-
Andika kwa umoja
Tumewaondoleeni matatizo yenu, yafaa mtushukuru.
Date posted:
June 27, 2019
-
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Mwanamke wa kisasa anazaliwa na kukulia katika mazingira yaliyobadilika mno.
Matazamio yake maishani ni tofauti na yale ya wanawake walioishi mapote mawili
yaliyopita; wanawake makamu ya nyanyake na mamaake-kuu.
Yeye hatarajii kuzaliwa, kukua, kuolewa, kuwa mke wa bwana, kumzalia watoto, na
daima dawamu kuwa ‘mwendani wa jikoni’ akawapikia watoto na bwanake chakula; na
akitoka jikoni aelekee shambani kulima, kichakani kuchanja kuni, mtoni kufua nguo na
kuteka maji ya kutumia nyumbani. Mwanamke wa kisasa huandamana na mwanamume.
Akanyangapo mume naye papo huutia wayo wake.
Mwanamke wa kisasa huenda shule na kujifunza yote yafunzwayo huko. Hushindana na
wanawake kwa wanaume na kuibuka mshindi si mara haba. Huibuka mshindi katika
masomo ya lugha, historia, jiografia, hesabu, sayansi na mengineyo, sawa na
mwanamume.
Mwanamke wa kisasa hutaka kufanya kazi za kibega, akazifanya. Akataka kuwa
mwalimu, akawa. Akataka kuwa daktari, akafanikiwa. Almuradi, siku hizi mwanamke
hufanya kazi yoyote ile afanyayo mwanamume. Kuna wanawake marubani wa ndege,
masonara, waashi, wahandishi, madereva wa magari, mawakili, mahakimu, mawaziri
wakuu na hata marais wa nchi. Hakuna kazi isiyofanywa na mwanamke siku hizi.
Mwanamke wa kisasa hateswi akafyata ulimi. Anapohiniwa yeye hupigania haki yake
kwa dhati na hamasa. Katu hakubali ‘mahali pake’ katika jamii alipotengewa na
wanaume wenye mawazo ya kihafidhina yaliyopitwa na wakati.
Siku hizi mwanamke huolewa tu wakati amepata kazi ya kumwezesha kujikimu maishani
au pale anapokuwa na hakika kwamba biashara yake, iwapo ni mfanyi biashara, imepiga
hatua ya kutomrudisha ukutani.
Mwanamke wa kisasa haamuliwi katika jambo lolote, bali hufanya maamuzi yake
mwenyewe. Kwa upande mwingine, mwanamume wa ‘kisasa’, ambaye bado amefungwa
pingu na taasubi za kiume, hapendezwi na mwanamke huyu. Huuma kidole akatamani ya
kale, lakini wapi! Analazimika kumkubali mwanamke huyu kama mshirika sawa
maishani, na kuishi naye, apende asipende. Shingo upande analazimika kukubali kwamba
mabadiliko haya sio mithili ya kiwingu kipitacho, bali ni ya aushi.
a) Msemo ‘mwendani wa vijungu jiko’ unadhihirisha hali gani ya
mwanamke katika jamii?
b) Jamii imemfanya mwanamke kuwa hayawani wa mizigo. Fafanua
c) Eleza maana ya ‘akanyagapo mume papo huutia wayo wake.’
d) Zungumzia maswala ya ndoa na elimu huku ukilinganisha mwanamke wa
kiasili na wa kisasa.
e) Mwanamume wa kisasa anamwonaje mwanamke wa kisasa?
f) Taja mifano minne ya ‘mawazo ya kihafidhina.
g) Eleza maana ya:
(i) Akafyata ulimu……………………………………………
(ii) Ukatani…………………………………………………….
(iii) Taasubi za kiume………………………………………….
(iv) Aushi…………………….………………………………..
Date posted:
June 27, 2019
-
Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia kirejeshi ( kihusiano) cha ngeli cha mwisho
Mwanafunzi anayefanikiwa maishani ni yule anayesoma kwa bidii na pia
anayetii wakuu wake
Date posted:
June 27, 2019
-
Tumia semi hizi katika sentensi kuonyesha maana:
(i) Kuchokoachokoa maneno
(ii) Kumeza shubiri
Date posted:
June 27, 2019
-
Tunatumia viashiria vya kuthibitisha kwa mfano kitabu kiki hiki. Sasa kamilisha
Ni mbwa …………………….. aliyekula chakula cha mtoto
Date posted:
June 27, 2019
-
Eleza tofauti mbili muhimu za kimaumbile kati ya wanyama
(i) Kifaru
(ii) Nyati
Date posted:
June 27, 2019
-
Watu wafuatao wanafanya kazi gani
(i) Mhasibu
(ii) Mhazili
Date posted:
June 27, 2019
-
Tumia viunganishi vingine badala ya vile vilivyotumiwa katika sentensi hizi:
(i) Anayetafuta hachoki hata akichoka keshapata
(ii) Ngonjeeni hadi washiriki wote wafike
Date posted:
June 27, 2019
-
Taja madini mawili ambayo yametukuzwa zaidi, moja kwa thamani yake ya
kifedha na nyingine kwa kutengeneza vyuma vigumu kuliko madini mengine
Date posted:
June 27, 2019
-
Onyesha kielezi, kivumishi, kitenzi na jina katika sentensi:
Watu wane walipeperushwa juu kwa juu na upepo mkali
Date posted:
June 27, 2019
-
Akifisha kifungu hiki:
Nilopomwendea aliniangalia kisha akaniambia siamini kuwa ni wewe uliyeandika
insha hii.
Date posted:
June 27, 2019
-
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata
Kuna sayansi mpya inayoitwa “cloning” kwa lugha ya Kiingereza. Pengine kwa sasa tuite
“kutumbisha.” Sayansi hii tayari imeleta mapinduzi makubkwa katika uzalishaji mimea
na uvunani. Imesemekana ya kwamba, ghairi ya wivu na kijicho baina ya jamii
mbalimbali ulimwenguni, aina hii ya sayanzi ina uwezo na kuangamiza kabisa janga la
njaa katika sayari hii yetu. Kivipi? Rahisi kabisa. Ni kwamba mbegu moja tu ya aina
yoyote ya mmea, baada ya kuneemeshwa vyumba vyake vidogo ambavyo ndivyo hasa
msingi wa uhai vinaweza kunyunyiziwa dawa maalum ili vitawanyike mara hata
mamilioni na kuwa mimea kamili…. Mamilioni!
Sayansi hii tarari inatumiwa kukuza viazi na vyakula vingine. Hii ina maana ya kwamba
mashamba makubwa si muhimu siku hizi, yaani vyakula vingi kabisa vinaweza kukuzwa
mahali padogo sana. Kwa hivyo hivi karibuni tu, kutakuwa hakuna haja ya kupigania
mashamba.
Vyema. Hebu sasa tuangalie zilizokwishapigishwa hii sayansi ya “kutumbisha” na mahali
binadamu alipofika kimaendeleo kwa sababu ya hatua hizo. Jambo la kwanza sayansi hii
tayari imeshatumiwa kuzalishia wanyama wengi, wengi sana wadogo wadogo kwa lengo
la kuendeleza mbele utafiti. Kufikia sasa, wanyama hawa waliotengenezwa na binadamu
katika maabara yake bado wanahifadhiwa mumo humo walimotengenezwa. Hii ni hatua
kubwa na binadamu anastakili pongezi kwa jinsi anayotumia akili yake kuvumbua ibura
hizi zote.
Hata hivyo imesemwa kwamba kuchamba kwingi ni kuondoa mavi. Binadamu kama
ijulikanavyo, anajaribu sana jujitakasa kwa kujitenga mbali sana na asili yake ya unyama
ili aufikie ubinadamu mkamilifu. Hapana ubaya hapo. Lakini tukirudi nyuma tunakuta ya
kwamba binadamu sasa aneingia tama kubwa sana kuliko wakati wowote ule. Tamaa hii
imeletwa na ujuzi wake katika sayansi hii ya “kutumbisha.” Sasa binadamu ana jua
vizuri sana kwamba kwa vile ana ujuzi wa kutengeza panya na hata kondoo katika
maabara basi hata ujuzi wa kutengeneza binadamu pia anao! Na hapo ndipo tatizo lilipo.
Swali hi hili: Je, ujuzi huu utatufikisha wapi? Na kikomo chake kitakuwaje?
Binadamu sasa ujuzi wake unamtia wasiwasi. Wataalam wa sayansi hii wamejiuliza mara
nyingi nini kitakachotokea ujuzi huu utakapomilikiwa na mwenda wazimu mweledi.”
Watu kadha wa kadha, miongoni mwao wakiwa wanasiasa wamejiuliza mara
zisizohesabika swali hili: kama Hitler angekuwa na ujuzi huu, angekuwa na lazima gani
ya kuwaulia mbali wayahudi milioni sita wasiokuwa na hitia isipokuwa na nywele
nyeusi na hawakuwa weupe sana kama wazungu? Hitler aliamini ya kwamba “mtu
mzuri” ni mwenye pua ya upanga (kama mzungu), macho ya buluu nywele rangi ya dhahabu na mwenye kimo cha futi sita au zaidi kidogo. Hivyo lengo lake lilikuwa ni
kubuni taifa la watu wazuri pekee ambao mwisho watautawala ulimwengu na kuenea
duniani kote. Katika mpango wake, watu weusi wote wangefaa kuangamizwa tu ili watoe
nafasi kwa watu aliowaona yeye kuwa bora.
Sasa baada ya sayansi hili ya “kutumbisha” kuvumbuliwa, wataalam wametishika sana.
Wamewaza jinsi ambavyo Hitler angeweza kufanya kama angekuwa mjuzi wa taaluma
hiyo.
Kitisho hiki kimezidi kuwatwanga wataalam na wasiokuwa wataalam hivi majuzi tu
ilipogunduliwa maiti ya msichana wa miaka kumi na mine huko milima ya Andes,
Amerika ya kusini. Msichana huyo alikuwa ametolewa kafara miaka karne tano zilizo
pita lakini hakuoza kwa sababu ya baridi kali ya barafu milimani.
Kwa sababu ya dukuduku la uvumbuzi ambalo haliishi dhana za kiajabu ubongo wa
binadamu, wataalamu wa “kuchezea” maumbile walipomwona msichana huyo maiti,
upesi upesi wakampima. Walipofanya hivyo wakagundua ya kwamba mayai yake ni
timamu kabisa wala hayajaharibiwa na mpito wa karne. Papo hapo wengine wakajiwa na
wazo la kuyatoa mayai hayo na kuyahifadhi kwenye mabara. Tamaa ikazidi zaidi ya
zaidi. Baadhi ya wataalamu wakajiwa na wazo la “kuyaneemesha” mayai hayo na mbegu
za uzazui za wanaume. Kwa lengo gani? Kuunda watoto amabo mama yao alikufa
zamani za kale ili waonekane watakuwa watu wa aina gani!
Sasa fikiria mwenyewe! Watoto hawa wa maabara wakiwa weledi zaidi ya binadamu
yeyote yeyote wa kisasa lakini watiifu kama mbwa na paka itakuwaje? Hakuna
atakayefikiria “kutumbisha” ili tuwe na vijitumwa vyetu vipenzi majumbani mwetu
vinavyofanana nasi badala ya paka na mbwa wasiovishwa nguo?
(a) Andika kichwa kifaacho kwa nakala hii
(b) Kutumia sayansi ya “kutumbisha” kunaweza kumsaidia binadamu kuangamiza
mabaa gani mawili yanayomkabili sasa?
(c) Unadhani ni kwa nini wanyama waliozalishwa kwa kutumia sayansi hii bado
wamo maabarani?
(d) Fafanua methali “kuchamba kwingi nikuondoka na mavi” kulingana na muktadha
wa habari hii
(e) Kuna ubaya gani kutumbisha watu?
(f) Mwandishi anaonekana kutishwa sana na uwezekano wa sayansi ya kutumbisha
kuishia mikononi mwa “wendawazimu weledi” kwani kuna hatari gani?
(g) Eleza kwa ukamilifu matatizo yanayoweza kuukumba ulimwengu iwapo mayai ya
msichana wa Andes yatatumbishwa
Date posted:
June 27, 2019
-
Bila kunyambua, andika maneno mawili ambayo yanatokana na shina
moja na neno: imani
Date posted:
June 27, 2019
-
Tunga sentensi ya neno moja ambayo ina visehemu vifuatavyo vya
sarufi
- Kiima
- Wakati
- Kirejeleo
- Kiswahili kitendwa
- Kitenzi
Date posted:
June 27, 2019
-
Mahali palipohamwa panaitwa?
Date posted:
June 27, 2019
-
Eleza maana mbili mbili zinazotokana na sentensi zifuatazo
(i) Mtoto alitimua mbio, kuona nyoka
(ii) Juma alifagia chakula
(iii) Sisikii vizuri
Date posted:
June 27, 2019
-
Andika methali nyingine ambayo maana yake ni kinyume cha
Riziki kama ajali huitambui ijapo
Date posted:
June 27, 2019
-
Eleza maana ya misemo ifuatayo kwa kuitungia sentensi moja moja
Kuramba kisogo
Kuzunguka mbuyu
Date posted:
June 27, 2019
-
Bila kubadilisha maana, andika sentensi zifuatazo ukitumia kirejeleo cha ngeli
kifaacho
(i) Nyumbu alishinda farasi kukimbia
(ii) Milango yote yajifunga ovyo, nenda uakafunge
(iii) Hamisi amekata nyasi vizuri
(iv) Jiwe lile liliangukia matunda
Date posted:
June 27, 2019
-
Andika katika kauli ya kutendesha
(i) Nataka upike chakula hiki vizuri
(ii) Toa ushuru wa forodhani
Date posted:
June 27, 2019
-
Badilisha katika udogo kasha uukanushe udogo huo
(i) Guu lake limepona baada ya kuumwa na jibwa la jijini
(ii) Nyumba yenyewe ilijengwa bondeni karibu na mto
Date posted:
June 27, 2019
-
Eleza matumizi ya ‘Po’ katika sentensi hii
Nilipofika nilimwona pale alipokuwa amesimama
Date posted:
June 27, 2019
-
Kutokana na vitenzi tunaweza kuunda majina na pia kutokana na majina
tunaweza kuunda vitenzi. Mfano
Jina Kitendo
Mwuzaji Uza
Mauzo Uza
Wimbo Imba
Sasa kamilisha:
Jina Kitenzi
(i) Mnanda
(ii) Kikomo
(iii) Ruhusa
(iv) ashiki
(v) husudu
Date posted:
June 27, 2019
-
Tunasema: Mtoto huyu mzuri anapendeza
Ukitumia majina yafuatayo kamilisha sentensi ukifuata mfano ulio hapo juu
(i) Ngome
(ii) Mitume
(iii) Heshima
(iv) Ng’ombe
(v) Vilema
Date posted:
June 27, 2019
-
Eleza kazi ifanywayo na
(i) Mhariri
(ii) Jasusi
Date posted:
June 27, 2019
-
Fafanua maana za misemo ifuatayo kwa kuitungia sentensi
(i) Kula uyundo
(ii) Kula uhondo
Date posted:
June 27, 2019
-
Andika sentensi zifuatazo ukitumia kinyume cha neno lililoandikwa kwa herufi za
Mlazo
(i) Usijaribu kupaaza sauti unapoimba
(ii) Huyu ni mtu mwenye busara
(iii) Binadamu hawezi kumuumbua mwenzake
Date posted:
June 27, 2019
-
Eleza maana ya sentensi hizi
(i) Mikono yao imeshikana
(ii) Mikono yao imeshikamana
Date posted:
June 27, 2019
-
Sahihisha makosa yaliyomo katika sentensi mbili zifuatazo
(i) Bei za vitu zimepanda juu sana siku hizi
(ii) Weka mizigo kwa gari
Date posted:
June 27, 2019
-
Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali
Mababu walituachia msemo maarufu kuwa “ Kuzaa sio kazi. Kazi kubwa ni kulea.”
Busara iliyomo katika methali hii inatupambazukia peupe pindi tukianza kuchunguza
maisha ya vijana wa siku hizi katika jamii zote, hasa zile za Afrika. Kwa upande
mmoja, maisha ya vijana hawa yanaonyesha cheche ya matumaini kwa maisha ya siku
za usoni kwa sifa zao za mori na kupenda kujaribu na kushika mambo upesi kama
sumaku. Lakini kwa upande wa pili, tunashuhudia upotevu wa kimawazo na hulka
ambayo ndiyo kipingamizi cha kuendelea kwao kama raia wa kutegemewa.
Kuwanyeshea vijana lawama na kashifa za kila aina hakufai wala hakufui dafu katika
juhudi za kuwaongoza na kuwalea. Kwa hili hatuna budi kusadiki, “mtoto umleavyo
ndivyo akuavyo.” Basi hivyo badala ya kuwashambulia vijana wenyewe. Tutafanya
hivyo kwa imani kuwa “mwiba uchomeako ndiko utokeako.” Kiini cha matatizo ya
vijana wa leo ni namna ya mwongozo na vielezo wanavyopokea kutoka kwa wazazi,
waalimu, viongozi wa kijamii wakiwemo pia wale wa medhehebu tofauti na hasa kutokana na vyombo tofauti vya habari: vitabu majarida, filamu, magazeti na
kadhalika.
Jamii ina haki gani kuwashtumu vijana iwapo mzazi, tangu utotoni mwao
amewahubiria maji na huku mwenyewe anakunywa mvinyo? Kama fasihi na
maandishi mengine wanayoyabugia vijana yamejazwa amali, picha, jazanda na taswira
zinazohimidi ugeni na kutweza Uafrika, tutashangazwa na nini pale vijana
watakapoanza kupania zile zile amali za ugenini? Iwapo jamii na mazingira
wanamokulia vijana yanatukuza kitu kuliko utu. Hatupaswi kupepesa macho na
kukonyeza tunapowaona vijana wakihalifu sheria zote kwa tamaa ya kujinufaisha binafsi.
Ni hoja isiyopingika kuwa kulea sio tu kulisha na kuvisha au kumpeleka mtoto
shuleni sharti itambulike wazi wazi kuwa sehemu kubwa ya elimu na mwongozo
unaoathiri mienendo ya jijana na watoto haitokani na yale waambiwayo bali hasa yote
wanaoyashuhudia kwa macho na hisia zao.
(a) Katika aya ya kwanza, maisha ya vijana wa kisasa yameelezwaje?
(b) Kwa nini vijana hawapaswi kulaumiwa kulingana na mwandishi
Maneno 30 – 35
(c) Eleza sifa za malezi bora
(Maneno 20 – 25)
Date posted:
June 27, 2019