Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Huku ukitoa mifano jadili matatizo yanayokumba uundaji wa istilahi za kiswahili na jinsi yanavyoweza kutatuliwa

Huku ukitoa mifano jadili matatizo yanayokumba uundaji wa istilahi za kiswahili na jinsi yanavyoweza kutatuliwa

Answers


Faith
Kwanza,kuna istilahi mbalimbali ambazo hutumiwa kurejelea dhana moja,yaani zinatumiwa kama visawe.mfano
Nuklia/Tonoradi - Nuclear Bomb
Kansa/saratani - cancer
Vokali/irabu - vowel
Mifano Hii inaonyesha kwamba neno la kutoholewa na la kutafsiriwa yanatumika pamoja.Tatizo hili linaweza kutatuliwa iwapo neno moja liwe la kutoholewa au kutafsiriwa ndilo liwe maana halisi ya neno lile.
Pili,kuna istilahi zimetafsiriwa neno kwa neno yasni tafsiri sisisi na hivyo basi kipotosha maana .mifano
Cold war - vita baridi
Cocktail party - karamu ya mkia wa jogoo
Tatizo hili linaweza kutatuliwa iwapo misamiati mbadala ibuniwe kuliko kutumia tafsiri sisisi.
Tatu,kuna istilahi nyingi ambazo zimekopwa na kutoholewa hata pale amvapo neno asilia la kiswahili au la lugha yoyote ya kibantu lingetumiwa kwa mfano
Daktari. - tabibu au mganga
Hospital- gango
Tatizo hili linaweza kutatuliwa iwapo watumizi wa lugha ya kiswahili watajaribu kutumia maneno asili ya kiswahili au ya lugha yoyote ya kibantu kuliko kutumia yale yaliyokopwa.
Nne,kuna istilahi ambazo huendelezwa kwa njia tofauti kutegemea matamshi au maandishi ya maneno yanayokopwa.mifano
Ofisi/Afisi - Office
Agosti/Ogasti - August
Katika mifano hapo juu huwezi kujua huwa ni lipi neno sahihi la kutumia hivyo basi,tatizo hili linaweza kutatuliwa iwapo kutakuwepo na utaratibu mmoja wa kuunda istilahi hizo za maneno ya kiswahili.



Titany answered the question on December 6, 2021 at 11:25

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions