Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

"Kiswahili sio lugha ya Afrika Mashariki tu,bali ni lugha ya kimataifa."Jadili kauli hii

"Kiswahili sio lugha ya Afrika Mashariki tu,bali ni lugha ya kimataifa."Jadili kauli hii

Answers


Faith
1. Lugha ya kiswahili hufundushwa katika vyuo vikuu mbalimbali barani Afrika,huko Marekani kuna mipango ya kufundisha Kiswahili kwa wataalamu ambao wanatarajia kuja Afrika Mashariki kufanya kazi zao.
2. Lugha ya kiswahili hutangazwa katika idhaa mbalimbali barani Afrika, Marekani na Ulaya kama vile redio Rwanda, All radio India,Redio Chaina Kimataifa na BBC. Idhaa hizi huchangia sana kukuza na kueneza Kiswahili kote ulimwengu.
3. Lugha ya Kiswahili hutumiwa katika kuchapisha majarida katika mataifa mbalimbali kama vile mwanga nchini Rwanda,lugha nchini Sweden, Swahili Forum nchini Ujerumani.
4. Hivi sasa lugha ya kiswahili inasemekana kuwa katika nafasi ya kumi miongoni mwa lugha za Kimataifa zilizo na idadi kubwa ya wazungumzaji kote ulimwenguni. Wazungumzaji wa Kiswahili ulimwenguni wanakadiriwa kuwa takriban watu millioni mia moja.

Titany answered the question on December 6, 2021 at 11:27

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions