Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Questions and answers: Kiswahili

Q&A Categories


Do you have Q&A pairs? Post them here

2287 Questions  View: All | Solved | Unsolved



Search Results...
  • Sahihisha sentensi zifuatazo. i. Hao mandugu wamekosana juu ya pesa. ii. Mtu mwenye anakula mkate ametumana aletewe chai.(Solved)

    Sahihisha sentensi zifuatazo. i. Hao mandugu wamekosana juu ya pesa. ii. Mtu mwenye anakula mkate ametumana aletewe chai.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Geuza kwa wingi. i. Njia hii huenda Kisumu ii. Wembe huu utafaa.(Solved)

    Geuza kwa wingi. i. Njia hii huenda Kisumu ii. Wembe huu utafaa.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Kanusha sentensi ifuatayo: Ningalifuzu katika mtihani wangu ningalituzwa.(Solved)

    Kanusha sentensi ifuatayo: Ningalifuzu katika mtihani wangu ningalituzwa.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Sahihisha sentensi ifutayo. Sukari zilizowekwa mfukoni zimenyeshewa.(Solved)

    Sahihisha sentensi ifutayo. Sukari zilizowekwa mfukoni zimenyeshewa.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Onyesha vitenzi kisha uvieleze ni vya aina gani. i. Kakangu amewahi kutembelea makavazi ya kitaifa. ii. Hamisi ni daktari wa meno.(Solved)

    Onyesha vitenzi kisha uvieleze ni vya aina gani. i. Kakangu amewahi kutembelea makavazi ya kitaifa. ii. Hamisi ni daktari wa meno.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Ainisha sentensi hii: Kilichopikwa(Solved)

    Ainisha sentensi hii: Kilichopikwa

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Andika maneno yaliyo na aina za silabi zifuatazo: i. Silabi za irabu pekee ii. Silabi za konsonanti, nusu irabu na irabu iii. Silabi za konsonanti pekee(Solved)

    Andika maneno yaliyo na aina za silabi zifuatazo: i. Silabi za irabu pekee ii. Silabi za konsonanti, nusu irabu na irabu iii. Silabi za konsonanti pekee

    Date posted: November 25, 2022.  

  • SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI. Malezi mema Malezi bora si yale, mtoto kumdekeza Atafikia kilele, mzazi atampuza(Solved)

    SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI. Malezi mema Malezi bora si yale, mtoto kumdekeza Atafikia kilele, mzazi atampuza Utapiga makelele, wala hatasikiza. Daima usikubali, kuridhi kumpendeza Lazima uwe mkali, mengine kumkataza Na wala usikubali, maneno kuyaigiza. Mtoto ukimuita, hana budi kuginiza Sio mdomo kufyata, mamboye kuendeleza Ama dakika zapita,aje ikimpendeza. Mzazi usithubutu,mwanao kumteteza Uambiwapo na watu, mwanao alifanyiza Kuwa na hali ya utu, Kadhia kuchunguza. Iwapo amekusudi, makossa kuyatimiza Kumrudi huna budi,jukumu kutekekeza Lau usipomrudi, kosa taliendeleza. Maswali a) Eleza malezi mema jinsi yanavyosimuliwa na mshairi. b) Taja mambo matano wanayoshauriwa wazazi kutoyatenda c) Je, mzazi asipochukua jukumu lake, kuna athari gani kwa mtoto d) Toa methali moja inayoambatana na ujumbe wa Shairi hili e) Shairi hili lina mishororo ngapi f) eleza vina,vipande na mizani vya Shairi hili g) eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika Shairi. i. kumdekeza ii. kuginiza iii. mdomo kufyata iv. alofanyiza v. lau usipomrudi

    Date posted: November 25, 2022.  

  • “nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayuko" i. tambua kipera hiki ii. taja dhima moja ya kipera hiki kijumla(Solved)

    “nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayuko" i. tambua kipera hiki ii. taja dhima moja ya kipera hiki kijumla

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuatia Malenga mlotukuka, kwa tungo zenu teule Tungo zenye kusifika, zenye nasaha tele(Solved)

    Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuatia Malenga mlotukuka, kwa tungo zenu teule Tungo zenye kusifika, zenye nasaha tele Naomba la uhakika, jawabu enyi wavyele Wa kuume tangu lini, kuukata wakushoto! Tangu dahari miaka, mikono ina upole Meungana pasi shaka, ni miwili vile vile Mmoja ukisumbuka, mwingine hujaa ndwele Wa kuume tangu lini, kuukata wa kushoto! MASWALI a. Shairi hili ni la arudhi. Dhibitisha kwa kutoa sababu tatu b. Nakili kibwagizo cha shairi hili c. Eleza ujumbe mmoja unaojitokeza kwenye shairi

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Matumizi ya lugha hutegemea mambo kadhaa. Yaeleze yoyote manne.(Solved)

    Matumizi ya lugha hutegemea mambo kadhaa. Yaeleze yoyote manne.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Tunga sentensi moja na uonyeshe kiwakilishi kimilikishi.(Solved)

    Tunga sentensi moja na uonyeshe kiwakilishi kimilikishi.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Kwa kutumia sentensi moja onyesha vitenzi sambamba.(Solved)

    Kwa kutumia sentensi moja onyesha vitenzi sambamba.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Bainisha kivumishi katika sentensi hii. Matunda mawili yaliuzwa.(Solved)

    Bainisha kivumishi katika sentensi hii. Matunda mawili yaliuzwa.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Taja dhana zinazowakilishwa kisarufi na viambishi vilivyopigwa mistari. Walituchezea(Solved)

    Taja dhana zinazowakilishwa kisarufi na viambishi vilivyopigwa mistari. Walituchezea

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Bainisha ngeli ya nomino iliyopigiwa mistari. Jeshi la Kenya lilihamisha kifaru hadi mbuga ya Masai mara.(Solved)

    Bainisha ngeli ya nomino iliyopigiwa mistari. Jeshi la Kenya lilihamisha kifaru hadi mbuga ya Masai mara.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Tambua aina za maneno zilizopigiwa mistari. Mwanafunzi mrefu alienda Nairobi(Solved)

    Tambua aina za maneno zilizopigiwa mistari. Mwanafunzi mrefu alienda Nairobi

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Tunga sentensi moja na uonyeshe nomino dhahania.(Solved)

    Tunga sentensi moja na uonyeshe nomino dhahania.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Tambua sauti yenye sifa zifuatazo. konsonanti, kipasuo, ghuna, sauti ya mdomo.(Solved)

    Tambua sauti yenye sifa zifuatazo. konsonanti, kipasuo, ghuna, sauti ya mdomo.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Taja ala sogezi mbili za kutamkia.(Solved)

    Taja ala sogezi mbili za kutamkia.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali FUNGUA SESAME Jina la Nimrod lilipotea mara tualipoanza kufanya kazi jijini Nairobi.(Solved)

    Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali FUNGUA SESAME Jina la Nimrod lilipotea mara tualipoanza kufanya kazi jijini Nairobi. Marafiki na jamaa zake waliamini kuwa alikuwa ameajiriwa huko mjini ingawa hakuna aliyeijua kazi yenyewe vizuri. Hata hivyo waliamini kuwa lazima alikuwa na kibonge cha kazi kwa sababu alivalia kinadhifu na kuishi maisha ya starehe. Tena yeye mwenyewe alikazania kusema kuwa amejiriwa kazi ya maana. Marafiki zake walimfahamu kama “Bwana Sesame”. Mtu wa kwanza aliyempa jina hilo alisema alipendezwa na ujuzi na maarifa yake. “huyu hakosi ufumbuzi wa tatizo lolote. Ni kama ule mlango wa kisa cha Ali Baba na Wezi arobaini. Ukisema ‘fungua Sesame’ unafungu katu,” alisema mtu huyo. Jamaa walioishi naye katika mtaa wa Urumo walishangazwa na utaratibu wake wa kazi. Mchana kutwa alishinda chumbani mwake. Mara nyingi utamkuta ametulia akitazama runinga yake ndogo. Wakati mwingine atakuwa akifanya kazi yake ndogo ndogo huku akipiga mluzi bubu, ambao haukusikika vizuri. Wakati mwingine atakuwa akiusikiliza muziki kwenye chombo chake cha muziki kilichotingisha jingo zima kutokana na sauti yake nene. Kwa kawaida alitoka chumbani jioni. Waliomjua walimchangamkia kutokana na uchangamfu wake. Alipenda sana mizaha. Waliopenda kupiga soga walivutiwa na maongezi yake hasa kuhusiana na magari. Aliyajua magari mengi. Mimi naweza kuijua aina ya gari kwa kuusikiliza mlio wake tu”, alisema kila wakati. “wacha kutuvungavunga Bwana wee, haiwezekani !” atasema mwingine. “nini? Unajua mimi ndiye Bwana Sesame mwenyewe!” atasema, halafu wote wataangua kicheko. Ilifika wakati kampuni kadha zilipoamua kuwapunguza wafanyakazi wake kutokana na hali mbaya ya kiuchumi. Lakini Bwana Sesame hakuwa mmoja wa hao. Hali yake ilibakia vile vile. Aliendelea kuvalia kinadhifu na kuishi maisha yake ya fawaishi. Wakati wenzake wanalalamikia hali ngumu ya maisha, Bwana Sesame hakuwa na lolote la kumsumbua. Aliendelea kukaa bila kazi wala bazi. Lakini watu walitambua kuwa alikua na mazoea yakutoka chumbani majira ya jioni. Hakuna aliyejua alirejea lini. Sikumoja Bwana Sesame alitoka jioni kama kawaida na kuelekea kwenye shughuli zake za kawaida. Siku hiyo jamaa mmoja wa mtaani alikumbana naye kwenye lango kuu. “Bwana Sesame,leo wapi yahe?alimwuliza. Bwana Sesame alimwangalia na kusema, “natoka nje kidogo yahe. Jiji hili lataka ustaarabu,’ alijibu. Yule jamaa alimwangalia na kumwabia, “nina shida kidogo, sijui kama utanifaa mwenzangu. Wajua tena hali zenyewe siku hizi,” alisema. Nini tena?’ aliuliza Bwana Sesame. “Nina gari langu ambalo halina redio. Natafuta moja ya bei nafuu.... Kitu kama sony hivi,” alisema. Bwana Sesame alimwangalia na kusema, “hiyo kazi nyepesi kwangu yahe, papai kwa kijiko!” alisema Bwana Sesame akicheka. Jamaa Yule alishukuru na wakaagana. Bwana Sesame alishika njia kuelekea sehemu zake za kawaida majira kama haya.Naye Yule jamaaa kapinda kama anaangalia mtaani, lakini baada ya muda akageuka na kuamua kumfuata Bwana Sesame. Bwana Sesame alishika tariki mpaka sehemu ya mazoea. Yule jamaa alimfuata kwambali na mwendo wa paka. Alimwona Bwana Sesame akiingia mahali palipokuwa na banda kuukuu. Muda si muda alitoka na jamaa wengine wakiwa wamevalia maguo ya ajabu. Yule jamaa aliwafuata hadi mahali palipokuwa na ujia mwembamba ulioachana na barabara kuu. Alijificha mahali, na kutokana nahali ya sehemu ile akawa haonekani. Muda si muda palitokeza gari dogolililokuwa likiendeshwa na mwanamke mmoja. Bwana Sesame na wenzake walitokeza na kutupa gogo lililomzuia Yule mwanamke. Ghafla bin vuu walimvamia; wakaifungua milango ya gari mbio na kujivurumisha ndani. Gari lilitimuliwa kama risasi kuelekea upande wa pili. Wakati huo Yule jamaa ashaliangalia gari lenyewe na kuzihifadhi nambari zake. Alishika njia kurudi zake chumbani. Siku iliyofuata huyo jamaa hakuwa kazini. Alipokuwa akifungua kinywa alisikia sauti ya kugongwa kwa mlango. Aliinuka na kwenda kuufungua. Bwana Sesame aliingia ndani. “vipi yahe? Hujenda kazini leo? Au umelala sana Bwana?’ alisema Bwana Sesame kwa uchangamfu wake. Muda si muda alimwonyesha redio ya gari aliyokuwa nayo. “umeipata mara moja hii kumbe?’ aliuliza Yule jamaa. “si nilikwambia yahe! Mimi ndiyeBwana Sesame mwenyewe. Hii kwangu si kazi. Ninafahamiana na jamaa wengi wanaoifanya kazi hii,” alisema Bwana Sesame. “naona kweli. Ehh Bwana we! Ndipo waswahili wakasema,ukitaka kuvua vua na wavuvi! Alisema Yule jamaa. “ni kweli kabisa!’” alijibu Bwana Sesame huku akicheka kwa furaha. Yule jamaa alisimama kuelekea chumbani. Bwana Sesame alitulia akisubiri kupokea ujira wake. Muda mfupi ulipita, kasha mlango wa nyumba ukagongwa. “yahe Bwana, kunagogwa huku!” Bwana Sesame akasema. Yule jamaa alitoka chumbani na kuelekea mlangoni. Mlango ulipofunguliwa waliingia askari polisi wawili. Bwana Sesame hakuwa na upenyu wakutokea. Alitiwa mikononi.Hakujua kumbe Yule jamaa alikuwa kachero. Hapakuwa na ujanja tena. Siku hiyo pwagu alipata pwaguzi. Fungua Sesame haikufaa tena. Maswali 1. Kwa nini Nimrod alibatizwa ‘Bwana Sesame’? 2. Kwa nini watu walioishi mtaani Urumo walishangazwa na utaratibu wa kazi wa Bwana Sesame? 3. Unafikiria ni kwanini Bwana Sesame alifahamu sana juu ya magari? 4. Je, unafikiri yule jamaa aliagiza aletewe radio alikuwa na haja sana na kifaa hicho kama alivyosema? 5. Bwana Sesame alikuwa kachero. Unakubali? Toa maelezo? 6. Yule jamaa alipoingia chumbani na kumwancha Bwana Sesame sebuleni unafikiria alikwenda kufanya nini 7. Je, hadithi hii ina mafunzo gani kwako? 8. Eleza maana ya misemo ifuaayo kasha itumie katika sentensi a) Piga mluzi b) Piga soga c) Shika tariki

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Taja vipera vitano vya semi.(Solved)

    Taja vipera vitano vya semi.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata. Mwatani: Rusha hiyo ball haraka tumechelewa five minutes. Twende daro. Omoshi: Harakisha mode anacome.(Solved)

    Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata. Mwatani: Rusha hiyo ball haraka tumechelewa five minutes. Twende daro. Omoshi: Harakisha mode anacome. Bwana Kipiti: Nendeni darasani haraka! Kisha kiranja awape vitabu vyenu vya insha ili mwandike barua. Mwatani: Sawa mwalimu. Samahani kwa kuchelewa uwanjani. Omoshi: Je, tutaandika barua rasmi au barua ya kawaida? Bwana Kipiti: Mwandike barua rasmi. Je, mnakumbuka muundo wake? Omoshi na Mwatani: Ndio mwalimu. Ulitufundisha jana. Asante sana mwalimu. Bwana Kipiti: Kumbukeni idadi ya maneno. Idadi ya maneno ni muhimu katika uandishi wa insha. (i) Eleza sajili katika dondoo. (ii) Eleza sifa nane za sajili hii zinazopatikana katika dondoo.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Ainisha vielezi katika katika sentensi ifuatayo. Mwanafunzi mzuri ni yule afanyaye mazoezi vizuri kila siku shuleni.(Solved)

    Ainisha vielezi katika katika sentensi ifuatayo. Mwanafunzi mzuri ni yule afanyaye mazoezi vizuri kila siku shuleni.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Tumia o-rejeshi kati katika sentensi ifuatayo. Kuta ambazo zilijengwa zimebomoka.(Solved)

    Tumia o-rejeshi kati katika sentensi ifuatayo. Kuta ambazo zilijengwa zimebomoka.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Kamilisha methali ifuatayo. Asiye na nadhari...(Solved)

    Kamilisha methali ifuatayo. Asiye na nadhari...

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Andika kwa wingi. Kuwepo kwa mshauri wake kulimfurahisha waziri.(Solved)

    Andika kwa wingi. Kuwepo kwa mshauri wake kulimfurahisha waziri.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Badilisha kitenzi kisaidizi kilicho kwenye sentensi ifuatayo kiwe kishirikishi. Mvule alikuwa akilala bwenini.(Solved)

    Badilisha kitenzi kisaidizi kilicho kwenye sentensi ifuatayo kiwe kishirikishi. Mvule alikuwa akilala bwenini.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Andika sentensi ifuatayo katika ukubwa. Uteo alionunuliwa umezeeka sana.(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika ukubwa. Uteo alionunuliwa umezeeka sana.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Yakinisha: Usipolipa usiingie ndani.(Solved)

    Yakinisha: Usipolipa usiingie ndani.

    Date posted: November 25, 2022.