Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kiswahili Karatasi Ya 2 Question Paper

Kiswahili Karatasi Ya 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2009



UFAHAMU
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.
Msemo"Ya kale hayako"unatukuzwa sana na vijana na hata ambao wanathamini usasa.Msemo huu umetishia kuumeza na kuutema utamaduni wa Mwafrika.Utamsikia kijana akiambiwa na mzazi wake,"Jamani itabidi ujifunze lugha yako ya mama,hivi hutaweza kuwasiliana na mababu zako kijijini."Naye kijana huyu hujibu,huku machozi kayatunga kwenye runinga,kidhibiti mbali mbali mkononi."Hayo ni yako.Lugha inahitajika kutumiwa pale mtu anapoishi.Mimi kijijini humo ntaishi lini?Na huyu babu,si anajua kiingereza?"
Huu ni mfano mmoja tu unaoonyesha mabadiliko ambayo yamezikumba jamii zetu.Watoto na hata watu wa umri ya makamo wamerithi desturi mchafukoge ambazo hazijulikani kama ni za Kiafrika au Kizungu.Mitindo ya mavazi ya kushangaza imezuka.Kuna wale wanaopendelea kutembea mabega wazi.Hawa huvaa vizibau vilivyoning'inizwa kwenye fito za nyuki.Kuna baadhi ambao huvaa suruali ndefu ambazo zimening'inia kiasi cha kuvifanya viuno kwenye miundi.Huu nao ni usasa ati.Unapouliza unazomewa na kuambiwa umechelewa kutambua hii karne ya ishirini na ngapi.
Tofauti za umri zimeanza kuwa finyu mno siku hizi.Si bura kumpata kijana akimpita mzee kama kwamba hajamwona.Anangoja mzee amsalimu yeye.Vijana wengine hudiriki kujibizana na wazee wao kama kwamba ni wa rika moja.Hawawapi wazee fursa ya kuzungumza,badala yake huwakata kauli kilamara wanapozungumza na kuwaudhi.Anapoulizwa kwa nini anamjibu vibaya mzee huyo,anasema nyakati za 'kuhubiriwa' bila kuuliza maswali zimepita na kuzikwa.
Teknolojia mpya imewapunguzia udhi,baadhi ya vijana ambao hawapendi kufanya kazi.Katika baadhi ya familia,utapata kwamba kuna mashine za kufulia nguo na kupangusia sakafu.Vijana wengi wanaoinuka hawawezi hata kujifulia nguo.Wale ambao kwao hakuna mashine,wana vijakazi ambao huwafanyia kila kitu.Lao ni kulala tu na kusoma.Mafunzo ya kazi ambayo vijana walipata siku za mababu yameanza kuzikwa kwenye kaburi la sahau.Hata katika familia ambazo utapata wazazi wana ari ya kuwafunza wanao umuhimu wa kutenda kazi za nyumbani,utapata kwamba watoto wenyewe hawazipendi kazi hizi.Wanahiari kucheza michezo ya kompyuta na kutazama kupigana miereka na masumbwi katika runinga.Si ajabu kwamba wengi wa vijana wanakua wakidhani njia ya kutatua migogoro na kupitia kwa makonde migoto vichwani
Suala unasaba lilikuwa na umuhimu mkubwa katika siku za kisogoni.Neno ndungu lilikuwa na maana pana katika jamii ya Mwafrika.Watoto wa ami,mjomba na shangazi walihifadhiana na kulindana kama ndungu.Siku hizi neno ndungu limejikita tu katika uhusiano wa karibu tu;motto wa mama au baba yako.Vijana wengi hawajui hata mabinamu zao.Jambo hii limewafanya wengine kuona watu wa ukoo wao bila kujua.Kwa hivyo,hata inapofika wakati wa kuoa,hao hukutana na wachumba wao mijini
Ingawa tunapasa kutambua kuwa wakati umebadilika,ni vyema kuwajibika.Hata pale tunapoiga mitindo ya kisasa kama vile mavazi,tuige kwa tahadhari.Mavazi tunayovaa yasikizane na maadili ya jamii zetu.Elimu ya kisasa isiwe kisingizio cha kusahau kitovu chetu.Tukumbuke methali isemayo'Usiache mbachao kwa mswala upitao"
MASWALI
a) Mwandishi amedhamiria kichwa mwafaka cha taarifa hii kuwa ya kale hayako.Eleza (Alama 2)
b) Tofauti za umri zimeanza kuwa finyu mno siku hizi.Fafanua kauli hii (Alama 2)
c) Mabadiliko yaliyokithiri katika jamii ni kutokana na vijana wasiowajibika.Toa ithibati (Alama 5)
d) Eleza chanzo cha mabadiliko ya vijana kulingana na taarifa.(Alama 4)
e) Eleza matumizi ya methali usiache mbachao kwa mswala upitao kulingana na taarifa (Alama 2)
2.UFUPISHO
Soma taarifa kisha fupisha kwa mujibu wa maswali yanayofuata.
Uwezo wa kuyakumbuka mambo ni hazina kuu kwa mtu yeyote yule aliye hai.Uwezo huu wa kukumbuka ni mojawapo ya shughuli changamano za ubongo.Ubongo wa mwanadamu hutekeleza shughli hii kwa namna tatu.Kwanza,ubongo hunasa jambo kisha hulihifadhi.Baadaye huanzisha mfumo wa kutoa kilichohifadhiwa.Ubongo ukiathirika kwa namna yoyote katika mojawapo ya njia hizi,basi uwezo wa kuyakumbuka mambo huvurugika.
Ingawa inaaminika kuwa uwezo wa kukumbuka hurithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine,wataalamu wa masuala ya kiakili wanabaini kuwa uwezo huu unaweza kuimarishwa.Uimarishaji huu huhitaji madhubuti.
Njia mojawapo ya kustawisha uwezo wa kukumbuka ni kupitia kwa lishe.Vyakula vinavyosheheni vitamini B vyenye amino asidi husaidia kuimarisha uwezo wa kukumbuka.Vyakula kama hivi ni mboga,nyama (hasa maini,bidhaa za soya,matunda,maziwa,bidhaa za ngano,samaki,pamoja na mayai.Vyakula vingine muhimu katika ustawishaji huu ni vile vyenye madini ya chuma.Madini haya huwezesha usambazaji wa hewa katika ubongo kwa wepesi.Vyakula ambavyo vina madini haya ni mboga za kijani ,mawele,dengu,soya,matunda kama maembe,ufuta(simsim) pamoja na nyama,hasa maini na mayai.
Ubongo wa mwanadamu aliye hai hufanya kazi kila wakati awe macho au amelala.Utendaji kazi wake huendeshwa na glukosi mwilini.Kwa hivyo,vyakula vyenye sukari hii muhimu kuliwa.Hata hivyo,lazima mtu awe mwangalifu na kuhakikisha kuwa mwili una kiwango cha sukari kisichohatarisha maisha.Haya yanawezekana kwa kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kama vile mboga na matunda.
Njia ya pili kupiga marufuku vileo kama pombe na nikotini.Vileo hivi huathiri utaratibu wa kunasa,kuhifadhi na kutoa yaliyo ubongoni.
Iwapo mtu ana tatizo la kuyakumba majina ya watu,ni muhimu kufanya mazoezi ya kusikiliza kisha kurudia majina hayo wakati wa mazungumzo.Ni bora kulihusisha jina na sura ya mtu.Kwa njia hii ubongo utanasa na kuhusisha jina na kile kinacholengwa.
Woga na kuvurugika kiakili ni mambo mengine tunayopaswa kuepuka kila wakati.Ni kawaida mtu kupata woga wakati anapokabili jambo asilokuwa na uhakika na matokeo yake kama mtihani au mahojiano.Lakini anapaswa kuwa makini.Woga huo usikiuke mpaka na kumvuruga kiakili.Vurugu hizi huathiri kilichohifadhiwa ubongoni na pia namna ya kukitoa.
Halikadhalika,mwili wenye siha nzuri huhakikisha kuwa ubongo ni timamu.Wataalamu wengi wa siha wanakubali  kuwa mazoezi ya kunyoosha viungo hustawisha ubongo na hivyo kuhakikisha kuweko kwa uwezo wa kukumbuka mambo.Ni muhimu kuwa na ratiba ya kunyoosha viungo kila wakati.Fauka ya hayo mazoezi ya kiakili,kama vile kusoma makala yanayovutia,kujaza mraba na michezo mingine kama mafumbo,vitanza ndimi na muhimu katika kustawisha uwezo wa kukumbuka.Jamii ya watu wenye uwezo wa kuyakumbuka mambo ni jamii iliyopiga hatua kimaendeleo.Ni jukumu la kila mmoja wetu kuimarisha uwezo wa kukumbuka kila wakati
Maswali
a) Kwa maneno 60-65,fupisha mchango wa chakula katika uimarishaji wa uwezo wa kukumbuka (Alama 6)
Nakala chafu
Nakala safi
b) Fupisha aya tatu za mwisho kwa maneno 80-90 (Alama 7)
Nakala chafu
Nakala safi
3.MATUMIZI YA LUGHA
a) Akifisha
Ala hujapeleka ng'ombe malishoni baba alimuuliza mwanawe (Alama 3)
b) Tenga mofimu katika neno lifuatalo kisha uandike majukumu yake kisarufi
Amempigisha (Alama 3)
c) Ainisha vivumishi katika sentensi ifuatayo:Majambazi kumi walivunja nyumba yetu (Alama 2)
d) Eleza tofauti katika sauti ya/p/b/ (Alama 1)
e) Andika katika udogo na ukubwa;Kitabu changu kina mistari midogo (Alama 2)
Udogo
Ukubwa
f) Unda nomino dhahania kutokana na kitenzi Vunda (Alama 1)
g) Kanusha
Angekuwa anampenda angemnunulia zawadi.
h) Sahihisha sentensi hii;
Kassim ambaye ni mwenye alichapwa alizirai (Alama 2)
i) Tunga sentensi kubainisha matumizi ya'ki'
a) Hali ya masharti (Alama 1)
b) Hali ya kitendo kuendelea (Alama 1)
j) Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii
Wenyeji wa Turkana hawaogopi baridi kama wageni (Alama 2)
k) Tunga sentensi kuonyesha aina zifuatazo za vihusishi (Alama 3)
i) Cha wakati
ii) Cha mahali
iii) Cha kiwango
l) Andika sentensi hii upya bila kutumuia 'amba'.Wanafunzi ambao hushinda ndio ambao hupewa zawadi (Alama 2)
m) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia mishale.
Mama na baba wanapumzika lakini watoto wao wanacheza uwanjani. (Alama 4)
n) Bainisha kishaza huru na kishazi tegemezi (Alama 2)
Mtihani ambao ulitungwa ni rahisi
o) Onyesha aina za shamirisho katika sentensi hii (Alama 3)
Nyaruai alijengwa nyumba na babake kwa matofali (Alama 3)
p) Eleza maana tofauti ya maneno haya (Alama 2)
Saka/Shaka
q) Onyesha viambishi awali na tamati katika neno: (Alama 2)
Alimtembelea
r) Tambulisha ngeli za nomino zifuatazo (Alama 1)
i) Chumvi
ii) Uta
4.ISIMU JAMII
Soma makala haya kisha ujibu maswali.
Nyani anaudaka mpira na kuelekeza kwake Mponda.Mponda anakwenda...anakwenda...aaa..ah!
Anaingiza goli moja murua sana.Lo! Wasikilizaji,goli lile nusura lipasue wavu
a) Hii ni sajili gani? (Alama 1)
b) Eleza sifa zozote nne za sajili hii (Alama 4)
c) Eleza dhima tano za lugha ya taifa (Alama 5)






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers