-
Tunga sentensi moja moja kudhihirisha ngeli zifuatazo:-
(i) U-U
(ii) Pokomo /Pa-ku-mu
Date posted:
October 5, 2019
-
Andika sifa bainifu za sauti
(i) e:-
(ii) n:-
Date posted:
October 5, 2019
-
Andika kwa udogo:-
Gari la Mzee Maritu limegonga ng’ombe wa jirani wake
Date posted:
October 5, 2019
-
Geuza zentensi zifuatazo katika kauli kwenye mabano:-
(i) Fundi ameharibu saa (kutendea)
(ii) Umemwona mgeni? (kutendewa)
Date posted:
October 5, 2019
-
Tunga sentensi ukitumia mzizi – choyo kama :-
(i) nomino
(ii) Kivumishi
(iii) Kiwakilishi
Date posted:
October 5, 2019
-
Bainisha aina za nomino zilizopigiwa mistari katika sentensi hii:-
Uhodari wa wanariadha wa Kenya unahitajika kote duniani
Date posted:
October 5, 2019
-
Eleza maana ya ‘jinsi’ kama inavyojitokeza katika sentensi zifuatazo
(i) Naomba unionyeshe jinsi ya kuendesha gari
(ii) Wakenya hawapendezwi na jinsi viongozi wanavyoendeleza ufisadi
Date posted:
October 5, 2019
-
Eleza mambo matano yaliyochangia kuenea kwa Kiswahili nchini kabla na baada ya uhuru
Date posted:
October 5, 2019
-
Unganisha sentensi hizi ukitumia kiunganishi cha kinyume:
Wananchi walikabiliwa na hatari
Wananchi waliendelea kuwaokoa majeruhi
Date posted:
October 5, 2019
-
Unda nomino moja moja kwa kila kitenzi
Shuku
Vumilia
shona
lia
Date posted:
October 5, 2019
-
Tunga sentensi moja kuonyesha tofauti ya maana kati ya ‘guna’ na ‘kuna’
Date posted:
October 5, 2019
-
Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mishale/mistari:-
Watoto wote wameamka mapema na wazazi wanatayarisha staftahi
Date posted:
October 5, 2019
-
Tunga sentensi yenye kiigizi na kihusishi cha mahali
Date posted:
October 5, 2019
-
Bainisha shamirisho kipozi, kitondo na ala katika sentensi ifuatayo:-
Maksuudi alimjengea Tamima Kasri kwa matofali mazuri
Date posted:
October 5, 2019
-
Tunga sentensi moja ukitumia kinyume cha neno ‘lewa’.
Date posted:
October 5, 2019
-
Eleza matumizi ya ‘ji’ katika sentensi hii:
Mwimbaji amejikata jidole lake kwa jiwe
Date posted:
October 5, 2019
-
Tunga sentensi ukitumia kitenzi ‘pwa’ katika kauli ya kutendea
Date posted:
October 5, 2019
-
Andika kwa ukubwa wingi:
Mke wa mzee huyu hupenda mtoto huyu sana.
Date posted:
October 5, 2019
-
Yakinisha sentensi ifuatayo:-
Chakula hakipikiki vizuri
Date posted:
October 5, 2019
-
Andika katika hali ya mazoea:
Mtambo ambao unakarabatiwa leo utatufaa
Date posted:
October 5, 2019
-
Tunga sentensi moja kubainisha kiwakilishi kiambata nafsi ya kwanza wingi
Date posted:
October 5, 2019
-
Tumia viunganishi vifuatavyo katika sentensi:-
(i) Minghairi ya
(ii) Wala
Date posted:
October 5, 2019
-
Onyesha viwakilishi katika sentensi zifuatazo kisha ueleze ni vya aina gani:-
i) Unamjua vyema kweli?
(ii) Hicho wanachokitaka hakipo
Date posted:
October 5, 2019
-
Pambanua viambishi mbalimbali katika sentensi ifuatayo
Waliwapendezea
Date posted:
October 5, 2019
-
Tungia vitenzi vifuatavyo sentensi katika hali zilizobanwa:-
(i) Fa(mazoea)
(ii) La(kutendeka)
(iii) Pa (kutendea)
Date posted:
October 5, 2019
-
Changanua kwa njia ya mishale
Mama anapika na baba akisoma gazeti
Date posted:
October 5, 2019
-
Akifisha sentensi ifuatayo:-
Sijaona kitabu kizuri kama mayai waziri wa maradhi, utaniazima siku ngapi bashiri
alimwuliza rita
Date posted:
October 5, 2019
-
Andika katika usemi halisi:-
Mama aliwahimiza warudi siku hiyo la sivyo wangekosa tuzo
Date posted:
October 5, 2019
-
Eleza matumizi mawili ya “ka“ na utunge sentensi kwa kila mojawapo
Date posted:
October 5, 2019
-
Unganisha sentensi hii kwa kutumia ‘O’ rejeshi :-
Wavu umekatika. Wavu ni wao
Date posted:
October 5, 2019