Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Jadili maudhui ya elimu kwa mujibu wa "Kanda la Usufi", "Shaka ya Mambo" na "Tazama na Mauti

      

Jadili maudhui ya elimu kwa mujibu wa "Kanda la Usufi", "Shaka ya Mambo" na "Tazama na Mauti

  

Answers


gregory
? Shule imesawiriwa kama mahali pa kuadilisha wanafunzi.
? Kuhakikisha kuwa wanafunzi wamo katika hali nzuri ya kiafya ili kuendeiea
katika masomo -mfano - desturi ya shule ya Askofu Timotheo kuwachunguza
wasichana wote kama wana mimba.
? Matokeo ya vitendo vya wanafunzi yanadhihirika katika hadithi tofauti.
Katika Kanda la Usufi, Sela na Masazu hawafanyi vyema kwenye mtihani
? Katika Tazamana na Mauti, ukosefu wa hamu ya masomo unamfanya Lucy
asifanye vyema kwenye mtihani.
? Wazazi hukatatam-aa watoto wao wanapoenda kinyume na matarajio yao.
? Elimu pia humpa binadamu uhuru kujipangia mustakabadhi wake.
? Masazu anapata kazi ya kijungu jiko huku Sela akitamani kumchukua mtoto
wake ajilele kwa vile hakuwa na la kufanya Masazu anapoenda kazini
? Katika Kanda la Usufi imeelezwa kuwa wasichana walitarajiwa kuendeleza
shughuli zao kwa utulivu na ustaarabu huku wakizingatia maadili ya hali ya
juu. Elimu pia inatarajiwa kuwapa wanafunzi nafasi ya kukuza vipaji vyao
na kuingiliana ili kuelewana zaidi.
? Jukumu la mwanafunzi katika masomo limejitokeleza Bi Margaret mwalimu
mkuu wa shule ya Askofu Timotheo anapowahutubia wanafunzi na kusisitiza
uwajibikaji katika vitendo vyao.
? Katika Tazamana na Mauti Lucy anaamini kuwa jiji hili lina raha kamili bila
karaha.
? Anategemea mzungu atakayemwoa na kumpeleka London na baadaya
kufika London akaanza kutegemea kifo cha Bw. Crusoe ambacho kingempa
urithi na raha aliyotaka maishani
? Hili linadhihirika wakati mzee Butali anapomwuliza mwalimu kwa nini
wazazi huwapeleka watoto shuleni.
? Ukosefu wa elimu umeonyeshwa kama mojawapo ya njia zinazowapa vijana
mitazamo finyu kuhusu maisha.
? Esther katika Shaka ya Mambo alijua alichokuwa akitafuta.
? Kwa upande mwingine mustakabali wa Lucy ulitegemea wengine.
? Alikuwa amepanga ni kwa muda gani angeendelea kufanya kazi jinsi
atakavyopanga wakati wake baada ya kujiunga na chuo kikuu na
anachotaka kusomea.
gregorymasila answered the question on February 7, 2018 at 12:57


Next: How is the image on a pin hole camera increased?
Previous: Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. T. Arege: Barabara Barabara bado ni ndefu Nami tayari nimechoka tiki Natamani kuketi Ninyooshe misuli Nituliza akili. Lakini Azma yanisukuma Mbele ikinihimiza kuendelea Baada ya miinuko...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Kwa kutumia mifano mwafaka eleza majukumu matano ya nyimbo katika jamii(Solved)

    Kwa kutumia mifano mwafaka eleza majukumu matano ya nyimbo katika jamii

    Date posted: February 6, 2018.  Answers (1)

  • Ili kuweza kufanikisha uwasilishaji wa utanzu wa nyimbo kwa hadhira eleza mambo anayohitaji mwimbaji.(Solved)

    Ili kuweza kufanikisha uwasilishaji wa utanzu wa nyimbo kwa hadhira eleza mambo anayohitaji mwimbaji.

    Date posted: February 6, 2018.  Answers (1)

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Kilio cha Lugha Ni wimbo najiimbia, nijiliwaze Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi Lugha ya...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
    Kilio cha Lugha
    Ni wimbo najiimbia, nijiliwaze
    Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
    Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
    Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia
    Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa
    Hamna nami imani, wala kupanga siasa,
    Mwasema sayansini, siku ningalitosa,
    Mwanambia nikotosa, kuiva sijafika.
    Ela muelewe sana, Maamuma na Imamu,
    Mulipokuwa vijana, kwenu nilikuwa timamu,
    Sasa mumesoma sana, mwaniona ni haramu,
    Mujue kuwa dawamu, utumwa mwauridhia.
    Mzaliwapo mwalia, 'maa', maneno ya kwanza,
    Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza,
    Wa lugha muwedoria, muweze na kuikuza,
    Sio kujipendekeza, uzungu kuigiza.
    Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza,
    Lugha mulithamini, Kiswahili kufukiza,
    Hata kule risavuni, kizungu hanikuwaza,
    Sasa mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia?
    Sayansi sio asili, msamiatiwe sinao,
    Sayansi yataka mbali, msamiati ni wa hao
    Nitakuwa Kiswahili, kiomba majina yao
    Lugha kujikuza kwao, huomba linalofaa.
    Enyi viongozi wetu ipangeni nadharia,
    Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria
    Lugha hata 'mbusha watu, tuche kuriaria,
    Sifa ni kwa chake mtu, cha mwenzi hutoringia.
    Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote,
    Msamiati huwa, ni wa Afrika yote,
    Na methali za kuasa, nahau na ngeli zote,
    Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilika.
    Afrika ndipo petu, pa wabantu halisi,
    Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi,
    Warabu na wengi wetu, sio wangu Adinasi
    Kwao 'meomba kiasi, ili kujizidisha.
    Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya,
    Lugha takuwa imara, ukabila tutafinya,
    Kiswahili ni ibara, kila mtu kiimanya,
    Methali imetuonya, mtumwa si mwasilia
    Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana,
    Kukua imeridhia, msamiati kufana,
    Wengine wataijulia, kwa marefu na mapana,
    Lugha yenu ya maana, mwaipuuza yalia.
    (a) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu.
    (b) Kwa kutoa hoja ime, eleza kwa nini shairi hili likaitwa kilio cha lugha.
    (c) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari.
    (d) Eleza toni ya shairi hili.
    (e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano milatu.
    F)Bainisha nafsineni katika shairi.
    G)Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi.
    (i) nasongwa
    (ii) kuriaria
    (iii) adinasi

    Date posted: February 6, 2018.  Answers (1)

  • "... dawa ya adui ni kummegea unachokula." (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Jadili jinsi dawa inayorejelewa inavyozorotesha hali katika mji wa Cheneo.(Solved)

    "... dawa ya adui ni kummegea unachokula."
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Jadili jinsi dawa inayorejelewa inavyozorotesha hali katika mji wa
    Cheneo.

    Date posted: February 6, 2018.  Answers (1)

  • "Anwani Mstahiki Meya ni kinaya." Jadili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea tamthilia.(Solved)

    "Anwani Mstahiki Meya ni kinaya." Jadili ukweli wa kauli hii
    kwa kurejelea tamthilia.

    Date posted: February 6, 2018.  Answers (1)

  • Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. (Solved)

    Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

    Date posted: February 6, 2018.  Answers (1)

  • Fafanua mjukumu ya elimu na dini katika jamii kwa mujibu wa riwaya: Kidagaa Kimemwozea.(Solved)

    Fafanua mjukumu ya elimu na dini katika jamii kwa mujibu wa riwaya:
    Kidagaa Kimemwozea.

    Date posted: February 6, 2018.  Answers (1)

  • Jadili dhima ya fasihi katika jamii(Solved)

    Jadili dhima ya fasihi katika jamii

    Date posted: February 6, 2018.  Answers (1)

  • Fafanua sifa za Kenga kama zinavyojitokeza wazi katika tamthilia ya kigogo.(Solved)

    Fafanua sifa za Kenga kama zinavyojitokeza wazi katika tamthilia ya kigogo.

    Date posted: January 31, 2018.  Answers (1)

  • Eleza changamoto zilizoukabili usanifishaji wa kiswahili.(Solved)

    Eleza changamoto zilizoukabili usanifishaji wa kiswahili.

    Date posted: January 30, 2018.  Answers (1)

  • Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali yanayoifuatia. Watu wengi hawawezi kunywa chai au uji bila kutia sukari. Wanatumia sukari kwa hamu na ghamu bila kutambua kuwa...(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali yanayoifuatia.

    Watu wengi hawawezi kunywa chai au uji bila kutia sukari. Wanatumia sukari kwa hamu na ghamu bila kutambua kuwa hiyo ni sumu wanayojiongezea mwilini.


    Ni ukweli usiopingika kuwa wazee wetu wa jadi waliishi muda mrefu wakiwa na siha njema kuliko sisi. Hii ni kwa sababu waliishi katika kipindi ambacho sukari inayotengenezwa viwandani haikuweko. Iwapo ilikuweko, ilikuwa bidhaa ya wateule wa ungwana kutengenezea vitu kama keki, mahamri na vitumbua. Akina yahe hawangeweza kuigharamia.


    Watafiti wa masuala ya afya wamegundua kuwa sukari inayotayarishwa viwandani sasa hivi haina virutubishi vyovyote. Hali kadhalika, utaratibu wa viwandani wa kutayarisha sukari ili iwe nyeupe na kuichuja huharibu virutubishi vinavyoweza kuwa muhimu mwilini. Umuhimu wa sukari wakausaza kuwa kutia ladha tamu tu. Umuhimu huu hauwezi kulinganishwa na madhara yanayoletwa na sukari hii. Baada ya kusagika mwilini, sukari hii huacha masalio ya sidi mwilini yenye sumu inayoathiri siha.

    Matumizi ya sukari kwa wingi husababisha madhara mbalimbali mwilini. Huchangia kuoza na kuharibika kwa meno. Sukari nyeupe imehusishwa na ongezeko la maradhi ya kisukari, moyo na hipoglisimoia au upungufu wa sukari mwilini. Matumizi holela ya sukari huleta kipandauso au ugonjwa wa ghafla wa kuumwa na upande mmoja wa kichwa unaoambatana na kichefuchefu, kutapika na matatizo ya kuona. Sukari pia huleta maradhi ya ngozi na figo, pamoja na ongezeko la kemikali iitwayo kolestroli, ambayo ni ufuta unaonata na hutokana na kutoyeyuka kwa mafuta yote mwilini. Kemikali hii inaporundikana moyoni, hufanya mishipa inayotoa damu moyoni na kuisambaza mwilini kuwa myembamba na sugu. Moyo hulazimika kusukuma damu kwa nguvu na huenda ukachoka na kukoma kufanya kazi.


    Wataalamu wa lishe bora wamependekeza ulaji wa vyakula kama nafaka, matunda, mboga na miwa ambavyo vimejaa sukari asilia. Fauka ya hayo, sukari inayotokana katika asali ni bora zaidi kwa mwili wa mwanadamu. Asali huwa na sukari asilia, vitamini, madini na amino asidi. Hivi vyote huwa na manufaa mbalimbali mwilini. Asali huupa mwili nishati inayohitajika kuendesha shughuli za viungo.Licha ya hayo, asali huchangamsha mwili. Asali huwa na kemikali ambazo huwasaidia watoto kukua vizuri. Huweza kuzidisha kiwango cha himoglobini, hivyo kupunguza uwezekano wa watoto kuwa na anemia (upungufu wa damu). Asali husaidi katika usagaji wa chakula iwapo itatumiwa kabla ya mlo. Matumizi ya kijiko kimoja cha asali kila siku husaidia mwili kujikinga dhidi ya magonjwa ya kukohoa. Asali husaidia pia kuondoa harufu mbaya kinywani.


    Asali inaweza kutumiwa kujipaka. Inapotumika kwa njia hii, hutunza ngozi na kuifanya ing'are, huondoa vipele na ugumu wa ngozi, pamoja na kutibu kule ngozi ilikokatikakatika. Hali kadhalika asali hutibu vidonda. Viwanda vingi vya vipodozi vilevile hutumia asali kama malighafi muhimu katika utengenezaji wa bidhaa hizo.
    (a) Pendekeza anwani kwa taarifa uliyosoma.
    (b) Taja matumizi mawili ya sukari nyeupe
    (c) Eleza madhara matatu ya sukari nyeupe mwilini.
    (d) Bainisha aina ya sukari iliyo na manufaa mwilini mwa binadamu na ueleze ni yapi.
    (e) Eleza manufaa mawili ya asali:
    (i) Ndani ya mwili
    (ii)Nje ya mwili

    (f)Eleza maana ya msamiati huu kama uliyotumika katika kifungu.
    (i) Akina yahe
    (ii) Sugu
    (iii)Vipodozi

    Date posted: January 23, 2018.  Answers (1)

  • Ukifuata utratibu unaokubalika, onyesha hatua sita za uwasilishaji wa vitendawili. (Solved)

    Ukifuata utratibu unaokubalika, onyesha hatua sita za uwasilishaji wa vitendawili.

    Date posted: January 19, 2018.  Answers (1)

  • Huku ukitolea mifano ya kipera husika, fafanua dhima za maghani.(Solved)

    Huku ukitolea mifano ya kipera husika, fafanua dhima za maghani.

    Date posted: January 19, 2018.  Answers (1)

  • Je, miviga ina upungufu gani?(Solved)

    Je, miviga ina upungufu gani

    Date posted: January 17, 2018.  Answers (1)

  • Orodhesha sherehe nne za jamii yako zinazohusishwa na miviga (Solved)

    Orodhesha sherehe nne za jamii yako zinazohusishwa na miviga

    Date posted: January 17, 2018.  Answers (1)

  • Fafanua kikamilifu dhana zifuatazo za fasihi simulizi i) Nyiso ii) Mbolezi iii) Hodiya iv) Bembelezi v) Sifo(Solved)

    Fafanua kikamilifu dhana zifuatazo za fasihi simulizi
    i) Nyiso
    ii) Mbolezi
    iii) Hodiya
    iv) Bembelezi
    v) Sifo

    Date posted: January 17, 2018.  Answers (1)

  • Andika katika usemi wa taarifa “Karibu Bakari, tafadhali kaa”, Maimuna alisema. “Asante, je, habari za nyumbani?” Bakari aliuliza(Solved)

    Andika katika usemi wa taarifa
    “Karibu Bakari, tafadhali kaa”, Maimuna alisema. “Asante, je, habari za nyumbani?” Bakari aliuliza

    Date posted: January 17, 2018.  Answers (1)

  • Andika katika hali ya kutendewa: Kuku hawa wamemsumbua Sabina kwa muda mrefu.(Solved)

    Andika katika hali ya kutendewa:
    Kuku hawa wamemsumbua Sabina kwa muda mrefu.

    Date posted: January 17, 2018.  Answers (1)

  • Andika kwa wingi Wimbi hilo la maji lilimhofisha mvuvi akashindwa kutupa wavu wake majini. (Solved)

    Andika kwa wingi
    Wimbi hilo la maji lilimhofisha mvuvi akashindwa kutupa wavu wake majini.

    Date posted: January 17, 2018.  Answers (1)

  • Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia virejeshi vya tamati: Mwanafunzi anayefanikiwa maishani ni yule anayesoma kwa bidii na pia anayewatii wazazi wake. (Solved)

    Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia virejeshi vya tamati:
    Mwanafunzi anayefanikiwa maishani ni yule anayesoma kwa bidii na pia anayewatii wazazi wake.

    Date posted: January 16, 2018.  Answers (1)