Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Nandi North District Mock -Kiswahili Paper 2 Question Paper

Nandi North District Mock -Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2006



KISWAHILI
102 / 2
UFAHAMU ( ALAMA 15) *NDI*
Soma makala yafutayo kisha ujibu maswali*NDI*
Limeibuka suala kwamba polisi waliokuwa wakiongoza mashtaka mahakamani sasa watakuwa chini
ya himaya ya mkuu wa sheria wala si kamishina wa polisi. Ni hatua iliyo na mashiko katika
utekelezaji na usimamizi wa sheria.
Hatua hiyo itasaidia kuhakikisha kwamba washtakiwa watapata haki kamili na kuzuia visa ambapo polisi wakati mwingine walikuwa wakiwasingizia washtakiwa madai ya uongo na kisha kuwatolea mashtaka.
Polisi hawapaswi kutekeleza majukumu fulani katika maongozi ya sheria kwa kuruhusiwa kuwatia nguvuni washtakiwa, kuwatayarishia mashtaka na halafu kuwafikisha mahakamani.
Maofisa husika sharti wafunzwe upya kuongoza mashtaka kuambatana na sheria, wala si kanuni za polisi wanaoongoza mashtaka, wawe mawakili waliosomea wanasheria ipasavyo sawa na mawakili hao wengine. Hali hii itazuia visa ambapo wakili huwa anafahamu sheria kuliko kiongozi wa mashtaka.
Mawakili zaidi wa umma wafaa kutengewa washtakiwa wasio na pesa za kuwalipa mawakili wa
kibinafsi kuwatetea.
Hatua hizo zitaharakisha kesi zirundikanazo mahakamani na pia kupunguza idadi ya washtakiwa
wanaowekwa rumande kutokana na hitilafu za kisheria.
Maswali
a) Yape makala anwani mwafaka Alama 1*NDI*
b) Utekelezaji wa sheria mahakamani umetiwa sura mpya . Fafanua kwa mujibu wa makala.
Alama 2*NDI*
c) Dhihirisha kuwa washtakiwa nchini Kenya wamekuwa wakikosa haki. Alama 2*NDI*
d) Shughuli za mahakama na utekelezaji sheria zahitaji kuboreshwa. Eleza. Alama 3*NDI*
e) (i) Orodhesha majukumu ambayo polisi hawafai kuyatekeleza kisheria. Alama 3*NDI*
(ii) Eleza sababu muhimu inayowakataza polisi kutekeleza majukumu uliyoyaorodhesha katika
sehemu ya e (i) Alama 1*NDI*
f) Eleza maana :- Alama 3*NDI*
i) Kuwatia nguvuni*NDI*
ii) himaya*NDI*
iii) rumande*NDI*
2. MUHTASARI*NDI*
Soma makala haya kisha ujibu maswali
Ni dhamira ya mwanafunzi yeyote kupata matokeo mazuri katika mtihani wa kitaifa punde tu
anapojiunga na shule iwe ni ya sekondari au msingi.
Matokeo hayo hutokea baada ya miaka minane katika shule za msingi na miaka minne katika shule za sekondari. Hata hivyo, punde tu matokeo yanapotangazwa, wengine hujipata wanyonge kwa kugundua kuwa wamefeli au wameambulia nunge kwa mtihani wao wa mwisho.
Miongoni mwa mambo yanayosababisha hali kama hii ni mwelekeo mbaya wa wanafunzi katika
baadhi ya masomo. Tunajua kweli kuwa palipo na ushindani lazima kuwe na mshindi na mshindwa.
Iwapo ungemwuliza mtahiniwa akueleze jinsi anavyohisi baada ya kushindwa kwenye mtihani wa
kitaifa, hatakuwa na la ziada ila kukueleza kuwa hajaridhishwa na matokeo.
Wengine wao hata huvuka mipaka na kuyataja matokeo yao mabaya kusababishwa na vizingiti fulani au kuwakashifu walimu kwa kudai kuwa kulikuwa na hali ya kuonewa darasani. Unapochunguza zaidi, utakuta ya kuwa wanaodaiwa kuwa werevu ni walio stadi katika masomo ya sayansi yanayofikiriwa kuwa magumu.
Wakati wanaofikiriwa kuwa werevu wanapofanya vyema katika mitihani yao, wale wanaokisiwa
kuwa wajinga ambao wamefeli hujipata wakiomboleza kwa huzuni kwa muda mrefu.
Swali la miaka mingi kuhusu elimu limekuwa ni kwa nini wanafunzi wote hawawezi wakafanya
vyema na kufaulu katika mitihani ya kitaifa. Utafiti uliofanywa umebainisha wazi kwamba kunazo sababu kadhaa zinazochangia matokeo mabaya.
Mojawapo ya sababu hizo, na ambayo ni muhimu sana ni ukosefu wa nidhamu shuleni. Mwanafunzi
wa aina hii hajali anachoambiwa na walimu na aghalabu muda wake mwingi unapotelea katika
adhabu.
Wakati mwanafunzi anapokosa nidhamu iwe kwa wazazi au walimu wake, masomo yake huathirika.
Matokeo yake katika mitihani hayatakuwa mazuri. Ni Lazima tabia ya mwanafunzi iambatane na
matokeo yake. Sababu nyingine ni mshituko unaowapata punde tu wanapoketi kwenye viti vyao
kufanya mitihani ya kitaifa. Mtahiniwa anapojikuta katika hali hii, kuna uwezekano asifaulu katika masomo yake.
Kuna uwezekano wa wanafunzi aliyefeli katika mtihani wa darasa la nane kufanya vyema katika shule ya upili na kupita mtihani wake wa kidato cha nne. Ilibainika pia kuwa wale waliofaulu katika mtihani wa darasa la nane hulegeza juhudi zao masomoni na huwa hawapati alama zinazoambatana na zile walizopata katika shule za msingi.
Sababu nyingine ya kuwafanya wanafunzi kutofanya vyema katika mtihani ni kubaguliwa kwa
wanafunzi hafifu na walimu na kukosa kushughulikiwa ipasavyo. Baadhi ya walimu wanapogundua
kuwa wanafunzi fulani hawafanyi vyema katika masomo fulani, hawatumii muda wao mwingi
kuwasukuma ili kuyaboresha matokeo. Badala yake huwashughulikia wanaoelewa haraka darasani.
Kuna wanafunzi wengine wanaochukua muda mrefu kuelewa, si ya kwamba ni wajinga, la, ni katika somo moja tu. Ni wajibu wa mwalimu kuhakikisha mwanafunzi kama huyu anapata nafasi ya kuelewa anachofunzwa.
Wanafunzi wengine hawafanyi vyema kwa sababu wazazi wao hawamudu kuwalipia karo kwa sababu
ya umaskini, hawawezi hata kulipia masomo ya ziada kwa shule zinazosomesha wanafunzi wakati wa
likizo.
Kulingana na takwimu za elimu, muda wa kawaida hautoshi kukamilisha mtaala wa masomo ya
mfumo wa 8-4-4, kwani ni mpana sana. Walimu wanaombwa kushughulikia mafunzo ya ziada.
MASWALI
a) Bila kubadilisha maana, fupisha aya tatu za mwanzo. Maneno (55 – 60). Alama 7*NDI*
Matayarisho
Nakala safi
b) Fafanua sababu zinanzowafanya wanafunzi kutofua dafu katika masomo yao. Maneno ( 50 – 55)
Alama 6) *NDI*
Matayarisho
Nakala safi
(utiririko alama 2) *NDI*
3. MATUMIZI YA LUGHA
a) Akifisha
Sikukuu ya madaraka nilikwenda eldama ravine kumwona yohana naye akasema atakuja
kuniona pamoja na mkewe mariamu siku ya jumapili. Alama 3*NDI*
b) Andika katika usemi wa taarifa
“Hivi vibanda vinatumiwa kulanguzia dawa za kulevya’’, mkuu wa polisi alilalamika.
Alama 2
c) Tunga sentensi ukitumia nomino zifuatazo pamoja na kivumishi – ingine Alama 2*NDI*
i) dau
ii) Urembo
d) Tumia mchoro wa matawi kuichanganua sentensi ifuatayo.
Mwanafunzi mzuri ametunukiwa zawadi. ( alama 3) *NDI*
e) Tumia amba katika sentensi hii. Alama 1*NDI*
Ua limealo huwa limetiwa mbolea.
f) Unda nomino kutokana na vitenzi hivi. Alama 2*NDI*
i) fisidi
ii) dhihaki
g) Pigia mstari vielezi katika sentensi hizi kisha utambue ni vya aina gani. Alama 4*NDI*
i) Wezi walipigwa barabara
ii) Wezi walipigwa kwa bunduki
(h) Tunga sentensi tatu tofauti zinazodhihirisha matumizi ya Ka. (Alama 3) *NDI*
i) Kanusha
Angelijua hasira yangu, angelifuata amri zangu. Alama 2*NDI*
(j) Tunga sentensi kwa kila mojawapo ya miundo hii. Alama 2*NDI*
i) Kishazi huru
ii) Kishazi tegemezi
k) Sahihisha Alama 2*NDI*
i) Alikuja kunipea pesa zangu
ii) Umemwona mwenye ameenda sokoni
(l) Tunga sentensi kutofautisha jozi hizi kimaana. Alama 2*NDI*
i) Kua
ii) Kuwa
m) Sentensi sahili ni sentensi ya aina gani? Tunga sentensi kudhibitisha maana. Alama 2
Maelezo .........................................................................................................................................
Sentensi
n) Andika kitenzi hiki katika kauli ya kutendeka Alama 1*NDI*
La
o) Tunga sentensi ukitumia misemo hii Alama 2*NDI*
(i) Fanya kikaka
(ii) Jia kikuku
p) Tumia kiunganishi hiki katika sentensi. Alama 1*NDI*
Japo
q. Andika udogo na ukubwa wa nomino - ng’ombe Alama 2*NDI*
r. Andika visawe vya. Alama
2*NDI*Masaibu
i) Kiwewe
s) Tunga sentensi moja ukitumia kihusishi cha - a Alama 1*NDI*
t) Kamilisha methali Alama 1*NDI*
Mti mkuu ukigwa
4. ISIMU JAMII*NDI*
Mahojiani baina ya daktari na mgonjwa. *NDI*
Daktari: Karibu ndani.
Mgonjwa: Ahsante.
Daktari: Unaitwa nani baba?
Mgonjwa: Naitwa Ali Makame.
Daktari: Unaishi wapi?
Mgonjwa: Ninaishi mtaa wa Majitu
Daktari: Una shida gani baba?
Mgonjwa: Mimi ninahisi baridi sana. Hata wakati ambapo jua linawaka, mimi huhisi
baridi na kutetemeka.
Daktari: (Anachukua kipima joto na kukiingiza kwenye kwapa la mgonjwa) Hali hii
ilianza lini?
Mgonjwa: Tangu juzi.
Daktari: Ni jambo gani linalokusumbua.
Mgonjwa: Naumwa na kifua bwana tabibu
Daktari: Je, baba unatumia sigara?
Mgonjwa: Nilikuwa nikivuta, lakini sasa nimeacha
Daktari: Unakohoa?
Mgojwa: Awali nilikuwa nikikohoa vibaya sana lakini sasa kikohozi kimepungua
Daktari: (Akiangalia kipima joto) Ala! Una joto jingi sana.
Mgonjwa: Nami huku naumia kwa baridi kali kabisa.
Daktari: Hebu tupime kifua chako (Anatoa stethoskopu shingoni na kud unga masikioni
kisha anamwekea mgonjwa mgongoni). Vuta pumzi ndani! Vuta tena. BasiToa pumzi nje. Basi kifua chako si kizuri sana. Itakubidi uchukuliwe picha ya eksirei (uyoka). Ninataka upimwe katika maabara kama una viini vinavyosababisha malaria.
Mgonjwa: Ninachotaka bwana mganga ni kupona tu.
Daktari: Utapona. Usiwe na wasi wasi (Anaita mwuguzi). Nitakudunga sindano moja
ya kuteremsha hicho kiwango chako cha joto. Kisha nenda ukapewe dawa
nilizokuandikia.
Mwuguzi: Nimefika daktari.
Daktari: Mchukue huyu mgonjwa umpeleke katika maabara apimwe malaria, baadaye achukuliwe picha ya eksirei.
Jibu maswali haya
a) Jadili sifa za lugha inayotumiwa. Alama 6*NDI*
b) Eleza maana ya vifaa vifuatavyo ambavyo hutumika katika mazingira ya hospitaliAlama
4*NDI*
(i) Uyoka*NDI*
(ii) Kipima joto*NDI*
(iii) Machela*NDI*
(iv) Mwuguzi*NDI*






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers