Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Thika District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper

Thika District Mock - Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2011



102/3
KISWAHILI
KARATASI YA 3
FASIHI
JULAI 2011
MUDA : Saa 2 ½
MTIHANI WA PAMOJA WA SHULE ZA MKOA WILAYANI THIKA – 2011
HATI YA KUHITIMU ELIMU YA SEKONDARI KENYA (K.C.S.E)
KISWAHILI
KARATASI YA 3
INSHA
MUDA : Saa 2 ½
MAAGIZO
(a) Jibu maswali manne pekee.
(b) Swali la Kwanza ni la lazima.
(c) Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani
Tamthilia, Riwaya, Hadithi Fupi na Fasihi simulizi.
(d) Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
(e) Karatasi hii ina kurasa 4 zilizopigwa chapa.
(f) Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa
chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
SWALI LA LAZIMA
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuatia
KIFO
1. Kifo kisonga pumzi, ‘siseme umeshakufa
Au damu si tembezi, kuduru yake masafa
Mwili hautaki kazi, ukisibiwa maafa
Si kifo ni tendekezi, kiumbe huja mshika
2. Na moyo ukibarizi ‘siseme umeshakufa
Mapigo haupwagizi, umepata hitilifa
Viungo havijiwezi baada chake kifafa
Si kifo ni ujilizi, wa mwisho mtu kufika
3. Kifo kaburi maka’zi ‘siseme umeshakufa
Na udongo shehenezi, ututikwe kwenye ufa
Na mwili uwe mwozi, unuke kuliko sifa
Si kifo ni malalazi mwisho wako umefika
4. Kifo ni kuwa u hai, na kumbe umeshakufa
Utu wako waburai, na kuzibeba kashifa
Waisha wala hujui kama vile ni sadifa
Hicho kifo nadai wengi tumeshawazika
5. Kifo kuwa hutambui na kumbe umeshakufa
Fasili huichukui, asiliyo na tarafa
Maovu na uadui, unaliuza taifa
Hicho kifo siyo ndui tena ushamung’unyuka
6. Watazama anuwai, na kumbe umeshakufa
Husemi rai hutoi, waogopa makhalifa
Wasemalo hukatai hewalla nyingi sharafa
Huoni na husikii, uitafutapo swifa
7. Kwa fundo wapiga tai, na kumbe umeshakufa
Ulimi huunyanyui. kwa kuhofia tilifa
Hadhi yako kama yai liangukapo hutifa
Hicho kifo singojei mimi kuja kunifika.
KIFO
MASWALI
(a) Shairi hili linarejelea ”kifo”. Fafanua vifo vinavyorejelewa. (alama4)
(b) Taja tamathali za usemi zilizotumika katika shairi na uzitolee mifano. (alama3)
(c) Eleza umbo la shairi hili. (alama4)
(d) Andika ubeti wa saba katika lugha nathari. (alama4)
(e) Kwa kutoa mifano, onyesha aina tatu za uhuru wa kishairi. (alama3)
(f) Eleza maana ya vifungu vifuatavyo kama vilivyotumika katika shairi. (alama2)
(a) Si kifo ni ujilizi.
(b) Utu wako waburai
TAMTHILIA
Kithaka wa mberia: Kifo kisimani.
2. “Moyo wangu uko taabani; nina huzuni!”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama4)
(b) Taja mbinu iliyotumika katika dondoo hili. (alama1)
(c) Eleza sifa na umuhimu wa msemewa. (alama7)
(d) “Maisha ya wanabutangi yamejaa taabu na huzuni.” Thibitisha. (alam8)
RIWAYA
Jibu swali la 3 au la 4.
Said A Mohamed: Utengano
3. Dunia mwendo wa ngisi” Jadili ukweli wa methali hii ukizingatia wahusika wafuatao.
(alama20)
(a) Maksuudi
(b) Maimuna
4. “Bibi wewe haini kwelikweli.Wewe ndiye uliyenihusudu mimi, unasema nini? Lakini
una maandizi yako kwa Mungu:
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama5)
(b) Eleza asili ya uchungu huo. (alama5)
(c) Ni nini hatima ya majibizano haya. (alama10)
HADITHI FUPI
K.W. Wamitila: Mayai waziri wa Maradhi na Hadithi nyingine.
Jibu swali la 5 au la 6.
5. Mbinu ya Jazanda imetumika sana katika Diwani ya Mayai Waziri wa Maradhi.
Thibitisha (alama20)
6 (a) Fafanua matatizo yanoyozikabili jamii kwa mujibu wa hadithi zifuatazo.
(alama10)
(i) Msamaria mwema
(ii) Ndimi za mauti
(b) Eleza sifa za viongozi ukirejelea hadithi ya Mayai Waziri wa Maradhi. (alama 10)
FASIHI SIMULIZI
7. (a) Fafanua sifa za ushairi zinazoufanya kuwa wimbo.
(alama5)
(b) Miviga ina hasara gani katika jamii?
(alama4)
(c) Eleza umuhimu wa misemo na nahau katika jamii.
(alama5)
(d) Je, tunaweza kufanya nini kuhakikisha kuwa fasihi simulizi inaendelea kuwako.
(alama6)






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers