Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Fafanua changamoto zinazokabili asasi ya ndoa ukirejelea hadithi ya Masharti ya kisasa

Fafanua changamoto zinazokabili asasi ya ndoa ukirejelea hadithi ya Masharti ya kisasa

Answers


Kavungya
• Kwa kuwa Dadi alimpenda kidawa alikubali masharti ya kisasa bila kuyaelewa
• Kidawa kufanya kazi za umetroni kunafanya asimwamini
• Ncha nyingi za maisha zinamfanya Kidawa atembeze bidhaa za uarabuni mitaani jambo lililozidisha shauku ya Dadi
• Dadi alichukia kujipamba kwa Kidawa akiona anafanya hivyo kwa minajili ya mwalimu mkuu
• Dadi pia alichukia namna Kidawa alivyosimama na kuongea na wanaume
• Bi Zuhura alimkejeli Dadi kwa kumtaka amparalie samaki
• Dadi aliogopa kuambiwa kuwa yeye si mwanaume tosha
• Maneno ya watu yalimfanya Dadi aache kusaidia kazi za nyumbani
• Dadi alkimfuata Kidawa hadi shuleni kubaini kama Kidawa alimwendea kinyume na mwalimu mkuu
• Dadi aliwakodolea macho wanawake waliovalia nguo zilizowafika magotini
Kavungya answered the question on May 6, 2019 at 08:13

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions