Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Mbinu Za Lugha Na Fasihi  Question Paper

Mbinu Za Lugha Na Fasihi  

Course:Bachelor Of Education

Institution: Kenyatta University question papers

Exam Year:2009



KENYATTA UNIVERSITY
UNIVERSITY EXAMINATIONS 2008/2009
SECOND SEMESTER EXAMINATION FOR THE DEGREE OF BACHELOR
OF EDUCATION AND BACHELOR OF ARTS

ECT 313: MBINU ZA LUGHA NA FASIHI

DATE: Friday 3rd April, 2009



TIME: 11.00-1.00pm
------------------------------------------------------------------------------------------------------------
MAAGIZO:
Jibu Maswali Matatu likiwamo swali la kwanza ambalo ni la lazima.

1.
a)
Eleza kwa ufupi maoni ya tume ya Ominde kuhusu Kiswahili.
b)
i)
Nini maana ya kusema kwamba lugha hufungamana na utamaduni?
ii)
Toa mifano mitatu kuthibitisha ukweli wa kauli hii (i)
iii)
Wewe kama mwalimu mtarajiwa unaweza kujifunza nini kuhusu jinsi ya kukabili ufundishaji wa Kiswahili kutokana na ukweli wa kauli hii?
c)
i)
Stadi ya kusikiliza na kuongea zinahusiana na kutofautiana vipi, na zina umuhimu gain katika mchakato wa kujifunza lugha?
ii)
Kwa kila mojawapo ya kundi lifuatalo la sauti andika sentensi moja utakayotumia kufanikisha uwezo wa wanafunzi wa kupambanua sauti katika usikizi wao.
• dh -z
• p – f
d)
Je, kwa maoni yako,isimu jamii inafaa kuwa sehemu mojawapo ya somo la Kiswahili? Toa hoja madhubuti kutilia maki jibu lako.

2.
a)
Jadili mambo yo yote manne ambayo mwalimu anawajibika kutilia maanani katika shughuli ya kuchagua mbinu za kufundishia lugha.
b)
“ Licha ya udhaifu na upungufu wake, mbinu ya kimapokeo bado ina nafasi katika ufundishaji wa Kiswahili katika shule za sekondari humu nchini” Je, ni kwa nini iwe hivi?
c)
Kwa mujibu wa kanuni mojawapo ya mawasiliano, “ mazoezi ambayo yanahusisha mawasiliano halisi hufanikisha kujifunza”
i)
Fafanua sifa zo zote tano zinazotambulisha mawasiliano halisi.
ii)
Kwa mujibu wa kanuni ya utendaji “ Mazoezi yanayohusisha matumizi ya lugha kutekeleza shughuli za maana, hufanikisha kujifunza” Je, kanuni hii hutoa funzo gani kwa mwalimu wa lugha kuhusu mwelekeo anaostahili kuwa nao anaposhugulikia ufundishaji wa lugha husika?

3.
a)
Je kwa maoni yako inafaa au haifai kuambatanisha lugha na fasihi na kuvifundisha kwa pamoja kama somo moja? Toa hoja za kutetea au kukosoa mpango huu.
b)
Ukirejelea tamthilia ya “ Kilio cha Haki” au riwaya ya “ Utengano”,
i)
Bainisha aina zo zote mbili za maudhui kutoka matini moja kati ya matini hizi.
ii)
Andika lengo moja la kipindi ambalo linawiana vizuri na maudhui hayo.
iii)
Eleza kinaganaga jinsi utakavyoshirikisha wanafunzi wako kufanikisha lengo lako ukitegemea hasa utumiaji wa mbinu ya mdahalo na majadiliano ya vikundi.

4.
a)
Ukitoa mifano mufti kutilia maki jibu lako, eleza jinsi lugha ya mama inavyoweza kuathiri Kiswahili cha mwanafunzi na kusababisha ufanyaji wa makosa ya kimsamiati na kisarufi.
b)
Mbinu na vifaa vya kufundisha lugha hupaswa kuchochea wanafunzi kusikiliza, kuongea , kusoma na kuandika Kwa kutoa mifano kamili, onesha jinsi, wewe kama mwalimu, unavyoweza kutekeleza jambo hili wakati wa kufundisha msamiati na sarufi.

5.
a)
Jadili sifa zo zote nne ambazo ungewasisitizia wanafunzi wako ukiwa na lengo la kuwawezesha kutambua tofauti za kimsingi baina ya vitendawili na methali.
b)
Fafanua tofauti baina ya dhana ya ufafanuzi na dhana ya uchambuzi katika muktadha wa somo la mashairi.
c)
“ Wanafunzi wengi katika shule za sekondari huchukia mashairi kwa madai kwamba ni magumu na hayana manufaa kwao.” Je, wewe kama mwalimu wa Kiswahili unaweza kuchukua hatua gani kuhakikisha kwamba wananfunzi wanayapenda mashairi pamoja na kutambua umuhimu wake katika maisha yao?















More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers