-
Eleza muundo wa majina katika ngeli ya A-WA
Date posted:
December 7, 2017
-
Eleza muundo wa silabi katika Kiswahili
Date posted:
December 7, 2017
-
Taja vipashio vinne vya lugha
Date posted:
December 7, 2017
-
Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo:
Mama aliwapakulia watoto chakula kwa sahani
Date posted:
December 7, 2017
-
Jadili uhusiano ulioko kati ya sintaksia na matawi mengine ya isimu huku uku ukitolea mifano mwafaka.
Date posted:
December 2, 2017
-
Mikakati inayotumiwa kukabiliana Na vikwazo vya mawasiliano katika lugha ya pili
Date posted:
November 30, 2017
-
Unda nomino mbilimbili kutokana na vitenzi hivi.
a)jaribu.
b)chuma
Date posted:
November 25, 2017
-
Taja aina mbili za viwakilishi nafsi
Date posted:
November 25, 2017
-
Unda vitenzi kutokana na nomino hizi.
i) Hotuba
ii) Tiba
Date posted:
November 25, 2017
-
Bainisha kielezi katika sentensi hii. Wageni hao waliwasili Julai mwaka jana.
Date posted:
November 25, 2017
-
Toa mifano miwili miwili kwa sauti zifuatazo:
i) Sauti ghuna ambazo ni vipasuo.
ii) Si ghuna ambazo ni vikwamizo.
Date posted:
November 25, 2017
-
Bainisha matumizi ya’ku’ katika sentensi hii.
Kufaulu kwako kutakuletea heshima ikiwa hukudanganya katika mtihani huo.
Date posted:
November 25, 2017
-
Eleza mtindo unaotumiwa kuainisha ngeli kisha utoe mifano miwili.
Date posted:
November 24, 2017
-
Ziandike sayari zote kwa Kiswahili.
Date posted:
November 23, 2017
-
Eleza hatua muhimu zinazofuatwa katika uandishi na usahihishaji wa Insha.
Date posted:
November 23, 2017
-
Eleza mtindo wa uainishaji wa ngeli.
Date posted:
November 22, 2017
-
Andika tarakimu hii kwa maneno: 10,001.
Date posted:
November 21, 2017
-
Ni kiungo kipi hutoa nyongo katika mwili wa binadamu? Andika wingi wa kiungo hicho.
Date posted:
November 21, 2017
-
ISIMUJAMII
Taja na ueleze njia tano zinazochangia maenezi ya lugha ya Kiswahili nchini.
Date posted:
November 20, 2017
-
Eleza matumizi ya vile katika sentensi hii.
Vile vile seremala alitengeneza meza.
Date posted:
November 20, 2017
-
Akifishe sentensi ifuatayo:
Lo amekimbia
Date posted:
November 20, 2017
-
Bainisha virai nomino, virai vivumishi, na virai vielezi katika sentensi ifuatayo:
Yule mwalimu mwenye ndevu amewasili ukumbini sasa hivi.
Date posted:
November 20, 2017
-
Sahihisha sentensi :
Mama mwenye alikufa amezikwa katika kaburini.
Date posted:
November 20, 2017
-
Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo:
Chakula chote kitaharibika. Chakula chochote kitaharibika.
Date posted:
November 20, 2017
-
Eleza sababu tano za kuchanganya na kubadili ndimi/msimbo.
Date posted:
November 20, 2017
-
Huku ukitoa mifano halisia eleza tofauti iliyopo kati ya kuchanganya ndimi/ msimbo na kubadili ndimi/msimbo.
Date posted:
November 20, 2017
-
Tunga sentensi moja itakayodhihirisha maana mbili za neno ‘kijinga’
Date posted:
November 20, 2017
-
Akifisha kifungu hiki.
Wanyama hawa kiboko ndovu tembo ngiri na ngawa wanyama wa pori wote hupatikana katika mbuga ya maasai mara.
Date posted:
November 20, 2017
-
Bainisha vitenzi katika sentensi hii.
Juma ndiye aliyekuwa akiiba mifugo wa jirani.
Date posted:
November 20, 2017
-
Andika katika usemi halisi Waziri alisema kuwa wangepata tiba ya bure kama bunge lingepitisha msuada huo.
Date posted:
November 20, 2017