Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

onyesha matumizi ya tashhisi katika hadithi fupi ya samaki wa nchi za joto

onyesha matumizi ya tashhisi katika hadithi fupi ya samaki wa nchi za joto

Answers


KELVIN
? Nilivaa tabasamu niliyowahifadhia wanaume, tabasamu ya geresha-Christine kwa Peter.
? Nilijaribu kumjibu lakini sauti ilinikwama kooni. Ukatokea mnong’ono.
? Aibu ilinivaa-Christine akitoka kwa Zac baada ya kukutana na Peter kwa kushindwa kumjibu Peter au kusema haja ya moyo wake.
? Nilikuwa nikiwangwa na kichwa changu kutokana na hedhi.
? Springi za kitanda kulalamikia uzito wake wa ziada-kutoa kelele Peter alipokalia na kuzidisha uzito.
? Mvinyo ulikuwa umenipa ujasiri fulani-Christine kutojishughulisha na Peter.
? Macho yake kila mara yalinihukumu-ya Deogracius.
? Wacha ukimwi uwateketeze-uwaangamize-wakati amemsindikiza Peter akielekea Nairobi.
? Kutokana na mpito wa wakati, nywele za Peter kuwa zinabadilika rangi pengine kutokana na shinikizo la biashara ya nchi za nje ya samaki.
? Nikaachwa nikiadhibiwa na mikondoo ya macho ya watu-baada ya kubusiwa shavuni na Peter.
? Jua liliendelea kuadhibu kila kiumbe –kuwaka vikali Christine akiwa katika matatu.

kalvinspartan answered the question on August 15, 2018 at 12:33

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions