Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Tathmini mchango wa tume ya Mackey (1981) na time ya Koech (1999) katika kustawisha Kiswahili nchini Kenya

Tathmini mchango wa tume ya Mackey (1981) na time ya Koech (1999) katika kustawisha Kiswahili nchini Kenya

Answers


Faith
MCHANGO WA TUME YA MACKEY (1981)
"Report of the presidential working party on the establishment of the second University in Kenya" tume hii ilipendekeza yafuatayo;
- Mfumo wa elimu wa 7-4-2-3 ubadilishwe na kuwa 8-4-4.
- chuo kikuu Cha pili kianzishwe na Kiswahili kifunzee chuoni humo Kama Somo la lazima. Hii ni kwa sababu kilikuwa na wanafunzi wengi waliofuzu kutoka chuoni lakini hawakuweza kujielsza kwa ufasaha katika lugha ya taifa.
Mambo yafuatayo yalitekelezwa:
* Mfumo wa elimu wa 8-4-4 ulianzishwa mwaka wa 1982 ambapo Kiswahili kilianza kuwa somo la lazima na la kutahiniwa katika mitihani wa darasa la name (K.C.P.E- 1985) na kidato Cha nne (K C.S.E).
* Chuo kikuu Cha Moi kilianzishwa pamoja na idara ya kiswahili mwaka wa 1987.
* Wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika vyuo vikuu vya kitaifa walianza kufunzwa vipengele vya kiswahili Kama sehemu ya kazi ya lazima ya mawasiliano.

MCHANGO WA TUME YA KOECH (1999)
Yafuatayo ni baadhi ya mambo yaliyopendekezwa:
- Mfumo wa elimu wa 8-4-4 ubadilishwe na kuitwa TIGET ( Totally Integrated Quality Education and Training) ambapo mitihani wa CPE unafanywa katika darasa la Saba na myihani wa GCSE utafanywa katika kidato Cha nne .
-Lugha ya kiswahili, lugha ya kingereza na hesabu ya masomo ya lazima katika shule ya msingi na za upili.
- Lugha ya kiswahili na fasihi ya kiswahili yafundishwe Kama masomo mawili tofauti. Kadhalika lugha ya kingereza na fasii ya kingereza yafundishwe Kama masomo mawili tofauti.
- Wanafunzi wa darasa la Kwanza Hadi la tatu aaruhusiwe kujifunza kwa lugha zao za Kwanza (lugha ya mama) kwa sababu wengi hawawezi kuwasiliana na kingereza lakini wake wanasoea mjini watumie Kiswahili.
- Masomo ya kiutendaji yafundishwe katika shule za msingi lakini yasitahiniwe kwa sababu yanapoteza wakati na tena yanawavunja moyo wanafunzi, wazazi na walimu.
-Katika mtihani wa CPE, masomo matano pekee yatahiniwe badala ya masomo Saba yanayotahiniwa katika KCPE.
- Katika mtihani wa GCSE kiwango cha chini Cha masomo yatakayotahiniwa ni masomo Saba lakini alama zitatolewa kwa masomo sita ambayo mwanafunzi atafanya vyema zaidi.
- Mtihani wa kidato Cha nne (GCSE) ufanywe Mara mbili kwa mwaka ambapo mwanafunzi wanaofeli Mara ya Kwanza wanaweza kuruhusiwa kufanya tena Mara ya pili.

Titany answered the question on December 6, 2021 at 11:15

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions