Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Eleza nafasi ya makundi yafuatayo katika ama kukua au kudhoofika kwa Kiswahili nchini Kenya kabla ya uhuru. (a) Watawala (b) Wamisheni (c) Walowezi

      

Eleza nafasi ya makundi yafuatayo katika ama kukua au kudhoofika kwa Kiswahili nchini Kenya kabla ya uhuru.
a) Watawala
b) Wamisheni
c) Walowezi
(alama 15)

  

Answers


ESTHER
a. Watawala
Watawala wengi kwa jumla hawakupendelea Kiswahili. Kwa mfano, mwaka wa 1900 Charlse Elliot aliyekuwa Gavana wa Kenya alipendekeza na kuhimiza matumizi ya lugha ya asili katika utawala badala ya Kiswahili.
Moja ya nguzo ya ukoloni ilikuwa ni siasa ya ubaguzi. Kulikuwa na shule za wazungu, Wahindi, waarabu na Waafrika. Lugha ya kufundisha katika shule za Waafrika ilikuwa ni lugha za kiasili huku Kiswahili kikifundishwa kama somo tu.
Tume baada ya tume za uongozi zilipinga matumizi ya Kiswahili isipokuwa katika maeneo yaliyotumia Kiswahili kwa wingi, mfano, tume ya Beecher 1942 ilipinga kabisa matumizi ya Kiswahili.
Hata hivyo, baadhi ya watawala wallitambua umuhimu wa Kiswahili na kikasanifishwa mwaka wa 1930 na kuanza kupata umaarufu.

b. Wamisheni.
Wamisheni walishughulikia sana suala la elimu na suala la lugha ni moja 7ya masuala yaliyojitokeza katika elimu. Badhi ya madhehebu yalipinga matumizi ya Kiswahili kama lugha ya kufundisha aukueneza dini lakini wengine walikitumia. Madhehebu ya Kiluteri ndiyo yaliyopinga sana huku Wakatoliki wakitumia lugha ya Kiswahili.
Lugha ya Kiswahili ilipingwa kwa madai kuwa ilihusishwa na Uislamu na pia ilihusishwa sana na biashara ya wwatumwa. Jambo hili lilikwamiza maenezi yake.
c. Walowezi
Juhudi za watawala wa kikoloni zilikuwa ni kuifanya Kenya nchi ya wazubgu. Wazungu walijinyakulia mashamba na kuwa masetla au walowezi. Hawakutaka Waafrika wafundishwe Kiingereza wakisema itakuwa kama kujivua nguo. Waliona kama Waafrika wangetumia Kingereza kutetea haki zao. Walowezi hivyo walipendekeza matumizi ya Kiswahili ingawa pia hawakutaka kujifundisha Kiswahili sanifu kwani walikidunisha. Kutokana na hili, Kiswahili kikaanza kuhusishwa na Wasetla na Waafrika wakawa wanakichukia.
ESTHER STEVE answered the question on April 30, 2018 at 20:21


Next: Jadili aina tatu za ‘maana’ huku ukizitolea mifano kutoka Kiswahili.
Previous: Jadili juhudi za TUKI katika kuendeleza na kustawisha Kiswahili katika ukanda wa Afrika Mashariki.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions