansi na teknolojia ambalo limeadhiri na kuibadili mwelekeo wa jamii nyingi duniani. Kuanzishwa kwa redio na magazeti ya Kiswahili si tu kwamba kumeisaidia katika kuikuza Kiswahili bali kimetoa mchango mkubwa katika ujenzi wa jamii moya;yaani jamii ya wasemaji Kiswahili katika nyanja zote za maisha.Katika jamii ya sasa utandawazi ni jambo lisiloepukika. Simala(2004/2006)anaeleza kuwa kimsingi utandawazi unarejelea jumla ya maisha ya watu duniani.

Mwanasoko(1995) anadai kwamba vyombo vya habari katika kufikisha ujumbe kwa usahihi kwa watu hutegemea sana uelewa nzuri wa istilahi zinazohusiana na mada anuwai wanazozishughulikia waandishi na watangazaji wa habari.Kwa upande mwingine anasisitiza kuwa ujuzi na ufahamu wa lugha ni kipengele muhimu katika uundaji na usambasaji wa habari katika vyombo vya habari.
Kwa ujumla jambo linalokubaliwa na watu wengi kutoka nchi hizi kwamba vyombo vya habari vimetoa mchango mkubwa katika kukuza na kuendeleza Kiswahili.Hata hivyo ni vema kutaja kwamba vyombo vya habari vina umuhimu na uwezo wa kuendeleza,kukwamisha au hata kupotosha lugha husika

Titany answered the question on December 6, 2021 at 10:01

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions