-
Tumia visawe vya maneno yaliyopigwa mstari kuandika tena sentensi ifuatayo:
Ukuta umemweumiza mvulana alipokuwa akiuparaga
Date posted:
June 28, 2019
-
Andika sentensi mbili zifuatazo kama sentensi moja kwa kutumia
kiwakilishi kirejeshi.
i) duka la Bahati lina bidhaa nyingi
ii) Juma anafanya kazi katika duka la Bahati.
Date posted:
June 28, 2019
-
UFAHAMU
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Wanasaikolojia wanabainisha kati ya sehemu mbili kuu katika akili ya binadamu:
Ung’amuzi na ung’amuzibwete. Ung’amuzi ni sehemu ya ubongo ambayo kimsingi
hupanua na kudadavua yanayotendeka hususan mchana. Ung’amuzibwete ni
kibinimethali chake; hufanya kazi wakati binadamu anapolemazwa na usingizi. Baadhi
ya mambo anayoshuhudia binadamu mchana yanaingia kwenye ung’amuzibwete wake na
kutokeza katika ndoto zake usiku.
Kwa mujibu wa mawazo ya Sigmund freud, mwanasaikolojia wa jadi anayechukuliwa
nawengi kama mwasisi wa taaluma ya saikolojia, mambo yanayopatikana katika
unga’amuzibwete mambo yana sifa hasi. Freud alidahili kuwa binadamu huyaficha na
kuyabania kwenye ung’amuzibwete mambo ambayo hawezi juyasema kadamnasi.
Alieleza kuwa matamanio yasiyokubalika, makatazo ya jamii, fikra na kauli
zilizoharamishwa na miko ya kijamii hubanwa katika ung’amuzibwete. Shehena hiyo
ndiyo inayochipuza kwa njia ya ishara za ndoto, mitelezo ya kauli, yaani maneno au kauli
zinazotukoka bila wenye kukusudia, ishara na lugha ya kitamathali katika uandishi wa
kibunifu na kadhalika.
Ung’amuzibwete un uwezo mkubwa wa kuathiri matendo ya binadamu. Huu ndio
msingi unaowafanya wanasaikolojia wengi, akiwepo freud, kusema kuwa tajiriba ya
motto inaweza kufichwa kwenye sehemu hiyo na hatimaye kuishia kutokeza katika utu
uzima wake. Kwa kuwa tunapoingiliana na binadamu wenzetu kila siku
tunayang’amuzibwete unapotawala binadamu wenzetu watashindwa kutuelewa. Hii
ndiyo hali anayokuwa nayo mwendawazimu. Ung’amuzibwete wake hutawala. Sisi
tunaotawaliwa na ung’amuzi tunashindwa kumwelewa; naye bila shaka anashindwa
kutuelewa.
Carl Gustav Jung, aliyewahi kuwa mwanafunzi wa Freud, aliupinga mwelekeo wa Freud
wa kuungalia ung’amuzibwete kama jaa la mawazo mabaya, matamanio, nia, fikira tuli
na dhana ambazo ni hasi. Jung alizuka na dhana mbili muhimu: Ung’amuzibwete wa
kibinafsi na un’gabuzibwete jumuishi. Alisema mambo, fikra na uzoefu wowote mbaya
unaomuhusu mtu binafsi . Dhana ya ung’a muzibwete jumuishi aliitumia kuelezea
sehemu ya akili ya binadamu ambayo inamfanya ayatende matendo Fulani kama
binadamu wenzake licha ya tofauti zao kiwakati na kijiografia. Kwa mfano, binadamu
wengi wana sherehe za kuzaliwa motto, kuoza, ibada au mviga unaohusiana na kifo licha
ya tofauti zao. Jung alisema kuwa kinachochochea hali hii ni urithi Fulani wa kila
mwanadamu. Urithi huo unapatikana katika ung’amuzibwete jumuishi.
Upo mwafikiano kati ya wataalamu hawa wawili kuwa ung’auzibwete una uwezo wa
kuathiri ung’amuzi matendo ya binadamu ya king’amuzi. Wanasaikolojia wanashikilia kuwa binadamu hawezi kukamilika bila kuzihusisha sehemu zote mbile kwa sababu
zinaathiriana.
a) Kwan in ung’amuzibwete unaelezwa kama kinyme cha ung’amuzi?
b) Eleza mtazamo wa Freud kuhusu ung’amuzibwete.
c) Kwa mujibu wa Freud yaliyomo kwenye ung’amuzibwete hudhihirika vipi?
d) Eleza tofauti ya mawazo kati ya Sigmund Freud na Carl Gustav Jung.
e) taja hoja inayowafungamanisha Jung na Freud.
Date posted:
June 28, 2019
-
ISIMU JAMII
Soma kifungu kifuatacho ujibu maswali yanayofuata.
Kwa mujibu wa sheria kifungu nambari 3 sehemu ya A ya sheri za nchi, umepatikana na
hatia ya kutatiza utulivu wa raia wapenda amani kwa kuwatusi na kutisha kuwapiga.
Kiongozi wa mashtaka amethibitisha haya wa kuwaleta mashahidi ambao wametoa
ushahidi usiotetereka kuhusu vitendo vyako katika tukio hilo. Korti hii imeonelea una
hatia na imeamuru ufungwe jela kwa muda wa miaka miwili bila faini ili liwe funzo
kwako na kwa wenzako wenye tabia kama zako. Una majuma mawili kukata rufani.
a) Lugha iliyo katika kifungu hiki hutumika katika muktadha upi?
b) Toa ushaidi wa jibu lako
c) Zaidi ya sifa zilizo katika kifungu hiki, eleza sifa zingine sita za matumizi ya
ligha katika muktadha huu.
Date posted:
June 28, 2019
-
Eleza matumizi ya “na” katika sentensi:
Sofia na Raeli wanaandaliwa chai na mpishi
Date posted:
June 28, 2019
-
Andika udogo na ukubwa wa neno ‘kiti’
Date posted:
June 28, 2019
-
Eleza matumizi ya ritifaa katika: ‘N” shamchukua
Date posted:
June 28, 2019
-
Tunga sentensi kuonyesha tofauti kati ya vitate vifuatavyo
Suku na zuka
Date posted:
June 28, 2019
-
Andika katika msemo wa taarifa. “Sitathubutu kumpa pesa zangu” Mkolwe
alisema.
Date posted:
June 28, 2019
-
Sahihisha sentensi:
Mtoto ambaye niliyemsomesha ameasi jamii
Date posted:
June 28, 2019
-
Andika kinyume cha:
Mwise alikunja nguo alizokuwa ameanika
Date posted:
June 28, 2019
-
Unganisha sentensi zifuatazo ukitumia neno “japo”
i) Selina alijitahidi sana .
(ii) Selina hakushinda mbio hizo
Date posted:
June 28, 2019
-
Onyesha hali katika sentensi zifuatazo:
i) Henda mvua ikanyesha leo.
ii) Miti hukatwa kila siku duniani.
Date posted:
June 28, 2019
-
Unda nomino kutokana na vitenzi:
i) Chelewa
ii) Andika
Date posted:
June 28, 2019
-
Bainisha Kirai Nomino na Kirai Tenzi katika sentensi:
Jirani mwema alinipa chakula
Date posted:
June 28, 2019
-
Tunga sentensi moja ukitumia neno “seuze”
Date posted:
June 28, 2019
-
Sentensi hizi ni za aina gani?
i) Lonare anatembea kwa kasi.
ii) Halima anaandika hali Ekomwa anasoma
Date posted:
June 28, 2019
-
Andika sentenzi zifuatazo kulingana na maagizo uliyopewa
i) Mhunzi mrefu alishinda tuzo (Anza kw: tuzo…
ii) Mwanafunzi huyu anasoma Kifaransa. (Anza kwa kiashiria kisisitizi)
Date posted:
June 28, 2019
-
Kitenzi fumbata kiko katika hali (kauli) ya?
Date posted:
June 28, 2019
-
Kanusha sentensi ifuatayo:
Ningalikuwa na pesa ningalinunua nyumba
Date posted:
June 28, 2019
-
Taja sauti mbili zinazotamkiwa midomoni.
Date posted:
June 28, 2019
-
Onyesha viambishi awali na tamati katika kitenzi: Alimchezea
Date posted:
June 28, 2019
-
Tunga sentensi inayodhihirisha matumizi ya ngeli ya I – I
Date posted:
June 28, 2019
-
MUHTASARI
Ajira ya watoto ni tatizo sugu linalokumba ulimwengu wa sasa , hasa katika nchi
zinazozoendelea. Jambo la kusikitisha ni kwamba hivi ndivyo ilivyo katika nchi nyingi
za ulimwengu huu. Kuna idadi kubwa ya watoto wanaoajiriwa katika nyanja mbalimbali
za jamii. Zipo sababu nyingi zinazowasukuma watoto kutafuta ajira barani Afrika kwa
mfano, familia nyingi huishi maisha ya ufukara hivi kwamba hushindwa kuyatimiza
mahitaji muhimu hususan kwa watoto. Kapanda kwa gharama ya maisha kunazidisha
viwango vya umaskini. Ukosefu wa lishe pia huwafanya watotto kutoroka nyumbani
kutfuta ajira. Janga la UKIMWI limesababisha kuwepo kwa idadi kubwa ya mayatima
wanaoshia kutafuta ajira ili kuyakimu maisha. UKIMWI umezifanya nyingi pia
kuwaondoa watoto shule ili waweze kuajriwa kwa lengo la kuanzisha pato la familia
hizo. Watoto wengine hutoroka makwao kwa sababu ya maonevu. Maonevu haya ni
kama vile kupigwa, kutukanawa kila wakati, kunyanyaswa kijinsia na kadhalika. Huko
nje hutaabishwa kimwili na kiakili. Hufanyishwa kazi za sulubu zenye malipo duni au
wasilipwe kabisa. Hili huwasononeshe na kuathiri afya yao.
Uundaji wa Umoja wa Afrika hivi majuzi ni hatua muhimu ya kushughulikia matatizo ya
Afrika kama vile ajura ya watoto, kuzorota kwa miundo msingi, magonjwa, njaa,
umaskini, ufisadi na ukabila. Katika kushughulikia haki za watoto, nchi za Afrika hazina
budi kuzingatia masharti yalivyowekwa na Umuja wa Mataifa kuhusu haki za watoto.
Nchi nyingi za Afrika ziliidhinisha mkataba wa marsharti hayo ikiwemo inchi ya Kenya.
Nchi hizi basi lazima zishughulikie haki za watoto kupitia sheria za nchi. Watoto ni
rasilimali muhimu na ndio tumaini la kuwepo kwa kizazi cha binadamu.
a) Eleza mambo yote muhimu anaazungumzia mwandishi katika aya ya kwanza
(maneno 45-50) (alama 7, 1 ya utiririko)
Matayarisho
Jibu
b) Bila kubadilisha maana aliyokusudia mwandishi, fupisha aya mbili za mwisho
(maneno 50-55) (alama 8, 1 ya utiririko)
Matayarisho
Jibu
Date posted:
June 28, 2019
-
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Ulimwengu unapaswa kuzuka na mbinu za Kulitadarukia tatizo la umaskini ambao
unakwamiza juhudi za maendeleo. Umaskini unaoyakabili mataifa yanayoendelea.
Unayatosa kwenye dhiki kubwa huku mataifa ya kimagharibi yakitpiga hatua kubwa
kimaendeleo. Ufa uliopo baina ya mataifa yanayoendelea na yalo yaliyoendelea kama
vile Marekani, nchi za Ulaya na Ujapani unapanuka kila uchao.
Vyanzo vya umaskinin huu ni anuwai mathalan, ufusadi, uongozi mbaya, turathi za
kikoloni, uchumi kuegemea mvua isiyotabarika, idadi ya watu inayoupik uwezo wa
uchumi wa taifa linalohusika na ukosefu wa nyenzo na amali za kuwakwamua raia
kutoka lindi la umaskini. Ukosefu adimu za ajira huchangia pia katika tatizo hili.
Jamii ya ulimwengu inapaswa kuelewa kuwa umaskini unaoathiri nchi Fulani una athari
pan asana. Uvunigu unaotokana na umaskini unaweza kuweza kuwa mboji ambako
matendo ya kihalifu ili kujinasua kutoka dhiki ile. Hii inaweza kuwa mbegu ya kuatika
maovu kama ugaidi na uhalifu wa kila aina.
Mataifa ya magharibi yanapaswa kuyaburai madeni mataifa yanayoendelea kama njia
mojawapo ya kupambana na umaskini. Asilimia kubwa ya pato la kitaifa katika mataifa
mengi hutumika kuyalipa madeni hayo. Katika hali hii inakuwa muhali kwa mataifa hayo
kujikwamua kutokana na pingu za umaskini. Njia nyingine ni kustahabu kutoa ruzuku za
kimaendeleo badala ya mikopo kwa nchi zinazoendelea.
Kwa upande wake, mataifa yanayoendelea yanapaswa kuibuka na mikakati bora ya
kupambana na umaskini. Ni muhimu pawepo na sera zinazotambua ukweli kuwa
asilimia kubwa ya raia wa mataifa hayo ni maskini. Pana dharural ya kuzalisha nafasi za
ajira, kupanua viwanda hususan vinavyohusiana na zaraa ambayo ni tegemeo kuu la
mataifa mengi, kuendeleza elimu na kuimarisha miundo msingi. Ipo haja pia ya mataifa
haya kuhakikisha kuwa mfumo wa soko huru unaotawala ulimwengu sasa huishii kuwa
chanzo cha kufa kwa viwanda asilia na kuendeleza masikini zaidi. Kwa ufupi, maamuzi
yote ya sera za kiuchumi lazima yazingatie uhalishi wa maisha ya raia wa mataifa hayo.
a) Kwa nini umaskini umetamalaki katika mataifa yanayoendelea?
b) Madeni yana athari gani kwa mataifa yanayoendelea?
c) Ni mapendekezo yapi ambayo mwandishi anatoa kwa mataifa machanga kuhusu
utatuzi wa tatizo la umaskini?
d) Mfumo wa soko huru una mathara gani kwa mataifa machanga?
e) Ukirejea kifungu, eleza maana ya:
i) Kulitadarukia
ii) Kuatika
iii) Kuyaburai madeni
Date posted:
June 28, 2019
-
Mbuni huzaa matunda gani?
Date posted:
June 28, 2019
-
Haya ni magonjwa gani?
I Matubwitubwi
II Tetewanga
Date posted:
June 28, 2019
-
Kati ya madini haya taja yale yanayopatikana baharini
Zinduna Zebaki
Lulu Ambari
Yakuti Marumaru
Date posted:
June 28, 2019
-
Jaza jedwali
Kiume Kike
Mjakazi
Jogoo
Fahali
Date posted:
June 28, 2019
-
Eleza maana ya:
(i) Sina pa kuuweka uso wangu
(ii) Ana mkono wa buli
Date posted:
June 28, 2019