Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Questions and answers: Kiswahili

Ask, answer and revise exam-style questions across Kenyan subjects and professional courses.

Q&A Categories

Exams With Marking Schemes

2200 Questions    View: All Solved Unsolved

Search Results...
  • UFAHAMU Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali :- Utandawazi Kufikia miongo michache iliyopita, ujumbe ulisafirishwa kwa njia zilizochukua muda mrefu sana kufika. Kwa mfano, mtu alipotaka kupiga simu katika nchi jirani barani Afrika, ilimbidi kupitia kwa opareta katika nchi za Ulaya ndipo aunganishwe. Kupigia simu kutoka Gambia kwenda Senegali ilibidi kutumia opareta wa Kule London na wa Paris, Ufaransa, na wa Senegal. Leo hii kuna njia nyingi za mawasiliano zilizo bora, za kutegemewa na zinazofikisha ujumbe kwa kasi sana. Ujumbe ambao ungechukua muda mrefu kuufikisha, sasa unapelekwa kwa sekunde moja. Miongoni mwa njia hizi ni mdahilishi, simu tamba na tuama, faksi, setelaiti, mitandao ya wavuti, n.k. Hamna eneo sasa hivi hata liwe mbali vipi lisilofikika na aina hizi za mawasiliano. Maendeleo haya ya mawasiliano yamechangia pakubwa sana kuufanya ulimwengu kuwa kijiji kimoja. Sasa kuna uhusiano wa karibu sana miongoni mwa mataifa duniani katika Nyanja zote za maisha. Hall hii ndiyo inayoitwa utandawazi au utandaridhi. Utandawazi umeleta mabadiliko mengi maishani. Mojawapo ni utoaji na uzalishaji wa mali. Mabadiliko ya mawasiliano yameruhusu mashirika ya kimataifa kusambaza utoaji na uzalishaji wa bidhaa zao katika maeneo mbalimbali duniani. Hali hii imepunguza gharama za usafirishaji sana. Bidhaa zinazoundwa na kiwanda chenye hakimiliki kilichoko kule New York masafa ya mbali, zinaweza kuzalishwa na kiwanda kilicho hapa Nairobi. Bila shaka umesikia kuhusu madawa ya kurefusha maisha ya wahasiriwa wa UKIMWI ambayo yanazalishwa na baadhi ya viwanda vya kutengeneza madawa humu nchini. Kiwanda chenye hakimiliki kipo jijini London. Viwanda ambavyo vilikuwa katika mataifa tajiri kama vile Uingereza, Ufaransa, Marekani, Ujerumani na Japani sasa vimeweza kutandaza vitandabui vyake kote duniani. Utandazaji huu hufanywa kwa njia kadhaa. Kwanza, viwanda hivi huvinunua viwanda vilivyoko katika mataifa yanayostawi. Vinaweza kuingia katika ubia na viwanda vya mataifa wanakotaka kuhamia. Viwanda hivi vya mataifa yanayoendelea hupatana kuwa watasimamia utoaji na uzalishaji wa bidhaa fulani na kukubaliana namna ya kugawa mapato. Utandawazi katika sekta ya uzalishaji na utoaji bidhaa umeleta manufaa kadhaa katika nchi zinazoendelea. Mojawapo ya haya ni kupatikana kwa nafasi za kazi. Pili, bidhaa za nchi zinazoendelea ambazo hazingeshindana na zile za mataifa yalioendelea sasa zimepata nafasi ya kushindana. Halikadhalika, wateja wana nafasi ya kupata bidhaa watakayo bila kuvunjwa moyo. Iwapo bidhaa anazohitaji mteja hazipatikani katika nchi, zinaweza kuagizwa moja kwa moja kutoka kwa kiwanda kingine chenye uhusiano nacho. Uagizaji hauchukui muda kutokana na hali ya mawasiliano inayoweza kutegemewa na inayofikisha ujumbe bila kupoteza wakati. Fauka ya haya, wateja hupata uwanja mpana wa kuchagua wanachokihitaji. Utandawazi umehimiza kustawi kwa mazingira ya mashindano katika utoaji na uzalishaji mali viwandani. Sasa hivi hakuna nchi yenye uwezo Wa kufungia bidhaa za nchi nyingine katika mipaka yake. Kufanya hivi ni kujitia kitanzi kiuchumi. Lazima nchi zifüngue masoko yao. Navyo viwanda vya kimataifa huweza kuwania masoko haya. Matokeo yake ni wateja kufaidika kwa kupata uwanja mpana wa bidhaa za kuchagua. Wateja pia hupata bidhaa za hali ya juu na kwa bei isiyo ghali kutokana na mashindano haya. Mashindano ya kimataifa ni kama ya paka na panya na kiwanda kisichojifunga nira vizuri, huwa kinajihatarisha. Kinaweza kujipata kimetupwa nje ya soko na kuangamia.Manufaa mengine ya utandawazi ni kuwa watu sasa hivi wanaweza kuwasiliana kwa urahisi na wepesi. Kwa kutumia simu, au mdahilishi, mtu anaweza kuwasiliana na mwenzake popote alipo licha ya masafa. Zaidi ya haya, utandawazi umewawezesha watu kutoka asili mbalimbali kuingiliana na kutangamana. Utangamano huu umeweza kuleta umoja baina ya watu kwa kutoa hisia za ubaguzi. Hata hivyo utandawazi umetokeza kuwa na madhara. Kwanza, uchumi wa nchi nyingi umeibukia kutawaliwa na matukio ambayo hayazihusu nchi hizo moja kwa moja. Uvamizi wa kijambazi wa Septemba 11,2000 kule Marekani uliathiri uchumi wa nchi nyingi sana. Matukio ya vita katika Mashariki ya kati nayo yamechangia kuzorotesha uchumi wa nchi nyingi hasa zile maskini ambzo zinategemea mafuta kutoka huko ilhali vita hivyo haviwahusu sikio wala ndewe. Athari kubwa ya utandawazi yaonekana katika sekta ya kijamii. Tamaduni nyingi za jamii katika nchi maskini zinaendelea kuvurugwa na maadili kuporomoka kutokana na ustawi wa kimawasiliano. Vijana wanaiga kutoka mataifa ya kimagharibi bila kuchuja. Si ajabu kuwa vijana wetu wanavaa mavazi yasiyositiri uchi wao vizuri na yasiyostahiki kwa jina la ustaarabu. Wavulana nao huzidisha kwa kutoga masikio na kusuka nywele usiweze kuwatofautisha na dada zao. Maswali (a) Utandawazi ni nini? (b) Ni mambo yapi yanayosababisha kutokea kwa utandawazi? (c) Mashirika ya mataifa yaliyostawi yanatumia mikakati ipi kutandaza vitandabui vyao kote duniani? (d) Fafanua: (i) Manufaa matatu ya utandawazi. (ii) Hasara tatu za utandawazi. (e) Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika taarifa. (i) Ubia (ii) Mashindano ya paka na panya. (iii) Kutoga (iv) Vitandabui

    Date posted: September 28, 2019
  • Tunga sentensi yenye kiingizi na kihusishi cha mahali.

    Date posted: September 26, 2019
  • Kanusha sentensi hii Nikimwona mwalimu wangu nitamjulisha habari hizo.

    Date posted: September 26, 2019
  • Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizo kwenye mabano. i) twaa (kutendeka) ii) Kosa (Kutendesha) iii) Cha (Kutendwa)

    Date posted: September 26, 2019
  • Maneno haya yamo katika ngeli gani? i) Fagio ii) Nyigu

    Date posted: September 26, 2019
  • Ngeli ni nini?

    Date posted: September 26, 2019
  • Soma taarifa ifuatavo kisha uiibu maswali Kiswahili ni lugha ambayo inakua na kuenea kila uchao. Imeenea kwa kasi hivi kwamba waliokuwa wameitweza wamelazimika kujifunza, kuizungumza na hata kuitumia katika maandishiLugha hii imetambuliwa kama mojawapo ya lugha za mawasiliano katika muungano wa Afrika. Magwiji wa Kiswahili wamechaguliwa kuunda msamiati mwafaka kutegemea mabadiliko ulimwenguni na kuingiza katika matumizi kupitia tarakilishi. Mpango huu utakapo faulu, mtu ataweza kutumia tarakilishi akiwasiliana kwa Kiswahili. Juhudi hizi heri zizidi kupongezwa na nyingine kuimarishwa Taasisi ya uchunguzi wa Kiswahili barani ni mojawapo wa hatua za kufanikisha juhudi hizi. Taasisi kama hiyo itatafiti historia ya lugha, mabadiliko yake na maenezi, msamiati wake na kuleta usawa wa mazungumzo kwa Kiswahili miongoni mwa mambo mengine.Kuweka lugha hii katika maandishi ni jambo litakalochangia kuimarisha lugha ya Kiswahili. Vitabu ,magazeti, na majarida yatakayolenga kiwango cha wasomaji yaandikwe na bei yake isiwe ghali mno ili wengi waweze kugharamia. Tanzu zote za lugha zizingatiwe.Lugha hii ifunzwe na kutahiniwa katika daraja zote za elimu. Lifanyapo hili, bila shaka lugha ya Kiswahili itaimarika.Uajiri wa wafanyikazi ukitambua ujuzi katika lugha hii hadhi yake itaimarika.Tafsiri ya kazi zilizoandikwa katika lugha mbalimbali zikifanywa katika Kiswahili, lugha hii itakua na kukitamizizi kwingi ulimwenguni.Watu wengi watapata hamu ya kusoma kazi asilia na ile ya tafsiri yake.Redio na magazeti ni vyombo muhimu katika kuwasiliana na kundi kubwa la watu kote duniani. Vyombo hivi vya mawasiliano kwa umma vikihimiza matumizi ya Kiswahili, bila shaka mchango mkubwa utaonekana katika kustawisha lugha hii. Vipindi maalumu matangazo na burudani vizingatie matumizi ya Kiswahili.Mashindano kati ya shule na shule,nchi na nchi ya kianzishwa na kuzingatiwa yanaweza kuimarisha Kiswahili pakubwa. Mashairi, mijadala, matokeo ya utafiti fulani, nyimbo, ngano na hadithi za kufunza umma ni njia za kuwezesha kufanyiwa mashindano kama hayo.Mikakati hii na mingine ikizingatiwa itakuwa mbolea nzuri ya kukuza lugha ya Kiswahili. Maswali i) Bila kubadilisha maana iliyokusudiwa ,fupisha aya mbili za mwanzo. (maneno 35 - 40) ii) Andika kwa muhtasari juhudi zinazofaa katika uimarishaji wa lugha ya Kiswahili kwa mujibu wa Makala haya. (maneno 70 -80)

    Date posted: September 25, 2019
  • Soma nakala yafuatayo kishaujibu maswali Ulimwengu unapaswa kuzuka na mbinu za Kulitadarukia tatizo la umaskini ambalo una kwamiza juhudi za maendeleo. Umaskini unaoukabili mataifa yanayoendelea. Unayatosa kwenye dhiki kubwa huku mataifa ya kimagharibi yakipiga hatua kubwa kimaendeleo. Ufa uliopo baina ya mataifa yanayoendelea na yaloyaliyoendelea kama vile Marekani, nchi za Ulaya na Ujapani unapanuka kila uchao. Vyanzo vya umaskini huu ni anuwai ; mathalan, ufisadi, uongozi mbaya, turathi za kikoloni, uchumi kuegemea mvua isiyotabirika,idadi ya watu inayoupiku uwezo wa uchumi wa taifa linalo husika na ukosefu wa nyenzo na amali za kuwakwamua raia kutoka lindi la umaskini. Ukosefu na adimu za ajira huchangia pia katika tatizo hili. Jamii ya xxxxxxx mpaswa kuelewa kuwa umaskini unaoathiri nchi fulani unaathari pana sana.Uvunigu unaotokana na umaskini unaweza kuwa msingi ambako matendo ya kihalifu ili kujinasua kutoka dhiki ile. Hii inaweza kuwa mbegu ya kuatika maovu kama ugaidi na uhalifu wa kila aina. Mataifa ya magharibi yanapaswa kuyaburai madeni mataifa yanayoendelea kama njia mojawapo ya kupambana na umaskini. Asilimia kubwa ya pato la kitaifa katika mataifa mengi hutumika kuyalipa madeni hayo. Katika hali hii inakuwamuhali kwa mataifa hayo kujikwamua kutokana na pingu za umaskini. Njia nyingine ni kustahabu kutoa ruzuku za kimaendeleo badala ya mikopo kwa nchi zinazoendelea. Kwa upande wake, mataifa yanayoendelea yanapaswa kuibuka na mikakati bora yakupambana na umaskini. Ni muhimu pawepo na sera zinazotambua ukweli kuwa asilimia kubwa ya raia wa mataifa hayo ni maskini. Pana dharura ya kuzalisha nafasi za ajira, kupanua viwanda hususan vinavyohusiana na zaraa ambayo ni tegemeo kuu la mataifa mengi, kuendeleza elimu na kuimarisha miundo msingi. Ipo haja pia ya mataifa haya kuhakikisha kuwa mfumo wa soko huru unaotawala ulimwengu sasa hauishii kuwa chanzo cha kufa kwa viwanda asilia na kuendeleza umasikini zaidi. Kwa ufupi, maamuzi yote ya sera za kiuchumi lazima ya zingatie uhalisi wa maisha ya raia wa mataifa hayo. a) Kwa nini umaskini umetamalaki katika mataifa yanayoendelea? b) Madeni yana athari gani kwa mataifa yanayoendelea? c) Ni mapendekezo yapi ambayo mwandishi anatoa kwa mataifa machanga kuhusu utatuzi wa tatizo la umaskini? d) Mfumo wa soko huru una mathara gani kwa mataifa machanga? e) Ukirejea kifungu, eleza maana ya: i) Kulitadarukia ii) Kuatika iii) Kuyaburai madeni

    Date posted: September 25, 2019
  • Damu Nyeusi na Hadithi nyingine : Ken Walibora na Said A. Mohamed "Asanteni sana kwa kuja, sisi. . . hukabiliana na mengi." i) Eleza muktadha wa dondoo hili. ii) Fafanua matukio yaliyosababisha mkutano huu. (alama 4) iii) Jadili changamoto sita zinazokumba jinsia ya kike katika hadithi hii.

    Date posted: September 25, 2019
  • Matatizo yanayowakumba wanacheneo ni kielelzo cha matatizo yanayowakumba wananchi wa mataifa mengi ya ulimwengu wa tatu. Thibitisha ukerejelea "Mstahiki Meya".

    Date posted: September 25, 2019
  • Huku ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea thibitisha kwamba vijana wana suluhu tosha kwa matatizo yanayoikumba jamii wanamoishi.

    Date posted: September 25, 2019
  • Andika kinyume. Sufuria iliyoinjikwa mekoni ni chafu.

    Date posted: September 25, 2019
  • Tunga sentensi kudhihirisha maana ya msemo ufuatao. enda benibeni.

    Date posted: September 25, 2019
  • Andika visawe vya maneno haya; i) Wajihi ii) Laazizi

    Date posted: September 25, 2019
  • Sahihisha kwa kutumia kirejeshi cha mazoea. Kambarau ambao iliyoundwa vyema haitatizi.

    Date posted: September 25, 2019
  • Tambua matumizi ya kiambishi -ji- katika sentensi ifuatayo. Jino la jitu hilo lililiwezesha kujilia chakula kingi kuliko mkimbiaji yule.

    Date posted: September 25, 2019
  • Andika upya sentensi ifuatayo ukianzia yambwa tendwa. Wakulima waliwakatia ngamia wote majani ya mti huo.

    Date posted: September 25, 2019
  • Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mistari, Wakazi waligawiwa vyandarua vya mbu lakini wanavitumia kujengea nyua.

    Date posted: September 25, 2019
  • Kanusha Ukiona vyaelea vimeundwa.

    Date posted: September 25, 2019
  • Tunga sentensi mbili tofauti kudhihirisha maana ya neno 'ilimradi'

    Date posted: September 25, 2019
  • Tunga sentensi moja yenye viungo vya sarufi vifuatavyo; i) Kikanushi ii) Kiima katika nafsi ya pili wingi. iii) Kiwakilishi cha wakati uliopita. iv) Mtendewa katika nafsi ya tatu wingi. v) Mzizi wa kitenzi cha silabi moja. vi) Mnyambuliko wa kitenzi kauli ya kutendea.

    Date posted: September 25, 2019
  • Taja sifa mbili bainifu za vokali /i/

    Date posted: September 25, 2019
  • Eleza maana ya sauti.

    Date posted: September 25, 2019
  • Soma kifungu kisha uiibu maswali Ubinafsishaji wa mashirika ya umma ni nguzo kuu katika ulimwengu wa leo. Kimsingi, ubinafsishaji ni hatua na harakati zinazochukuliwa kupunguza kushiriki kwa serikali katika uendeshaji wa mashirika na kuhimiza kupanuka kwa sekla ya kibinafsi.Serikali huweza kuhimiza, kutokana na uuzaji, uhawilishaji wa mali kutoka umiliki wa umma hadi kwenye umilikaji wa sekta ya kibinafsi. Aidha, serikali inaweza kuuza hisa zake kwenye mashirika ya umma. Njia nyingine ni kuchochea ugavi wa zabuni kupitia kwa mikataba ambayo inashindaniwa na mashirika au kampuni tofauti. Lengo kuu la ubinafsishaji ni kuigatuanafasi ya serikali katika utendakazi na uendeshaji wa mashirika.Uuzaji wamashirika ya kiserikali au hisa huwa chanzo cha mapato yanayoweza kutumiwa kuendesha miradi mingine, Hii ni njia ya kupunguza harija ya serikali inayotokana na uendeshaji wa mashirika yasiyoleta faida. Ubinafsishaji huzuia uwezekano wa kuingiliwa kwa mashirika na wanasiasa, huimarisha utamaduni mpya wa muundo wa mashirika na huvunja uhodhi wa kiserikali. Ubinafsishaji huweza kuatika mbegu za ujasiriamali wa raia kutamani kuanzisha amali tofauti. Ubinafsishaji huweza kuyaruhusu mashirika ya kimataifa kutwaa mashirika muhimu nchini, kufutwa kazi kwa wafanyikazi na kuongezeka kwa umaskini. Ubinafsishaji wa sekta zinazohusiana na elimu na afya huweza kuathiri vibaya wenye mapato ya chini. Ubinafsishaji haumaanishi ufanisi wa utendakazi wa makampuni na mashirika. Aidha, ikiwa haupo utaratibu mzuri wa kutathmini au kupima thamani za hisa pana uwezekano wa hisa zinazouzwa kupewa thamani ya juu au ya chini. Maswali a) Bila kupoteza maana iliyokusudiwa na mwandishi wa kifungu, andika muhtasari wa aya ya kwanza na ya pili. (Maneno 35 - 40). b) Dondoa hoja muhimu zinazojitokeza katika aya ya tatu na ya nne. (Maneno 45 - 50)

    Date posted: September 25, 2019
  • Soma taarifa inayofuata kisha uyajibu maswali Matumizi ya sheng' yameshamiri sana nchini Kenya hata miongoni mwa vijana. Ni kilugha ambacho kinakisiwa kuzuka katika miaka ya 60 na 70 katika makazi ya mashariki mwa jiji la Nairobi kama vile Kaloleni, Mbotela/ Bahati na kadhalika.Kwa sasa ni kilugha kilichoenea kwingi nchini Kenya na kuwa kitambulisho cha takriban vijana wengi. Wataalam mbalimbali wanabainisha nadharia mbalimbali kuhusu chanzo cha lugha hii. Kuna nadharia mbili kuu kuhusu asili ya lugha ya Sheng: kwamba kilugha hiki kiliibuka kutokana na wahuni na wakora jijini Nairobi ambao lengo lao Iilikuwa kuwasiliana kwa siri. Nadharia nyingine ni kuwa kilichipuka kutokana na vijana ambao walizua lugha ya kuwasiliana baada ya uhuru (kwa sababu walikichukia Kiswahili ambacho walikiona kama lugha ya uboi) Dhana hizi kwa muda mrefu, zimeathiri mitazamo kuhusiana na kilugha hiki. Kwa sasa ni kilugha ambacho ,yjiasambaa katika sehemu mbalimbali za Kenya na watu wa matabaka mbalimbali wanakitumia. Kilugha hiki kimeanza kuashiria uhalisia mkubwa wa maisha ya kisasa, zaidi katika jamii ya Wakenya. Aidha, sheng imejitanzua kutoka hali ya kuwa kilugha cha maongezi pekee na sasa kinatumiwa katika baadhi ya vitabu, hata waandishi wa vitabu wameanza kukitumia. Kwa mfano, katika miaka ya 80, David Mailu katika kitabu chake 'Without Kiinua Mgongo' alitumia Sheng. Katika siku za hivi karibuni, riwaya ya 'Kidagaa Kimemwozea' iliyoandikwa na Ken Walibora kilugha cha sheng kimepewa nafasi kama kitambulisho cha vijana kupitia kwa mhusika DJ Bob. Vilevile kumezuka vyombo vya habari kama redio, mfano idhaa ya Ghetto, redio ambayo inaendeleza mawasiliano kwa matumizi ya Sheng. Kuna vipindi vya matangazo ya kibiashara katika runinga ambayo yanaendelezwa kwa Sheng. Kwa mfano, katika 'gazeti la Taifa Leo, kuna ukumbi wa 'Mchongoano' ambao umekuwa ukiendelezwa kwa Sheng. Nchini Kenya ambapo asilimia 60% ya idadi ni vijana, Sheng imetokea kuwatambulisha vijana. Katika enzi hii ya Teknohama. wanaomiliki vyombo vya habari na sekta nyingine za biashara wamegundua kuwa matumizi ya Sheng ndiyo njia mwafaka zaidi ya kulifikia soko kubwa la vijana kwa ajili ya kueneza matangazo ya bidhaa na huduma za kibiashara. Kwa hivyo, Sheng imekuwa daraja la kuwafikia na kuwavutia vijana. Hata hivyo, kwa upande mwingine matumizi ya Sheng yamelaumiwa na walimu wengi katika shule za msingi na zile za upili kuwa ni sababu mojawapo kuu ya kushuka kwa matokeo ya lugha ya Kiswahili na Kiingereza miongoni mwa wanafunzi. Sheng imelaumiwa kwamba inasababisha wanafunzi kutozingatia mafunzo ya kanuni za sarufi na tahajia au maendelezo. Wataalam wanadai kuwa ni msimbo ambao hauzingatii sheria za sarufi na tahajia kwa sababu zisizofahamika, kwani ingawa muundo wake wa kisarufi hushahabiana na ule wa Kiswahili, Sheng hupuuza sarufi ya Kiswahili katika matumizi yake. Ingawa sheng imekuwa ikipigwa vita, kuna wataalam ambao wana mtazamo kwamba juhudi hizo haziwezi kufanikiwa kwani Sheng ni chombo cha mawasiliano miongoni mwa vijana na kwa hivyo ina umuhimu wake ambao hauwezi kufumbiwa macho. Wanasema kuwa ni chombo ambacho kinafumbata hisia na mshikamano wa kizazi kipya kama ilivyojitokeza katika kauli mbiu ya mgombeaji urais mwaka wa 2012,'Tunawesmake. Katika hali ambapo kiwango cha ubora wa matokeo ya Kiswahili yalidorora katika mtihani wa kidato cha nne (KCSE) mwaka wa 2012 na kuwa asilimia 35.81 pekee yakilinganishwa na asilimia 48.82 ya mwaka 2011, Sheng imekuwa ikilaumiwa kuwa ndicho chanzo cha kudorora kwa viwango vya ubora wa matokeo. Baadhi ya hao wataalamu wanasema kwamba Sheng haipaswi kuhujumiwa. kinachohitajika kufanywa ni kuwaelimisha vijana kuhusu mipaka ya matumizi yake. Maswali a) Taja mada ya kifungu hiki. b) Fafanua nadharia mbili zilizoeleza asili ya lugha ya sheng. c) Eleza matumizi bainifu ya kilugha cha Sheng katika jamii ya sasa. d) Taja matokeo hasi ya matumizi ya Sheng katika jamii. e) Ni kwa nini mwandishi Walibora ameshirikisha matumizi ya Sheng katika kazi yake ya Kidagaa Kimemwozea f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika kifungu hiki. i) Teknohama ii) kudorora iii) msimbo iv) Kuhujumiwa

    Date posted: September 25, 2019
  • Uozo katika jamii ni maudhui yaliyoshughulikiwa pakubwa katika diwani ya Damu Nyeusi na Hadithi nyingine. Kwa kurejelea hadithi zozote tano fafanua kauli hii.

    Date posted: September 25, 2019
  • Damu Nyeusi na Hadithi nyingine : Ken Walibora na Said A. Mohamed "Ingawa walifahamu sababu ya kuitwa pale mpango uliokuwepo ulikuwa usiku wa giza." (a) Fafanua muktadha wa maneno haya. (b) Eleza tamathali iliyotumika katika dondoo hili. (c) Onyesha vile wahusika mbalimbali hadithini waiivyoathiriwa na sababu ya kuitwa pale.

    Date posted: September 25, 2019
  • "Ndoto za uhuru barani Afrika imegeuka kuwa jinamizi, jinamizi inayowafanya wazalendo kulia Kidagaa kimetuozea". Ukirejelea riwaya ya kidagaa kimemwozea eleza sababu za wazalendo kulia Kidagaa kimetuozea.

    Date posted: September 25, 2019
  • RIWAYA YA KIDAGAA KIMEMWOZEA. Mtoto ni mtoto hata likiwa bonge la nyama. Mtu hupata ajaliwalo sio alitakalo. (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (b) Eleza tamathali ya lugha iliyotumika katika usemi huu. (c) Ukirejelea riwaya thibitisha kuwa mtu hupata ajaliwalo silo alitakalo.

    Date posted: September 25, 2019
  • Fafanua jinsi maudhui ya unafiki yamejidhihirisha katika tamthilia ya Mstahiki Meya, ukirejelea wahusika wowote watano.

    Date posted: September 25, 2019