Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Trans-Nzoia District Mock-Kiswahili Paper 2 Question Paper

Trans-Nzoia District Mock-Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007



Jina………………………………………………… Namba yako …………………….
Shule………………………………………………...
102/2
KISWAHILI
Karatasi 2
Julai / Agosti - 2007
Muda: Saa 2½
MTIHANI WA MWIGO – WILAYA YA TRANS- NZOIA - 2007
CHETI CHA ELIMU YA SEKONDARI KENYA.
102/2
KISWAHILI
Karatasi 2
Julai / Agosti - 2007
Muda: Saa 2½
• JIBU MASWALI YOTE
Karatasi hii ina kurasa 12 zilizopigwa chapa
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo
UFAHAMU
Soma habari hii kisha ujibu maswali yafuatayo.
Dawa Za Kulevya Na Jamii.
Tatizo la dawa za kulevya ni moja kati ya matatizo makuu katika jamii zetu. Pombe, ambayo
inaweza kujumlishwa katika kundi pana la Dawa za kulevya, imetumiwa kama, burudani katika
jamii kwa kipindi kirefu sana. Katika jamii za zama za leo, kuna shinikizo za kijamii na kitamaduni ambazo zinawafanya watu wengi kuishia kutumia pombe au bia na kuvuta sigara. Ikiwa utumiaji
wake unaathiri anayehusika pamoja na jamii yake, basi pana sababu kubwa ya kulishugulikia suala hili.
Sote tunafahamu kuwa dawa huwa na mchango wa matibabu. Lakini ikiwa dawa zimetumiwa kwa
sababu ambayo haihusiani na matibabu au kwa njia mbaya, huwa na matokeo mabaya. Chanzo kikuu cha kutumia dawa vibaya ni kuzipata athari Fulani zinazohusishwa na dawa zinazohusika. Matumizi ya aina hii huwa ni kusababisha utegemeaji wa dawa kiasi kwamba mtu hawezi kutenda kazi Fulani pasi na kuzitumia dawa zinazohusika. Utegemeaji huu wa dawa unaathiri mwili wa anayehusika na jinsi unavyofanya kazi. Kisaikolojia au kiakili anayehusika huweza kuzitegemea dawa kiasi kwamba hawezi kufanya hawezi kufanya lolote pasi na kuzitumia dawa Fulani.
Miongoni mwa watu wanaothiriwa kwa kiasi kikubwa na tatizo la dawa za kulevya ni vijana ambao wamo katika harakati za kuwa huru na kuusaka ujitambuaji. Baadhi yao wanaelekea kuamini kuwa dawa hizi zitawapa sifa muhimu za kujitambua kama ujasiri, kujiamini, hisia za kuwa huru na kadhalika. Asilimia kubwa ya vijana katika nchi nyingi zinazoendelea na zilizoendelea wamezongwa
na tatizo hili. Ikiwa asilimia kubwa ya vijana itaathirika basi pana hatari kubwa ya jamii za ulimwengu kuvipoteza vizazi vya kesho. Suala la dawa za kulevya sio tatizo la nchi zilizoendelea tu wala tatizo la maeneo ya mijini tu. Hili ni tatizo ambalo linasambaa kila sehemu kwa kasi ya ajabu sana.
Nchi zinazoendelea zinaathirika zaidi kwa kuwa maendeleo yao yanakitegemea kizazi cha vijana. Ni katika hali hii ambapo elimu ifaayo ni muhimu ili kusaidia kuwaelimisha wanaohusika pamoja na jamii nzima.
Moja kati ya sababu kuu zinazochangia kuweko kwa tatizo la utumiaji mbaya wa dawa, ni kuvunjika kwa muundo na mshikamano wa kijamii ambao ni msingi muhimu sana. Ikiwa msingi huu
uliotegemewa na wanajamii umevunjika, kuna uwezekano kuwa baadhi ya wanajamii watashindwa
kukabiliana na hali yao mpya. Hawa watajaribu kusaka kimbilio Fulani kwenye dawa za kulevya. Hii kwao inakuwa kama njia ya kujipumbaza na kujipumbaza kuwa wanaweza kuikabili hali hii mpya.
Katika mataifa mengi, kuna uhamaji mkubwa wa watu kutoka maeneo ya mashambani hadi mijini.
Asilimia kubwa ya watu hawa wanakabiliana na matatizo mengi wanapoingia mijini. Matatizo haya ni kama ukosefu wa ajira, malazi, chakula, na mahitaji ya kimsingi. Pili, wanakumbana na tatizo la ukiwa na upweke wa kutengana na jamii zao waliowasaidia kupambana na hali za maisha. Tatu, wanakumbana na hali ambazo hawakuzizoea katika utamaduni walimokulia. Matatizo yanayohusiana na ulimbukeni huo wa maisha ya mjini unaweza ukamtosa mtu kwenye dawa za kulevya.
Je, matumizi ya dawa za kulevya yanaiathiri vipi jamii? Jambo la kwanza ni kutambua kuwa suala la dawa za kulevya ni tanzia ya kijamii. Hili ndilo tatizo ambalo limetengewa sehemu finyu za jamii , linaathiri jamii nzima. Hili silo tatizo la ‘ mitaani’ tu bali limeziathiri jamaa, maeneo ya kazi, shule na taasisi nyingine zozote. Ni tatizo ambalo linawaathiri watu wa kila umri.
Katika kiwango cha jamaa matumizi, dawa za kulevia yanauathiri ushikamano na umoja wao.
Watumiaji wa dawa za kulevya wanazugwa na kurengwa na tabia yao kiasi kwamba haja za watu
wengine sio muhimu kwao. Anayehusika anaathirika kiafya na kisaikolojia. Jamaa yake nayo
inateseka kumwona mwenzao akiangamia kutokana na kuzitegemea dawa za kulevya. Ikiwa
wanaotumia dawa za kulevya ni watu wazima, pana uwezekano watoto wakaishia kuamini kuwa
kutumia dawa hizo ni jambo la kawaida na linalofaa. Utumiaji wa dawa za kulevya unaweza pia
kuingiza jamii inayohusika kwenye matatizo ya mtumiaji anayerengwa na dawa za kulevya huwa
tayari kufayanya lolote lile ili apate pesa za kununulia dawa hizo.
Katika kiwango cha shule, dawa za kulevya huwaathiri vijana vibaya sana. Kwanza huathiri ukuaji wa kijana anayehusika. Dawa hizi huuwa seli za ubongo na kuathiri uwezo wa mwanafunzi wa kuweza kuyafuatilia masomo yake vizuri. Pili, kutegemea dawa za kulevya huweza kuathiri ukuaji wakawaida wa mwili. Tatu, ukuaji wa kimaadili wa mwanafunzi unaharibika. Dawa za kulevya zinaathiri tabia za wanaohusika na kuwapa hisia ambazo haziwezi kusaidia jamii. Nne, matumizi ya dawa za kulevya huathiri uwezo wa wanafunzo kimasomo. Tano, matumizi ya dawa za kulevya shuleni yanachochea kuwapo kwa matendo yanayohusishwa nayo. Matendo haya ni kama wizi, uhalifu, ukahaba, unyang’anyi, utovu wa nidhamu pamoja na uuzaji wa dawa zenyewe. Jamii yoyote inayotaka kuendelea haina budi kuzipiga vita dawa za kulevya.
Maswali.
1. Mwandishi anasema pombe huweza kuwa dawa za kulevya. Hili hutokeaje? (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
2. Ni sababu gani zinazowavuta vijana kutumia dawa za kulevya? (alama3)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………

3. Eleza athari sita za dawa za kulevya kwa mwanafunzi. (alama 3)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………

4. Eleza madhara ya dawa za kulevya kwa jamaa. (alama 4)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
5. Eleza maana ya kifungu hiki: Suala la dawa za kulevya ni tanzia ya jamii. (alama1)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
6. Ni nini maana ya (alama 3)
i) shinikizo za jamii
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
ii) wazugwa na kurengwa
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
iii) wamezongwa
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
UFUPISHO
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Bila shaka walipiga ndipo waliponena kuwa bilisi wa mtu ni mtu. Walimaanisha nini sasa? Kwamba kwa kawaida mtu hujiingiza matatani mwenyewe halafu katika hali ya majuto, akaanza kulaumu kiumbe anayeitwa shetani, kuwa ndiye aliyemwendea kombo.
Wengi wa wanafunzi – watoto wa shule, siku hizi hawana wala hawaonyeshi shukrani kwa wazazi au wafadhili wao. Mbali na kwamba wazazi au wafadhili huwatafutia karo ya shule pamoja na masurufu, yaani pesa ya matumizi, wanafunzi wengine wanakosa shukrani na adabu na huwa hawatosheki wala hawaoni haja ya kutosheka. Hawa kwa hakika wanakuwa aina mbaya ya kina pangu- pakavu- patie mchuzi. Si ajabu ukisikia wakiwalaghai wazazi kwa uongo kama vile, ‘Baba, mwalimu alisema kila mwanafunzi apeleke shilingi mia na hamsini za kutufaa kwa karamu na zawadi. Mama, kila mwanafunzi anatakikana apeleke shilingi…. Kwa ufupi mzazi hujikuta akikerwa na kusumbuliwa na vijisababu visivyokuwa na mwisho, vya pesa kuhitajika shuleni.
Kwa nini tunailaani vikali tabia hii? Jambo ni kwamba huku mzazi akilemewa na mzigo mkali wa karo ya shule kwa mwanawe ; huku mzazi akijitahidi kwa jino na ukucha ili kuona kwamba mwanawe hafukuzwi shule ; huku mzazi akijinyima mengi ya lazima maishani, akipunguza hata matumizi muhimu nyumbani kama vile kiamshakinywa na mahitaji mengineyo ili kuona kwamba anamjengea mwanawe msingi imara wa kumwezesha kukabiliana na maisha yake ya baadaye, mwana kwa upande wake tayari anataka kuishi maisha ya ponda raha – kufa – kwaja!
Inasikitisha kuona mtoto anamdanganya mzazi wake ili apate pesa za kwenda kuharibu kwa matumizi ovyo ya sigara na pombe!
Tabia ya kuvuta sigara na kunywa pombe miongoni mwa watoto wa shule ni mbovu. Tabia hiyo
hupevuka na kuwa uraibu, yaani yale mazoea ya kuwa mtu amekuwa mtumwa wa jambo kiasi cha
kutoweza kuachana nalo. Katika hali ya namna hiyo, akikosa uraibu wake, matokeo yanakuwa jambo kama vile kuumwa na kichwa au kwa namna fulani, kutojisikia vizuri tu mwilini. Mbali na kushidwa kuzingatia ifaavyo masomo yao shuleni, wanafunzi wa aina hiyo huwa wanajipunguzia bure bilashi siku za uhai wao duniani.
Uraibu wa sigara kama na pombe una madhara yake. Sigara na pombe ni sumu mwilini. Mathalani, sigara kama wanavyoeleza maafisa wa afya, husababisha kifua kikuu. Matokeo ni kuwa humfanya mraibu kukohoa koh! Koh! Koh! Na kujikojolea kiholela, kiasi cha kuhurumiwa.
Pombe kwa upande wake nayo huduwaza akili huku ikidhoofisha na kulegeza mwili kiasi cha mraibu kuonekana kuwa kigofu cha mtu kilichoingia duniani kwa mwili kiasi cha kuonekana kuwa kigofu cha mtu kilichoingia duniani kwa madhumuni ya kuongeza idadi ya makaburi tu!
Kwa upande wako wewe mwanafunzi unayehusika, hebu pigia makini haya mzazi atafikirije,
atachukuaje, atahisi namna gani yeye akitambua kwamba pesa anazozitolea jasho huku akijinyima zinamalizikia katika uraibu usiokuwa na manufaa yoyote bali madhara mwilini?
Maswali
1. Mwandishi wa makala haya anazungumzia vipi jinsi ambavyo wanafunzi wengi hawana wala
hawaonyeshi shukrani na heshima kwa wazazi na wafadhili wao? ( maneno 60- 70 ) (alama6)
Nakala Chafu

……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
Nakala Safi
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………

2. Kwa nini mwandishi anailaani vikali tabia ya mwanafunzi kumdanganya mzazi wake?
(maneno 65-75 ) (alama 7)
Nakala Chafu

……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
Nakala Safi
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………

3. Eleza kwa ufupi madhara ya pombe na sigara mwilini. ( maneno 15- 20 ) (alama 2)
Nakala Chafu
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
Nakala Safi
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA
a) Hizi ni konsonanti za aina gani na zinatamkiwa wapi?
i)th
AINA? ZINATAMKIWA?
ii) r
(alama 2)
b) Eleza matumizi ya kisarufi ya neno ‘ taratibu’ katika sentensi hizi.
i) Halima alifanya kazi ile taratibu. (alama 2)
ii) Taratibu yake ilituchelewesha.
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
c) Bainisha aina ya maneno katika sentensi hii.
Ala! Unasimama mbele ya gari? (alama 2)
………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………..……………
d) Onyesha aina mbalimbali za nomino katika sentensi hii.
Makadirio ya matumizi ya fedha yatasomwa na kombo kwa baraza hilo. ( alama 2)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
e) Eleza dhana hizi
i) Shadda
ii) Kiimbo ( alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
f) Tunga sentensi ukionyesha matumizi ya alama zifuatazo za kuakifisha.
i) Ritifaa (alama 2 )
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) Koloni (alama 2 )
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
g) Taja manufaa manne ya kamusi (alama 2 )
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………

10
h) Onyesha kishazi huru na tegemezi katika sentensi hii.
Ijapokuwa kulikuwa na baridi kali niliondoka kwenda sokoni. (alama 2 )
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
i) Maneno haya yanapatikana katika ngeli ipi?
i) Kusadiki
ii) Pahali (alama1)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
j. Andika sentensi zifuatazo kama ulivyoagizwa.
i) Mwiba uchomeako ndiko utokeako.
( Geuza viambishi tamati viwe viambishi vya kadi. ) ( alama 1 )
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
ii) Nyoka huyu alimla ndege . ( andika kwa udogo ) (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
iii) “ Sijaona gari zuri kama hili , utaniazima siku ngapi ?” Juma alimwuliza
kamau. ( Andika kwa msemo wa taarifa ). ( alama 2 )
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
iv) Mchungwa ambao hauzai hukatwa. ( Kanusha sentensi ukitumia kirejeshi ‘ o’)
(alama 2 )
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
k) Ainisha mofimu katika fungutenzi hili na utaje ni za aina gani .
Alichomsaidia. (alama 3)

11
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
l) Tunga sentensi moja moja ukitumia
i) Kiwakilishi kirejeshi ( ukipigie mstari ). (alama2)
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
ii) Kiwakilishi nafsi kiambata ( ukipigie mstari ) (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
m. Pigia mstari vitenzi katika sentensi hizi na utaje ni vya aina gani.
i) Kamau amekuwa uwanjani.
ii) Huyu ndiye mwalimu mkuu. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
n. Changanua sentensi hii ukitumia mishale.
Mwanafunzi atakayesoma kwa bidii atafuzu mitihani. (alama 4)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………

o. Onyesha chagizo katika sentensi hii.
Anapenda kutembea ufuoni mwa bahari. (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………

12
ISIMU JAMII ( MASWALI )
• Je Unataabika kwa kukosa matibabu?
• Kaa masaa! Kaa chonjo!
• Unaugua mafua?
• Unaugua malaria?
• Unaugua macho au kukosa mpenzi?
• Daktari Mambo yote amewasili kutatua shida hizi na zinginezo.
• Bei best kwa matibabu best!
• Gwiji wa magwija anatibu magojwa zaidi ya elfu!
• Kufika ni kujionea!
• Come one ! come All .
• Nambari 0700200780 ni nambari ya mawasiliano na Daktari
• Chukua kontroo kabla ya maradhi kukukontroo!!
Maswali
1. Lugha hii inatumika wapi na kwa madhumuni gani? (alama 2 )
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
2. Dondoa sifa nne za sajili hii ya lugha na utolee mifano. ( alama 8 )
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
Mwisho__






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers