-
Eleza ufaafu wa anwani Chozi la Heri
Date posted:
November 9, 2018
-
Sitaki kazi za uchafu hapa sagamoyo", eleza muktadha wa Dondoo hili katika tamthilia ya Kigogo.
Date posted:
October 18, 2018
-
Mkondo wa shairi ni nini?
Date posted:
October 9, 2018
-
Jadili umuhimu wa tunu katika tamthilia ya kigogo.
Date posted:
October 6, 2018
-
Kamilisha methali zifuatazo:
i))Jogoo hulia uta...
ii)Ukitaka kula nguruwe...
iii)Penye kuku wengi...
iv)Fahali wawili wapiganapo...
v)Bendera hufuata...
vi)Paka akiondoka...
Date posted:
October 1, 2018
-
Kamilisha methali hizi:
a)Ahadi ni...
b)Asiyekuwepo na...
c)Asiyefunzwa na mamake...
d)Barua ni nusu...
e)Debe tupu...
f)Dua la kuku...
g)Akili ni...
h)Akili ni nywele...
I)Maji yakimwagika...
j)Hasira...
Date posted:
October 1, 2018
-
Kamilisha vitendawili vifuatavyo:
1.Nameza lakini sishibi-
2.Mlima sipandi-
3.Kiti cha dhahabu hakikaliwi na watu –
4.Yaenda mbali lakini haiondoki ilipo-
5.Tarishi wangu huwa naye mfukoni-
6.Natembea na nyumba yaangu –
7.Ubwabwa wa mwana mtamu-
8.Kipo lakini sikioni-
9.Tajiri hunitia mfukoni ,maskini hunitupa-
10.Wanangu watatu daima wako pamoja-
11.Likitoka halirudi-
Date posted:
October 1, 2018
-
Kamilisha methali hizi:
a)Njia ya mwongo...
b)Akiba...
c)Mla nawe hafi nawe...
d)Tamaa mbele...
e)Dawa ya moto ...
f)Kikulacho ki...
g)Kuishi kwingi ni...
h)Ukitaka cha mvunguni...
I)Siku za mwizi...
j)Chovyachovya...
Date posted:
October 1, 2018
-
Kamilisha vitendawili vifuatavyo:
1.Anataga huku akitembea-
2.Akitokea kila mtu humwona-
3.Nina saa yangu isiyotiwa ufunguo-
4.Amefunika kote kwa blanketi lake jeusi-
5.Popoo mbili zavuka mto-
6.Ndege wengi baharini-
7.Ajifungua na kujifunika-
8.Amefunua jicho jekundu-
9.Askari wangu wote wamevaa kofia upande-
10.Chakula kikuu cha mtoto-
Date posted:
October 1, 2018
-
Kamilisha vitendawili vifuatavyo:
1.Huku ng’o na kule ng’o-
2.Nyumba yangu ina milango mitatu-
3.Nyumba yangu ina madirisha mengi-
4.Kamba yangu ndefu haifungi kuni-
5.Huku mwamba na huku mwamba-
6.Mama nieleke-
7.Haukamatiki wala haushikiki-
8.Afahamu kuchora lakini hafahamu achoracho-
9.Cheupe chavunjika manjano yatoka-
10.Daima namsikia tu lakini simwoni-
Date posted:
October 1, 2018
-
Eleza maana ya maneno haya:
Sitiri-
Aidha-
Tuza-
Date posted:
October 1, 2018
-
Eleza maana ya maneno haya:
Shawishi-
Fuzu-
Ari-
Aghalabu-
Date posted:
October 1, 2018
-
Eleza maana ya semi hizi:
Mkono mrefu-
Kuwa popo-
Kula kalenda-
Kutaka radhi-
Funga ndoa-
Date posted:
October 1, 2018
-
Eleza maana ya semi hizi:
Angua kicheko-
Chungu nzima-
Kupiga mbizi-
Kupiga teke-
Ezeka kofi-
Ona cha mtema kuni-
Date posted:
October 1, 2018
-
Bainisha silabi katika neno:
Wanyweshavyo.
Date posted:
September 24, 2018
-
Tunga vitenzi kutokana na nomino hizi:
watafanyiwa tathmini-
Kupata suluhu-
Date posted:
September 24, 2018
-
Andika neno moja lenye mofimu zifuatazo:
Nafsi ya kwanza wingi,wakati uliopita,yambwa,mzizi,kauli tendesha.
Date posted:
September 24, 2018
-
Tunga sentensi yenye kishazi kirejeshi ambacho ni kivumishi.
Date posted:
September 24, 2018
-
Andika sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa:
Nyumba hizo zilijengwa mbali na mji ule.
Date posted:
September 24, 2018
-
Tunga sentensi yenye muundo ufuatao;
Nomino ya jamii,kirai kihusishi,kitenzi kishirikishi,kielezi cha mahali.
Date posted:
September 24, 2018
-
Tumia viwakilishi badala ya nomino zilizo katika sentensi:
Mtalii atazuru Mbuga.
Date posted:
September 24, 2018
-
Andika sentensi hii katika hali ya mazoea:
Mmomonyoko wa udongo ulipozuiliwa mashamba yalinawiri.
Date posted:
September 24, 2018
-
Onyesha matumizi ya `ka’ katika sentensi ifuatayo:
Mumbi alitia embe kapuni likaiva.
Date posted:
September 24, 2018
-
KIDAGAA KIMEMWOZEA : Ken Walibora
2. “Nilikwambia twende ukakataa……si kuona, tuone ndipo tuambe”
(a) Weka dondoo katika muktadha wake (al.4)
(b) Fafanua hulka za mswemewa (al.6)
(c) Taja tamadhali ilitumika katika dondoo (al.2)
(d) Eleza umuhimu wa yanayorejelewa (al.4)
(e) Jadili umuhimu wa msemaji (al.4)
)
Date posted:
September 7, 2018
-
Taja aina nane na miundo ya tungo katika mashairi ya arudhi.
Date posted:
September 4, 2018
-
Elezea tofauti Kati ya kuchanganya ndimi na kuhamisha ndimi?
Date posted:
August 29, 2018
-
Lugha ya 'sheng' imekua lugha ambayo vijana wameipenda saana. Taja sifa saba ya sheng?
Date posted:
August 29, 2018
-
Elezea hatua za usanifishaji?
Date posted:
August 29, 2018
-
Nini sababu zinazochangia kuwepo Kwa uwingi lugha?
Date posted:
August 27, 2018
-
Elezea maana ya lafudhi na sababu za kuwa nazo.
Date posted:
August 27, 2018