-
Tumia neno “ngali” kutunga sentensi kuonyesha
(i) Kitenzi kisaidizi
(ii) Kitenzi kishirikishi
Date posted:
October 8, 2019
-
Tunga sentensi ukitumia neno ganda katika kauli ya kutendana.
Date posted:
October 8, 2019
-
Tofautisha sentensi zifuatazo kwa kutia shadda
Wataka kazi
Wataka kazi
Date posted:
October 8, 2019
-
Andika mifano ya sauti zenye sifa zifuatazo:
(i) Kipasuo cha kaakaa laini
(ii) Nazali ya ufizi
Date posted:
October 8, 2019
-
Maneno hayo yako katika ngeli gani?
(i) Ridhaa
(ii) Nanasi
Date posted:
October 8, 2019
-
Andika maana mbili za sentensi:
Nenda ukamwone mwenyewe, usiogope.
Date posted:
October 8, 2019
-
Kuza sentensi ifuatayo.
Nguo iliyoraruka itashonwa tena na fundi
Date posted:
October 8, 2019
-
Tumia neno “haraka” katika sentensi kama:
(i) Nomino
(ii) Kielezi
Date posted:
October 8, 2019
-
Andika maana mbili za neno mradi.
Date posted:
October 8, 2019
-
Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo.
Mtoto alipikiwa uji na mamake jana jioni kwa jiko.
Date posted:
October 8, 2019
-
Chai hiyo iliwavutia watalii (Anza : Watalii…………..)
Date posted:
October 8, 2019
-
Neno “mlango” lina maana ya “uwazi wa kuingilia nyumba.” Tunga sentensi mbili
kubainisha matumizi mawili ya neno hili
Date posted:
October 8, 2019
-
Andika sentensi tatu ambazo zaweza kuwa sahihisho la sentensi hii
Pale ndiko alimoingia
Date posted:
October 8, 2019
-
Tambua mzizi katika neno:
Tuliwalimia
Date posted:
October 8, 2019
-
Tumia kiulizi kifaacho kukamilisha maswali yafuatayo:
(i) Waashi wale wanaishi kwa
(ii) Mtoto alitaka majina…
(iii) Wanitania hivyo
Date posted:
October 8, 2019
-
Bainisha viwakilishi katika sentensi kisha useme ni vya aina gani.
i) Mimi nitaondoka kesho
(ii) Huyo alichaguliwa na wengi
Date posted:
October 8, 2019
-
Panga nomino hizi katika ngeli mwafaka
(i) Kipofu- .
(ii) Uyoga- .
Date posted:
October 8, 2019
-
Eleza maana ya misemo:
(i) Fuga mtu –
(ii) Kuwa na faragha -
Date posted:
October 8, 2019
-
Onyesha maana mbili ya neno taka
Date posted:
October 8, 2019
-
Kanusha sentensi ifuatayo kwa udogo
Mbuzi wake ana manyoya mengi na harufu kali
Date posted:
October 8, 2019
-
Bainisha kishazi huru na kishazi tegemezi katika sentensi ifuatayo
Darasa lililojengwa limefunguliwa rasmi
Date posted:
October 8, 2019
-
Andika usemi huu kwa usemi wa taarifa
“Kefule! Mtoto huyu ni kaidi kama kirongwe. Hamheshimu babake!” alisema mzee Kamau.
Date posted:
October 8, 2019
-
Kamilisha na kueleza maana ya methali hii
Mfinyanzi -...........
Date posted:
October 8, 2019
-
Irabu a, i, na u hutamkwa wapi kwenye ulimi?
Date posted:
October 8, 2019
-
Kwa kutoa mifano, onyesha namna mbili vile kiambishi –j- hutumiwa
Date posted:
October 8, 2019
-
Eleza maana mbilimbili za sentensi zifuatazo;
(i) Bibi yake amefika
(ii) Alimpigia mpira
Date posted:
October 8, 2019
-
Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi
Abiria waliojeruhiwa sana walipelekwa hospitali haraka
Date posted:
October 8, 2019
-
Andika vinyume vya vitenzi vilivyopigwa mistari
(i) Alikashifiwa kwa kazi aliyofanya
(ii) Kuimba kulifurahisha hadhira
Date posted:
October 8, 2019
-
Wafuatao wana ulemavu upi?
(i) Toinyo
(ii) Huntha
Date posted:
October 8, 2019
-
Kati ya nomino za Kiswahili taja ngeli mbili ambazo nomino zake hazibadiliki katika umoja
na katika wingi. Kisha utoe mfano mmoja kwa kila ngeli
Date posted:
October 7, 2019