Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Bungoma District Mock- Kiswahili Paper 2 Question Paper

Bungoma District Mock- Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007



JINA: …..………………………………………………………………… NAMBARI: ………..……
SHULE:………..……………………………………………………………………………………...…
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA PILI
LUGHA
JULAI / AGOSTI 2007
MUDA: SAA MBILI NA NUSU
MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA BUNGOMA
HATI YA KUHITIMU KISOMO CHA SEKONDARI KENYA
(K.C.S.E) 2007
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA PILI
LUGHA
JULAI / AGOSTI 2007
MAAGIZO
 Jibu maswali yote.
 Majibu yako yaandikwe katika kijitabu cha maswali
 Watahiniwa wanaweza kuadhibiwa ikiwa hawatafuata maagizo yaliyotolewa katika karatasi
hii.
Karatasi hii ina kurasa kumi na mbili zilizopigwa chapa. Mtahiniwa ahakikishe kwamba kurasa zote zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
SWALI LA KWANZA –UFAHAMU
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuatia.
Teknolojia mpya ni tawi la maarifa linalohusiana na sayansi kwa upande mmoja na uhandisi
(uinjinia) kwa upande mwingine. Sayansi ni elimu inayotokana na uchunguzi na majaribio katika maabara nao uhandisi ni ujuzi wa kuunda mitambo. Maarifa ya sayansi yanapotumiwa kutengeneza vitu viwandani, hali hii inakuwa teknolojia.
Zao mojawapo la teknolojia mpya ni simu tamba. Watu vijijini sasa wanawasiliana na jamaa
zao walio mbali. Akina nyanya wanapopanda njugu, kupalilia migomba, kukama ngamia au kukuna
nazi, wanaweza kuzunguuza na wajukuu zao walio uingereza, uchina au kwingine kule.
Hakuna mahali ambapo hapajafikwa na teknolojia mpya. Tukitembelea baadhi ya nyumba
tutaona vifaaa kama vile tanuri la miale au mikrowevu ambalo linapika maharagwe yakaiva kwa
dakika chache tu. Majokofu nayo yanatusaidia kuhifadhi vyakula bila kuharibika. Hata maiti na mizoga inaweza kuhifadhiwa kwa miaka mingi kwa ajili ya utafiti bila kuoza katika ufuo au mochari.
Kwa upande wa kilimo, teknolojia imefanya makubwa. La kustaajabisha ni mtu mmoja kulima
eneo kubwa la shamba kwa trekta halafu akapanda kwa tandazi, akanyunyizia dawa kukausha
magugu, akavuna na kukoboa mahindi akiwaa peke yake. Siku hizi inawezekana kukuza mimea na
kufuga wanyama wanaokomaa kwa muda mfupi na kutoa mazao maradufu kwa sababu ya teknologia
mpya.
Teknolojia hii imewezesha watu kuvumbua aina nyingi za nishati. Badala ya
kutegemea umeme unaotokana na maji tu, sasa watu wanatumia mvuke, nguvu za upepo na nishati ya jua kupata umeme. Kwa sababu hii, hata mababu zetu vijijini wanatazama televisheni bila shida wala wahka.
Kwa upande mwingine, teknolojia ina madhara yake. Kwa mfano, uundaji wa silaha kali
unaendelea kuwaangamiza watu wengi. Mabomu ya kitonoradi yaliyoangushwa Hiroshima na
Nagasaki Japan mwaka 1945 ni zao la kisayansi. Haya yaliwaua watu wengi na madhara yake bado yanadhihirika hata leo katika maumbile ya watoto wanaozaliwa na upungufu. Tena magaidi na wahalifu wa kimataifa wanatumia teknolojia mpya kuimarisha mbinu zao za kutenda maovu. Isitoshe,inawezekana kutumia teknolojia kuagizia benki kutuma pesa nje ya nchi ya bila mwenye hazina kujua.
Wahalifu wanaweza kusikiza mawasiliano ya watu kwa simu hata ikiwa ni baina ya polisi.
Kisha matatizo mengi ya kiafya yasemekana yanatokana na vyakula vilivyokuzwa kutumia teknolojia mpya.
Katika usafiri, kuna gari moshi lenye kutumia stima badala ya makaa. Hili ni zao la teknolojia mpya vile vile. Ingawa mwendo wake ni wa kasi, kasi hiyo na stima huweza kusababisha ajali mbaya mno.
Ingawa madhara yapo lakini manufaa ya teknolojia ni mengi zaidi kuliko madhara yenyewe.
Faida ni kuwa teknolojia hurahisisha shughuli za watu kama vile kufua na kusafiri. Pia hufanya matokeo ya shughuli kuwa bora zaidi. Kazi iliyopigwa chapa kwa kompyuta huwa safi na bora. Vile vile, vitu vinavyotengenezwa siku hizi ni vidogo na vyepesi lakini bora zaidi. Tukichukua mfano wa magari tunaona kuwa ni madogo lakini yenye muundo wa kuvutia. Tatizo tu ni ile kasi kubwa ambayo ni moja ya mambo yanayosababisha ajali nyingi.
Gharama ya vitu vinavyotengenezwa kutumia teknolojia mpya ni nafuu. Teknolojia hii
inatumia malighafi ya kisasa na hivyo kuhifadhi madini yetu. Pia huunda vitu ambavyo matumizi yake yanadhuru mazingira.
Tusisahau kuwa hata hapa kwetu matekinia wa ‘jua kali’ wanapiga hatua. Wanajitahidi usiku
na mchana kuunda vitu vya kutuuzia kwa gharama nafuu. Mitambo ya kusukuma maji sasa
inapatikana. Vyombo vya kusafirisha mizigo, vifaa vya kunyunyizia maji, tanuri ya kuoka
inayohifadhi nishati na vingine vingi, sasa vinaundwa ili kuimarisha sekta hii. Ikiimarika, Kenya
inaweza kuwa nchi yenye uwezo wa viwanda.
Maswali
(a) Eleza umuhimu wa teknolojia mpya kwa zaraa (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(b) “Kwa hakika uhandisi umepiga hatua.” Thibitisha kauli hii kulingana na taarifa. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(c) Unga mkono kauli kwamba hakuna mahali ambapo hapajafikiwa na teknolojia. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(d) Uvumbuzi wa teknolojia umeisaidiaje ulimwengu kupunguza gharama ya uzalishaji wa
bidhaa? (alama 3)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(e) Taja athari zozote mbili za kughasi za uvumbuzi. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(f) Eleza jinsi uvumbuzi umeibuka na anasa ya kipekee. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(g) Eleza maana za maneno haya jinsi yalivyotumiwa katika kifungu. (alama 2)
(i) Malighafi
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(ii) Matekinia
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
SWALI LA PILI UFUPISHO
Soma taarifa ifuatayo kasha ujibu maswali yanayofuata
Uwezo wa kuyakumbuka mambo ni hazina kuu kwa mtu yeyote yule aliye hai. Uwezo huu wa
kukumbuka ni mojawapo ya shughuli changamano za ubongo. Ubongo wa mwanadamu hutekeleza
shughuli hii kwa namna tatu. Kwanza, ubongo hunasa jambo kisha hulihifadhi. Baadaye huanzisha mfuno wa kutoa kilichohifadhiwa. Ubongo ukiathirika kwa namna yoyote katika mojawapo ya njia hizi, basi uwezo wa kuyakumbuka mambo huvurugika.
Ingawa inaaminika kuwa uwezo wa kukumbuka hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi
kingine, wataalamu wa maswala ya kiakili wanabaini kuwa uwezo huu unaweza kuimarishwa.
Uimarishaji huu huhitaji mikakati madhubuti.
Njia mojawapo ya kustawisha uwezo wa kukumbuka ni kupitia kwa lishe. Vyakula
vilivyosheheni vitamini B vyenye amino asidi husaidia kuimarisha uwezo wa kukumbuka. Vyakula kama hivi ni mboga, nyama (hasa maini) bidhaa za soya, matunda, maziwa, bidhaa za ngano, samaki pamoja na mayai. Vyakula vingine muhimu katika ustawishaji huu ni vile vyenye madini ya chuma.
Madini haya huwezesha usambazaji wa hewa katika ubongo kwa wepesi. Vyakula ambavyo vina
madini haya ni mboga za kijani , dengu, mawele, soya, matunda kama maembe, ufuta (simsim)
pamoja nyama, hasa maini na mayai.
Ubongo wa mwanadamu aliye hai hufanya kazi kila wakati, awe macho au amelala. Utendaji
kazi wake huendeshwa na glukosi mwilini kwa hivyo vyakula vyenye sukari hii ni muhimu kuliwa.
Hata hivyo, lazima mtu awe mwangalifu na kuhakikisha kuwa mwili una kiwango cha sukari
kisichohatarisha maisha. Haya yanawezekana kwa kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kama vile mboga na matunda.
Njia ya pili ni kupiga marufuku vileo kama pombe na nikotini. Vileo hivi huathiri utaratibu wa kunasa, kuhifadhi na kutoa yaliyo ubongoni.
Iwapo mtu ana tatizo la kuyakumbuka majina ya watu, ni muhimu kufanya mazoezi ya
kusikiliza kisha kurudia majina hayo wakati wa mazungumzo. Ni bora kulihusisha jina na sura ya mtu.
Kwa njia hii ubongo utanasa na kuhusisha jina na kile kinacholengwa.
Woga na kuvurugika kiakili ni mambo mengine tunayopaswa kuepuka kila wakati. Ni kawaida
mtu kupata woga wakati anapokabili jambo asilokuwa na uhakika na matokeo yake kama mtihani au mahojiano. Lakini anapaswa kuwa makini. Woga huo usikiuke mpaka na kuvuruga kiakili. Vurugu hizi huathiri kilichohifadhiwa ubongoni na namna ya kukitoa.
Hali kadhalika mwili wenye siha nzuri huhakikisha kuwa ubongo ni timamu. Wataalamu
wengi wa siha wanakubali kuwa kuwa mazoezi ya kuyoosha viungo hustawisha ubongo na hivyo
kuhakikisha kuweko kwa uwezo wa kukumbuka mambo. Ni muhimu kuwa na ratiba ya kunyoosha
viungo kila wakati. Fauka ya haya mazoezi ya kiakili kama vile kusoma makala yanayovutia, kujaza mraba na michezo mingine kama mafumbo, vitanza ndimi, ni muhimu katika kustawisha uwezo wa kukumbuka.
Jamii ya watu wenye uwezo wa kuyakumbuka mambo ni jamii iliyopiga hatua kimendeleo. Ni
jukumu la kila mmoja wetu kuimarisha uwezo wa kukumbuka kila wakati.
(Ijaribu na uikarabati Isaac Ipara/ Francis waititu Uk 180 – 181)
Maswali
(a) Kwa maneno 60 – 65, fupisha mchango wa chakula katika uimarishaji wa uwezo wa
kukumbuka.
Matayarisho
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
Jibu
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(b) Fupisha aya tatu za mwisho za mwisho kwa maneno 80-90
Matayarisho
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
Jibu
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
SWALI LA TATU – MATUMIZI YA LUGHA
(a) Konsonanti hizi zinatamkiwa wapi? ( alama 3)
(a) n ……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(b) k ……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(c) p ……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(b) Tambulisha aina za vielezi vya namna katika sentensi zifuatazo (alama 2)
(i) Nyanya hutembea kwa mkongojo
(ii) Mwalimu alimkemea kijeshi
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(c) Eleza matumizi ya kiambishi ‘ji’ katika sentensi zifuatazo
(i) Mtoto amejikata kidole.
(ii) Yeye ni mchoraji.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(d) Ainisha sentensi ifuatayo kwa kutumia jedwali. (alama 5)
Wao watarudi mapema lakini mimi nitabaki.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(e) Kanusha sentensi ifuatayo (alama 2)
Huyu ndiye nimtakaye
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(f) Bainisha virai na utaje ni vya aina gani (alama 3)
(i) Atapona baada ya juma moja.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(ii) Alimnyemelea kwa woga
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(g) Andika sentensi zifuatazo katika hali ya udogo. (alama 2)
(i) Chungu changu kimevunjika.
……………………………………………………………………………………………………
(ii) Ng’ombe wangu ana ndama mkubwa.
……………………………………………………………………………………………………
(h) Andika katika kauli ya kutendeshea. (alama 1)
Kwa nini unamfanya mtoto wake kulia?
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(i) Ainisha mofimu za sentensi ifuatayo. (alama 3)
Alimlia
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(j) Badilisha maneno yaliyopigiwa mstari yawe katika hali iliyopigiwa mstari. (alama 2)
(i) Alimtia hasira alipotoa uamuzi huo. (kitenzi)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(ii) Kazi hii imefanywa kwa ustadi. (kielezi)
10
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(k) Andika katika usemi wa taarifa. (alama 2)
“Sisi tunapenda mchezo wa soka,” Otieno alisema
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(l) Bainisha yambwa kitondo na yambwa kipozi katika sentensi zifuatazo. (alama 2)
Rama aliwapikia wageni wake chakula kitamu.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(m) Akifisha. (alama 2)
Riwaya ya siku njema imesomwa na wengi.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(n) Andika katika ukubwa. (alama 1)
Nguo zake zimeloa maji.
……………………………………………………………………………………………………
(o) Akifisha sentensi ifuatayo kwa njia tatu kuleta maana tatu tofauti. (alama 3)
Mashaka akasema amempata.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(p) Tumia ‘A’ unganifu katika sentens kudhihirisha matumizi ya: (alama 2)
(i) Kivumishi
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(ii) Kiwakilishi
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(q) Andika katika wingi (alama 1)
Baka lililoko kipajini linatisha.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(r) Ni hisia zipi zinazodhihirika katika matumizi haya ya vihusishi?
(i) Maskini! Alianguka mtihani wa kitaifa.
(ii) Mashala! Mtoto huyu ameuubwa akaumbika.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
SWALI LA NNE – ISIMU JAMII
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuatia.
Kijana: Mama unakwenda?
Mama: Kwenda wapi?
Kijana: Ala, wapi kwingine ila mjini?
Mama: Siendi.
Kijana: Haya basi. Dere wacha mioto! Beba mmoja, kwako! Dada njoo, usisafirie
mtumba…. Nafasi ya mtu mmoja, Commercial….. usiachwe, gari ni ishirni
tu…… bei ya chini kuliko mkate.
Dada: Nina ashu, utanibeba?
Kijana: Ah, dada! Ongeza dada, tayari nimekupunguzia kwa kukwambia mbao.
Kawaida huwa ni finje
Dereva: Auntie anasema nini?
Kijana: Ananyonga ashuu.
Dereva: Basi mbebe sare.
Kijana: Dada dere amekulipia. Basi dere gari iko seti, stage ya kwanza jijini.
Maswali
(a) (i) Mazungumzo haya hutokea katika muktadha gani? (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(ii) Toa ushahidi. (alama 3)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(b) Eleza sifa za matumizi ya lugha katika muktadha huu mbali na ulizotaja katika (a) (ii) hapo juu.
(alama 6)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers