📘 Access 10,000+ CBC Exams With Marking Schemes

Prepare your learners for success! Get CBC-aligned exams for Grades 1–9, PP1–PP2, Playgroup and High School - all with marking schemes.

Browse Exams

Instant download • Trusted by 100,000+ teachers • Updated weekly

Kcse Kiswahili Paper 1 Question Paper

Kcse Kiswahili Paper 1 

Course:Kiswahili

Institution: Form 3 question papers

Exam Year:2010



SEHEMU A: USHAIRI(Alama 20)

1.(LAZIMA)

Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuatia.

DHAMIRA YANGU.

Dhamira imenifunga shingoni.
Nani kama mbuzi nimefungwa
Kwenye mti wa utu. Kamba ni fupi
Na nimekwishachora duara.
Majani niwezayo kufikia yote nimekula.
Ninaona siwezi kuyafikia: kamba,kamba.

Oh! Nimefungwa kama mbwa.
Nami kwa mbaya bahati, katika
Uhuru kupigania, sahani ya mbingu
Nimeipiga teke na niigusapo kwa mdomo
Mbali zaidi inakwenda na siwezi tena
Kuifikia na hapa nilipofungwa
Nimekwishapachafua na kuhama siwezi.

Kamba isiyoonekana haikatiki.
Nami sasa sitaki ikatike, maana,
Mbuzi wa kamba alipofunguliwa, mashamba
Aliharibu na mbwa aliuma watu.
Ninamshukuru aliyenifunga hapa
Lakini lazima nitamke kwa nguvu
"Hapa nilipo sina uhuru!"

(E.Kezilahabi)


a)Taja mambo manne ambayo mshairi analalamikia. (alama 4)

b)Kwa nini mshairi haoni haja ya yeye kuwa huru? (alama 2)

c)Eleza maana ya mshororo ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi.
"Kama isiyoonekana haikatiki" (alama 2)

d)Taja na utoe mifano ya aina mbili za tamathali zilizotumika katika
shairi hili. (alama 4)

e)Kwa kutoa mifano miwili, eleza jinsi matumizi ya mishata yanavyojitokeza
katika shairi hili. (alama 4)

f)Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari (alama 4)

SEHEMU B: RIWAYA.
S.A Mohamed: Utengano
Jibu swali la 2 au 3

2."...wewe kwako toka lini mwanamke kuwa mtu? Wangapi umewatenda?"
a)Eleza muktadha wa dondoo hili? (alama 4)

b)Kwa kutoa mifano minne mwafaka, dhihirisha ukweli wa dondoo hili. (alama 16)

3.Kwa kurejelea vipengele vifuatavyo vya matumizi ya lugha katika riwaya ya
Utengano, onyesha jinsi mwandishi amevitumia kufanikisha maudhui:
i) uzungumzinafsi; (alama 10)
ii) taswira; (alama 10)

SEHEMU C: TAMTHILIA
Kithaka Wa Mberia: Kifo Kisimani
Jibu swali la 4 au 5

4."Dalili ya mvua ni mawingu."
Kwa kuzingatia utawala wa Mtemi Bokono, thibitisha usemi huu. (alama 20)

5."Nitoeni!Nitoeni! kaburini. Ondoeni udongo. Ondoeni udongo nitoke kaburini."
a)Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b)Taja na ueleze tamathali za usemi mbili zilizotumiwa katika dondoo hili (alama 4)
c)Kwa kurejelea tamthiliya nzima, fafanua hoja sita kuonyesha jinsi dondoo
hili linavyoonyesha kinyume cha mambo. (alama 12)

SEHEMU D: HADITHI FUPI NA FASIHI SIMULIZI.
K.W.Wamitilia: Mayai wa Maradhi na Hadithi Nyingine.
Jibu swali la 6 au la 7

6."Ana nini mtoto huyu! Ninamtesekea na ufakiri wote huu nilionao..."
a)Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b)Eleza tatizo alilokuwa nalo anayerejelewa kisha ufafanue vitendo
vinavyodhihirisha kwamba alikuwa na tatizo. (alama 6)
c)Anayetoa kauli hii alikuwa na msimamo gani kuhusu tatizo tatizo la mtoto? (alama 4)
d)Kwa kutoa mifano mitatu mwafaka, eleza hali zinazoweza kulaumiwa kwa tatizo
la anayerejelewa. (alama 6)

FASIHI SIMULIZI.

7.Huku ukitoa mifano mwafaka,linganisha na utofautishe kipera cha vitendawili
na kile cha methali. (alama 20)






More Question Papers


Exams With Marking Schemes

End Term 3 Exams

Mid Term Exams

End Term 1 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers