Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Kiswahili Kidato Cha Pili Question Paper

Kiswahili Kidato Cha Pili 

Course:Kiswahili

Institution: Form 2 question papers

Exam Year:2011



SHULE YA UPILI YA SHINERS
KIDATO CHA PILI
MUHULA WA KWANZA 2011

1. Tofautisha kati ya vitawe na visawe (al 2)

2. Tenganisha mofimu mbalimbali zinazounda maneno yafuatayo (al 6)
a. Tuliowapenda

b. Aliyeniletea

3. Kanusha sentensi zifuatazo (al 2)
a. Mchoraji amechora picha nzuri

b. Mimi naja kwenu

4. Andika vinyume vya maneno haya (al 3)
a. Sifu

b. Uhayawani

c. Bora

5. Andika sentensi zifuatazo kwa wingi (al 3)

a. Mtu alikimbilia msituni

b. Ua lenu lanukia

6. Ainisha sentensi zifuatazo (al 4)
a. Baba na mama wanakuja kesho

b. Wale wazuri walitunukiwa zawadi

7. Onyesha nomino katika sentensi zifuatazo (al 4)
a. Jambazi lile litashtakiwa na polisi

b. Watieri ana watoto sita

8. Andika maana ya istiari zifuatazo (al 3)
a. Wairimu ni tausi

b. Maswali haya ni mawe

c. Maria ni chiriku

9. Onyesha vivumishi katika sentensi zifuatazo (al 2)
a. Kioo kile ni kikubwa kuliko kioo hiki

b. Mpira huu ni wa nani?

10. Andika nomino mwafaka kukamilisha sentensi zifuatazo (al 2)
a. ________ (maji, mkuki ) yatachotwa na nani?

b. ________ (chuo, mlango) utafungwa.






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers