Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Got a question or eager to learn? Discover limitless learning on WhatsApp now - Start Now!

Kiswahili Form Two Question Paper

Kiswahili Form Two 

Course:Kiswahili

Institution: Form 2 question papers

Exam Year:2007



FRIENDS SCHOOL KAMUSINGA
KIMILILI


KISWAHILI
102/2
MJARABI WA 3
KITADO CHA 2
MUHULA WA 1 2007

KUTUZA
A – 20 B – 40 C – 20 JUMLA



MAAGIZO

• Jibu maswali yote katika nafasi zilizoachwa wazi baada ya kila swali.

Soma sahiri lifuatalo kasha ujibu maswali

1
Ghulamu: Meachwa kining’inia, kati yake panda njia
Mola yendayo kulia, ya tamaduni sikia
Ya kushoto nakwambia, ya kigeni furahia
Mesaki naning’inia.

2
Nimebaki papasia, ja kipofu kukisia
Nimeshinwa kuteua, ipi nitafuatia
Kifuata mbili njia, msamba tapasukia
Mesaki naning’inia.

3
Nimechoshwa simamia, kati nani talezea
Wenzangu nauza pia, pani mwongozo tanifaa
Nuru kiniangazia, mpate kuniopoa
Mesaki naning’inia.

4
Mamboleo: Acha nikupe zinduo, ewe mwenzangu kijana
Sisi wana mamboleo si fani yetu ya jana
Kwetu zina mwelekeo, za kingeni zitafaa
Tamaduni tuziase.

5
Mhenga: Kijana ‘ngekuwa bora, kutosikiza ya pofu
Ewayo yangu mafikira, za kigeni nazihofu
Mwacha mila hana fora, katu siwezi msifu
Siase tamadunizo.

6
Ghulamu: Lipi mlonishauri, mwataka niwe kinyonga
Hayo mimi sitakiri, kuwa fisi siwi jinga
Nalotaka la fahari, na mbele niweze songa
Nisibaki nimesaki.

7
Kithamini tamaduni, najikuta tatisoni
Nendapo huku mjini, kujipitia njiani
Na kwao wangu uneni, nambwa katoka shambani
Nabaki nimesaki.


8
Nifatapo ya kigeni, mavazi na maongezi
Nifikapo mashambani, kiwafanyia mapozi
Adabu sina muhuni, ati kakosa malezi
Kutofata tamaduni.

9
Mzee busara: Langu mwana nisikia, kwa kweli litakufaa
Papo penye panda njia, unda kati yako njia
Tamaduni ngeni pia, chukua yalo murua
Zote asi nusunusu.


(a) Wahusika wamepea majina ya majazi. Eleza kwa ufupi sifa kuu ya kila mhusika kutokana na jina alilopewa. (alama 4)









(b) Mshairi ametumia maneno yasiyokuwa ya lugha sanifu. Taja mifano mitano ya maneno kama hayo kasha uyaandike kwa lugha sanifu. (alama 5)









(c) Yaandike maneno ya mzee Busara kwa lugha nathari. (alama 4)








(d) Shairi hili laweza patikana katika bahari mbili. Fafanua. (alama 4)














(e) Eleza maana ya mafungu ya maneno kama yalivyotumiwa katika shairi. (alama 4)
i. Ja kipofu kukisia


ii. Acha nikupe zinduo



iii. Kuwa fisi siwi jinga


iv. Kiwafanyia mapozi



SEHEMU YA B – MATUMIZI YA LUGHA . ALAMA 40

(a) Andika sentensi hizi upya kwa kufuata maagizo yaliyo katika mabano
(i) Ukienda uhabeshi, utajifunza lugha ya kiyahudi. (Rekebisha makosa) (alama 2)


(ii) Usipoziba ufa, utajenga ukuta (Yakinisha) (alama 2)


(iii) Juma alizinunua mbuzi, kumbekumbe na ndizi alipoenda mjini Mandizini. (Andika kwa ukubwa) (alama 5)





(b) (i) Andika majina mawili ambayo hupaatikana katika Ngeli ya I – I (alama 2)


(ii) Eleza tofauti iliyoko kati ya mofimu na silabi. (alama 4)




(iii) Ainisha mofimu za neneo lifuatalo; (alama 4)
Wanapambana


(iv) Ainisha viambishi katika neno hili. (alama 6)
Waliwakimbilia


(c) (i) Taja aina 6 za nomino na kutoa mifano kwa kila moja. (alama 6)










(ii) Tunga sentenzi kudhihirisha matumizi ya kila aina ya kivumishi ulichopewa.
(a) Kivumishi cha kuuliza. (alama 1)


(b) Kivumishi kisisitisi. (alama 1)


(c) Kivumishi cha jina. (alama 1)


(d) Kivumishi cha A- unganifu. (alama 1)


(e) Kivumishi cha kumiliki. (alama 1)



(d) Kwa kutumia mifano mwafaka onyesha matumizi tatu ya alama ya uakifishaji ya Ritifaa. (alama 3)







FASIHI SIMULIZI
1. Eleza tofauti katika aina hizi za nyimbo.

(a) Kimai na Wawe. (alama 2)


(b) Eleza sifa tatu za nyimbo za mbolezi. (alama 3)




2. Kamilisha methali zifuatazo. (alama 5)
(i) Ndugu wakigombana chukua jembe……………………………………………….
(ii) Pema usijapo pema……………………………………………………………..
(iii) Usimlaumu ………………………………………………nazilimeliwa na mwezi.
(iv) Mgomba hupaliliwa ……………………………………………ni nguo
(v) Kiendacho kwa mganga…………………………………………………………..


3. Eleza maana ya misemo ifuatayo. (alama 5)
(i) Kaa tahayatu…………………………………………………………………
(ii) Kaa kiungani……………………………………………………………………
(iii) Kata kalima…………………………………………………………………..
(iv) Meza maneno…………………………………………………………………
(v) Mfua uji…………………………………………………………………………..


4. Tajana na ueleza aina tano za ngano. (alama 5)










More Question Papers


Popular Exams



Return to Question Papers