Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Form 4 102/3 Kiswahili Fasihi Karatasi 3 Machi 2018 Question Paper

Form 4 102/3 Kiswahili Fasihi Karatasi 3 Machi 2018 

Course:Kiswahili

Institution: Form 3 question papers

Exam Year:2018



102/3
KISWAHILI
FASIHI
KARATASI 3
MACHI 2018
SAA: 2 DAKIKA 30


SHULE YA UPILI YA SAWAGONGO
MJARABU WA 3 2018 MUHULA WA KWANZA
KIDATO CHA TATU

Maagizo
- Jibu maswali matatu pekee
- Swali la Kwanza ni Lazima
-Maswali hayo mengine mawili yachaguliwe kutoka sehemu mbili zilizobaki yaani Tamthilia na Fasihi Simulizi
-Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja
-Watahiniwa ni lazima wahakikishe Kwamba kurasa zote zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo

SEHEMU A: USHAIRI

SWALI LA LAZIMA
soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

MAGATUZI

Mwanakenya kujali, arobaini na saba
Wengine wenye maziwa, wengine wanazo shaba
Talanta wajaliwa, walokuwa na uhaba
Walokuwa wasokuwa, wapokea kwa mikoba

Rasilimali usawa, maliasili akiba
Wanaonyonya ja chawa, dawa yao ni katiba
Wadokozi lidokowa, dokodoko na kushiba
Ugatuzi ni usawa, hakuna wizi kuiba

Wananchi kupewa, madaraka si haba
Wanasiasa kutemwa, wasomi sio haba
Gavana kushitakiwa, akiukapo katiba
Silimali twalinda, ziko nyingi za akiba

Hakuna kubaguliwa, tugawapo faida
Mashinani twapewa, haki zetu bila shida
Jinsia wakilishiwa, ugavi sawa bila shida
Nchini twabarikiwa, sikusiku kuku soda

Mazuri mengi ingawa, hapakosekani shida
Kitaifa kutugawa, maseneta maakida
Kutenda yasiyosawa, bungeni ni ushuhuda
Ugavi wapigania, vita kama Algaida.

MASWALI

a). Eleza dhamira ya mshairi (Al.2)

b). Fafanua ujumbe unaojitokeza katiba ubeti wa mwisho (Al.2)

c). Eleza mbinu alizotumia mshairi ili kutosheleza mahitaji ya kiarudhi (Al.4)

d). Fafanua muundo wa shairi hili (Al. 4)

e). Andika ubeti wa nne kwa lugha tutumbi
(Al. 4)

f). Taja tamathali mbili zilizotumika katika shairi hili (Al. 2)

SEHEMU YA B: TAMTHILIA: KIGOGO (P. KEA)
Jibu swali la 2 au 3

2."Ha-ha-ha-ha! Profesa wa siasa na historia ashasema"

a). Eleza muktadha wa dondoo hili. (Al. 4)

b). Taja na utolee mifano mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo hili
(Al. 4)

c). Jadili mbinu mbalimbali ambazo viongozi katika tamthilia ya kigogo wanatumia ili kujidumisha mamlakani (Al. 2)

Au
3.Fafanua maudhui yoyote kumi yanayojitokeza katika tamthilia ya Kigogo
(Al. 20)

SEHEMU C: FASIHI SIMULIZI
Jibu swali la 4 au 5

4a). Jadili mambo matano ambayo hufanikisha uwasilishaji wa fasihi simulizi (Al. 10)

b). Eleza changamoto zinazokabili uendelezaji wa Fasihi Simulizi (Al. 10)

Au

5a).Eleza maana ya ngano (Al. 2)

b). Hadithi zilitambwa wakati gani? Eleza sababu za hadithi kutambwa wakati ulioitaja. (Al. 5)

c).Taja aina nne za hadithi na uzitolee ufafanuzi mwafaka. (Al. 8)

d) i) Taja fomyula ya ufunguzi wa hadithi
(Al. 1)

ii) Eleza umuhimu wa fomyula hii.
(Al. 4)






More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers