-
Geuza kwa wingi.
i. Njia hii huenda Kisumu
ii. Wembe huu utafaa.
Date posted:
November 25, 2022
-
Ainisha sentensi hii:
Kilichopikwa
Date posted:
November 25, 2022
-
Andika maneno yaliyo na aina za silabi zifuatazo:
i. Silabi za irabu pekee
ii. Silabi za konsonanti, nusu irabu na irabu
iii. Silabi za konsonanti pekee
Date posted:
November 25, 2022
-
SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI.
Malezi mema
Malezi bora si yale, mtoto kumdekeza
Atafikia kilele, mzazi atampuza
Utapiga makelele, wala hatasikiza.
Daima usikubali, kuridhi kumpendeza
Lazima uwe mkali, mengine kumkataza
Na wala usikubali, maneno kuyaigiza.
Mtoto ukimuita, hana budi kuginiza
Sio mdomo kufyata, mamboye kuendeleza
Ama dakika zapita,aje ikimpendeza.
Mzazi usithubutu,mwanao kumteteza
Uambiwapo na watu, mwanao alifanyiza
Kuwa na hali ya utu, Kadhia kuchunguza.
Iwapo amekusudi, makossa kuyatimiza
Kumrudi huna budi,jukumu kutekekeza
Lau usipomrudi, kosa taliendeleza.
Maswali
a) Eleza malezi mema jinsi yanavyosimuliwa na mshairi.
b) Taja mambo matano wanayoshauriwa wazazi kutoyatenda
c) Je, mzazi asipochukua jukumu lake, kuna athari gani kwa mtoto
d) Toa methali moja inayoambatana na ujumbe wa Shairi hili
e) Shairi hili lina mishororo ngapi
f) eleza vina,vipande na mizani vya Shairi hili
g) eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika Shairi.
i. kumdekeza
ii. kuginiza
iii. mdomo kufyata
iv. alofanyiza
v. lau usipomrudi
Date posted:
November 25, 2022
-
“nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayuko"
i. tambua kipera hiki
ii. taja dhima moja ya kipera hiki kijumla
Date posted:
November 25, 2022
-
Matumizi ya lugha hutegemea mambo kadhaa. Yaeleze yoyote manne.
Date posted:
November 25, 2022
-
Tunga sentensi moja na uonyeshe kiwakilishi kimilikishi.
Date posted:
November 25, 2022
-
Kwa kutumia sentensi moja onyesha vitenzi sambamba.
Date posted:
November 25, 2022
-
Tunga sentensi moja na uonyeshe nomino dhahania.
Date posted:
November 25, 2022
-
Tambua sauti yenye sifa zifuatazo.
konsonanti, kipasuo, ghuna, sauti ya mdomo.
Date posted:
November 25, 2022
-
Taja ala sogezi mbili za kutamkia.
Date posted:
November 25, 2022
-
Taja vipera vitano vya semi.
Date posted:
November 25, 2022
-
Kamilisha methali ifuatayo.
Asiye na nadhari...
Date posted:
November 25, 2022
-
Kanusha sentensi katika hali ya kuamrisha wingi.
Kimbia haraka –
Amka -
Date posted:
November 25, 2022
-
Tunga sentensi yenye kivumishi cha jina.
Date posted:
November 25, 2022
-
Tambulisha na ufafanue viambishi vilivyotumika katika Anamfundisha.
Date posted:
November 25, 2022
-
Huku ukitoa mifano taja miundo ya silabi.
Date posted:
November 25, 2022
-
Taja nomino zozote mbili katika ngeli A-WA na uonyeshe miundo yake.
Date posted:
November 25, 2022
-
Andika udogo wa:
Anacheza ngoma.
Date posted:
November 25, 2022
-
Tumia kiunganishi kifaacho kuunganisha sentensi hizi.
Mwizi alishikwa. Mwizi alipigwa sana.
Date posted:
November 25, 2022
-
Bainisha aina za vielezi katika sentensi hii.
Mtoto alikimbia mara sita uwanjani kisha akatembea kitausi.
Date posted:
November 25, 2022
-
Tunga sentensi yenye kitenzi kishirikishi kipungufu.
Date posted:
November 25, 2022
-
Tunga sentensi katika wakati uliopita hali timilifu.
Date posted:
November 25, 2022
-
Andika sauti zenye sifa zifuatazo:
(i) Nazali ya kaa laini
(ii) Kikwamizo ghuna cha mdomo na meno
(iii) Irabu ya nyuma wastani
(iv) Kimadende
Date posted:
November 25, 2022
-
Soma shairi ifuatayo kisha ujibu maswali
CHEMA HAKIDUMU
Chema hakidumu, kingapendekeza,
Saa ikitimu, kitakuteleza
Ukawa na hamu, kukingojeleza,
Huwa ni vigumu, kamwe hutaweza
Chema sikiimbi, kwamba nakitweza
Japo mara tumbi, kinshaniliza,
Na japo siombi, kipate n’ongeza,
Mtu haniambi, pa kujikimbiza
Chema mara ngapi, kinniondoka,
Mwanangu yu wapi? Hakukaa mwaka,
Kwa muda mfupi aliwatilika,
Ningefanya lipi, ela kumzika?
Chema wangu babu, Kibwana Bashee,
Alojipa tabu, kwamba anilee
Na yakwe sababu, ni nitengenee,
Ilahi Wahhabu, mara amtwee.
Chema wangu Poni, kipenzi nyanyangu,
Hadi siku hini, yu moyoni mwangu,
Yu moyoni ndani, hadi kufa kwangu,
Ningamtamani, hatarudi kwangu.
(Abdalla, Abdilatif, Sauti ya Dhiki)
MASWALI:
(a) Hili ni shairi la aina gani?
(b) Taja na ueleleze aina zozote mbili za bahari katika shairi hili.
(c) Eleza umbo la shairi hili.
Date posted:
November 25, 2022
-
Nyambua
Filisisha (tenda)
Date posted:
November 24, 2022
-
Tumia kitenzi jina na kivumishi kutunga sentensi.
Date posted:
November 24, 2022
-
Andika sentensi hii katika ukubwa.
Huyo nyoka alikatwa mkia na mvulana yule.
Date posted:
November 24, 2022
-
Taja visawe vya maneno yafuatayo.
(i) Damu
(ii) Mjinga
Date posted:
November 24, 2022
-
Andika katika udogo na wingi
Njusi aliyekuwa na jicho moja alianguka mtoni.
Date posted:
November 24, 2022