Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Taja na ueleze vipera vyovyote vitano vya utanzu wa hadithi

Taja na ueleze vipera vyovyote vitano vya utanzu wa hadithi

Answers


Mageto
Hurafa-ni hadithi ambazo wahusika huwa ni wanyama wanaowakilisha matendo sawa na binadamu katika ulimwengu halisi.

Visasili-ni hadithi ambazo huonyesha vyanzo vya matendo au tabia.kwa mfano kwa nini nyoka hana miguu,chanzo cha kifo.

Visakale-ni hadithi ambazo huonyesha matendo ya kihistoria katika jamii.kwa mfano fumo liyongo ambaye ni anapigana kuikomboa jamii.Luanda magere katika jamii ya waluo.

Ngano za mazimwi-ni aina ya hadithi inayowazilisha ujumbe kutumia viumbe wenye uwezo mkubwa na wenye kutisha katika jamii.kwa mfano majitu.

Hekaya-ni hadithi za mambo ya kijanja.kwa mfano hekaya za abunuwasi

Real Educator answered the question on April 18, 2018 at 13:12

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions