Trusted by millions of Kenyans
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Ni vipi Kiswahili kinaweza kuimarisha umoja katika Afrika Mashariki na kati?

Ni vipi Kiswahili kinaweza kuimarisha umoja katika Afrika Mashariki na kati?

Answers


Faith
• Kufundisha Kiswahili katika vyuo vikuu na pia shule zote za Afrika Mashariki na kati. Kwa njia hii wahadhiri na walimu wa Kiswahili wanaweza kuajiriwa katika nchi yoyote.
• Kutangaza Kiswahili katika vyuo vingi vya redio na runinga za nchi za Afrika Mashariki na pia vituo hivyo vinaweza kuwa na mipango ya kubadilisha vipindi kwa Kiswahili.
• Kuwa na soko la pamoja la uuzaji wa vitabu vya Kiswahili.Kwa njia hii,vitabu vilivyochapishwa nchini Kenya vinaweza pia kuuzwa katika nchi zingine na vikatumika katika shule na vyuo vya huko.
• Kuwa na Baraza la Kiswahili la Afrika Mashariki na kati linalojumuisha wasomi na wapenzi wa Kiswahili kutoka nchi zote za Afrika Mashariki na kati.Kwa njia hii wataweza kushirihikiana katika usanifishaji na ukuzaji wa Kiswahili.
• Kutumia Kiswahili kama lugha rasmi ya mawasiliano katika vikao vya jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo tayari imefufuliwa na pia katika vikao vingine vya kibiashara na vikao vingine you.
• Kuchapisha na kusambaza magazeti na majarida ya Kiswahili katika nchi zote za Afrika Mashariki na kati.Majarida hayo kama vile Mulika,Taifa leo na kadhalika.
• Kuhimiza bendi za wanamuziki wa Afrika Mashariki na kati kutunga nyimbo nyingi kwa Kiswahili na pia kuzuru nchi jirani kuwatumbuiza wananchi wa huko.
• Kutumia Kiswahili kama lugha ya taifa na lugha rasmi ya kuendesha shughuli za serikali katika nchi zote za Afrika Mashariki na kati.


Titany answered the question on December 6, 2021 at 11:29

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions