πŸ“˜ Access 10,000+ CBC Exams With Marking Schemes

Prepare your learners for success! Get CBC-aligned exams for Grades 1–9, PP1–PP2, Playgroup and High School - all with marking schemes.

Browse Exams

Instant download β€’ Trusted by 100,000+ teachers β€’ Updated weekly

Form 2 Kiswahili Question Paper

Form 2 Kiswahili 

Course:Kiswahili

Institution: Form 2 question papers

Exam Year:2012



ST BERNARD SECONDARY SCHOOL
KIDATO CHA PILI – KISWAHILI
MWISHO WA MUHULA WA KWANZA
Maagizo: Jibu maswali yote
SEHEMU A – UFAHAMU (Alama 15)
Mwanadamu ni kiumbe aliyeumbwa na maulana. Katika maisha yake mwanadamu ana mahitaji yake ya msingi . mahitaji haya ni kama chakula, mavazi na makazi. Ukosefu wa mambo haya hufanya maisha yake kwenda mbaya. Nimatumaini la mwanadamu kuishi maisha mazuri yasiyo na bughudha yoyote.
Licha ya mahitaji ya kimsingi, binadamu anazo haki zinazotambulika na kuidhinishwa kimataifa.
Ni haki ya kila mwanadamu kuishi. Maisha ya binadamu ni kitu bora na chenye kuthaminiwa. Mwanadamu hapaswi, kwa sababu yeyote ile, kutolewa au kujitoa uhai wake.
Ibada ni mojawapo ya matendo yanayomkurubisha mwanadamu na muumba wake. Hivyo, mtu ana haki mradi tu asimbughudhi mwingine.
Binadamu ana haki ya kujieleza au kutoa maoni bila kudhibitiwa kwa njia yoyote ile. Nihaki ya binadamu kutangamana na binadamu wenzake katika asasi kama vile vyama vya kishirika, kisiasa, kushughulikia masuala ya kijamii na vinginevyo.
Elimu humwezesha mtu kukabiliana maisha ipasavyo. Humwezesha pia kujiimarisha kiakili, kiuchumi na kijamii. Ni sharti kila mwanadamu apate elimu.
Kupata huduma bora za afya ni nguzo muhimu ya kumstawisha mtu binafsi na jamii kwa jumla. Ni haki ya kila binadamu kupata huduma hizo.
Katika shughuli zake za kila siku, binadamu huweza kujichumia mali. Ana haki ya kuwa nayo na kuitumia mradi tu ameipata kwa njia ya halali.
Mungu aliwaumba binadamu wote wakiwa sawa ; weupe kwa weusi warefu kwa wafupi na wembamba kwa wanene. Mwenyewe ndiye aliyewaweka katika hali hizo. Wote wako sawa. Hivyo basi si haki kumbagua yeyote kwa misingi wa kikabila dini. Rangi, matabaka na kijinsia.
Zilizotajwa hapa ni baadhi tu ya haki za binadamu.
Maswali:
1. Taja mambo matatu ya kimsingi ambayo mwanadamu anahitaji ?

2. Mbali na haki zilizorejelewa, taja haki zingine tatu za kibinadamu?

3. Taja faida mbili za elimu?

4. Kwa nini ni vibaya kubagua wengine?

5. Chakula kina umuhimu gani kwa mwanadamu?

6. Makazi ni muhimu kwa mwanadamu . Eleza

7. Toa maana ya maneno yafuatayo kama yalivyohtumiwa katika kifugu hiki:
(a) Mahitaji
(b) Kuidhinishwa
(c) Asasi
(d) Kutangamana
(e) Kujiimarisha

8. Kutokana na ufahamu toa kichwa kinachofaa.


SEHEMU B – MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 45)

1 Andika sentensi hizi kwa wingi (alama 5)

(a) Nilinunua kitabu kikihiki ulichonacho
(b) Amevaa nguo iyo hiyo tangu juzi.
(c) Mwizi alitumia upanga uohuo bawabu
(d) Jumba lilihili ullionalo lilijengwa mwakani wa 1930.
(e) Shauri lenu likiwa ni lilohilo litamkasirisha mwalimu.

2 Tunga sentensi ukitumia hali ya ukubwa na nomino hizi (alama 10)

a) Ngoma
b) Nyoka
c) Kidole
d) Mdomo
e) Mbwa

3 Akifisha sentensi hizi zilete maana tofauti kasha uelezee maana zilizotolewa na kila moja (alama 10)

(a) i). Ameenda (alama 4)
ii). Ameenda

(b) i). Ali anakula (alama 4)
ii). Ali anakula

4 Changua kiunganishi mwafaka kukamilisha sentensi zifuatazo

i). Mimi nimechoka ____________ nimechoka sana (alama 1)
ii). Niliosha vyombo ____________ nikaenda kusoma (alama 1)

5 Tunga sentensi tano ukitumia β€œ-enye” (alama 5)

6 Andika vitenzi vifuatavyo katika hali ya kutendeshana (alama 5)
i). Penda
ii). Enda
iii). Lia
iv) Funga
v). panga

7 Tunga sentensi ukitumia nomino zifuatavyo (alama 5)
i). Nakili
ii). Enda
iii). Licha ya
iv). Rabsha
v). Tekeleza

8 Maneno haya yamo katika ngeli ngani? (alama 5)
i). Upishi
ii). Maembe
iii). Mahali
iv). Mdomo
v). Ngoma






More Question Papers


Exams With Marking Schemes

End Term 3 Exams

Mid Term Exams

End Term 1 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers