Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
a) Linakatisha tamaa kwa sababu
i. Mwanamke anapolima, hafaidiki na mavuno bali yote huchukuliwa na bwanake
ii. Mwanamke hubaguliwa na kuonewa ofisini
iii. Mahali pake ni jikoni, ujakazi n.k lakini halipwi na tena hapewi likizo (hapumziki)
iv. Hutumiwa kama chombo cha mapenzi kukidhia uchuu wa mwanamke
v. Hamna anayemheshimiwa kwa chochote eti kwa sababu ni mke
b) UMBO
i. Beti sita
ii. Mishororo sita kwa kila ubeti
iii. Vina vya wisho vya mishororo ya kwanza miwili (mwanzo na mloto) ni –ni- isipokuwa ubeti wa sita (mwisho)
iv. Kila ubeti hususan wa kwanza hadi wa tano umeanza kwa neno Nomwona isipokuwa ubeti wa sita – kupelekea shairi hili kuwa kikwamba
v. Kila ubeti una kituo tofauti
c) Lugha Nathari
Mwanamke hushinda katika boma akipika, akilea, na hata kufua nguo. Licha ya hayo halipwi na tena hapewi nafasi ya kupumzika Tuza 4. Tathmini matumizi ya lugha nathari
d) Tamathali iliyotawala
i) Taswira – hali ya kumwona mke nyumbani na kwingineko katika shughuli mbalimbali
kama - akiwa nyumbani akipika
- akiwa kitandani uchi
- akiwa mkekani katika utungu wa kujifungua.
Kutuza : Kutaja mbinu
e) Mifano ya taasubi ya kiume
i. Katika ubeti wa kwanza, mume anayachukua mavuno kutoka kwa mkewe
ii. Wanaume katika ubeti wa pili wna ubaguzi na kuonea wanawake
f) Msamiati- Mzima utashi
i) Mwenye udiu/ tama kubwa Maungoni
ii)- maumbo, viungo vya mwili vinaonekana wazi
maurice.mutuku answered the question on October 9, 2019 at 07:13
- KIPI NIKITENDE? Tayari ni sarakani, niambie yote johara,Mosi nimpe shukrani, kanizaa bira zira,Wapo haiko hisani, ningefaa kwa uparara,Kipi takachokitenda, ni nene heko kwa mama?Miezi tisa...(Solved)
KIPI NIKITENDE?
Tayari ni sarakani, niambie yote johara,
Mosi nimpe shukrani, kanizaa bira zira,
Wapo haiko hisani, ningefaa kwa uparara,
Kipi takachokitenda, ni nene heko kwa mama?
Miezi tisa tumboni, yote nina kajinyima,
Kanikopa uchunguni, safari ndefu kazima’
Kama kinda kiotani, kiniasa huyu mama’
Kipi takachokitenda, ninene heko mama ?
Baba siku jana madadi, kawa vingaito mambo,
Kaolewa na asadi, kachalazwa kwa wimbombo,
Kaona – bali jadili, kuchao puani bombo,
Kipi takachokitenda, ninene heko mama?
Kila kuchao zarani, kupalilia kondeni,
Kachanika mpinini, chungu povuka motoni,
Kaviyariya fingani, kinijali jikoni,
Kipi tukachokitenda , ninene heko mama?
Wa siku hizi vijana, wakahujuru nyumbani,
Wengine wao jagina, kawa lofa mutaani,
Hali ukashiba nina, afikapo tu, “kongoni!”
Kipi takachokitenda, ninene heko mama?
Nawe bwana siwe maya, vita hasha kiwa kombo,
Tena simfanye yaya, ya kikoa ndio mambo,
Simtende ya hizaya, siwe mwao kila jambo,
Kipi takachokitenda, ninene heko mama?
Sasa jamvi nakuja, kisa nimesakarika,
Naomba niliyotaja, tatia manani kaka,
Nenayo yasiwe ngoja, ili nipokee baraka,
Mema nitamtendea, apate futahi pia.
(a) Eleza umbo la shairi hili
(b) Kwa nini msanii amshukuru mamaye ?
(c) Ni kina nani wanaokashifiwa na msanii ? Kwa nini ?
(d) Onyesha tofauti katika ujumbe iliyoko katika beti nne za kwanza na mbili zinazofuata
(e) Toa majina mengine yenye maana sawa na haya yaliyotumiwa katika shairi hili :
(i) Mama
(ii) Dawati
(iii) Imara/thabiti
(f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika kaika shairi:
(i) Kawa vangaito mambo
(ii) Wimbombo
(iii) Kongoni
Date posted: October 9, 2019. Answers (1)
- 1. Nitampa nani, sauti yangu ya dhati
Kwa kipimo gani, ingawa kiwakatiti
Amefanya nini, la kutetea umati
Kipimo ni kipi?
2. Yupi wa maani, asosita katikati
Alo na maoni, yasojua...(Solved)
1. Nitampa nani, sauti yangu ya dhati
Kwa kipimo gani, ingawa kiwakatiti
Amefanya nini, la kutetea umati
Kipimo ni kipi?
2. Yupi wa maani, asosita katikati
Alo na maoni, yasojua gatigati
Atazame chini, kwa kile ule wakati
Kipimo ni kipi?
3. Alo mzalendo, atambuaye shuruti
Asiye mafundo, asojua mangiriti
Anoshika pendo, hata katika mauti
Kipimo ni kipi?
4. Kipimo ni kipi, changu mimi kudhibiti
Utu uko wapi, ni wapi unapoketi
Nje kwa mkwapi, au ndani kwa buheti
Kipimo ni kipi?
a) Eleza umbo la shairi hili
b) Taja na ueleze jinsi mwandishi alivyotumia uhuru wa ushairi
c) Eleza ujumbe unaowasilishwa na mshairi
d) Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari
e) Taja bahari tatu zinazojitokeza katika shairi na utoe sababu
f) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi hili
i) Katiti
ii) Gatigati
iii) Mangiriti
Date posted: October 9, 2019. Answers (1)
- 1. Mke wangu wameshanipoka
Ndugu zangu, wamedai ububu
Wazazi kuzoea kunigombeza(Solved)
HATIMA YANGU
1. Mke wangu wameshanipoka
Ndugu zangu, wamedai ububu
Wazazi kuzoea kunigombeza
2. Juzi mali lilimbikiza
Furaha lilitanda
Makanwa yalijaziwa
Hoi hoi ikawa desturi
3. Kilabu tulikwenda
Nyama tulichoma
Mahali tulizuru
Tuliteremsha!
4. Leo mambo yamenigeuka
Wao masahibu siwaoni
Matumbo yakaninguruma
Kama radi ya mvua
5. Nyumbani nimebaki pweke
Mke amenitoroka
Watoto wameparara
Skuli kugharamia
Imegeuka balaa belua
6. Ndipo nimeamua
Afadhali kitanzi badala ya balaa
Kumbe kupanga ndiyo maana
Maisha na waasia
(a) Eleza mambo muhimu yanayoelezwa katika shairi hili
(b) Fafanua sifa mbili za anayezungumza katika shairi
(c) Dondoa na ufafanue mbinu zozote mbili za lugha katika shairi hili
(d) Eleza maana ya:-
(i) Ndugu zangu wamedai ububu
(ii) Kumbe kupanga ndiyo maana
Date posted: October 9, 2019. Answers (1)
- WAFULA KABILIANA NA KISU
Ee mpwa wangu,
Kwetu hakuna muoga,
Uoga ukikufikia, huenda ni wa akina mamayo,
Fahali tulichinja ili uwe mwanamme,
Eewe mpwa wangu, kisu kikali ajabu !
Iwapo utatingiza...(Solved)
WAFULA KABILIANA NA KISU
Ee mpwa wangu,
Kwetu hakuna muoga,
Uoga ukikufikia, huenda ni wa akina mamayo,
Fahali tulichinja ili uwe mwanamme,
Eewe mpwa wangu, kisu kikali ajabu !
Iwapo utatingiza kichwa,
Uhamie kwa wasiotahiri.
Wanaume wa mbari yetu,
Si waoga wa kisu,
Wao hukatwa kuanzia macheo hadi machweo,
Wewe ndiye wa kwanza,
Iwapo utashindwa,
Wasichana wote,
Watakucheka,
Ubaki msununu,
Simama jiwe liwe juu,
Ndege zote ziangamie.
Simu nimeipokea,
Ngariba alilala jikoni,
Visu ametia makali,
Wewe ndiye wangojewa,
Hadharani utasimama,
Macho yote yawe kwako,
Iwapo haustahimili kisu,
Jiuzulu sasa mpwa wangu,
Hakika sasa mpwa wangu,
Hakika tutakusamehe, mwaka kesho unakuja.
Asubuhi ndio hii,
Mama mtoto aamushwe,
Upweke ni uvundo,
Iwapo utatikisa kichwa,
Iwapo wewe ni mme,
Kabiliana na kisu kikali,
Hakika ni kikali!
Kweli ni kikali!
Wengi wasema ni kikali!
Fika huko uone ukali!
Mbuzi utapata,
Na hata shamba la mahindi,
Simama imara,
Usiende kwa wasiotahiri
(a) Hili ni shairi la aina gani ? Thibitisha
(b) Ni nani anayeimba shairi hili na analiimba kwa nani ?
(c) Toa ithibati kwenye shairi hili kuthibitisha kuwa msimulizi ana taasubi za kiume
(d) Taja kwa kutolea mifano mbinu zozote nne za uandishi katika shairi hili
(e) Taja shughuli zozote mbili za kiuchumi za jamii inayorejelewa katika shairi hili
(f) Eleza kwa mifano, uhuru wa kishairi katika shairi hili
(g) Msamiati ufuatao umetumika kwa maana gani katika shairi hili ?
(i) Mbari
(ii) Msununu
(iii) Ngariba
(iv) Uvundo
Date posted: October 9, 2019. Answers (1)
- Sinisumbuwe akili, nakusihi e mwandani.Afya yangu dhahili, mno nataka amaniNawe umenikabili, nenende sipitaliniSisi tokea azali, twende zetu mizumuniNifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?Mababu hawakujali, wajihisipo...(Solved)
Sinisumbuwe akili, nakusihi e mwandani.
Afya yangu dhahili, mno nataka amani
Nawe umenikabili, nenende sipitalini
Sisi tokea azali, twende zetu mizumuni
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?
Mababu hawakujali, wajihisipo tabani
Tuna dawa za asili, hupati sipitalini
Kwa nguvu za kirijali, Mkuyati uamini
Kaafuri pia kali, dawa ya ndwele fulani
Nifuateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?
Mtu akiwa hali, tumbo lina walakini,
Dawa yake ni subili, au zongo huanoni
Zabadili pia sahali, kwa maradhi yalo ndani
Au kwenda wasaili, wenyewe walo pangani
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?
Mtu kwenda sipitali, ni kutojuwa yakini
Daktari k’ona mwili, tanena kensa tumboni
Visu visitiwe makali, tayari kwa pirisheni
Ukatwe kama fagili, tumbo nyangwe na maini
Nifuateni sipitalini, na dawa ziko nyumbani?
Japo maradhi dhalili, kutenguliwa tegoni
Yakifika sipitali, huwa hayana kifani
Wambiwa damu kaliti, ndugu msaidieni
Watu wakitaamali, kumbe ndiyo bunani
Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?
Mizimu wakupa kweli, Wakueleze undani.
Maradhiyo ni ajali, yataka vitu thamani
Utete huku wawili, wa manjano na kijani
Matunda pia asali, vitu vyae shamoni
Nifuateni sipati, na dawa zi langoni?
(a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka
(b) Mtunzi alikuwa na lengo gani alipotunga shairi hili
(c) Mbona mshairi hataki kwenda hospitalini
(d) Eleza umbo la shairi hili
(e) Kwa nini mshairi alitumia ritifaa katika ushairi ?
(f) Andika maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa kwenye shairi :-
(i) Dhalili –
(ii) Azali-
(iii)Sahali-
Date posted: October 9, 2019. Answers (1)
- Umekata mti mtima
Umeangukia nyumba yako
Umeziba mto hasira
...................(Solved)
SHAIRI ‘A’.
Umekata mti mtima
Umeangukia nyumba yako
Umeziba mto hasira
Nyumba yako sasa mafurikoni
Na utahama
Watoto Wakukimbia
Mbuzi kumkaribia chui
Alijigeuza Panya
Akalia kulikuwa na pala
Kichwani
Mchawi kutaka sana kutisha
Alijigeuza Simba
Akalia na risasi kichwani
Jongoo kutaka sana kukimbia
Aliomba miguu elfu
Akaachwa na nyoka
Hadija wapi sasa yatakwenda
Bwanako kumpa sumu ?
Hadija umeshika nyoka kwa mkia
Hadija umepitia nyuma ya punda
SHAIRI ‘B’
Piteni jamani, Piteni haraka
Nendeni, nendeni huko mwendako
Mimi haraka, haraka sina
Mzigo wangu, mzigo mzito mno
Na chini sitaki kuweka
Vijana kwa nini hampiti ?
Kwa nini mwanicheka kisogo ?
Mzigo niliobeba haupo.
Lakini umenipinda ngongo na
Nendako
Haya piteni ! Piteni haraka ! Heei !
Mwafikiri mwaniacha nyuma !
Njia ya maisha ni moja tu.
Huko mwendako ndiko nilikotoka
Na nilipofikia wengi wenu
Hawatafika.
Kula nimekula na sasa mwasema
Niko nyuma ya wakati
Lakini kama mungepita mbele
Na uso wangu kutazama
Ningewambia siri miaka
Mingi.
(a) Haya ni mashairi ya aina gani ? Toa saabu
(b) Washairi hawa wawili wanalalamika. Yafafanue malalamishi yao
(c) Onyesha jinsi kinaya kinavyojitokeza katika tungo hizi mbili
(d) Ni vipi Hadija :-
(i) Amekata mti mtima ?
(ii) Amepita nyuma ya Punda
(e) Toa mifano 2 ya uhuru wa mashairi kwa kurejelea mashairi haya
(f) Kwa kurejelea shairi ‘B’ eleza maana ya:-
(i) Mzigo
(ii) Siri
(iii) Kula nimekula
(iv) Niko nyuma ya wakati
Date posted: October 9, 2019. Answers (1)
- Mzee Oluoch :....................................................................ni kweli hayo!
Mzee Mwenda : Ndio. Huyu mtoto wangu nimemsomesha mpaka akahitimu chuo kikuu na anafanya kazi ya uhasibu.
Mzee Oluoch : Na wangu...(Solved)
Mzee Oluoch :....................................................................ni kweli hayo!
Mzee Mwenda : Ndio. Huyu mtoto wangu nimemsomesha mpaka akahitimu chuo kikuu na anafanya kazi ya uhasibu.
Mzee Oluoch : Na wangu amehitimu na sasa ana shahada ya uzamili. Yeye ni mhandisi
mkuu. Chukua tu mbuzi hamsini na utukubalie kujenga uhusiano wa ukwe.
Mzee Mwenda : Je, mbuzi hao ni wa ‘mfuko’ au ni .......?
(a) Mazungumzo ya aina hii hutokea katika muktadha wa aina gani?
(b) Eleza sifa nane za lugha inayotumika katika wa aina hii
Mzee Oluoch : Kuna wa mfuko ......thelathini na hao wengine ishirini.
Mzee Mwenda : Basi lete hao ulio nao. Wengine hamsini watabaki deni. Utakuwa
ukinilipa polepole. Idhini yangu nimetoa ili mipango iendelee.
Date posted: October 9, 2019. Answers (1)
- AZIZ : Ingia 46! Adams mbao Kenyatta, railways beba! 46 Adams mbao kenyatta, railways!
SHIKU : Namba nane ngapi?
AZIZ : Mbao ingia, blue.
SHIKU : Nina hashuu.
AZIZ...(Solved)
AZIZ : Ingia 46! Adams mbao Kenyatta, railways beba! 46 Adams mbao kenyatta, railways!
SHIKU : Namba nane ngapi?
AZIZ : Mbao ingia, blue.
SHIKU : Nina hashuu.
AZIZ : Blue Auntie.
SHIKU : Sina.
AZIZ : Ingia. 46 Adams mbao, kenyatta railways gari bebabeba.
AHENDERA : Mimi sinako shirini. Chukuako tu kumi.
AZIZ : Dinga inakunywanga petrol mzee.
AHENDERA: Kumi mingi.
AZIZ : Haaya ingia twende. Driver imeshon twende.
(i) Eleza muktadha wa mazungumzo haya
(ii) Taja sifa sita za lugha iliyotumika katika mazungumzo haya
Date posted: October 9, 2019. Answers (1)
- Eleza juhudi tano zinazotumika kukiendeleza Kiswahili(Solved)
Eleza juhudi tano zinazotumika kukiendeleza Kiswahili
Date posted: October 8, 2019. Answers (1)
- Bw. Mosuka : Mheshimiwa spika, naichukua fursa hii kuipinga hoja iliyowasilishwa na
mbunge wa Mahira, mheshimiwa Kochaberi kuhusu suala la kuavya....
(a) Hii ni sajili gani?
(b) Eleza...(Solved)
Bw. Mosuka : Mheshimiwa spika, naichukua fursa hii kuipinga hoja iliyowasilishwa na
mbunge wa Mahira, mheshimiwa Kochaberi kuhusu suala la kuavya....
(a) Hii ni sajili gani?
(b) Eleza sifa za mazungumzo ya sajili hii
Date posted: October 8, 2019. Answers (1)
- A : Ohh, dada NaomiB : Dada Ruth (anamsogea kwa bashasha wanakumbatiana). Ahh Mungu asifiwe!A: Asifiwe sanaB: Ehh dadangu, miezi ...mingi...sijakuonaA: dada wee...Nilitumwa huko kusini...(Solved)
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali :
A : Ohh, dada Naomi
B : Dada Ruth (anamsogea kwa bashasha wanakumbatiana). Ahh Mungu asifiwe!
A: Asifiwe sana
B: Ehh dadangu, miezi ...mingi...sijakuona
A: dada wee...Nilitumwa huko kusini ...Kuwahubiria watu injili (mtuo mdogo)singeweza kukata...
B: Ehh, usiwe kama Yona
A: Habari ya siku nyingi?
B; Nzuri Mungu bado ameendelea kunibariki
A: Amen!
B: Nimeendelea kuiona neema yake
A: Amen! Asifiwe Bwana
B: Halleluya
A: Ni Mungu wa miujiza!
B : Amen. Hata nami nimeona neema yake
Bado niko imara katika wokovu katika siku hizi za mwisho
A : Amen !
B : Ni Mungu wa ajabu kweli !
A : Nilikumbana na matatizo lakini nikategemea sala
Kama Paulo na sila… Na nikashinda (anatua). Sikuweza kumpa shetani nafasi…maana
ameshindwa
B : Ameshindwa kabisa
(i) Hii ni sajili ya wapi ? Fafanua
(ii) Taja na ueleze sifa za sajili hii
(iii) Taja na ueleze mambo mawili muhimu yaliyosaidia katika maenezi ya Kiswahili
Afrika mashariki na kati
Date posted: October 8, 2019. Answers (1)
- Niaje wasee! Ma-holiday ndizo hizo tena. Najua ma-mission ni mingi! Lakini jo,
mambo imebadilika ! Ni kubaya maze. Usifikirie kila kitu unaona ni reality, ukadhani ni...(Solved)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata:-
Niaje wasee! Ma-holiday ndizo hizo tena. Najua ma-mission ni mingi! Lakini jo,
mambo imebadilika ! Ni kubaya maze. Usifikirie kila kitu unaona ni reality, ukadhani ni gold !
Hiyo siyo real life maze ! Round hii maze ni ‘‘Ku-chill!’’ Usipige ma-stunts zingine zitakuacha uki-regret later! NI POA KU- CHILL au aje maze?
a) Bainisha rejista ya mazungumzo haya
b) Kwa kurejelea kifungu andika sifa za rejista hii.
c) Kwa nini watu hutumia lugha zaidi ya moja.
d) Orodhesha hatua tatu zinazoweza kuchukuliwa kusuluhisha matatizo yanayokumba Kiswahili nchini.
Date posted: October 8, 2019. Answers (1)
- Fafanua changamoto tano zinazozuia maenezi ya haraka ya lugha ya Kiswahili(Solved)
Fafanua changamoto tano zinazozuia maenezi ya haraka ya lugha ya Kiswahili
Date posted: October 8, 2019. Answers (1)
- Fafanua mikakati mitano inayoweza kuchapuza kukua na kuenea kwa kiswahili nchini Kenya(Solved)
Fafanua mikakati mitano inayoweza kuchapuza kukua na kuenea kwa kiswahili nchini Kenya
Date posted: October 8, 2019. Answers (1)
- Uchunguzi uliofanywa umeonyesha kuwa anasumbuliwa na uto mwingi mwilini. Uto unaweza kudondoshwa kwa kufanya mazoezi, kupunguza ulaji wa vyakula vya wanga na hata protini. Protini...(Solved)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata
Uchunguzi uliofanywa umeonyesha kuwa anasumbuliwa na uto mwingi mwilini. Uto unaweza kudondoshwa kwa kufanya mazoezi, kupunguza ulaji wa vyakula vya wanga na hata protini. Protini iwapo nyingi mwilini hugeuzwa kuwa glukosi ambayo huhifadhiwa mwilini. Hii huwa msingi wa unene pia ambao unahatarisha afya. Jamaa yake aliyeaga dunia alikuwa mgonjwa wa bolisukari ambayo inaweza kurithishwa. Kimsingi, lazima awe na welewa bora kabisa wa lishe. Mwenzake naye aliathiriwa na aflatoxins zilikuwa kwenye chakula alichokula.
(a) Sajili hii inapatikana wapi? Kwa nini?
(b) Taja sifa zinazohusishwa na sajili yenyewe
Date posted: October 8, 2019. Answers (1)
- Lugha ya kiswahili inakabiliwa na matatizo mengi sana. Yataje na kuyaeleza.(Solved)
Lugha ya kiswahili inakabiliwa na matatizo mengi sana. Yataje na kuyaeleza.
Date posted: October 8, 2019. Answers (1)
- Saidi : Hallo............Hallo....Huyo ni Bw. Mohamed?Mohamed : Ndio...uko wapi...Saidi : Shuleni...sasa...ulinifikishia ujumbe?Mohamed : La. Parade ilikuwa imehitimishwaSaidi : Sina credit. Nipigie tafadhali.Mohamed : Sina...(Solved)
Isimu Jamii
Saidi : Hallo............Hallo....Huyo ni Bw. Mohamed?
Mohamed : Ndio...uko wapi...
Saidi : Shuleni...sasa...ulinifikishia ujumbe?
Mohamed : La. Parade ilikuwa imehitimishwa
Saidi : Sina credit. Nipigie tafadhali.
Mohamed : Sina pia, nitatuma sms
Saidi : Iwe saa hii eh?
Mohamed : Baada ya dakika tano
Saidi : Good day
Mohamed : Welcome
(a) Taja na uthibitishe sifa zinazojitokeza katika mazungumzo haya
(b) Eleza sababu za wazungumzaji kutumia mbinu zifuatazo katika mazungumzo yao
(i) Mdokezo
(ii) Lugha mseto
Date posted: October 8, 2019. Answers (1)
- Nomino zifuatazo ni za ngeli gani?
i) Nzi
ii) Soksi(Solved)
Nomino zifuatazo ni za ngeli gani?
i) Nzi
ii) Soksi
Date posted: October 8, 2019. Answers (1)
- Bainisha aina za shamirisho katika sentensi ifuatayo Soroveya atapimia wanunuzi viwanja.(Solved)
Bainisha aina za shamirisho katika sentensi ifuatayo
Soroveya atapimia wanunuzi viwanja.
Date posted: October 8, 2019. Answers (1)
- Changanua sentensi ifuaatayo kwa kielelezo visandu.
Mwanafunzi aliyeleta kitabu chake amepongezwa(Solved)
Changanua sentensi ifuaatayo kwa kielelezo visandu.
Mwanafunzi aliyeleta kitabu chake amepongezwa
Date posted: October 8, 2019. Answers (1)