Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Laikipia District Mock- Kiswahili Paper 2 Question Paper

Laikipia District Mock- Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2010



JINA…………………………………………….……………….NAMBARI
YAKO………………………..
SHULE…………………………………………………………………………………………………
………….
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA PILI
LUGHA
JULAI/AGOSTI 2010
MUDA 2½
MTIHANI WA LAICOMET KIDATO CHA NNE
Kenya Certificate of Secondary Education 2010
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA PILI
LUGHA
JULAI/AGOSTI 2010
MAAGIZO
_ Andika jina lako na nambari yako.
_ Jibu maswahili yote.
_ Andika majibu katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali.
1. UFAHAMU
Soma makala yafuatayo kisha utekeleze maagizo yafuatayo
Utotoni niliamini kwamba kusoma ndiko ufunguo wa kila kitu ulimwenguni kwa jinsi
kunavyoonekana kuwatoa watu katika uzuzu, ukata na ugonjwa: na kuweka kwenye maisha bora
ya mwangaza wa kujua kusoma na kuandika, utajiri wa kuweza kuvaa hata suti ya vipande, vitatu, na kuwa na afya ya kuonekana kwa kitambi. Hizo ni zamani zile ambapo shule ya vidudu haikuwa sharti la mtoto kukubaliwa katika darasa la kwanza. Mtoto angelisha au kusaidia kwa kazi za nyumbani mpaka kufika umri labda wa miaka kumi kisha, kufumba na kufumbua, afisa wa serikali angeonekana akishauriana na mzazi wa mtoto. Matokeo yangekuwa mtoto huyo kuanza safari ndefu ya kila siku, apate asipate chakula.
Mimi kwa upande wangu sikujali maisha pata-nenda shule, kosa – bado – nenda – shule.
Sikujali kero za baridi kali wala karaha za vua la asubuhi. Kuanzia utotoni niliwahusudu wenzangu waliokuwa wakirauka kiasi cha kufikiriwa kuwa walilala kwa shati na kaptula zao, au kwa blauzi na skati na kaptula zao. Nilipendezwa na yunifomu zao nikatamani na hata kuapa kwamba siku moja notavaa kama wao na kutembea kwa marinog kama wao. Zaidi nilitamani kufika walikokuwa wakienda na kufanya walivyokuwa wakifanya huko.
Penye nia hapakosi njia. Nia yangu ilidhihirika pale nilipojiunga na darasa la kwanza. Darasa la kwanza lilinisoma kisogo baaada ya siku mbili tu. Nalo la pili likanipungia mkono baada ya juma moja. Miaka mitano baadaye nilikutana na kiunzi cha kwanza kwenye mtihani wa kitaifa wa chumba cha saba uliokuwa kifungua mlango wa kuingilia kidato cha kwanza.
Baada ya miaka minne nilikutana na mlango funge mwingine ambapo nilibisha na
ukanifuungukia kwa kutia fora katika mtihani wa kiwango cha elimu ya upili. Katika miaka
miwili liyofuatia nilijiunga na shule maarufu ya kitaifa siku hizo.
Masomo hayakuendelea kuwa mteremko kwangu kwani uchachefu wa karo na masurufu
ulimaanisha kuwa siku nyingi nilikuwa nje ya kuta za darasa letu. Hata ivyo nilijifunga
masombo.Hatimaye nilifunguliwa milango ya kuingia ndaki.
Baada ya kuhitimu kwa shahada ya kimsingi ya uzamili, kisha uzamifu au udaktari falsafa
hatimaye, nilifanywa meneja kufikia leo. Hata nikiwa ukubwani bado ninazidi kusoma na kutafiti ili nisiote ukurutu wa akili.
Cheo na madaraka haya ya umeneja yamaanisha kila siku nivae suti kamili na shati nyeupe pe,
ambayo shingoni imeambatanishwa na kipande maalumu cha kitambaa kinacholewalewa kifuani.
Nijiangaliapo kiooni hujifananisha na mtu ambaye amejitia kitanzi shingoni.
Nina kitambi ambacho labda ni taashira ya utajiri. Hata hivyo ingawa mimi si tajiri mwenye
sauti kubwa kiuchumi, ninaweza kujivunia elimu yangu iliyoniwezesha kujimudu kidogo
maishani. Sasa nina shamba-langu mwenyewe, nyumba yangu mwenyewe ambayo imejaa mali
yangu mwenyewe. Nina redio yangu mwenyewe, rununu –yangu mwenyewe na wanyama wangu
mwenyewe.
Lakini mwenzungu ambaye zilimwishia ukingoni katika shule za nasari, hana elimu, pesa wala
anaahu kuzikiwa wakati mpira utakapomwia mwingi.
MASWALI
a) Eleza imani ya mwandishi kuhusu elimu. (alama 3)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
……………………………………………………………………………………………………
b) Taja dhiki zilizomkabili mwandishi alipokuwa shuleni ( alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
…………
c) Onyesha uhusiano uliopo kati ya elimu, kazi na ukwasi kwa mujibu wa habari hii.
(alama 3)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
……………………………………………………………………………………………………
d) Ukirejelea makala haya, fafanua msemo, ‘elimu ni bahari haina kikomo’ (alama 3)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
e) Hatima ya wale ambao hawakupata elimu ni ipi? (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
…………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
……………………………………………………………………………………………………
f) Badala ya maneno yafuatayo mwandishi angetumia msamiati gani? (alama 3)
i. Niliwahusudu…………………………………………………………
ii. Ndaki………………………………………………………………..……
iii. Taashira………………………………………………………..…………
2. MUHTASARI
Imesemwa na kurudiwa tena na tena kwamba, iwapo tuna maono ya kujiondoa katika
umasikini wa kupindukia, ni lazima tukipe kilimo umuhimu.
Zaidi ya Wakenya 10 milioni wamo hatarini ya kufa njaa katika maeneo mbali mbali kwa sasa
kufuatia uhaba wa chakula nchini.
Kiini kikubwa cha njaa hiyo ni mapuuza ya muda mrefu katika sekta ya kilimo.
Imesahaulika kuwa karibu asilimia 75 ya wakenya wanategemea kilimo kwa chakula na mapato ya
kifedha kila siku. Kilimo hutoa karibu robo tatu ya nafasi za kazi kwa wananchi na pia kuiletea serikali karibu robo ya mapato yake kutokana na mazao ya mauzo katika mataifa ya nje.
Wataalamu wa masuala ya zaraa wanaeleza kuwa pato la nchi linalotokana na kilimo
huangamiza njaa mara nne zaidi ya mapato yanayotokana na shughuli nyinginezo za kiuchumi. Hiyo ni kwa sababu shughuli za kilimo hulenga kuzalisha vyakula moja kwa moja.
Imebainika kuwa, katika mataifa mengi yanayostawi,asilimia 75 ya wananchi huishi katika maeneo ya mashambani na idadi hii hutegemea kilimo kujimudu kimaisha ilhali hapa Kenya ni asilimia nne pekee ya bajeti inayowekezwa katika kilimo.
Kwa wakati huo, ushuru unaotozwa bidha za kilimo katika maeneo ya Kusini mwa Sahara
umebainika kuwa mkubwa. Hii imepelekea uwekezaji katika kilimo kupungua na hivyo kuchangia
kukithiri kwa baa la njaa.
Wakati umewadia kwa serikali za Afrika na wapangaji wa masuala ya uchumi kuweka juhudi
maradufu katika kushabikia kilimo ili kumalizaa njaa na umasikini.
Kuna haja ya kuwajulisha, kuwahimiza na kuwaelimisha wakulima wa mashamba madogo madogo
kwa mfano, kuhusu mihimili ya zaraa kama vile uzalishaji wa matunda na mboga, ufugaji wa ndege, samaki na ng’ombe mbali na kuweka mikakati ya kuanzisha nafasi za kazi katika sekta ya kilimo.
Serikali itafiki lengo hili iwapo itaanza kufadhili kilimo, kupunguza gharama za pembejeo za kilimo, kuweka sera zinazodhibiti uuzaji na ununuzi wa vyakula hasa baina ya mataifa na kuongeza sehemu ya bajeti inayotengewa kilimo.
Bila hilo hatutakuwa na lingine bali kukimbilia mataifa yaliyiostawi kuomba misaada ili kuwanusuru raia wetu kutokana na ghadhabu ya njaa.
(a) Kwa kutumia maneno kati ya 70-75 eleza ni kwa nini kuna haja ya serikali kutilia maanani
na kuimarisha kilimo nchini (alama 6 1 ya mtiririko)
Matayarisho
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………

Jibu
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
(b) Eleza namna serikali inovyoweza kumaliza njaa na umaskini nchini.
(maneno 60-70) (alama 9, 1 ya mtiririko)
Matayarisho
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………

Jibu
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
3. MATUMIZI YA LUGHA
a) Andika nomino moja ambayo inapatikana katika ngeli ya U-I. (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………
b) Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo :- (alama 2)
Bi. Kija anajiona
(i)……………………………………………………………………………………………………
………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
(ii)……………………………………………………………………………………………………
……………………………………..
………………………………………………………………………………………………………
………………………………….
c) Kanusha sentensi ifuatayo:- (alama 2)
Alipofika hotelini, aliomba chakula akapewa
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
d) Tunga sentensi ya neno moja yenye kiima, wakati, kitendewa/kitendwa na kitenzi.
(alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
e) Andika sentensi ifuatayo katika hali ya ndogo: – (alama 2)
mwanamke huyo aliipiga ngoma hiyo mpya hadi ikapasuka
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
f) Kamilisha jedwali lifuatalo ili kuonyesha jinsi irabu zinavyotamkwa.
irabu Hali ya ulimi Hali ya mdomo
e
u
(alama 2)
g) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya vishale( ).
Juma analima shamba lakini Asha anasoma. (alama 3)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
…………
h) Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli ya kutendeana. (alama 2)
(i) La
………………………………………………………………………………………..
………………………………………………………………………………………..
(ii) Pa
………………………………………………………………………………………
………..
i) Andika sentensi ifuatayo upya kwa kutumia visawe vya maneno yaliyopigiwa msitari
Bikizee alipoingia ukumbini alimkuta mvulana chotara ameketi. (alama 2)
........................................................................................................................................................
........................................................................................................................................................
................................................
j) Pigia kistari kirai nomino katika sentensi ifuatayo:- (alama 2)
Kuimba kwake kunapendeza ajabu
k) Tunga sentensi yenye kiwakilishi cha nafsi tegemezi. (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
l) Taja matumizi manne ya mshazari au mkwaju. (alama 2)
(i)………………………………………………………………………………………………….
(ii)…………………………………………………………………………………………….......
(iii)………………………………………………………………………………………………..
(iv)………………………………………………………………………………………………..
m) Andika sentensi ifuatayo upya ukitumia kiunganishi cha neno moja chenye maana sawa na
kilichopigiwa msitari
Sitafika shuleni kesho kwa sababu nina shughuli za dharura. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
n) Andika sentensi ifuatayo upya kwa kutumia ‘o’ rejeshi tamati:
Kipofu ambaye alishinda mbio alituzwa nishani ya dhahabu. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
o) Onyesha aina za yambwa katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
Yaya alimpa mtoto maziwa kwa chupa
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
p) Huku ukitoa mifano ya sentensi, eleza matumizi mawili ya kiambishi ‘po’. (alama 4)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ia kiimbo eleza sentensi zifuatazo ni za aina gani. (alama 3)
(i) Mama yuko jikoni
………………………………………………………………………………………………
(ii) Njoo hapa!
………………………………………………………………………………………………
(iii) Lo!Ameanguka vibaya sana.
………………………………………………………………………………………………
r) Tunga sentensi tatu ukitumia neno jasiri kama:-
(i) Kivumishi
………………………………………………………………………………………………
(ii) Kitenzi
……………………………………………………………………………………………
(iii) Nomino
………………………………………………………………………………………………
4. ISIMU JAMII
(a) Fafanua mambo matano yanayosababisha kutokea kwa lahaja. (alama 5)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
(b) Eleza matatizo yanayomkabili mtu anapoitumia lugha yoyoye isipokuwa ile ya kwanza
(alama 5)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers