Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Fafanua jinsi mwandishi wa ‘Tumbo Lisiloshiba’ alivyotumia kinaya kufanikisha maudhui yake

Fafanua jinsi mwandishi wa ‘Tumbo Lisiloshiba’ alivyotumia kinaya kufanikisha maudhui yake

Answers


Kavungya
Jeshi la polisi linawalinda askari wa baraza wanapowabomolea raia makazi yao badala ya kuwalinda raia waliokuwa wakidhulumiwa na askari wa baraza.
-Ni kinaya kwamba wanasheria wanaofaa kutetea haki kwa wanyonge hawafanyi hivyo .Hii ndio sababu Mzee Mago anawahimiza raia kuwatafuta wanasheria waaminifu watakaowasaidia kutatua sheria ngumu zilizowakabili.
-Ni kinaya viongozi kuliendesha taifa bila kuwashirikisha raia kwa sababu ya kuwa maskini.Tanambiwa kuwa`Nani angewashauri wao mburumatari?’
-Viongozi wanajenga jijini hadi inakosekana nafasi ya mtu kuvuta pumzi.
-Ni kinaya viongozi kuwapoka raia ardhi bila kuwazia hatima yao.
-Ni kinaya serikali kuwahujumu raia badala ya kuwalinda.Imeweka vitego na vikwazo vya sheria ili kuwazuia kutetea mali zao.
Ni kinaya jitu kuingia mkahawani na kula chakula chote;chakula ambacho kingeliwa na watu kadhaa.
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 08:14

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions