Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Bondo District Mock - Kiswahili Paper 2 Question Paper

Bondo District Mock - Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007

Jina………………………………………………… Nambari . ……………………………….
Shule ………………………………………………...
102/2
Kiswahili
(LUGHA)
Karatasi 2
JULAI/AGOSTI 2007
Muda: Saa 2 ½
WILAYA YA BONDO MTIHANI WA MWIGO WA K.C.S.E - 2007
Hati ya Kuhitimu Kisomo Cha Sekondari Kenya (K.C.S.E.)
102/2
Kiswahili
(LUGHA)
Karatasi 2
JULAI/AGOSTI 2007
Muda: Saa 2 ½
MAAGIZO
• Andika jina lako na namba yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
• Jibu maswali yote.
• Majibu yako yaandike katika nafasi zilizoachwa katika kijitabu hiki cha maswali.
Karatasi hii ina kurasa 12 zilizopigwa chapa
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo.
1. UFAHAMU
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali.
Lugha imekuwa kikwazo kikubwa katika kukuza teknolojia ya habari na mawasiliano
(TEKNOHAMA) barani Afrika. Lugha ambazo zimekuwa zikitumiwa ni za kimagharibi kama vile
Kijerumani, Kifaransa na Kiingereza. Idadi kubwa ya Waafrika, hasa wanaoishi vijijini,
hawazifahamu lugha hizi.
Uamuzi wa Shirika la Microsoft wa kutumia lugha ya Kiswahili katika programu za kompyuta kuanzia mwaka 2005 ni mchango mkubwa. Kuzinduliwa kwa mradi huu ni tukio la kipekee kuimarisha teknolojia sehemu za mashambani. Mradi huu umewawezesha wananchi takribani milioni 150 wa
janibu za Afrika Mashariki kufaidi huduma za tarakilishi.
Utekelezaji wa mradi huu halikuwa jambo jepesi. Kwanza, ilibidi Shirika la Microsoft chini ya uongozi wa Bill Gates kulishawishi Bodi lake la wakurugenzi. Bodi liliposhawishika kuwa Kiswahili ni lugha inayotumiwa na mamilioni ya watu liliidhinisha kuzinduliwa kwa mradi. Hatua iliyofuatia ilikuwa kuteua maneno 700,000 ya kimsingi ya Kiingereza ambayo yangetafsiriwa kwa Kiswahili.
Hatua iliyofuata ilikuwa ushirikiano na dola pamoja na mashirika ya kibiashara na taasisi za kielimu ulimwenguni. Ilipobainika kuwa matumizi ya lugha ya Kiswahili yangehamasisha uwekezaji katika vituo vya mtandao vijijini, ushirikiano katika kuendesha mradi huu uliafikiwa bila shida. Mradi huu ulichukua muda wa miezi 18 kukamilika. Uliwashirikisha wahusika katika uwanja wa teknolojia ya habari, mawasiliano, elimu, biashara na idara za Kiswahili katika vyuo vikuu vya Afrika Mashariki.
Vyuo vikuu hivi ni pamoja na Dar es Salaam, Nairobi, Kenyatta na Makerere.
Wataalamu walioshirikishwa walisaidia katika kubuni faharasa ya istilahi za Kiswahili 3,000. Hizi ni zile ambazo zinafaa kwa matumizi ya kompyuta ya kawaida na ya kila siku. Mradi huu umeshangiliwa na wakereketwa na wapenzi wa Kiswahili katika nyanja zote. Wasomi, wanariadha,wanamuziki, watalii, wafanyabiashara, wanasiasa, wafuasi wa dini mbali mbali na wakulima; wote wamefurahia hatua ya Kiswahili kuingizwa kwenye mtandao.
Watu ambao walikuwa hawawezi kutumia tarakilishi kwa sababu ya kutojua Kiingereza sasa hawana kisingizio. Matumizi ya Kiswahili yatapanua na kuimarisha mawasiliano baina ya watu wanaoishi vijijini na pembe zote za ulimwengu.
Jambo la kutia moyo zaidi ni kuwa sasa vyuo vikuu vinavyotoa masomo kwa kutumia mitandao
vimepewa idhini ya kutumia programu hizi. Walimu na wanafinzi wanapata habari moja kwa moja
kwa Kiswahili bila kutafsiri. Kuna uwezekano sasa wa kusambaza mafunzo katika nyanja na viwango vyote kwa mfumo wa elimu ya mbali.
Katika ulimwengu wa utandawazi, tukio kama hili lina manufaa makubwa. Wananchi wa vijijini
wanaweza kupata habari na maarifa kutoka pembe zote za dunia na kuhusu masuala tofauti tofauti kwa lugha wanayoielewa barabara.
Kusambaa kwa matumizi ya ngamizi vijijini kutaimarisha biashara inayofungamana na teknolojia ya mawasiliano. Hali hii itainua maendeleo ya kiteknolojia na kiwango cha maisha vijijini. Bila shaka mwachano uliopo baina ya sehemu za mijini na vijijini utapungua.
Haya ndiyo maendeleo anayokamia kila mja wa siku hizi. Lililopo ni serikali kupania kupanua na kusambaza muundo mbinu kama umeme na simu katika sehemu zote za nchi. Pamoja na haya, kuna haja ya kupunguza bei ya ngamizi na vipuri vyake ili kuwatia motisha watu kununua kompyuta kwa wingi. Ikumbukwe kuwa lengo la kuanzisha mradi huu lilikuwa kuisaidia serikali kupanua na kusambaza matumizi ya huduma za kompyuta na mtandao katika shule, vituo vya kijamii na maeneo ya makaazi. Huduma hizi ni msingi wa elimu, biashara na mawasiliano ya kisasa.
Maswali
a) Eleza hatua zilizotekelezwa ili kuingiza Kiswahili katika mtandao. (lama 4)
……………………………………………………………………………………………………………

b) Lugha imekuwa kikwazo kikubwa katika kukuza teknolojia ya habari na mawasiliano Barani
Afrika. Thibitisha kauli hii. (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
c) Fafanua faida za mradi wa kutumia Kiswahili katika ratiba ya tarakilishi. (alama 3)

d) Serikali inahitaji kufanya nini zaidi ili kufanikisha mradi huu. (alama 3)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
e) Andika visawe vya maneno haya. (alama 1)
(i) kikwazo
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
(ii) Mwachano
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika taarifa. (alama 3)
(i) Faharasa
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
(ii) Wakereketwa
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
(iii) Ngamizi
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
2. UFUPISHO
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Waatalamu wa maswala ya kielimu wanadai kuwa huenda nchi hii ikalaumiwa kwa kuendeleza
mfumo wa elimu unaozingatia maslahi ya wakwasi na kuwapuuza wachochole. Mfumo huu wa elimu
umezua mfumo mwingine wa kijamii ambapo watoto wa wenye hadhi wanapata elimu bora kuliko
watoto wa maskini. Pengo baina ya haya matabaka linazidi kupanuka kama ardhi na mbingu.
Watoto kutoka jamii hohehahe wanasomea katika shule za umma zisizo na lolote wala chochote na watoto wa kifahari wanasomea katika shule za kibinafsi zilizo na vifaa mufti na mazingira faafu.
Mfumo wa jinsi hii ni wa kuitia jamii kitanzi kwa sababu ya kuzuka kwa matabaka yanayohasimiana.
Katika nchi ambapo asilimia sitini ya watu inaishi katika hali ambayo ni chini ya dola moja kila siku,watoto wengi huenda shuleni bila kula chochote na hushinda hivyo kutwa nzima na wasiamue chochote darasani. Walimu wao nao hawana ilhamu au kariha ya kufanya kazi kwa sababu mazingira ya kikazi ni mabovu na huenda shuleni shingo upande kama wakulima bila pembejeo. Madarasa yao ni mabanda na wengine husomea chini ya miti ambayo inaweza kukatwa wakati wowote na wachoma makaa waliokosana na mazingira. Unapowatazama watoto hawa, kile kinachoitwa sare ya shule kinakirihisha na kuyaudhi macho. Ni matambara yaliyosheheni viraka vya kila aina katika mseto wa ufakiri. Hawa ni wenzetu eti!
Tatizo hili limekuwa nyeti hasa kutokana na utandawazi na mfumo wa soko huru ambao unaruhusu shule za kibinafsi kuendeshwa kama mashirika ya kibiashara. Karo inayolipwa katika shule hizi ni ya kibiashara, majengo na vifaa ni vya kibiashara, walimu ni wa kibiashara, ilimuradi kila jambo lalenga maslahi ya kibiashara ya walala hoi. Hapa ndipo chimbuko la makabila mawili maarufu nchini yaani matajiri walamba vidole na maskini wanaostakimu madongo-kuinama.
Uchunguzi umethibitisha kwamba zaidi ya asilimia sitini ya wanafunzi wanaojiunga na shule za kitaifa hutoka katika shule za kibinafsi zinazomilikiwa na matajiri. Mbinu ya wizara ya Elimu ya kugawa nafasi kwa njia ya haki katika shule za kitaifa haijafua dafu kwa sababu matajiri wajanja huwasajili watoto wao kufanyia mtihani katika shule zisizokuwa na ushindani mkubwa zilizomo mashambani. Kwa kufanya hivyo watoto wa maskini huwa wamefungiwa njia kotekote na kuporwa haki yao. Ama kwa kweli mwenye nguvu mpishe kwani dau la mnyonge haliendi joshi.
Wanafunzi katika shule za kibinafsi hufunzwa katika makundi madogo madogo ambayo humwezesha
mwalimu kushughulikia mahitaji ya kibinafsi ya kila mtoto. Wazazi wao pia huwaajiri walimu wakati wa mapumziko ili kugongomeza au kushadidia mada ambazo hawakuzielewa vizuri shuleni. Upeo wa lugha wa watoto hawa hauwezi kulinganishwa na wa wenzao kwa sababu shule zao zina maktaba za kisiasa, vifaa vya kisasa na vitumeme na hufunzwa teknolojia za kileo kuhusu mawasiliano. Watoto hawa huandaliwa ziara za kielimu ili kutanua uelewa wao wa mambo na vile vile hualikiwa watu wanaosifika katika jamii ili kuwahutubia shuleni kwao kuhusu mada mbali mbali. Wawasilishaji hawa huwa ni kielelezo tosha kwa watoto hawa. Mzazi aliyesoma hujua umuhimu wa elimu na hivyo basi huandaa mikakati mahsusi ili kumfaulisha mwanawe kinyume na wazazi wakata.
Ni bayana kuwa iwapo hivi ndivyo mambo yalivyo basi hata vyuo vikuu vitakuwa himaya ya watoto wa matajiri huku watoto wa kimaskini wakisubiri kuajiriwa nao kama walinzi na matopasi. Sera za elimu nchini haziwezi kufanikiwa pale ambapo rasilmali muhimu zinatengewa watu wachache katika jamii. Watoto wa waunda sera hizi husomea katika shule ambazo hufuata mifumo ya kimataifa ambayo haina mkuruba na yetu hafifu. Katika majukwaa ya kisiasa utawasikia wakisifu mfumo
ambao watoto wao wanaukwepa kama ukoma. Imekuja kudhihirika kuwa wale wanaosemekana kuwa
viongozi wa kesho ni wale ambao sasa hivi wanasomea katika hizo akademia na kufuata mifumo ya kigeni au akademia zinazofuata mfumo wetu katika mazingira teule. Swali ni hili, kesho ya mtoto wa kimaskini ni ipi?
Inahitajika mikakati ya kimakusudi ili kulitanzua swala hili kabla ya milipuko ya kijamii kama vile,ujambazi,uuaji, ubakaji, uraibu na mihadarati, na kadhalika. Ipo lazima ya kujenga shule vielelezo katika kila wilaya ambazo zitafadhiliwa na serikali kwa kupewa mahitaji yote muhimu na lazima ya kuanzisha mpango wa lishe bora katika shule ili kukidhi matilaba ya watoto wote. Udahili wa wanafunzi katika shule za kitaifa na katika vyuo vikuu ni sharti uvalishwe vazi la utu na uzalendo bila ubaguzi. Shule za umma ziwe na walimu na madarasa ya kutosha ili kuondoa matatizo yaliyoibuka kutokana na kuanzishwa kwa mpango wa elimu ya bure katika shule za msingi. Sera kuhusu shule za chekechea lazima uzinduliwe kitaifa ili kusawazisha msingi wa kila mtoto kielimu. Walimu wa shule hizi za malezi lazima wawe na maandalizi sawa yatakayowawezesha kusawazisha viwango kitaalamu.
Mitaala yetu ilenge kuzalika kwa binadamu ambaye atajinufaisha yeye binafsi na taifa kwa jumla.
MASWALI
a) Bila kupoteza maana, fupisha aya mbili za mwanzo (maneno 45 – 55) (alama 4)
Matayarisho
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
Jibu

c) Yepi mambo muhimu yanayojitokeza katika aya ya tatu hadi ya saba? (alama 7)
(maneno 150 – 165)

c) Ni mapendekezo yapi yanayotolewa katika aya ya mwisho (maneno 55 – 65) (alama 3)
Matayarisho
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
Jibu
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
3. MATUMIZI YA LUGHA
a) Tumia kiulizi – ngapi kujaza mapengo.
i) Ni mitende ………………………….. iliyo kwenye shamba? (alama 1)
ii) Ni vitwana …………………………. watakaofanya kazi? (alama 1)
b) Maneno yafuatayo yanapatikana katika ngeli gani?
i) Waraka (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
ii) Mihadarati (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
c) Andika sentensi mbili kuonyesha matumizi tofauti ya alama ya mshazari. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
d) Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi ya ‘ki’. (alama 2)
10
e) Andika katika usemi halisi
Baba alimwambia mwanawe anyamaze kwa kuwa alikuwa akisikiza redio na akamwonya kuwa kama
hangefanya hivyo angemchapa. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
f)Andika sentensi zifuatazo upya kwa kufuata maagizo uliyopewa.
i) Mama aliomboleza kifo cha mwanawe. (Anza kifo….) (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
ii) Umekuja. Tumefurahi sana (unganisha sentensi hizi kwa kuanza na kuja….) (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
g) Andika sentensi zifuatazo kwa wingi.
(i) Ajae kisimani mbele hunywa maji maenge. (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
(ii) Zigo la kuliwa halilemei. (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
h) Ainisha matumizi ya ‘ingine’ na ‘ingineo’ katika sentensi zifuatazo.
(i) Marimba ni ala nyingine inayotumiwa katika tamasha za muziki. (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
(ii) Usiniletee bilauri nyingineyo nataka ile niliyokwambia. (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
i) Tumia kirejeshi cha mwisho katika sentensi ifuatayo (alama 2)
i) Yule ambaye hutupa tope hujichafua mwenyewe.
11
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
j) Bainisha viwakilishi nafsi katika sentensi hii.
Alimpiga mwanafunzi mtundu. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
k) Eleza maana mbili ya kifungu kifuatacho (alama 2)
Mgeni alifagia chakula
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
l) Tunga sentensi yenye kiingizi na kihusishi cha mahali . (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
m) Kanusha
Kono lake limepona baada ya kuumwa na joka. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
n) Tambulisha kielezi katika sentensi hii na ueleze ni cha aina gani.
Mtoto mdogo alikuja upesi akimkimbilia mamake. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
o) Tumia nomino zifuatazo kama vivumishi katika sentensi
i) Kanzu (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
ii) Mlevi (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
12
p) Tunga sentensi kutofautisha vitate hivi kimaana.
Hawara (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
Hawala (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
q) Sehemu hizi za mwili hufanya kazi gani?
i) Fuvu (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
ii) Figo (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
R. Tunga sentensi yenye aina zifuatazo za vishazi (alama 2)
i) Huru, huru
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
ii) Tegemezi, huru
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
S. Andika sentensi kuonyesha maana tofauti ya neno ‘chuma’ (alama 2)
i)
……………………………………………………………………………………………………………
ii)

4. ISIMU JAMII
a) Eleza majukumu matatu ya lugha ya taifa. (alama 3)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
B) Fafanua mtindo wa lugha uliotumiwa katika taarifa ifuatayo huku ukieleza sababu za matumizi ya
vitambulisho maalum vya lugha. (alama 4)
Wananchi, mimi sina mengi. Hapana katika nyinyi asiyenielewa. Sina la kusema, ila
ninawakumbusheni kuwa mnahitaji kiongozi atakayeshughulikia maslahi ya taifa zima. Mtu
huyo ni mimi na ninajitahidi niwezavyo kujenga masoko, barabara, shule zaidi na mazahanati
na maisha yenu yatakuwa ya raha zaidi.
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
c) Thibitisha kuwa adabu za lugha hazizingatiwi miongoni mwa wanajamii siku hizi. (alama 3)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
END

More Question Papers

Popular Exams

Return to Question Papers