Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Trans-Nzoia West District Mock-Kiswahili Paper 2 Question Paper

Trans-Nzoia West District Mock-Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2008




Jina ………………………………………………………… Namba Yako ……………………
Shule ……………………………………………………….
102/2
KISWAHILI
Karatasi ya 2
(Ufahamu, Ufupisho, Matumizi ya lugha na Isimu Jamii)
Julai / Agosti 2008
MUDA: Saa 2 ½
MTIHANI WA MAJARIBIO (MWIGO) WILAYA YA TRANS-NZOIA MAGHARIBI - 2008
HATI YA KUHITIMU KISOMO CHA SEKONDARI-KCSE

MUDA: Saa 2 ½
MAAGIZO:
Jibu maswali yote
KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE
SWALI JUMLA
Ufahamu 15
Ufupisho 15
Matumizi ya lugha 40
Isimu jamii 10
JUMLA
Karatasi hii ina kurasa 10 zilizopigwa chapa
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo.
UFAHAMU
1. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuatia: (JUMLA ALAMA 15)
Nchi yetu imeraukia mawio ya machafuzi ya kisiasa baada ya shughuli za uchaguzi zilizogonga mwamba mkuu. Hili lilijiri baada ya Tume ya Uchaguzi kukosa kuendeleza uchaguzi kwa njia iliyostahiki. Jambo hili lilizaa msukosuko wa kisiasa usiomithilishwa katika historia ya taifa letu.
Hivi sasa Wakenya wanaishi kwenye kambi za watu wasio na makazi. Hiki ni kinaya kikuu kwani matukio haya yamezuka baada ya zaidi ya miongo minne ya uhuru. Vilio vya Wakenya vimeshamiri na kupaaza sauti vikilalamikia kukosa makazi, lishe na hata ndoa kusambaratika. Ndoa zimevunjika baada ya ‘wenyeji’ kuwatimua ‘wageni’ na damu kumwagika.
Misukosuko ya kisiasa kama hii imekumba mataifa mengi ya Afrika miaka nenda rudi na kuchangia bara kudumaa na kuvia kiuchumi.
Kenya imekuwa miongoni mwa mataifa yanayowapa faraja wakimbizi kutoka nchi jirani zinazokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, zikiwemo Somalia na Sudan. Kinaya ni kwamba Wakenya wamekuwa wakimbizi katika nchi yao wenyewe. Vita katika Somalia vimesababishwa na koo mbali mbali zinazopigania uongozi hali ambayo imekwamisha shughuli zote za kiuchumi. Hali ya sasa ya Kenya imechochewa na msururu wa sababu.
Ukabila na tamaa ya uongozi zilionekana wazi katika miundo ya vyama vikuu vya kisiasa na katika kampeni zao. Wakenya walipiga kura kwa misingi ya kikabila kila upande ukitazamia mtu wao kushinda uchaguzi huo.
Kwa upande mwingine, viongozi hao kutokana na tamaa ya uongozi walikuwa wameamua kushinda uchaguzi huo kwa vyovyote vile. Leo tunavuna matunda ya siasa za ukabila na tamaa ya mamlaka.
Maelfu ya Wakenya ni wakimbizi nchini na katika nchi jirani ya Uganda. Wakenya hao wanahitaji msaada wa chakula na mahitaji mengine ya kimsingi. Serikali na Shirika la Msalaba Mwekundu zimefanya juhudi kuwasaidia wahasiriwa Lakini, kuna tetesi kwamba ubaguzi umejipenyeza katika ugawaji wa msaada huo.
Waliopewa jukumu la kugawa msaada huo ni sharti waelewe kuwa waathiriwa ni Wakenya wenzao na hawafai kubaguliwa kwa misingi ya makabila yao.
Matukio kama haya hayastahili kutukia asilani katika taifa hili.
Twahitaji zao aali la viongozi wasiojitwika ubabe bali wawe watumishi wa wananchi. Wanastahili kutupilia mbali tamaa za kujilimbikizia mali na kung’ang’ania uongozi. Pia katiba inafaa irekebishwe. Wakenya wanastahili kuelimishwa
kuhusu udugu na utaifa. Fauka ya haya, masuala yanayohusiana na umiliki wa ardhi yanafaa kutadarukiwa kwa dhati.
Maswali ya Ufahamu
a. Toa anwani mwafaka kwa makala haya. (alama 1)
b) Taja madhara manne ya ukabila. (alama 2)
c) Shughuli za ugawaji wa misaada zimekumbwa na changamoto gani? (alama 1)
d) Eleza tofauti ya chanzo cha vita nchini Somalia na Kenya. (alama 2)
e) Mwandishi anatoa mapendekezo yepi kwa kutatua tatizo hili la ukabila. (alama 4)
f) Eleza kinaya cha maisha ya wanakenya kwa sasa. (alama 1)
g) Eleza maana ya maneno haya yalivyotumika katika kifungu cha ufahamu.
a) Mawio
b) Kuvia

3
c) Aali
d) Tadarukiwa.
(Alama 4)
UFUPISHO
Soma makala haya kisha ujibu maswali yafuatayo.
HAKI ZA BINADAMU
Binadamu wana mazoea ya kufikiria kuwa jinsi wafanyavyo, waongeavyo na wafikiriavyo kuhusu vitu ndivyo inavyopasa kuwa. Kama binadamu tunaamini njia yetu ndiyo sahihi, yenye mantiki na inayopasa kufuatwa na kila mtu. Msingi huu huu unakwenda kinyume na kutambua kila binadamu ana haki ya kufikiri, kusema au kuongea na kutenda mradi asikiuke
haki ya mwenzake iliyo sawa na yake. Nguzo mojawapo inayogongomelea hoja hii ni Haki za Binadamu. Azimio la kutangaza Haki Bia za Binadamu liliafikiwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 10 Desemba, 1948.
Baraza kuu hilo liliyasisitizia mataifa wanachama umuhimu wa kuyasambaza, kuenezea, na kusisitiza kusambazwa kwa azimio hilo katika shule na taasisi za kielimu. Msingi wa uhuru, haki na amani ulimwenguni ni kutambua binadamu wote wana haki sawa. Ingawa kimsingi jamii na mataifa yote ya ulimwengu yanapaswa kuthamini, kusambaza na kuhimiza umuhimu wa Haki za Binadamu zipo jamii ambazo hukiuka haki hizo. Matokeo ya ukiukaji huu yana athari hasi sana kama ilivyotokea nchini Rwanda na Bosnia. Herzegovina kulikotokea mauaji ya halaiki.
Azimio la Haki za Binadamu linajumuisha vipengele kadha ambavyo ni mihimili mikuu ya Azimio lenyewe. Kipengele msingi kabisa kinasisitiza kuwa kila kiumbe anazaliwa huru na ana haki na hadhi sawa na kiumbe mwingine. Ukweli wa kauli hii ulikokotezwa na kauli ya mwanafalsafa maarufu Jean Jacques Rosseau aliyesema kuwa kila kiumbe huzaliwa huru lakini huwa katika pingu ulimwengu mzima. Kauli hii ilitambua ukiukaji huu wa kipengele hiki. Kipengele cha pili kinasisitiza kuwa binadamu wote wana haki za kufurahia uhuru wao pasi na kutengwa au kubeuzwa kwa misingi yoyote ile si rangi, kabila, jinsia, lugha, dini, asilia, utajiri au chochote kile.
Vipengele vingine vinatukumbusha kuwa kila mtu ana haki ya kuishi na kupata ulinzi. Hamna mtu anayepaswa kuishi maisha ya utumwa au unyonge wa kutumikishwa kwa namna yoyote ile. Suala hili linasisitizwa na kipengele cha sita kinachokataza kudhalilishwa kwa watu au kutunzwa kwa namna yoyote ambayo inamfedhehesha kama kiumbe. Azimio la Haki za Binadamu linasisitiza kuwa binadamu yoyote yule ana haki ya kupata ulinzi wa kisheria. Binadamu huyo hapasi kubaguliwa na ana haki ya kupata fidia ya kisheria taraa haki zake za kimsingi zikikiukwa.
Hata hivyo sio watu wote ulimwenguni ambao wanazifurahia haki hizi za kimsingi. Zipo lukuki za jamii ulimwenguni ambako haki za kimsingi zinakiukwa. Katika nchi ambazo zinaongozwa na watawala wa kiimla, si ajabu kuona haki za binadamu zikikiukwa. Viongozi wa aina hiyo huwa wamegeuzwa ng'ombe wa shemere na tamaa, ubinafsi na ukatili usiojua thamani ya utu. Viongozi wa aina hii wanasahau kuwa kila binadamu ana haki ya kuishi maisha huru, asipotumikishwa wala kulanguliwa kama bidhaa.
Nchi za kiimla aghalabu huongozwa na itikadi kuwa kiongozi ndiye pekee ambaye ana uwezo wa kufikiri, kuamua na kutenda. Watu wengine wanapaswa kumfuata kisilka kama yule mbwa wa Pavlov ambaye alitokwa na mate kila kengele ilipopigwa. Viongozi wa aina hii hawachelei kuwatenza nguvu raia zao; kuwadhalilisha kwa namna nyingi. Viongozi wa aina hiyo huiona sheria ya nchi kama iliyowekwa kwa watu wengine bali sio wao.Msimamo huu unakwenda kinyume na kipengele cha saba cha Haki Bia za Binadamu kisemacho kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria.
Baadhi ya haki zinazokiukwa katika jamii za kimabavu ni haki ya watu kuungana, kuwaza, kushiriki katika maamuzi ya serikali, kuwa mwanachama wa jumuia waitakayo, kumiliki mali, kutembea, kuishi anakotaka, kutohukumiwa bila ya kuwako na utaratibu wa kisheria. Ni muhimu hata hivyo kujua ni muhimu kwa raia wenyewe kujielimisha na kuzijua haki zao. Serikali inapaswa kuwa mlinzi wa sheria zenyewe. Lakini muhimu kujua pia kuwa mlinzi naye hulindwa pia.
a) Kwa maneno kati ya 90 – 100 fafanua Haki Bia za Binadamu zilizoafikiwa na Baraza kuu la umoja wa Mataifa.
(Alama 10)
Nakala Chafu
Nakala Safi
b) Kwa nini viongozi wa kiimla hukiuka haki za binadmu. (Maneno 50 -60).
Nakala Chafu (Alama 5)
Nakala Safi
III SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA
1. Andika methali inayoafikiana na maelezo haya
Kwa kawaida, mtu hupendelea nafsi yake (alama 2)
2. Andika katika udogo
Mwanamke alimuua mbuzi kwa shoka. (alama 2)
3. Weka shadda katika neno ‘barabara’ ili kuibua maana tofauti ya neno hilo
i) Barabara (maana)
ii) Barabara (maana)
4. Tunga nomino mbili kutokana na vitenzi hivi. Hakikisha viko katika umoja. (Alama 2)
Kitenzi Nomino Nomino
Elewa
Suka
5. Onyesha mofimu katika neno lifwatalo na utaje ni za aina gani
Kilichowaumiza. (alama 3 ½ )
6. Tunga sentensi yenye mpangilio huu wa kisarufi. (alama 2 ½ )
I + W + T + N + V.
7. Tunga sentensi kudhihirisha maana tofauti kati ya
(a) Jozi
(b) Njozi (alama 2)
8. Andika sentensi hii katika usemi wa taarifa.
“Ninataka kumwona askari aliyemletea mfungwa tupa sasa hivi,” alisema Batu. (alama 2)
9. Eleza na uonyeshe matumizi manne tofauti ya kiambishi ‘ku’ (alama 4)
(i) …………………………………………………………………………………………………
(ii) ………………………………………………………………………………………………..
(iii) ……………………………………………………………………………………………….
(iv) ……………………………………………………………………………………………….
10. Kanusha sentensi hii katika wingi
Mgonjwa mwenye kichomi aliyelazwa hospitalini ameaga dunia. (alama 2)
11. Changanua sentensi hii kwa kutumia matawi na useme ni sentensi ya aina gani
Wale wanafunzi stadi walioibuka na alama bora zaidi, wameajiriwa kazi.
a) Aina ………………………………………………………………….. ( alama ½ )
b) Mchoro (alama 7 ½ )
12. Onyesha virai vitatu katika sentensi hii na utaje ni vya aina gani.
Mtoto yule mdogo amekunywa maziwa kwa kikombe. (alama 3)
(i)…………………………………………………………………………………………………
(ii)………………………………………………………………………………………………
(iii)………………………………………………………………………………………………
13. Tunga sentensi tatu ukitumia neno papara liwe na sifa hizi. (alama 3)
a) Kielezi
b) Nomino
c) kivumishi
14. Sauti hii hutamkiwa wapi na huitwaje?
|Ch| (alama 1)
IV ISIMU JAMII. (alama 10)
(a) Jadili sifa tatu kuu za lugha ya taifa. (alama 3)
b) Eleza majukumu saba ya lugha za taifa. (alama 7)
Mwisho






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers