Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Kiswahili Question Paper

Kiswahili 

Course:Kiswahili

Institution: Form 2 question papers

Exam Year:2012



1)Toa vivumishi vilivyoko katika sentensi hizi na uweke vya kuuliza.

a)Unywele wote umepakwa rangi.

b)Wachezaji wazuri walituzwa jana.

2)Tunga sentensi ukitumia viwakilishi hivi.

a)Cha sifa.

b)Kimilikishi.

3)Tunga sentensi ukitumia viunganishi hivi

a)Ingawa

b)Madhali

4)Unda nomino kutokana na maneno haya

a)Hodari

b)Mtihani

5)Tunga sentensi ukitumia vihisishi hivi

a)Hima

b)Makiwa

6)Toa sifa bainifu za kimatamshi za konsonanti /d/ na /z/

7)Ziandike upya sentensi hizi ukifuatia maagizo.

a)Tulishangazwa na kufa kwa mtoto huyo (Anza:Kufa...)

b)Mtu yule ana sura ya kuogofya. (Andika kwa wingi)

8)Toa maana mbili za sentensi hii:

Mtoto alimfungia mama.

9)Akifisha sentensi hii:

Dobi atafua nguo zetu siku ya jumatatu.

10)Twasema:Mtoto alililia hapa.Toa lia weka finya.

11)Andika sentensi hii katika wakati ujao.

Mama amemlisha mtoto.






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers