-
Tumia “O” rejeshi katika sentensi hii.
Mwanafunzi ambaye hudurusu ndiye hupita mtihani.
Date posted:
October 8, 2019
-
Eleza maana mbili za:
Mwandishi alikwenda sokoni peke yake.
Date posted:
October 8, 2019
-
“Avunjaye nazi ni lazima afaidi tui."
Eleza maana ya methali hii
Date posted:
October 8, 2019
-
Bainisha maneno yafuatayo yapo katika ngeli gani kisha tunga sentensi mwafaka:
(i) Manukato
(ii) Uwati
Date posted:
October 8, 2019
-
Sahihisha sentensi zifuatazo
(i) Mtoto ambaye aliyekuwa anacheza ameanguka.
(ii) Vitabu hizi ambazo zimesahihishwa ni za wanafunzi.
Date posted:
October 8, 2019
-
Neno kijana linaweza kutumiwa kama kivumishi au nomino, tunga sentensi kudhihirisha
(i) Kivumishi
(ii) Nomino
Date posted:
October 8, 2019
-
Tunga sentensi moja inayojumulisha sehemu hizi, Ala, kipozi, kitondo na chagizo
Date posted:
October 8, 2019
-
Ainisha mofimu zinazojitokeza katika kitenzi hiki
Waliochekeshwa
Date posted:
October 8, 2019
-
Changanua sentensi ifuatayo ukitumia matawi
Mzee ambaye hukuza pamba amefaidika sana
Date posted:
October 8, 2019
-
Andika sentensi ifuatayo katika hali ya udogo wingi
Njia nyembamba ni hatari kwa usafiri wa gari
Date posted:
October 8, 2019
-
Tunga sentensi mbili kutofautisha matumizi ya vitate hivi: Dua na tua
Date posted:
October 8, 2019
-
Tofautisha kati ya sauti ghuna na sauti si ghuna huku ukitolea mifano miwili kwa kila aina
Date posted:
October 8, 2019
-
Yakinisha sentensi ifuatayo :
Mama hakutuchapa, hakutupa chakula wala maji
Date posted:
October 8, 2019
-
ISIMU JAMII
Jadili mambo yanayotatiza kuenea kwa Kiswahili kabla ya 1962 nchini Kenya.
Date posted:
October 8, 2019
-
Eleza matumizi ya ‘ka’ na ‘hu’ katika sentensi zifuatazo.
(i) Nilienda kanisani nikamkuta, nikamwamkua, nikamwomba msamaha.
(ii) Baba hufika nyumbani usiku wa manane
Date posted:
October 8, 2019
-
Tumia ‘O’ rejeshi tamati
Nguo iliyonunuliwa si ile uliyoitaka
Date posted:
October 8, 2019
-
Andika sentensi ifuatayo upya kwa mwanzo wa kiwakilishi
Mama huyu anapika wali
Date posted:
October 8, 2019
-
Tambua aina mbili ya virai katika sentensi ifuatayo
Mwanafunzi shupavu aliponea chupuchupu
Date posted:
October 8, 2019
-
Akifisha
je, unaipenda hali ilivyo mwenzake alitaka kujua
Date posted:
October 8, 2019
-
Tambua mofimu katika neno lifuatalo
Waimbao
Date posted:
October 8, 2019
-
Linganisha na ulinganue sauti /k/na/g/
Date posted:
October 8, 2019
-
Tunga sentensi sahihi ukitumia vitenzi
(i) Kishirikishi kipungufu
(ii) Kikuu
Date posted:
October 8, 2019
-
Tambua aina ya nomino katika utungo ufuatao.
Mji wa sokomoko una masaibu mengi
Date posted:
October 8, 2019
-
Kanusha
Nikimwona ndugu yangu nitamjulisha habari hizi
Date posted:
October 8, 2019
-
Tambua matumizi ya ni – katika sentensi hii
Mwanafunzi ni mtukutu
Ameenda ibadani
Date posted:
October 8, 2019
-
Changanua kwa jedwali
Chakula ambacho kilipikwa vizuri kimeliwa na watu wote
Date posted:
October 8, 2019
-
Tumia kirejeshi kuonyesha mazoea katika sentensi ifuatayo:
Mtoto anayelia ni huyu
Date posted:
October 8, 2019
-
Unda kitenzi kutokana na neno bora na utunge sentensi katika hali ya wingi.
Date posted:
October 8, 2019
-
Yakinisha katika nafsi ya pili umoja
Tusipoonana na mgeni hatutafaidi
Date posted:
October 8, 2019
-
Eleza maana mbili ya sentensi ifuatayo.
Askari alimkimbilia mwizi.
Date posted:
October 8, 2019