📘 Access 10,000+ CBC Exams With Marking Schemes

Prepare your learners for success! Get CBC-aligned exams for Grades 1–9, PP1–PP2, Playgroup and High School - all with marking schemes.

Browse Exams

Instant download • Trusted by 100,000+ teachers • Updated weekly

Kiswahili Form One Question Paper

Kiswahili Form One 

Course:Kiswahili

Institution: Form 1 question papers

Exam Year:2007



FRIENDS SCHOOL KAMUSINGA
KIMILILI

KISWAHILI
KIDATO CHA 1 MUHULA WA 1 2007
TAMRINI YA 1
MUDA: SAA 2

A. UFAHAMU (ALAMA 20)

Soma taarifa kasha jibu maswali yafuatayo

Maendeleo ya teknolojia duniani yamepiga hatua kubwa sana katika nyanja kama simu tamba. Kifaa hiki kinabebeka kwa urahisi. Anachohitaji mtu ni kuiweka pochini au mfukoni. Popote aendapo, ataweza kuwasiliana na watu hata kama wako mbali naye.

Ingawa simu tamba zimerahisisha mawasiliano, zimeweza kuzusha matatizo kwa watu kwa ajili ya matumizi mabaya.

Kwanza, simu tamba zimetumiwa vibaya na madereva barabarani na kuchangia kutokea kwa ajali. Mathalani, madereva wengi wamesababisha ajali kwa kuongea kwa simu tamba huku wameshika usukani. Nadhari au urazini wa dereva hutekwa kwenye simu na husahau kuwa ana jukumu jingine la kuendesha gari. Mambo yanaharibika zaidi wakati ambapo anayoyasikia humpandisha hisia zake akachangamka, akasikitika au akakasirika. Haya humfanya apoteze fahamu na kusababisha ajali. Hii ndiyo sababu sheria inaharamisha matumizi ya simu tamba wakati wa kuendesha gari.

Ajali hazisababishwi na madereva tu. Hata watembeaji wamechangia wanapotumia simu tamba bila uangalifu. Kwa mfano, watu wengi wanapopigiwa simu, huanza kuongea na kutekwa na mazungumzo hadi wakasahau walichokuwa wakifanya. Ikiwa alikuwa akivuka barabarani, husahau haya na kuzingatia mazungumzo. Iwapo gari lilikuwa linakuja kwa kasi wakati mwingine hushindwa kusimama na moja kwa moja kumpiga dafrao.

Visa vimetokeo kote duniani jinsi simu tamba zimeleta balaa na beluwa. Kuwa kisa cha daktari aliyepigiwa simu tamba wakati alikuwa akifanya upazuaji. Aliacha kushugulikia mgonjwa na kuzingatia mazungumzo. Mgonjwa alivuja damu hadi akafariki.

Simu tamba hubebeka popote mtu aendapo. Hili nalo limewachongea baadhi ya watu. Watu wameweza kufichua siri zao hadharani. Mathalani mtu anaweza kuelezea mipango yake kuwa anaenda benki kuchukua pesa. Anasema haya kwa kinywa kipana ili hali hawajui abiria wenzake katika matatu. Baadaye anaandamwa na watu asiowajua na kumpora vyote. Atabaki kwenye mtaa akishindwa wezi hao walijuaje kuwa ana kitita cha fedha. Asilolijua ni kuwa ni yeye aliyejikaanga kwa kumwaga mtama penye kuku wengi kwa njia simu tamba.

Pana kundi la watu wanapoongea kwenye simu tamba, huwakirihi wenzao kwa kupaza sauti utafikiri wanahutubia umati wa watu bila kipazasauti. Zaidi ya makelele ya watu, pana milio ya simu tamba ambayo pia huchukiza na kukatiza shughuli za watu, kama vile maabadini. Fikra zote za watu hutekwa na kuelekezwa katika mawasiliano na Muumba wao. Kisha milio ya simu tamba inaposikika, shughuli zao hutatizika kwani watu hutekwa na milio hiyo. Maombi nayo yanakatishwa. Hii ndiyo sababu matumizi ya simu tamba yamepigwa marufuku katika sehemu kama vile mahakamani, maabadini benkini na nyinginezo.

Ingawa zimerahisisha mawasiliano, wakati huo huo, simu tamba zinaweza kuleta suita fahamu kati ya watu. Inasemekana kuwa Bwana mmoja alimwona bibi wa rafiki yake akiwa na mzee mmoja katika mkahawa. Mazungumzo yao yalikuwa yenye vicheko vingi. Bwana alimtuhumu yule bibi kuwa na jicho la nje na kuamua kumpigia mwenzake simu mara moja. Mwenzake alipopokea ujumbe, alikuwa chapuchapu kwa kufumba na kufumbua, alipoelekezwa. Alikuwa amejaa mori na kuhamaki, tayari kumeza mkewe mzimamzima. Alipigwa na butwaa kuona kuwa aliyekuwa akiongea na bibi yake ni babake mzazi. Baada ya kutafakari, alidhani rafiki yake alitaka kuivuruga ndoa yao. Ndoa nyingine nyingi zimefurugika kwa njia hii ya matumizi ya simu tamba.

Kiafya, simu tamba zina madhara. Kuna miale ya hatari inayotoka kwenye simu. Miale hii inaathiri mtu kiafya anapoitumia mara nyingi na kwa muda mrefu. Hii ndiyo sababu watu wengi hulalamika kuwa wanaumwa na kichwa baada yakuzitumia kwa muda.

Ni muhimu kwa wanaozimtua wawe waangalifu ili kupunguza matatizo haya. Madereva wanapaswa kutii sheria inayopiga marufuku matumizi ya simu tamba wanapoendesha. Sheria nayo yatakiwa iwe imara vilivo kwa wanaozikiuka. Watu wanaotatiza wenzao yafaa wakomeshe tabia hizo.

Maswali

1. Andika kichwa kinachoafiki habari uliyosoma. (alama 2)


2. Taja madhara sita yatokanayo na simu tamba. (alama 6)

3. Kwa nini matumizi ya simu tamba yamepigwa marufuku mahakamani?
(alama 4)


4. Toa ushauri kwa wale wanaotumia simu tamba vibaya wakawatatiza wenzo.
(alama 3)




5. Eleza maana ya matumizi haya ya lugha. (alama 5)
(a) Haramisha


(b) Maabadani



(c) Balaa na beluwa;

(d) Kujaa mori!

(e) Kumwaga mtama penye kuku wengi;


B. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

1. Tambua vielezi katika sentensi hizi. (alama 4)

(a) Wachezaji wetu walicheza vizuri sana.

(b) Wachezaji watatu watawasili kesho jioni.


2. Neno “Huyu” limetumiwa vipi katika sentensi hizi. (alama 2)

(a) Huyu amekuja kwangu.

(b) Mgeni huyu amekuja kwangu

3. Bainisha aina za maneno katika sentensi hizi. (alama 5)

(a) Kipofu yule anaandika haraka sana.


(c) Rodgers alijitahidi lakini hakufaulu mtihani


4. Ainisha mofimu katika sentensi hii. (alama 4)

Ameshinda






5. (a) Taja sauti ya kitambaza. (alama 1)

(b) Sauti ya kitambaza hutamkiwa wapi? (alama 1)

(c) Taja vipasho viwili vya mdomo. (alama 2)

(d) Taja sauti sita ambazo hutamkwa kwenye ufizi. (alama 3)






6. Sauti za konsonanti hutamkwa kutegemea vigezo viwil; vitaje. (alama 2)



7. Eleza maana ya maneno yafuatayo yanayorejelea matamshi ya sauti na kisha utolee mfano kila mojawapo.

a. Kiimbo (alama 2)


b. Shadda (alama 2)


8. Eleza maana ya sauti ghuna. (alama 2)


Andika mfano mine ya sauti ghuna. (alama 2)

9. Andika maneno mawili yenye mpangilio ufuatao wa silabi. (alama 4)

a. Konsonanti mbili na irabu (KKV)


b. Konosonanti tatu na vokali/irabu . (KKKV)

10. Kamilisha methali zifuatazo. (alama 4)

a. Polepole ya kobe…………………………………………………………
b. Angaruka juu kipungu……………………………………………………
c. Msafiri………………………………………………………………………
d. Mwenda tezi na omo…………………………………………………………

C. (a) Nini maana ya fasihi. (alama 2)




(b) Eleza madhumuni matano ya fasihi (alama 10)












(c) Orodhesha vipera vya ngano. (alama 5)








(d) Tofautisha baina ya fasihi andishi na fasihi simulizi kwa kutumia sifa tatu.
(alama 3)


















More Question Papers


Exams With Marking Schemes

End Term 3 Exams

Mid Term Exams

End Term 1 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers